15/07/2026
SABABU 5 KWA NINI USISIKILIZE BONGO FLEVA
1. KILA WIMBO UNA ROHO NYUMA YAKE
Nyimbo zina nguvu ya kuingia rohoni kupitia masikio yako hayo.
Kwanini uache mara moja kusikiliza bongo uchafu kwa sababu nyimbo za Bongo Fleva zimejaa lugha chafu,tamaa,uasherati,majivuno, na maisha yasiyompendeza Mungu.
Biblia inasema:
“Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mithali 4:23
Ukisikiliza kitu kila siku, kinaanza kutawala mawazo yako na tabia zako.
2. UTAPOTEZA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU
Watu wengi wanajikuta
wanaimba nyimbo za dunia kuliko nyimbo za Mungu,
wanakumbuka mistari ya muziki kuliko mistari ya Biblia,
wanapenda starehe kuliko uwepo wa Mungu.
Wiombo unaousikiliza unaweza kukupeleka karibu na Mungu au mbali na Mungu.
Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Dunia ina namna yake na watu wa Mungu Wana namna Yao ya kuishi
3. MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA
Vijana wengi hupenda huiga mavazi, maneno, mienendo,
na maisha ya wasanii.
Tatizo ni kwamba si kila Mtu maarufu ni mfano mzuri wa kuigwa.
1 Wakorintho 15:33
“Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”
Ukimsikiliza mtu sana, mwisho unaweza kuanza kufanana naye kitabia iwe ni kwa mema au kwa mabaya.
4. HUSHUSHA KIWANGO CHA UTAKATIFU
Nyimbo za bongo fleva huchochea
tamaa za mwili,
mawazo machafu,
na dhambi.
Ndio maana k**a kijana ni ngumu kuishinda zinaa k**a Bado unasikiliza nyimbo za Aina hii
Roho Mtakatifu anapenda mazingira safi ya kiroho.
Wafilipi 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Jiulize swali hili
Wimbo ninaousikiliza unanijenga kiroho au unanishusha kiroho ?
5. KUPOTEZA MUDA WAKO WA THAMANI
Vijana wengi hutumia masaa mengi
kusikiliza muziki,
kufuatilia wasanii,
na kuimba nyimbo za dunia,
lakini hawana muda wa
maombi,
kusoma Biblia,
wala kujijenga.
Waefeso 5:15-16
“Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda… mkiukomboa wakati.”
Kile unachokipa muda mwingi kinaonyesha kina nafasi gani moyoni mwako.
MUNGU AKUBARIKI