11/08/2026
MAISHA NI HADITHI,IANDIKE YAKO VIZURI.
Kwa bahati mbaya ni kwamba,hakuna anayeijua siku yake ya kuondoka hapa duniani,na hakuna anayejua mshale wake wa saa umebaki kuzunguka mara ngapi.
HIVYO
Nikusihi wakati ungali bado uko hai jitahidi kufanya mambo yafuatayo.
Jitahidi sana kuishi maisha ya Utakatifu kila saa na kila wakati wakati uwapo hapa duniani.Ishi maisha yaliyo bora binafsi kuanzia kiroho,
pata muda wako binafsi na Mungu wako,jishugulishe na mambo yatakayokufanya kuwa bora kiroho,ie soma neno,pata muda wa kushiriki ibada,pata muda wa kuongea na kumsikia Mungu,toa sadaka,shiriki matukio ya kiroho mahali unapoabudu.
Jitahidi kufunga,na ukifunga funga kweli yaani maanisha.
*Kimwili* jitahidi kujijali pata muda wako binafsi, pata muda wa kujijali k**a kupumzika,k**a hujafunga kula vizuri kwa kadri ya uwezo wako, jipende vaa vizuri,lala sehemu nzuri samehe watu(hii ni sehemu ya kujijali na kujipenda.
Kwa habari ya *familia* yako fanya chochote unachoweza kilicho ndani ya uwezo wako kwaajili ya familia yako,k**a ni wazazi fanya kitu kizuri kwao kilicho ndani ya uwezo wako,wajulie hali kila mara,watengenezee mazingira mazuri ya wao kufurahia uzazi wao kwako .
Ndugu zako wa damu na hata ndani ya familia be good to them pale unapoweza jitoe kwao kwenye mambo yao ya muhimu
K**a mke au mme jitahidi uwekeze kwa mwenza wako,mtengenezee mazingira bora ambayo hata kesho ukiondoka asihangaike,mpende na mwonyeshe upendo .
Watoto wako vilevile wekeza upendo wa dhati kwao,jitoe kwao wewe pekee ndiye utakayewapenda bila sababu, upendo wa watu wengine huja kwasababu lakini upendo wa mzazi ndiyo ule tunauita upendo wa Agape,usiwekeze kwa watu wa nje ukasahau watoto wako,wapende kwa kuwapa muda,kwa kuwa sikiliza na kuwafanyia vitu vilivyo ndani ya uwezo wako kwaajili ya kuwajenga na kuwafanya kuwa bora .
Siku utakayoondoka kila mtu aweza kukusahau lakini siyo watoto waliotoka kwenye tumbo/viuno vyako
Pastor Winnie