22/08/2026
DHANA YA DHAMBI K**A ILIVYOFUNDISHWA KATIKA MAANDIKO YA KIEBRANIA YA BIBLIA - 1
Musa alieleza jinsi Adamu hakuamini neno la Mungu ambalo aliambiwa na hivi ndivyo dhambi iliingia katika shughuli za mwanadamu.
Hii ilionyeshwa k**a kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Hata hivyo, neno ‘dhambi’ lilitumiwa kwa mara ya kwanza kuelezea tendo la mwanadamu katika Mwanzo 4.
Mwanzo 4:7 K**a ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Neno ‘dhambi’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘chattah’ . Muundo wa kitenzi cha neno ‘chattah’ ni neno ‘chata’ linalomaanisha kukosa, hasara, kupungukiwa au kutokuwepo.
Marejeleo ya neno ‘chattah’.
Mwanzo 20:6 Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.
Mwanzo 20:9 Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.
Mwanzo 31:39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku.
Neno ‘hasara’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘chata’ (muundo wa kitenzi cha neno ‘chattah’) ambalo hudokeza ukosefu, au kitu kilichokosekana au kutokuwepo.
Neno ‘chattah’ lilitafsiriwa kuwa ‘dhambi’ katika maandiko yafuatayo;
Mwanzo 18:20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha S***ma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
Mwanzo 31:36 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N'nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
Mwanzo 50:17 Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.
Kutoka 10:17 Basi sasa, nawasihi, nisameheni dhambi yangu mara hii moja tu, mkamwombe Bwana, Mungu wenu, aniondolee kifo hiki tu.
Mambo ya walawi 4:3 k**a kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa Bwana ng'ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi …23 akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ataleta mbuzi awe matoleo yake, mume, mkamilifu;
Mambo ya walawi 26:18 Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu… 21 Nanyi ikiwa mwaenenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, k**a dhambi zenu zilivyo.
Hesabu 5:6 Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yo yote, ifanywayo na binadamu, kumwasi Bwana, na mtu huyo akawa na hatia;
Hesabu 12:11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.
Mika 6:13 Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nami nimekupiga kwa pigo liumizalo sana; nimekufanya kuwa ukiwa, kwa sababu ya dhambi zako.
Neno ‘chattah’ lilitafsiriwa kuwa ‘adhabu’ katika andiko lifuatalo.
Zakaria 14:19 Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.
Vivyo hivyo tafsiri ya KJV inatafsiri neno hilo k**a adhabu (punishment) katika andiko hili chini japokua tafsiri ya Kiswahili inachagua kubaki na neno “dhambi”.
Lamentations 4:6 For the punishment of the iniquity of the daughter of my people is greater than the punishment of the sin of S***m, that was overthrown as in a moment, and no hands stayed on her. (KJV)
Isaya katika maandiko yake alieleza hali ya dhambi kuwa ‘ugonjwa’ katika maneno yake ili kumaanisha upungufu, yaani, kitu kilichokosekana au kutokuwepo.
Isaya 29:18 Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho chuo, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
Isaya 32:3 Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza.
Isaya 35:5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 6 Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka k**a kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.?
Isaya 42:7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Isaya 53:4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. (5) Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona..
Nabii Isaya anahusianisha ugonjwa na hali ya kiroho ya mwanadamu katika dhambi.
Alitaja dhambi kuwa ni uziwi, upofu na giza.
Kwa maneno mengine, dhambi ina maana ya kasoro, kushindwa, upungufu, kutokuwepo au hasara.
Kwa hiyo, alifafanua wokovu kuwa ‘uponyaji’ wa hali ya kiroho ya mwanadamu katika dhambi.
Swali linalokuja kichwani ni hili; Ni nini kilikosekana au kutokuwepo au kupungua?
Acha tuchunguze maandishi ya Musa ili tuone yaliyotukia hapo mwanzo;
Mwanzo 1:1 1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. 5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
Kumbuka kwamba katika Mstari wa 1, kulikuwa na rejea ya maneno ‘mbingu na nchi’.
Mbingu Na Nchi*
Kumbuka kwamba neno 'mwanzo' lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania 'reshiyth' ambalo linamaanisha ‘ya kwanza’, ‘bora’; au ‘iliyo kuu’.
Inarejelewa kwa mpangilio, wakati au cheo (rank).
Neno ‘mbingu’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘shamayim shayem’ ambalo linamaanisha anga.
Linarejelewa kuelezea ambapo maumbo ya angani (celestial bodies) yanazunguka.
Hata hivyo, neno ‘mbingu’ pia lilitumiwa kufafanua makao ya Mungu.
Hii inaweza kuzingatiwa na kuonekana katika maandishi ya Musa.
Mwanzo 28:17 17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha k**a nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. 18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha k**a nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. 22 Na jiwe hili nililolisimamisha k**a nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Musa aliandika kuhusu kukutana kwa Yakobo na Mungu na akaeleza mbinguni kuwa ni nyumba ya Mungu.
Alifafanua zaidi mbinguni k**a mahali ambapo Mungu anakaa.
Kutoka 20:22 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.
Kumbukumbu la Torati 4:36 Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto.
Musa alieleza mbinguni k**a mahali ambapo Mungu alisema kutokea hapo.
Kumbukumbu la Torati 26:15 Uangalie kutoka makazi yako matakatifu mbinguni, uwabarikie watu wako Israeli, na nchi uliyotupa k**a ulivyowaapia baba zetu, nchi imiminikayo maziwa na asali.
Vivyo hivyo, neno ‘nchi’ katika Mwanzo 1:1 lililotafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘erets’ linamaanisha shamba (field), nchi au ardhi.
Angalia jinsi lilivyorejelewa na Musa katika maandishi yake.
Mwanzo 1:26 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; 30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Mwanzo 6:6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya..
Mwanzo 11:1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
Musa alielezea “nchi” k**a mahali ambapo mwanadamu hukaa, kuchunguza na kuratibu shughuli zake.
Kwa hiyo, matumizi ya neno “nchi” yanaeleza nafasi ya mwanadamu na shughuli zake ndani yake.
Kumbuka kwamba Musa alitumia maneno kufafanua mambo halisi ya kiroho kwa picha ya ahadi ya Mungu.
Maneno ‘mbingu na nchi’ yalirejelewa pamoja na Musa ili kueleza muungano wa Mungu na mwanadamu mahali pamoja (wanadamu).
Musa alizungumza juu ya ahadi ya Mungu ya kukaa ndani ya mwanadamu.
Alifafanua zaidi jambo hili katika Mwanzo 1 mstari wa 2 k**a roho ya Mungu juu ya uso wa maji.
Mwanzo 1:2 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
Roho/Uzima/Nuru Ya Mungu
Kumbuka kwamba neno ‘ukiwa’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘tohu’ ambalo linamaanisha utupu, hakuna kitu, au upotevu.
Neno ‘giza’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘choshek’ ambalo linamaanisha kutojulikana, hakuna kitu kinachoonekana.
Linamaanisha ’bila nuru’.
Kishazi ‘uso wa vilindi’ ni sawa na kile Musa alichoeleza kuwa ‘uso wa maji’ katika mstari huo huo.
Neno ‘uso’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘paniym’ ambalo linamaanisha mwonekano (appearance).
Kwa hiyo neno ‘ukiwa tena utupu’ ndilo ambalo Musa alieleza kuwa ‘giza juu ya uso wa vilindi’.
Chunguza kwa karibu kauli zinazofuata;
…Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mst 3 Mungu akasema, Iwe nuru, ikawa nuru.
Neno ‘roho ya Mungu’ lilitafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania ‘elohiym ruach’.
Neno la Kiebrania ‘ruach’ linamaanisha upepo, hewa au pumzi inayozungumzia uhai.
Hivyo, roho ya Mungu ni uhai (pumzi) ya Mungu.
Musa alielezea utendaji wa Mungu k**a uwepo wa roho ya Mungu juu ya uso wa maji.
Alifafanua zaidi k**a uwepo wa nuru yake.
Felician Makarios Phos
Kainos Creation Church (KCC)
0742107009