28/06/2026
Yajue matibabu yanayotolewa kumsaidia mtu asipate maambukizi ya VVU baada ya tendo la ndoa.
Tuseme leo umeshiriki tendo la ndoa halafu kondom ikapasuka au ikachomoka au umebakwa unafanya nini baada ya hapo? Kwa sasa k**a umetokewa na hali mojawapo kati ya hizo kuna tiba ya kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU. Tiba hiyo ndio inaitwa PEP. Kuna tiba nyingine inayoitwa PrEP hii pia inasaidia kuzuia maambukizi ya VVU lakini yenyewe inatumika kabla ya tendo la ndoa kwa watu ambao wako kwenye hatari ya kupata maambukizi mfano wafanyabiashara za ngono (hii tutakuwa na somo lake siku nyingine)
Twende kwenye PEP sasa;
PEP kirefu chake ni Post-exposure prophylaxis. Hii ni tiba ambayo inatolewa kwa mtu ambaye ameshiriki tendo la ndoa ama kwa hiyari au kwa kubakwa ili kumsaidia asipate maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Tiba hii inatolewa iwapo kulikuwa na mgusano wa moja kwa moja wa uke na uume kwa mfano kondom ilipasuka au ilichomoka au mtu alibakwa.
Unaipataje PEP
Iwapo umetokewa na hali yoyote kati ya hizo ama kondom imechomoka au imepasuka au umebakwa, nenda kwenye kituo cha afya cha karibu kabla masaa 72 hayajaisha. Dawa hizi zinatolewa na daktari. Daktari atachukua maelezo yako kwa kina juu ya afya yako kwa ujumla. Baada ya hapo atakuambia ufanye vipimo vya HIV na hapo kutakuwa na mambo matatu:-
Kwanza; k**a hautakubali kufanya vipimo vya HIV utaambiwa uondoke na hautapewa dawa za PEP.
Pili; ukipima ukakutwa na maambukizi utapelekwa clinic za kawaida za watu wanaoishi na VVU ili wakuanzishie dawa.
Tatu; ukipima ukakutwa hauna maambukizi ndipo unapewa dawa za PEP ili zikusaidie usipate maambukizi iwapo mtu uliyefanya nae ngono alikuwa na maambukizi.
Dawa za PEP zinatumiwa kwa muda wa siku 28. Lakini iwapo umeanza dawa na mwenzako akawa tayari kupimwa na akapimwa akawa hana maambukizi basi daktari anaweza kukuachisha dawa.
Dawa hizi zinatolewa ndani ya masaa 72. Iwapo masaa 72 yamepita utashauriwa upime baada ya wiki 6 na k**a utakuwa umepata maambukizi utaanza dawa za ARV .
Ukimaliza PEP utarudia vipimo baada ya wiki 6 na baadae miezi mitatu. Iwapo utakuwa hauna maambukizi hautafuatiliwa tena iwapo utakuwa na maambukizi utaanza matibabu ya ARV k**a wagonjwa wengine.
Wakati wote unapotumia PEP usichangie damu(ndani ya miezi 12) na usishiriki tendo la ndoa bila kutumia kondom.