Apostolic Ministry Tanzania AMT

Apostolic Ministry Tanzania AMT Kweli itakuweka huru.

15/09/2024

Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu.
Zaburi 84:1

15/09/2024

Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Zaburi 84:11

13/11/2022

Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.
Zaburi 21:2

19/02/2021

KATIKAKATI YA HABARI MBAYA
Kuna Habari Njema
Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa k**a tai;
Zaburi 103:5

18/09/2020

Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba.
2 Timotheo 4:17

25/06/2020

Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Zaburi 17:15

31/05/2020

Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
1 Wakorintho 1:9Amini tuu akisema amesema

1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa...
06/05/2020

1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 Timotheo 4:1

2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
2 Timotheo 4:2

6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
2 Timotheo 4:6

7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
2 Timotheo 4:7

8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
2 Timotheo 4:8

Mwalimu wangu,baba yangu

Yale maneno Yako. Yanaishi
Nitakuona tena siku moja

17/04/2020

1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
Luka 18:1

2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
Luka 18:2

3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
Luka 18:3

4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
Luka 18:4

5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
Luka 18:5

6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
Luka 18:6

7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
Luka 18:7

8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Luka 18:8
Omba omba Mungu azuie corona inawezeka kwake aminie tuuu

05/03/2020

SOMO LA LEO

NEEMA(GRACE)

Neema ni nini-- Neema ni upendeleo wa Mungu kwetu ambao hatukustahili.
Kwa maneno mengine ingawa tulikuwa wenye dhambi wenye kustahili hukumu, alitutazama kwa upendo akatusamehe bure.

KUNA TABIA MBILI ZA NEEMA

1) Neema ya kawaida ambayo ni upendeleo wa Mungu kwetu.
2) Neema ambayo ni nguvu ya kuwezesha.
Matendo.4:33; wakatoa ushuhuda kwa nguvu nyingi.
Matendo. 14:26; Kwanini Neema ilikuwa mhimu kwa kanisa la mwanzo? Ilikuwa nguvu ya kuwezesha kutenda kazi.

1) PENDELEO WA MUNGU;
Ambao hatukustahili.Efes. 2:8-9; Tunaokolewa kwa neema sikwa matendo yetu.

2) NEEMA K**A NGUVU YA KUWEZESHA;

Sio tu katika wokovu tuna upendeleo tu bali pia tuna nguvu ya kutuwezesha kushinda dhambi na kubadilika! ni kwa nguvu zake.Zekali.4:6;

2korintho.5:17; hata imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya!

* Neema hii inaendelea kutembea nasisi tunapoendelea kuwa na Yesu katika maisha yetu.

Neema ya Mungu anatuwezesha kukua na kuwa na nguvu. 2Petro.3:18; inasema tukue katika Neema (nguvu ya kuwezesha)

NEEMA ILIVYOTUMIKA KUWEZESHA WATU WA MUNGU:

Nguvu ya kuwezesha(Neema)ilifunuliwa ndani ya watu katika Biblia.
Kila shujaa wa Imani alitembea na Mungu huku akijua udhaifu wake na kutokuweza kwake mwenyewe. ilikuwa kwake yeye mwenyewe kuruhusu NEEMA (nguvu ya kuwezesha) katika maisha yake ifanye kazi.

Ungeweza kuwa mtu ambaye Mungu anataka uwe. na kutimiza mpango na kusudi ambalo Mungu alikuwa nalo katika maisha yako ukitambua nguvu ya kuwezesha katika maisha yako(yaani neema)

1) NEEMA KATIKA MAISHA YA M***A
kutoka.3:11-13; 4:1-13; Misri lilikuwa Taifa kubwa la kuogopwa sana duniani
Farao mfalme alikuwa anaogopwa sana.
Mungu alipomwambia Musa kwenda kwa Farao kumwambia awaruhusu Israel. M***a aliogopa alijiona hawezi ni dhaifu na Farao katiri mwenye mamlaka bila msaada wa Mungu hawezi,

Yafuatayo ni majibu ya M***a baada ya kuambiwa na Mungu kwenda KWA Farao na haya alikuwa anamwambia Mungu.
1)Kutoka.3:11; Mimi in nani?
2)kut.3:13; Nina lako nani?
3)kut.4:1; Hawataniamini.
4)kut. 4:10; Mimi si msemaji!
5)kut. 4:13; Bwana tuma mwingine.

Maneno hayo M***a alikuwa akimwambia Mungu akikwepa kwenda kwa Farao kwa jinsi alivyokuwa anamfahamu maana alishawahi kuishi kwake!

Lakini baada ya M***a kupokea Neema ya Mungu(nguvu ya kuwezesha) alikwenda Misri na kwa Ishara na maajabu wana wa Israeli walitoka Misri.

2) NEEMA KATIKA MAISHA YA GIDIONI.
Waamuzi.6:1-24; Mungu alitaka Gidioni awakomboe Israel toka utawaka wa kijeshi wa Midiani.

Israeli walifahamu kushindwa tu kwa miaka mingi hivyo ilimpa Gidioni wasiwasi mwingi na kutojiamini!
Alijiona hawezi na hakuamini. Ukisoma mstari wa.13 utaona anaonyesha wasiwasi wake!
Bwana alimtia moyo lakini bado haamini mstari, 15;

Lakini NEEMA YA MUNGU (nguvu ya kuwezesha) Gidioni baada kuipata aliweza kuwaokoa Israeli akiwa na watu wachache tu.

3) MAISHA YA PAULO
Mdo.15:40; kabla Paulo na Sira hawajaondoka kanisa la Antiokia liliomba kwa ajili yao wapewe Neema ya Bwana
Kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele yao.

Paulo 2Kor.11:22-33; alikuwa na Neema ya Mungu katika maisha ya kumwezesha kuishi. 2kor.12:9;

4) PIA KATIKA MAISHA YETU TUNAPEWA NEEMA.
Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na mambo mengi ya kukatisha tamaa.
Mwitikio wa Mungu kwetu ni kuleta nguvu ya kushinda(Neema)

Tuamini kile Neno la Mungu linasema.
Unaweza kuzuia NEEMA kufanya kazi kwako kwa kutokuamini kwako!
Amini omba Neema utamwona Mungu akitokea upande wako:

KUNA AHADI AMBAZO MUNGU AMETUPA

1) Tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa Neema. Ebrania.4:16; Tukikaribie kiti cha Neema kwa ujasiri ili tupate Neema(nguvu)ya kutuwezesha wakati wa nahitaji

Tunapaswa kuyatambua haya ili tusogee kwenye Neema ilikupata nguvu ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

2) Mungu anaweza kuwajaza kila Neema kwa wingi(yaani nguvu kwa wingi) ili tuwe na riziki nyingi Sikh zote.2korintho.9:8; Na kuzidi katika matendo mema.

Mungu anaweza kutupa NEEMA kwa wingi tuombe sasa ili tupewe.
Omba Mungu atakupa NEEMA zaidi kwa ajili ya Mahitaji yako;

Mungu akubariki

Address

Moshi
Moshi

Telephone

+255755356048

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Apostolic Ministry Tanzania AMT posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share