05/03/2024
NYAKATI ZA KUJILIWA KWETU!!!
Maneno haya si mapya masikioni na machoni pa wengi.
Mnapoona vita na majanga yanayo endelea! mnadhani tupo nyakati gani?
Mnapoona Upendo kwa ndugu umepoa! mnadhani tupo nyakati gani?
Mnapoona Wanandoa wana chinjana na kutalakiana! mnadhani tupo nyakati gani?
Mnapoona viongozi wa dini wana bariki ushoga na usagaji! mnadhani tupo nyakati gani?
Usiku na mchana kupishana kwa kasi ya ajabu (Siku kuisha haraka)! mnadhani tupo nyakati gani?
Mnapoona wanatengenezwa watu feki )ROBOTI) tuishi nao! mnadhani tupo nyakati gani?
Mnapoona watu wanafunga ndoa na wanyama! mnadhani tupo nyakati gani?
Shetani amedanganya watu wasimwabudu Mungu wao! wakisikia injili waone upuuzi na ushamba!!
Watu kukosa imani na Mungu wao hata kuto mwabudu! mnadhani tupo nyakati gani?
Ulikua mtoto, ukawa kijana sasa unakimbilia uzee,, bado haumtaki YESU, eti hauoni wala hausikii!!....Unawaambia watu kiyama haipo wana tudanganya,, tangu utoto sasa nazeeka Yesu hajarudi.
Lakini kumbuka baada ya Kifo ni hukumu,,hivyo mtu akifa hakuna kusamehewa tena makosa aliyotedha duniani nyakati za uhai wake hata akiombewaje...
Najua una uhakika wa kifo na kaburi, maana wengi uliowapoenda walikufa muda!! nawe huijui kesho yako, muda wowote unaweza kufa watu wakakusahau...
Sasa kwa nini kusubiri kiyama wakati baada ya kifo ni hukumu?
AU UNAJITOA AKILI KUJIFANYA HUONI, HUSIKII??
Dunia k**a gari,, haina dereva, brake zimeng'olewa, matairi yamepasuka kwenye mteremko mkali,, Abiria (binadamu) wapo bize na mambo yao hata hawajali!!!
SHETANI YUPO SERIOUS KUPOTEZA WATU!!
MUNGU YUPO SERIOUS KUOKOA WALIO TAYARI KUOKOLEWA!!
YESU ANAKUJA UPESI! DUNIA INAUELEKEA MWISHO KWA KASI,,, USIJITOE AKILI.
DALILI ZOTE UNAZIONA LAKINI UNALETA MZAHA.
K**A KUFA NI LAZIMA, VIVO HIVYO KUMTUMAINI MUNGU NA KUMWABUDU UNGALI HAI NI LAZIMA.
JEHANUM INAKOLEZWA MOTO TAYARI KWA WENYE DHAMBI.