Ufufuo na Uzima Church Morogoro

Ufufuo na Uzima Church Morogoro Ufufuo na Uzima Morogoro The Ufufuo na Uzima-Morogoro Province Mega Church is under the leadership of Dr. Godson Zacharia (also a Bishop and Senior Pastor).

Pastor Godson has trained several church leaders who are now serving our Lord Jesus Christ diligently. Ufufuo na Uzima-Morogoro is fully operational at 22 Mega Division Churches including Dumila, Tuliani, Mvua, Gairo, Kilosa, Kilombero, Ifakara, Mahenge (Ulanga), Mbingu, Kingolwira, Sokoine Mvomero, Lupilo, Chakwale & Dakawa under anointed Senior Pastors.

Matendo ya Mitume 18:8"Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi walipo...
07/09/2026

Matendo ya Mitume 18:8

"Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa".

SOMO: KUBATIZWA KIBIBLIA NA KUITIMIZA HAKI YOTE                                          UFUFUO NA UZIMA MOROGOROBY BISH...
06/09/2026

SOMO: KUBATIZWA KIBIBLIA NA KUITIMIZA HAKI YOTE
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
BY BISHOP PROF. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI SEPTEMBA 6, 2026

Neno ubatizo linatokana na neno la kiyunani “Baptiso” lenye maana ya “kuzamisha”. Hivyo basi ili mtu abatizwe lazima azamishwe kwenye maji, huu ndio ubatizo wa Kibiblia. Yesu mwenyewe ambaye ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yetu alibatizwa kwa kuzamishwa kwenye maji na Yohana mbatizaji.

Kumekuwa na mafundisho mengi potofu kuhusu ubatizo lakini ukweli ni kwamba ubatizo wa Kibiblia unafanyika kwenye maji mengi ambapo mtu huzamishwa. Watoto wadogo hawawezi kubatizwa kwa sababu hawana uelewa wa neno la Mungu, watoto wadogo wanabarikiwa au kuwekwa wakfu.

Ubatizo wa Biblia

“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.
Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali”.(Mathayo 3:13-15)

Bwana Yesu alikwenda mto Yordani kwenye maji mengi ambapo Yohana alikuwa anawabatiza watu. Yohana alitaka kumzuia lakini Yesu alimwambia anataka abatizwe ili aitimize haki yote. K**a Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alikubali kubatizwa ubatizo wa maji mengi ili aitimize haki yote, mimi na wewe ni nani hata tupinge ubatizo wa maji mengi?

Wapo watu wanasema k**a mnataka kubatizwa k**a Yesu na nyie muende Yordani. Huu ni upotoshaji na ukosefu wa maarifa. Ubatizo wa Kibiblia ili utimie si lazima kwenda mto Yordani bali lazima maji mengi yawepo ya kumfanya mtu kuzama.

Hatua za Ubatizo wa Biblia

(i)Kuamini

Kabla ya mtu hajabatizwa anatakiwa kuamini; sio kumuamini mke/mume wake, mjomba, shangazi, bibi, babu, mchungaji, paroko, askofu, nabii, mtume bali aliamini neno la Mungu. Kuna watu walibatizwa walipokuwa watoto wadogo halafu wakaamini baadaye walipokuwa wakubwa jambo ambalo si sahihi. Unatakiwa uamini kwanza halafu ubatizo ufuate kwa sababu huwezi kuvaa suti kabla hujavaa nepi.

“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”(Warumi 10:17)

Krispo alikuwa kiongozi mkubwa wa Kanisa lakini jambo la ajabu alikuwa bado hajamuamini Yesu. Baada ya kulisikia neno la Mungu aliamini, alitubu na akabatizwa.

“Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa".(Matendo 18:8)

(ii)Lazima kuwe na maji tele
“Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa”.(Yohana 3:23)

Yohana alikwenda kubatiza Ainoni kwa sababu kulikuwa na maji tele. K**a Yohana ambaye ndiye mbatizaji mkuu alikuwa anawabatiza watu kwenye maji mengi tunatakiwa kujiuliza huu ubatizo wa kumpaka mtu maji kichwani umetoka wapi?

“Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe”?(Matendo 8:26-35-36)

Towashi alipoyaona maji mengi alimuomba Filipo ambatize kwa sababu alijua ili ubatizwe kwa usahihi sharti maji mengi yawepo. K**a ulibatizwa kwenye kikombe leo ufahamu ukweli huu na ubatizwe Kibiblia.

(iii)Kutubu dhambi
Kutubu dhambi maana yake ni kuacha uasi, kuacha matendo mabaya na kumuamini Mungu.Baada ya kuamini unatakiwa kutubu dhambi zako halafu ubatizo ufuate.Mtu anayetubu dhambi zake huwa anapata leseni ya kubatizwa. Yesu anasema makahaba na watoza ushuru watawatangulia kuingia mbinguni kwa sababu mtu yeyote anayetubu Mungu humsamehe.

Shetani hapendi kuona mtu anatubu ili aendelee kummiliki ndiyo maana unaweza kumuona kiongozi mkubwa wa serikali amelitia taifa hasara kubwa lakini hawezi kujitokeza hadharani na kuomba radhi. Leo tubu dhambi zako, msamehe aliyekukosea kabla hujaenda kubatizwa kinyume na hivyo utapoteza muda.

“Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.(Matendo 2:37-38)

Watu wale walipolisikia neno la Mungu lililohubiriwa na Petro walichomwa mioyo yao na walitubu dhambi zao kabla hawajabatizwa.

(iv).Fanya haraka ukabatizwe
Baada ya kulisikia neno la Mungu halafu ukaamini na kutubu unatakiwa kufanya haraka kubatizwa bila kumuuliza shangazi yako, mjomba, dada, kaka, bibi, babu kwa sababu kila mtu atabeba furushi lake mwenyewe.

Kumbuka kwamba ubatizo wa Kibiblia haufanyiki kwa watoto wadogo kwa sababu hawawezi kuisikia injili hivyo hawawezi kuamini. Yesu mwenyewe wakati anafanya huduma hakuwahi kuwabatiza watoto wadogo bali aliwabariki.

“Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto k**a hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu k**a mtoto mdogo hatauingia kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia”.(Marko 10:13-15)

Faida za Ubatizo

(i)Kuwa mwana wa utii
Unapokubali kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na kubatizwa kibiblia unakuwa mwana wa utii, mtoto anayefuata maelekezo ya wazazi. Kinyume na hivyo utahesabika kuwa mwana wa uasi.

“nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi” (Waefeso 2:1-2)

(ii)Kuonyesha umekufa na Kristo na umefufuka na Kristo
“Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi k**a Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima”.(Warumi 6:4)

Unapobatizwa kibiblia unathibitisha kuwa ulizikwa na Kristo na ulifufuka naye. Hivyo ubatizo huu ni jambo la msingi sana kwenye maisha yako.

(iii)Kusamehewa dhambi
(iv)Kufutwa kwa hati ya mashtaka

Je, Mtu Anaweza Kubatizwa Zaidi ya Mara Moja?

Unaweza kubatizwa mara ya pili ulipobatizwa mara ya kwanza ulibatizwa bila kuzamishwa kwenye maji mengi au ulibatizwa ulipokuwa mtoto.

Je Lazima Kubadili Jina Baada ya Kubatizwa?
Jina la mtu ndio mtu mwenyewe!unapobatizwa si lazima ubadili jina lakini k**a jina lako halina maana nzuri na limekuwa chanzo cha matatizo yako nakushauri badilisha baada ya kubatizwa. Mfano unaitwa Matatizo, Majuto, Tabu haya si majina mazuri kwa mustakabali wa maisha yako, vizuri ubadili jina hilo.

MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
FIKA KANISANI, UFUFUO NA UZIMA
MKUNDI MWISHO -MOROGORO
AU WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Ufufuo na Uzima Church Morogoro
Follow us on INSTAGRAM: Ufufuo na Uzima Church Morogoro
Follow us on YOUTUBE: Ufufuo na Uzima Church Morogoro
Email:Ufufuo na Uzima Church [email protected]
TEL: 0719 798 778/0757 550878

🔥 IBADA KUBWA YA JUMAPILI — USIKOSE! 🔥“Ungana nasi” katika ibada hii ya Sifa, Kuabudu, kusikia Neno la Mungu na Maombi🔥📅...
05/09/2026

🔥 IBADA KUBWA YA JUMAPILI — USIKOSE! 🔥

“Ungana nasi” katika ibada hii ya Sifa, Kuabudu, kusikia Neno la Mungu na Maombi🔥

📅 JUMAPILI, 6 SEPTEMBA 2026
⏰ SAA 02:00 ASUBUHI
📍 MKUNDI MWISHO, MOROGORO
🎙️ BISHOP GODSON ZACHARIA

🙌 Njoo na familia yako, rafiki yako na wapendwa wako.

🔥 Njoo kwa matarajio.
🙏 Njoo na hitaji lako.
❤️ Njoo kumwabudu Mungu.



27:25

03/09/2026

```Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.```

📖*ZABURI 91:10*📖

📚 KABLA HUJAZALIWA ULIKUWEPO
🔊 Askofu Dr. Josephat Gwajima
🗓️ 03 September 2026

KARIBU KATIKA MWEZI WA SEPTEMBA!JIANDAE KUUONA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA UKAMILIFU WAKE. ✨🔥Tunauingia mwezi huu kwa imani,...
01/09/2026

KARIBU KATIKA MWEZI WA SEPTEMBA!

JIANDAE KUUONA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA UKAMILIFU WAKE. ✨🔥

Tunauingia mwezi huu kwa imani, matarajio na moyo wa kumtegemea Mungu. Tunaamini Septemba itakuwa mwezi wa kuona mkono wa Mungu, neema yake na utukufu wake ukidhihirika katika maisha yetu.

WELCOME TO THE MONTH OF SEPTEMBER!
GET READY TO SEE GOD’S GLORY IN ITS FULLNESS. 🙏✨

🔥 IBADA YA MATENDO MAKUU! 🔥Leo ni siku ya kukutana na Mungu katika uwepo wake, nguvu zake na matendo yake makuu. 🙌🏽✨Usik...
31/08/2026

🔥 IBADA YA MATENDO MAKUU! 🔥

Leo ni siku ya kukutana na Mungu katika uwepo wake, nguvu zake na matendo yake makuu. 🙌🏽✨

Usikubali Jumatatu ipite bila kushiriki ibada hii yenye neema na utukufu wa Mungu.

📅 Jumatatu, 31 Agosti 2026
⏰ Saa 10:00 Jioni (04:00 PM)
📍 Mkundi Mwisho – Minara Mitatu
🎤 Bishop Prof. Godson Zacharia
Njoo ukiamini, ondoka ukiwa na ushuhuda! 🔥

🕊️ Mungu bado anatenda Matendo Makuu!

📸 MATUKIO KATIKA PICHA | IBADA YA THE JOYFUL SUNDAY AUGUST 30,2026🙏🔥Kila picha ni ushuhuda, kila tabasamu ni furaha, na ...
30/08/2026

📸 MATUKIO KATIKA PICHA | IBADA YA THE JOYFUL SUNDAY AUGUST 30,2026🙏🔥

Kila picha ni ushuhuda, kila tabasamu ni furaha, na kila hatua ni kumbukumbu ya Mungu ambaye hajawahi kutuacha. 🔥
🙏 “Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.” — Zaburi 107:1



🔥 USIPANGE KUKOSA THE JOYFUL SUNDAY! 🔥Jumapili hii ni siku ya furaha, amani na urejesho katika uwepo wa Mungu. 🕊️✨Mungu ...
29/08/2026

🔥 USIPANGE KUKOSA THE JOYFUL SUNDAY! 🔥

Jumapili hii ni siku ya furaha, amani na urejesho katika uwepo wa Mungu. 🕊️✨

Mungu anakwenda kubadilisha ghadhabu kuwa furaha, huzuni kuwa shangwe, na machozi kuwa ushuhuda! 🙌🔥

🗓 Tarehe: 30 Agosti 2026
⏰ Muda: Saa 2:00 Asubuhi (08:00 AM)
📍 Mahali: Ufufuo na Uzima Morogoro — Mkundi Mwisho, Minara Mitatu
🎙️ Bishop Prof. Godson Zacharia

❤️ Njoo na moyo wa kutarajia. Mungu ana jambo jipya kwa ajili yako!



KUONDOA VIFUNIKO VYA KICHAWIUFUFUO NA UZIMA MOROGOROBY PROF. GODSON ISSA ZACHARIAJUMAPILI   AGOSTI 23, 2026Kifuniko ni k...
23/08/2026

KUONDOA VIFUNIKO VYA KICHAWI
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
BY PROF. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI AGOSTI 23, 2026

Kifuniko ni kitu kinachowekwa juu ya kitu kingine ili kukifunika, kukilinda, kukificha au kukizuia kisionekane. Kifuniko cha kichawi ni kifuniko kinachofanya kazi ya kumzuia mtu asionekane, asifanikiwe au asitambulike katika jambo fulani.

Kifuniko cha kichawi huwezi kukiona kwa macho ya nyama lakini kinaweza kufunika biashara yako ukakosa wateja, vyeti vyako ukakosa kazi, tumbo la uzazi ukakosa watoto, uso wako ukakosa mke/mume.

Vifuniko vya Kichawi

Vifuniko vya kichawi ni mapepo/mashetani kutoka kuzimu ambayo wachawi huyatuma kwa mtu na kujigeuza kuwa kifuniko kwenye maisha yake. Mapepo/mashetani haya yakimwingia mtu yanageuka kuwa kifuniko kwenye kazi, ndoa, biashara, n.k.
Shetani anauwezo wa kufunika tangu zamani, anaweza kufunika tumbo usizae, kufunika akili ukachanganyikiwa. Shetani hapo mwanzo hakuwa Shetani, alikuwa ni malaika mzuri, kerubi afunikaye lakini akamwasi Mungu, ndipo akaamua kumfukuza atoke mbinguni.

“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” (Ufunuo 12:7-9)

Kufunikwa ni k**a vile kupaka make up; unaweza kuona mtu ni mweusi lakini katika siku yake ya harusi anapakwa make up anabadilika kabisa. Amefunikwa ukimuona k**a hana chunusi vile sasa subiri aoge utashangaa!


Mungu alimuweka shetani kuwa malaika kwa kufunika mbingu kwa utukufu. Shetani akajiinua kwa kiburi mwisho akafukizwa atoke mbinguni. Kinachoharibu watu wengi ni urembo na uzuri unaofanya watu wawe na kiburi.

“Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, k**a kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.” (Ezekiel 28:16)

Shetani hawezi kufanya kazi bila kuungana na waganga na wachawi; kule mbinguni alikuwa anafunika kwa uzuri lakini alipokuja duniani akaanza kufunika kwa ubaya ili watu waharibikiwe. Unashangaa mtu anakuwa kanisani, ni muombaji ni Mchungaji kabisa anafunikwa kisha anahama kanisa na anaanza kusema vibaya huduma iliyomjenga.


“Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga”(Hesabu 22:6)


Mfalme wa Moabu baada ya kuona amezungukwa na Wana wa Israeli akaamua kumfuata mchawi ambaye alikuwa anaitwa Baalamu iili amsaidie kumlaania(kuwafunika) wana wa Israeli kwa kuwa walikuwa na nguvu ya kumshinda.

Kuna wafanyabiashara wenzako wakiona unauza kuliko wao wanakwenda kwa waganga kukufunika, kazini wakiona una bidii na utapandishwa cheo wanakufunika.

Matokeo ya Kufunikwa Kichawi

1. Kuonekana tofauti
Mchawi anaweza kukufunika na ukaonekana tofauti. Unaweza ukawa ni binti mzuri ukawa huolewi kumbe wanaume wakikuangalia wanakuona k**a bibi wa miaka sabini.

2. Kutoonekana
Unaweza ukawa una juhudi kazini lakini hupandishwi cheo, duka lako ni zuri lakini wateja hawaji, hapo ujue ushafunikwa ili uonekane tofauti.

3. Kutendewa tofauti na stahiki zako
Shetani anaweza kumfunika mtu na akakosa stahiki zake; umesoma hadi Phd lakini unalipwa mshahara wa Certificate.

4. Kufika mahali usipopaswa kufika

Ukifunikwa na kifuniko cha kichawi, unaweza kuhamishwa na kupelekwa sehemu ambayo hupaswi kufika. Unaweza kufunikwa unageuka kuwa omba omba. Kufunikwa kunamfanya mtu kuondolewa heshima yake, akiingia mtaani wanamwangalia wanacheka, Watoto wanamwangalia wanacheka.

MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
FIKA KANISANI, UFUFUO NA UZIMA
MKUNDI MWISHO -MOROGORO
AU WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Ufufuo na Uzima Church Morogoro
Follow us on INSTAGRAM: Ufufuo na Uzima Church Morogoro
Follow us on YOUTUBE: Ufufuo na Uzima Church Morogoro
Email:Ufufuo na Uzima Chuch [email protected]
TEL: 0719 798 778/0757 550878

🔥🔥 KESHO NI SIKU YA KUKUTANA NA NGUVU ZA MUNGU! 🔥🔥Je, uko tayari kukutana na Nguvu za Mungu? 🙌Kesho tutakutana kumwabudu...
22/08/2026

🔥🔥 KESHO NI SIKU YA KUKUTANA NA NGUVU ZA MUNGU! 🔥🔥

Je, uko tayari kukutana na Nguvu za Mungu? 🙌

Kesho tutakutana kumwabudu Mungu, kusikia Neno lake, kuomba na kupokea nguvu mpya kwa ajili ya safari ya maisha. 🔥🙏

📖 Yohana 1:39
"Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona."

Usikose! Njoo uone kile Mungu atakachokutendea. 🙌🔥

📅 JUMAPILI, AGOSTI 23, 2026
📍 MKUNDI MWISHO
⏰ SAA 02:00 ASUBUHI

Address

Ufufuo Na Uzima Mkundi Minara Mitatu, P. O. Box 4092
Morogoro
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufufuo na Uzima Church Morogoro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ufufuo na Uzima Church Morogoro:

Shortcuts

Share