Efatha Church Morogoro

Efatha Church Morogoro KARIBU KANISA LA EFATHA MOROGORO. Marko 7:34
"Akatazama mbinguni, akaugua, akamwambia, EFATHA, maana yake, Funguka."

☎️ 0787432654 I 0743672904

WORD OF THE DAY PASTOR ALLAN W. MLAKITOPIC: HOW DO YOU RECEIVE THE JOY OF THE LORD?The joy of the Lord is obtained throu...
04/09/2026

WORD OF THE DAY
PASTOR ALLAN W. MLAKI

TOPIC: HOW DO YOU RECEIVE THE JOY OF THE LORD?

The joy of the Lord is obtained through the following:
1. Reading and understanding the Word of God and making it part of your life. You begin to form the joy of the Lord within you. Joy slowly takes shape as you live the Word, because the Word makes you light, and you begin to feel joy.

2. Knowing that God is with you, being fully assured that God is with you at all times, in every matter and in every situation, then the joy of the Lord abides with you. (1 Kings 20:1–6)

3. Knowing that you are forgiven by God. The joy of the Lord will be with you. Anyone who is forgiven is free and has peace and joy in their heart. (Luke 7:48; Isaiah 38:1–8)

4. Knowing that despite the challenges and hardships you go through, God has not abandoned you, but is helping you and giving you victory, this brings the joy of the Lord.

5. When a person reaches a place of recognizing where they came from, where they are, and where they are going, the joy of the Lord begins to form within them, because in reflecting on God’s greatness there is the joy of the Lord.

6. Understanding the purpose of creation. Anyone who understands the purpose for which they were created forms the joy of the Lord within them, because the joy of the Lord is attached to purpose.

IMPORTANT

Removing ignorance is one of the things that leads to the joy of the Lord.
• Not reading the Word is a form of ignorance.
• Ignoring instructions given at the altar is also a form of ignorance.

NENO LA SIKU MCHUNGAJI ALLAN W. MLAKISOMO: UNAIPATAJE FURAHA YA BWANA?Furaha ya Bwana inapatikana kupitia mambo haya:-1....
04/09/2026

NENO LA SIKU
MCHUNGAJI ALLAN W. MLAKI

SOMO: UNAIPATAJE FURAHA YA BWANA?

Furaha ya Bwana inapatikana kupitia mambo haya:-
1. Unaposoma Neno la Mungu na kulielewa, likawa sehemu ya maisha yako basi tayari umeanza kutengeneza Furaha ya Bwana ndani yako. Furaha inaanza kuumbika ndani yako polepole kadri unavyoliishi Neno kwakuwa Neno linakufanya kuwa nuru, unaanza kusikia furaha.

2. Unapojua Mungu yuko na wewe, ukawa na uhakika Mungu yuko pamoja nawe wakati wote, kwa jambo lolote na hali yoyote, hapo ndipo furaha ya Bwana inakuwa na wewe. (1Wafalme 20:1-6)

3. Ukijua umesamehewa na Mungu, Furaha ya Bwana inakuwa na wewe. Hii ni kawaida kabisa, Yeyote aliyesamehewa yuko huru, ana raha na furaha moyoni. (Luka 7:48; Isaya 38:1-8)

4. Unapojua kwamba pamoja na changamoto unazopitia, magumu unayopitia bado Mungu hajakuacha, anakusaidia na kukushindia, unapata furaha ya Bwana.

5. Mtu anapofikia mahali pa kutambua ametoka wapi, yuko wapi na anaenda wapi basi furaha ya Bwana inaanza kuumbika ndani yake, maana katika kutafakari ukuu wa Mungu kuna furaha ya Bwana.

6. Unapoanza kuelewa Kusudi la Kuumbwa: Mtu yeyote anayeelewa kusudi la kuumbwa kwake, Furaha ya Bwana inaumbika ndani yake, kwasababu ndani ya kusudi kumeambatanishwa Furaha ya Bwana.

MUHIMU:
Kuondokana na ujinga ni moja ya kitu kinachopelekea Furaha ya Bwana.
=)Kutokusoma Neno ni mojawapo ya ujinga.
=)Kupuuza Maagizo yanayotolewa madhabahuni ni mojawapo ya ujinga.

NAIBARIKI IJUMAA YANGU. Nafurahi katika BWANA, maana BWANA wa Mabwana, NENO yuko ndani yangu, na Mimi ndani Yake; maadui...
04/09/2026

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.

Nafurahi katika BWANA, maana BWANA wa Mabwana, NENO yuko ndani yangu, na Mimi ndani Yake; maadui zangu wote wapo chini ya Miguu yangu, hakuna cha kunishinda. Mimi ni Mshindi.

Asante YESU

03/09/2026

KUSANYIKO LA MWAKA HUU NI LA TOFAUTI KABISA!

Kusanyiko la mwaka huu ni la kipekee, kwa sababu litahusika na ukombozi katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu:

Ukombozi katika ndoa zetu
Ukombozi katika biashara zetu
Ukombozi katika vipato vyetu
Ukombozi katika ibada zetu
Ukombozi katika familia zetu na kizazi chetu
Na zaidi, ukombozi wa ndugu na jamaa zetu ambao bado hawajaingia na kusikia habari ya umilele.

Hili si kusanyiko la kawaida. Ni wakati wa Mungu kuleta ukombozi na kurejesha kile kilichopotea.

Usikose Kusanyiko la Mwaka 2026! Mwalike ndugu, rafiki na jamaa yako.

Mapenzi ya Mungu, Ukombozi wangu!



WORD OF THE DAYMINISTER EDNA W. MLAKITOPIC: HOW TO PUT INSTRUCTIONS INTO PRACTICE📖Joshua 1:8–9“This Book of the Law shal...
03/09/2026

WORD OF THE DAY
MINISTER EDNA W. MLAKI

TOPIC: HOW TO PUT INSTRUCTIONS INTO PRACTICE

📖Joshua 1:8–9
“This Book of the Law shall not depart from your mouth, but you shall meditate on it day and night, so that you may be careful to do according to all that is written in it. For then you will make your way prosperous, and then you will have good success. Have I not commanded you? Be strong and courageous; do not be afraid or dismayed, for the Lord your God is with you wherever you go.”

God gives guidance on how to put His instructions into action in the Book of Joshua. He says that if you observe the instructions you are given, you will be full of joy, you will succeed, and there will be no hindrance or failure.

God explains the benefits above as follows:

▫️ This Book of the Law shall not depart from your mouth; God wants you, when you are given instructions, to speak them at all times so they are not forgotten from your lips. If you forget what you were instructed, you will do what is not required, like others who ignore the instructions they are given.

▫️ But meditate on its words day and night, When you are given instructions, you must reflect on them by thinking about them, so that your mind remembers and finds the best way to carry them out.

▫️ So that you may be careful to do according to all that is written in it, It is your responsibility to carry out the instructions exactly as directed. It is like an electronic device that comes with a manual explaining how to open and use it. When you follow those instructions, you will get good results; if you don’t, it becomes a curse to you. When you are always attentive to instructions, you will be a different person from others; and it is that difference that God delights in.

NENO LA SIKU MTUMISHI EDNA W. MLAKISOMO: NAMNA YA KUTENDEA KAZI MAAGIZO.YOSHUA 1:8-9 "KITABU HIKI CHA TORATI KISIONDOKE ...
03/09/2026

NENO LA SIKU
MTUMISHI EDNA W. MLAKI

SOMO: NAMNA YA KUTENDEA KAZI MAAGIZO.

YOSHUA 1:8-9 "KITABU HIKI CHA TORATI KISIONDOKE KINYWANI MWAKO, BALI YATAFAKARI MANENO YAKE MCHANA NA USIKU, UPATE KUANGALIA KUTENDA SAWASAWA NA MANENO YOTE YALIYOANDIKWA HUMO; MAANA NDIPO UUTAKAPOIFANIKISHA NJIA YAKO, KISHA NDIPO UTAKAPOSTAWI SANA. JE! SI MIMI NILIYEKUAMURU? UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA; USIOGOPE WALA USIFADHAIKE; KWA KUWA BWANA, MUNGU WAKO, YU PAMOJA NAWE KILA UENDAKO."

Mungu anatoa mwongozo wa kutendea kazi maelekezo yake katika KITABU cha Joshua. Anasema ukizingatia maagizo unayopewa utakuwa na furaha tele, utafanikiwa, hakuna kizuizi wala kukwama.

Mungu anaelezea faida hapo juu kuwa:

▫️Kitabu cha torati kisiondoke kinywani mwako; Mungu anataka unapopewa maagizo uyaseme wakati wote ili yasisahaulike kinywani mwako.Ukisahau ulichoagizwa utafanya isivyotakiwa k**a watu wengine wasiozingatia maelekezo wanayopewa.

▫️Bali yatafakari maneno yake mchana na usiku: Unatakiwa unapopewa maagizo uyazingatie kwa kuyawaza ili kuifanya akili yako ikumbuke na ione namna ya kutekeleza kwa ubora.

▫️Upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo: NI jukumu lako kufanya maagizo uliyopewa k**a ilivyoelekezwa. Ni k**a chombo cha kielektroniki kilicho na mwongozo unaoelekeza namna ya kufungua na kutumia. Unapofuata hayo maelekezo utapata matokeo mazuri, usipofuata ni laana kwako. Ukiwa mzingativu wa maelekezo wakati wote utakuwa mtu wa tofauti na wengine; na huo utofauti ndio Mungu anaoufurahia.

Je, unafahamu kuwa Kusanyiko la 2026 ni wakati wa upendeleo wa kimbingu kwa ajili yako?Ukombozi uliokuwa ukiutamani kwa ...
03/09/2026

Je, unafahamu kuwa Kusanyiko la 2026 ni wakati wa upendeleo wa kimbingu kwa ajili yako?

Ukombozi uliokuwa ukiutamani kwa muda mrefu, unaenda kukamilishwa katika maisha yako.

Siku saba za mabadiliko. Siku saba za ukombozi. Siku saba za kuiona nguvu ya Mungu ikitenda kazi!

🔥 KUSANYIKO LA UKOMBOZI 2026
MAPENZI YA MUNGU — UKOMBOZI WANGU!





NAIBARIKI ALHAMISI YANGU. Nafurahi katika BWANA; kwangu hakutapungua Kicheko, Furaha, Tafrija, Karamu na Utele, maana NE...
03/09/2026

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Nafurahi katika BWANA; kwangu hakutapungua Kicheko, Furaha, Tafrija, Karamu na Utele, maana NENO yuko ndani yangu. Mimi Nimebarikiwa na BWANA.

Asante YESU.

Uko tayari kwa Kusanyiko la Ukombozi 2026?Jiandae kwa jambo jipya ambalo Mungu ameliandaa kwa ajili ya maisha yako!Mwezi...
02/09/2026

Uko tayari kwa Kusanyiko la Ukombozi 2026?

Jiandae kwa jambo jipya ambalo Mungu ameliandaa kwa ajili ya maisha yako!

Mwezi wa Kumi, kwa siku saba, tunakutana katika Bonde la Kukata Maneno, Precious Centre, Kibaha.

Ni wakati wa ukombozi, urejesho na mwanzo mpya!

Usikose kuwa sehemu ya kusanyiko hili.

🔥 MAPENZI YA MUNGU — UKOMBOZI WAKO!

NENO LA SIKUNa MCHUNGAJI ALLAN MLAKI SOMO: TAMBUA MCHANGO WAKO NDANI YA KANISA.2Wakoritho 13:14" Neema ya Bwana Yesu Kri...
02/09/2026

NENO LA SIKU
Na MCHUNGAJI ALLAN MLAKI

SOMO: TAMBUA MCHANGO WAKO NDANI YA KANISA.

2Wakoritho 13:14" Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

Kila aliyeokoka anamchango katika ufalme wa Mungu. Hakuna mtu aliyekuja kwa hasara duniani bali ni kwa faida. Mfano Yakobo alileta tumaini, Yuda alikuwa ni mtu wa shekeli(fedha), Yohana alikuwa ni mtu wa upendo. Hata wewe unakitu cha kufanya ndani ya Kanisa.

Je! Wewe unajua mchango wako ni nini?

Mwana wa Mungu siku ukijua mchango wa mwingine ndipo mtakapoheshimiana. Hivyo lazima ujue mchango wako ndani ya kanisa ni upi. Kuna watu wana maneno ya hekima ya kujenga na maneno ya kubomoa hivyo lazima ujue mchango wako ni upi.

Tumechaguliwa ili kuujenga ufalme wa Mungu hivyo ufalme unajengwa, Je! Wewe unamchango gani?

Je! unautambua mchango wako. Mwana wa Mungu jitafakari una mchango gani. Maana neno linasema ubaya hauondoki kwa ubaya, bali ubaya huondoka kwa wema.
Uthamani wa mtu upo katika jinsi anavyoleta faida katika ufalme wa Mungu. Hivyo uthamani wako upo katika kuleta mtu kwa Yesu. Mfano wazazi wanaonekana wa thamani katika familia kwa sababu wanasababisha familia inastawi.

Uthamani wako unaonekana mbinguni kwa kumleta mtu kwa Yesu. Thamani yako iko katika faida. Namna unavyozaa matunda ndivyo unavyozidi kuonekana bora mbele za Mungu na kwa wanadamu pia.

Address

607
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Morogoro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church Morogoro:

Shortcuts

Share