29/01/2022
SILAHA ANAYOTUMIA SHETANI.
Na, ADAM .J. NYAMINYA...✍️
Biblia inasema
Yohana 10:10
"Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele".
Shetani ana majukumu matatu anayotekeleza Kwenye maisha ya wanadamu ili kuwapoteza wasiingie Kwenye Ufalme wa Mungu duniani na Mbinguni. Kazi hizo ni
1: Kuiba
2: Kuchinja
3: Kuharibu
👉 Shetani huiba utakatifu wa watu ili kuwaondoa katika Safari ya Kumuona Mungu.
Waebrania 12:14
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
✍️Utasikia anainua mtu, anakuambia wewe inaonekana hauna Nguvu za kiume.
✍️Unajifanya mama mchungaji sana.
✍️Una sali sana utakufa maskini wewe.
UKISIKIA KAULI HIZO UJUE shetani yupo kazini.
✍️Shetani anachinja na kuharibu maono makubwa ya watu.
Atakuletea wazo la kujiona wewe hufai kwa sababu ya hali ya maisha unayopitia.
✍️Atakuambia wewe ni mbuzi wa maskini, yaani huwezi kutimiza ndoto na maono yako kwa sababu ya changamoto unazopitia.
UKIONA HIVYO ujue tayari ameanza kuharibu na Kuchinja maono yako.
👉Atakuletea Hali ya kutojiamini
👉Atainua watu wakukatae na kukudharirisha
👉Atakuinulia maadui kila kona, Lengo kubwa ni kuiba, kuharibu na Kuchinja ndoto zako.
🗣️Na Silaha yake kubwa ni UONGO
Yohana 8:44
[44]Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
✍️Shetani kwa kupitia uongo wake, ameua, ameiba, ameharibu na Kuchinja watu kiroho na kimwili.
👉Watumishi wengi wameanguka kwa sababu ya uongo wa shetani.
👉Maono ya wengi yamekufa kwa sababu ya uongo wa shetani.
Yuda Iskariote alijikuta ameanguka Kwenye utume wake kwa sababu ya uongo wa Shetani.
Adamu na Eva wakijikuta wanafukuzwa Edeni kwa sababu ya uongo wa shetani.
Biblia inasema "Mtu huanza kujaribiwa na tamaa yake huku akivutwa na kudanganywa na shetani............".
Yakobo 1:14-15
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
😥Dhambi ndio chanzo Cha matatizo yote kwa mwanadamu, lakini shetani ndio kichocheo kikubwa kinachopelekea watu wengi washindwe kutii amri za Mungu na kujikuta wameingia Mautini.
🗣️Tuna njia moja ya kumshinda shetani, nayo ni KUMKARIBIA MUNGU
Yakobo 4:7-8
[7]Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
[8]Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
🗣️The moment mwanadamu anapoamua kuacha Dhambi na kumkaribia Mungu kwa sala na utakatifu ndipo shetani humkimbia mtu huyo Kwenye maisha yake.
We cure sin, by using Obedience antidote.
Kumbuka kuwa, Silaha ya shetani ni UONGO au Udanganyifu ambao huzaa dhambi. Na hutumia Dhambi K**a chombo Cha kumuongoza mwanadamu ili waende naye jehanamu akijua kuwa muda wake uliobakia ni mchache sana.
Ufunuo wa Yohana 12:12
[12]Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
MKARIBIE MUNGU akusaidie kuteka nyara kila wazo linalokuja kwako kinyume na injili ya KRISTO, hapo utaweza kumshinda shetani.
2 Wakorintho 10:3-5
[3]Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Be blessed 🙏
.