Kunambi Breaking News

Kunambi Breaking News Huu ni ukurasa maalumu utakaokuwa unakuletea taarifa mbalimbali zinazotokea ulimwengu mzima....

BALLON D'OR | Mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia   ni kiungo Rodri , raia wa Hispania anayekipiga klabu ya Man C...
29/10/2024

BALLON D'OR | Mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia ni kiungo Rodri , raia wa Hispania anayekipiga klabu ya Man City ya England.

Nafasi ya pili imekwenda kwa Vinicius Jr., na namba tatu ni Jude Bellingham, wote kutoka Real Madrid.

Timu bora upande wa klabu ni Real Madrid, kocha bora ni Carlo Anceloti wa Real Madrid na golikipa bora wa dunia ni yuleyule Emiliano Martinez wa Aston Villa.

Aliyechukua Ballon d'Or upande wa soka la wanawake ni Aitana Bonmati wa Barcelona.

Je, una la kusema??

πŸ‡ͺπŸ‡ΈπŸš¨ π‘π€π’πŒπˆ: BREAKING Kiungo wa Man City Rodri ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ballon D'or 2024.
28/10/2024

πŸ‡ͺπŸ‡ΈπŸš¨ π‘π€π’πŒπˆ: BREAKING Kiungo wa Man City Rodri ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ballon D'or 2024.

Msanii wa Bongo Fleva  ameamua kukomesha mjadala ambao ulikuwa ukiendelea kumhusu yeye wakimshindanisha na Msanii mkongw...
28/10/2024

Msanii wa Bongo Fleva ameamua kukomesha mjadala ambao ulikuwa ukiendelea kumhusu yeye wakimshindanisha na Msanii mkongwe kwenye muziki wa Bongo fleva ambapo amesema huo ni mjadala ambao hauna mashiko na wakijinga kuwahi kutokea.

Zuchu amefunguka kuwa Lady Jaydee ni miongoni mwa wasanii ambao amekua akiwatazama na kuvutiwa naye kwa maana ya kwamba ni dada yake ki-muziki kwa kutengeneza njia kwa ajili ya muziki huo wa Bongo fleva ambao umewapatia heshima kubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram zuchu ameandika kuwa"HUU NI MJADALA USIO NA MASHIKO NA WAKIJINGA KUWAHI KUTOKEA .LADY JAYDEE NI MOJA KATI YA ROLE MODELS WANGU NAMPA HESHIMA KUBWA SANA SABABU YEYE NI MOJA KATI MIFANO BORA SANA TULIYONAYO KWENYE TASNIA ESPECΔ°ALLY MABINTI. KUNISHINDANISHA MIMI NA DADA ZANGU WALIOTENGENEZA NJIA K**A DADA KOMANDO NI KUIVUNJIA HESHIMA TASNIA.NAKOMESHA MIJADALA HII MARA MOJA"


Mchezaji wa Real Madrid ambaye ni mmoja Kati ya wanaowania tuzo ya Ballon D’or, Vinicius Jr hatosafiri kwenda Paris kwen...
28/10/2024

Mchezaji wa Real Madrid ambaye ni mmoja Kati ya wanaowania tuzo ya Ballon D’or, Vinicius Jr hatosafiri kwenda Paris kwenye sherehe za tuzo hiyo kwa vile Real Madrid wanajua kuwa Vinicius hatoshinda tuzo hiyo.

Imeelezwa kuwa Hakuna mfanyakezi yeyote kutoka Real Madrid atakayedhuria sherehe hiyo.

Sio Florentino PΓ©rez, wala Carlo Ancelotti, hata Jude Bellingham pia hatoshiriki

Cc:

Leo ni siku ya ugawaji wa tuzo ya Ballon D'or , Kwako wewe nani anastahili kutwaa tuzo hiyo?
28/10/2024

Leo ni siku ya ugawaji wa tuzo ya Ballon D'or , Kwako wewe nani anastahili kutwaa tuzo hiyo?

Klabu ya Machester United imefikia uwamuzi wa kuachana na aliyekuwa Kocha wao Mkuu Erik ten Hag baada ya tathimini ya Uo...
28/10/2024

Klabu ya Machester United imefikia uwamuzi wa kuachana na aliyekuwa Kocha wao Mkuu Erik ten Hag baada ya tathimini ya Uongozi wa Klabu hiyo juu ya mwenendo mbovu wa matokeo

Taarifa iliyotolewa na Manchester United kwenda kwa Umma inasema kuwa:-

"Erik aliteuliwa mnamo Aprili 2022 na aliiongoza klabu kushinda vikombe viwili vya ndani, akishinda Kombe la Carabao mwaka 2023 na Kombe la FA mwaka 2024.

"Tunamshukuru Erik kwa kila kitu alichofanya wakati wa muda wake nasi na tunamtakia mafanikio katika siku za usoni. Ruud van Nistelrooy atachukua jukumu la kuwa kocha mkuu wa muda, akisaidiwa na timu ya ukocha iliyopo, wakati kocha mkuu wa kudumu anatafutwa".

🚨 π— π—–π—›π—˜π—­π—’ π—ͺ𝗔 π—¦π—œπ— π—•π—” 𝗦𝗖 π˜ƒπ˜€ π—π—žπ—§ π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” π—¨π— π—˜π—”π—›π—œπ—₯π—œπ—¦π—›π—ͺ𝗔.Mchezo uliopangwa kuwakutanisha Simba SC dhidi ya JKT Tanzania umeahir...
28/10/2024

🚨 π— π—–π—›π—˜π—­π—’ π—ͺ𝗔 π—¦π—œπ— π—•π—” 𝗦𝗖 π˜ƒπ˜€ π—π—žπ—§ π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” π—¨π— π—˜π—”π—›π—œπ—₯π—œπ—¦π—›π—ͺ𝗔.

Mchezo uliopangwa kuwakutanisha Simba SC dhidi ya JKT Tanzania umeahirishwa ikumbukwe Gari lililokuwa limebeba timu ya JKT lilipata ajali jana asubuhi wakati wakiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma na kusababisha baadhi ya wachezaji wao kuumia.

Wakati Klabu ya Simba ikisubiri kupangwa kwa tarehe mpya ya kuchezwa kwa mchezo huo kikosi hicho kitaendelea na maandalizi ya mechi inayofuata dhidi ya Mashujaa itakayopigwa Novemba Mosi

YANGA NA JKCI YATIA SAINI MKATABAHUDUMA YA AFYA NA ELIMU KWA UMMAKlabu Ya YANGA na Taasisi Ya MOYO Jakaya Kikwete ( JKCI...
28/10/2024

YANGA NA JKCI YATIA SAINI MKATABA
HUDUMA YA AFYA NA ELIMU KWA UMMA

Klabu Ya YANGA na Taasisi Ya MOYO Jakaya Kikwete ( JKCI ) Leo imetia saini Mkataba Wa Huduma Za Afya na Elimu Kwa UMMA

Akizungumza Na Waandishi wa Habari Afisa Habari Wa Klabu Ya YANGA ALLY KAMWE Amesema wataendelea Kushirikiana na Taasisi ya JKCI Ili Kuhakikisha Wanaboresha na Kutoa Elimu Kuhusu Maradhi Ya Moyo

Address

P. O. Box 1878
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kunambi Breaking News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share