samwelmmasa

samwelmmasa welcome to our page! Meet Pastor Samwel Mmasa who will teach and share word of God in this page.

Karibuu sana katika semina hii ni kuanzia kesho
20/05/2026

Karibuu sana katika semina hii ni kuanzia kesho

13/03/2026

Imani ya kweli huvuka vikwazo vyote na huleta ushindi.

19/02/2026
> * KUWA NA TARAJIO * Maisha yetu yamejengwa katika msingi wa matarajio.Unachokitarajia ndicho kinaamua utendaji wako wa...
18/12/2025

> * KUWA NA TARAJIO *

Maisha yetu yamejengwa katika msingi wa matarajio.
Unachokitarajia ndicho kinaamua utendaji wako wa kila siku,
Wengi tunaenda kazini kwasababu tunatarajia mwisho wa Mwezi kuna kitu tutapata kazini._
Tunaamua kuoa kwasababu kuna mambo tunatarajia kuyapata kwenye ndoa,
Tunaenda kanisani kwa sababu kuna mambo tunatarajia kupata kanisani,
Tunaanza biashara kwasababu kuna faida tunaitarajia kwenye biashara.
Kwahiyo kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya matarajio yako na utendaji wako wa kila siku .

Na hapo ndipo hatari inapoanzia kwani,
ukitarajia madogo utatenda kwa udogo_
na kinyume chake ukitarajia makubwa basi hata juhudi yako kwenye hili jambo inakua ya tofauti sana .

Waaamini wengi tumejikuta waanga wa kufanya mambo madogo madogo kwasababu ya kushindwa kutumia vizuri uwezo mkubwa tulionao, kuwaza mambo makubwa badala yake tumejikuta tunatarajia mambo madogo madogo .

*Kumbuka:*
_Mungu hakatai mwanzo mdogo, ila anakataa kidumu kwenye udogo. Utukufu mkubwa wa Mungu ni matokeo ya matarajio ya makubwa yaliozaa imani kubwa .
Jizoeze kutarajia mambo makubwa utende makubwa.

Warumi 4
18 : Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, k**a ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Msitari unamzungumza mzalendo wa imani katika biblia yaani baba wa imani Ibrahimu alikua na matarajio makubwa kiwango ambacho yameitwa yasioweza kutarajiwa .

Ni maombi yangu kwa Mungu ujaze mambo makubwa akili yako ambayo watu wanaokuzunguka watakushangaa yakitimia hata wewe utajishangaa yakikamilika .

Mungu akubariki sana

NALIFURAHI WALIPONIAMBIA TWENDE NYUMBANI MWA BWANA. ZABURİ 122:1NYUMBANI MWA BWANA KUNA AMANI, KUNA UZIMA, KUNA PUMZIKO,...
13/12/2025

NALIFURAHI WALIPONIAMBIA TWENDE NYUMBANI MWA BWANA. ZABURİ 122:1
NYUMBANI MWA BWANA KUNA AMANI, KUNA UZIMA, KUNA PUMZIKO, KUNA FURAHA.

TUNAPOKUTANA NYUMBANI MWA BWANA NI MAALUM KWA AJILI YA
1. KUMWABUDU MUNGU
2. KUPONYWA NA KUGUSWA NA MUNGU
3. KUUIMARISHA USHIRIKA WETU
4. KUMTOLEA MUNGU
5. KUMSIKIA MUNGU KWA NJIA YA NENO LAKE.

Usiache kwenda nyumbani Bwana siku ya kesho

Address

Shewa Street
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when samwelmmasa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to samwelmmasa:

Shortcuts

Share