EAGT SINAI Ubaruku Mbarali Mbeya

EAGT SINAI Ubaruku Mbarali Mbeya SISI WATOTO WA BABA MCHUNGAJI NA ASKOFU EMMANUEL KITUNDU . KARIBU

YESU ASIFIWE, HAPA NI MAHALI PA KUPATA MAFUNDISHO ,MAJADILIANO ,NYIMBO KUTOKA EAGT SINAI MBARALI, NA KWAYA MBALI MBALI.NA ZA KIMUNGU TU.

Watu wanaokoka karibu
20/07/2023

Watu wanaokoka karibu

Semina
16/04/2022

Semina

23/10/2021

Mganga na mchawi ni wale wale utofauti ni hatua za utendaji kazi sawa na wali ,Michele mpunga kitu kimoja isipokuwa hatua za maandalizi tu sikia hapa

Mchungaji na Askofu Kitundu mwenyeji wa mkutano akiwaombea wenye shida hapa mkutanoni
23/10/2021

Mchungaji na Askofu Kitundu mwenyeji wa mkutano akiwaombea wenye shida hapa mkutanoni

Umati huu wa watu ni hapa hapa kanisani EAGT SINAI UBARUKU WATU WAKISIKILIZA MAHIBIRI MAZURI NA YENYE KUSISIMUA NAMNA MA...
23/10/2021

Umati huu wa watu ni hapa hapa kanisani EAGT SINAI UBARUKU WATU WAKISIKILIZA MAHIBIRI MAZURI NA YENYE KUSISIMUA NAMNA MAJINI YANAVYO FANYA KAZI KWA WANADAMU , PIA MAMBO YA UGANGA NA UCHAWI SIRI ZOTE HADHARANI KARIBU USIKILIZE

WALIOMBALI TUTAWEKA MAHUBIRI HAPA MSIJALI

Mkutano mkubwa was injili ulioanza tarehe 19/10/2021 bado unaunguruma na mhubili wa Kimataifa. Mwinjilist Josephine , Ma...
23/10/2021

Mkutano mkubwa was injili ulioanza tarehe 19/10/2021 bado unaunguruma na mhubili wa Kimataifa. Mwinjilist Josephine , Mama anaye usema na kuujua uchawi nje ndani karibu Na YESU ATAKUPONYA KARIBU IBADA YA KESHO KANISANI EAGT SINAI UBARUKU

GVC CHOIR WAKITUMBWIZA KWENYE SEND OFF YA MWANA CGM NA MWIMBAJI WA KWAYA HIYOILIKUWA SHANGWE SAANA NEEMA ABDALLAH KIYEYE...
16/10/2021

GVC CHOIR WAKITUMBWIZA KWENYE SEND OFF YA MWANA CGM NA MWIMBAJI WA KWAYA HIYOILIKUWA SHANGWE SAANA NEEMA ABDALLAH KIYEYEU

16/10/2021

Morning breakfast!!!

"KELELE ZA YEZEBEL ZISIKIFANYE USAHAU UKUU WA MUNGU WAKO NA UWEZA WAKE"

1 Wafalme 19
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.

² Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, k**a roho ya mmojawapo wa hao.

³ Naye alipoona hayo, aliondoka, AKAENDA AIHIFADHI ROHO YAKE, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.

Bwana Yesu asifiwe kanisa la Mungu ALIYE HAI..

USIKU huu nilipokuwa nasoma ANDIKO hili ndani yangu kukaumbika ujasiri ambao umenifanya niandike ujumbe huu Yamkini Kuna mtu Mungu amekusudia kumvusha nao..

Mara nyingi adui akiona umempiga Mahali panapo uma huwa hakati tamaa huwa harudi nyuma Kwa haraka Bali hutafuta mbinu ya kukudhoofisha na Moja ya Mbinu hutangaza vita na wewe Kwa NGUVU zaidi ya Ile ya Mwanzo atakupiga mikwala ambayo UKISIKIA moyo wako unaweza kuingiwa na hofu kubwa sana kiasi Cha kusahau UKUU WA MUNGU WAKO NA MATENDO MAKUU ALIYO KUTENDEA..

ELIYA MUNGU ALIMTENDEA MAMBO MAKUU MENGI KUPITIA KWA ELIYA MUNGU ALIFANYA ISHARA NA MIUJIZA MINGI SANA NA HATA AKAMTOKEA NA KULAMBA SADAKA MBELE YA MANABII WA BAALI 450 NA AKAFANIKIWA KUWAUA WOTE LAKINI NENO LA MWANAMKE YEZEBELI LILIMFANYA AKIMBIE AKAHIFADHI ROHO YAKE ...YAANI AKASAHAU MUNGU ALIYEJITUKUZA KWA MOTO MBELE YA MAADUI ZAKE MPAKA HUYU MUNGU BAALI ALISHINDWA KUTOKEA KWA KUMWOGOPA HUYU MUNGU WA ELIYA ETI SASA ANAMWOGOPA MWANAMKE YEZEBEL KWA KUITEGEMEA miungu YAKE AKASAHAU KABISA MAMLAKA YA UUNGU ALIYO NAYO AKAKIMBIA...

Nataka kusema Kuna wakati adui huinua vita...hupiga kelele ...hutoa vitisho ili tuogope na kuwakimbia na wakati mwingine vitisho vyao hufanya usahau hata namna Mungu alivyokutetea Jana na juzi dawa yao siku kuogopa Bali ni KUKUMBUKA UKUU WA MUNGU NA UWEZA WAKE ..ALIVYOKUTENDEA JANA NA JUZI HATA LEO ANAWEZA KUTENDA TENA MUNGU WETU HABADILIKI...HACHUJI...HAPUNGUI THAMANI...HAYEYUKI...NI MUNGU MKUU NA MWENYE UWEZO ..HATA SHETANI AJITUTUMUE NAMNA GANI AKUNA MBWEMBWE MPYA INAYOWEZA MFANYA MUNGU ASHINDWE KUTUTETEA

Nampenda DAUDI Maana alipoenda kupigana na Goliath alijaribu kupiga mbwembwe K**a hizi za Yezebeli akitegemea miungu yake na akadhani DAUDI ataogopa na kukimbia *DAUDI ALIJUA UWEZO WA MUNGU NA NGUVU ZAKE HAKUSAHAU MUNGU ALIVYO MSAIDIA KUUA SIMBA NA DUBU...HAKUSAHAU KUWA MUNGU HUYO HUYO ANAWEZA MSAIDIA HATA KUMPIGA NA HUYU MFILISTI ...👇👇👇

1 Samweli 17
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
*⁴⁵ Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.*

⁴⁶ Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

Haya maneno ni maneno ya kishujaa Sana ambayo mtu akisikia lazima aingiwe na hofu..

Mpendwa Nini kinakufanya uogope? Nini kinakufanya urudi nyuma..uahirishe Mpaka mipango yako na maono yako? Kweli umeamua kumkimbia YEZEBEL wako umesahau UKUU WA MUNGU WAKO? ...ni kweli unataka kukimbia changamoto za ndoa yako Kwa sababu ya sauti za makahaba? Ni kweli unataka kufunga duka kwa sababu ya Yezebeli aliyetangaza vita na wewe? Unataka kuacha masomo,kuacha kazi,kuacha huduma kisa tangazo la Yezebeli ... UMESAHAU USHINDI AMBAO MUNGU ALIKUPA KWENYE LILE PITO LAKO ? UMESAHAU ALIVYOKUPONYA UGONJWA WAKO?

"JIPIGE KIFUA JIAMBIE HAKIMBII MTU HAPA"💪💪💪💪 YULE MUNGU ALIYETENDA JANA ATATENDA NA LEO HAJAWAHI KUSHINDWA KELELE ZA YEZEBELI HAZITAKUTOA MAHALI MUNGU AMEKUWEKA ILA UKUU WA MUNGU UTAMWONDOA YEZEBEL NA WAPAMBE WAKE

Ukisoma maandika utaona Huyo Yezebeli aliyekimbiwa na Eliya aliishia kuliwa na Mbwa tu wala maiti yake haikuzikwa..👇👇👇

“Na mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli, wala hapatakuwa na mtu wa kumzika. Akaufungua mlango, akakimbia.”
2 Wafalme 9:10

USIOGOPE MIKWALA ADUI ZAKO NA TAMBO ZAO NA KELELE ZAO AISEE MUNGU WAKO ANAO UWEZO WA HAO ADUI ZAKO KUWAFANYA CHAKULA CHA MBWA K**A AMBAVYO YEZEBEL NA UBABE WAKE WOTE NA MIKWALA YAKE YOTE ALIISHIA KULIWA NA MBWA💪💪💪💪

Nawatakia siku njema damu ya YESU iwalinde ..

Na Mwl Gordian Newton..

Hongera Mr &Mrs Pascal J. Mayila kwa kufunga pingu za maisha hapa Sinai Ubaruku
18/07/2021

Hongera Mr &Mrs Pascal J. Mayila kwa kufunga pingu za maisha hapa Sinai Ubaruku

Semina, Semina mnakaribishwa wote imeandaliwa na CGM
05/06/2021

Semina, Semina mnakaribishwa wote imeandaliwa na CGM

KARIBUNI KATIKA IBADA YA KESHO JUMAPILI ITAKUWA IBADA YA BARAKA YENYE KUKUACHA HURUBY CGM
22/05/2021

KARIBUNI KATIKA IBADA YA KESHO JUMAPILI ITAKUWA IBADA YA BARAKA YENYE KUKUACHA HURU
BY CGM

Address

UBARUKU EAGT KANISANI
Mbeya

Telephone

+255764712981

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EAGT SINAI Ubaruku Mbarali Mbeya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to EAGT SINAI Ubaruku Mbarali Mbeya:

Share