09/09/2022
.
KITABU: *KISA CHA UKOMBOZI (The story of Redemption)*
SURA YA 45.
*SIRI YA KUASI*
_Mtume Paulo, katika barua yake ya pili kwa Wathesalonike,alitabiri ukengeufu mkuu ambao mwishowe ungetokea utawala wa Kanisala Kirumi. Alisema dhahiri ya kwamba siku ya Kristo haitakuja“usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi,mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu yakila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe huketikatika hekalu la Mungu, akijionyesha nafai yake kana kwambayeye ndiye Mungu.” Zaidi ya haya, natume awaonya ndugu zake yakwamba ile “siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 The 2:3” 4, 7. Hata zamani zile aliona makosa yakiingia polepole kanisani ambayo yangetengeneza njia ya kukuza utawala wa Kanisa la Kirumi. Polepole kwa hila, ile siri ya kuasi iliendeleza kazi yake ya udanganyifu na kumtukana Mungu; lakini kwakadiri ilivyozidisha nguvu na kuzitawala nia za watu, hivyo ndivyo alivyozidi kufanya kazi yake kwa wazi. Punde kwa punde, kwa kadiri isiyoonekana, madhehebu yamakafiri yaliingizwa katika kanisa la Kikristo. Kwa muda fulani ile nia ya kufanya mapatano na kuyaingiza madhehebu yamakafiri ndani ya kanisa ilizuiliwa kwa sababu ya mateso makaliambayo kanisa lilipata chini ya utawala wa upagani Lakini matesoyalipokoma, tena dini ya Kikristo ilipokaribishwa hata kwa majumba ya wafalme, kanisa lilianza kupunguza hali yake ya kufafanana Kristo na mitume kwa unyenyekevu na unyofu, wakaanza kufanya fahari na kiburi sawa na mahaini na watawala wa dini yakipagani; na badala ya matakwa ya Mungu, kanisa liliweka mafundisho na maelezo ya kibinadamu. Kulikuwa na shangwe kuu Konstantine alipoongoka mnamo mwanzo wa karne ya nne baadaya Kristo; lakini kuongoka kwake kulikuwa kwa jina tu; ndipomambo na matendo ya kidunia yakaingia kanisani yakawa k**a yakifunikwa na kuhalalishwa na haki ya kanisa. Halafu kazi ya uhalifu ikaendelea upesi. Dini ya upagani ijapokuwa ilionekana kana kwamba imeshindwa, ilikuwa ikishinda. Roho yake ndiyoiliyotawala kanisani. Madhehebu yake, kawaida zake na matendoyake ya sherehe, hata na mambo k**a ya ushirikina yalichanganywapamoja na imani na ibada ya wale wanaojidai kuwa ni wafuasi waKristo. Kwa ajili ya mapatano haya kati ya Upagani na Ukristo, aliadhimishwa yule mtu wa dhambi aliyetabiriwa kuwa ni mpingamizi,ajiinuaye nafsi yake juu ya Mungu. Maungo makubwa haya ya diniya uongo ndiyo kazi kubwa ya ajabu inayofanywa kwa nguvu yaShetani, inaonyesha kujitahidi kwake katika kujiweka katika kiticha enzi, na kuitawala dunia jinsi apendavyo. Kwa vile kanisa lilivyotamani kupata faida na heshima yakidunia, liliongozwa, kutaka fadhili na msaada kutoka kwa wakuuwa dunia; na kwa vile lilivyomkana Kristo, lilivutwa kujitia chini ya uongozi wa yule mwovu. Fundisho moja kuu la Kanisa la Kirumi ni ya kwamba papa ndiye kichwa kionekanacho cha Kanisa la Kristo katik**ahali pote, ambaye amepewa utawala kabisa juu ya maaskofu nawahubiri wote duniani pote. Zaidi ya hayo, papa amejitwalia majinayale yanayokuwa ya Mungu hasa.Shetani alijua dhahiri ya kwamba kwa kusoma Maandiko Matakatifu wanadaniu wangeweza kufahamu madanganyifu yakena kuzuia nguvu zake. Hata Mwokozi wa ulimwengu alimpinga naNeno Takatifu. Kristo alimshinda kila mara akimpiga na ngao ya ukweli wa Mungu, kwa kusema, “Imeandikwa.” Alilipinga kila shaurila adui kwa hekima na uwezo wa Neno. Basi k**a Shetani alitaka kudumu katika kuwatawala wanadamu na kuthibitisha mamlaka yaKanisa la Kirumi, ambalo lilijitwalia nguvu isiyo yake, ilimpasa Shetani kuweka watu katika kutofahamu Maandiko Matakatifu. Biblia ingemtukuza Mungu na kuwafahamisha wanadamu hali yao ya kweli; na kwa hiyo ilikuwa ni lazima kuyafunga na kuyasetiri mafundisho matakatifu ya Biblia. Tena Kanisa la Kirumi likatumia njiahii. Kwa karne nyingi kuvieneza vitabu vya Biblia kulikuwa haramu. Watu walikatazwa wasiisome Biblia wala kuwa nayo nyumbani ; tena mapadre na maaskofu wapotovu wakaeleza mafundisho ya Biblia kwa namna ilivyoweza kuthibitisha uongo wao. Kwa njia hii papa alipata kukubaliwa karibu duniani pote ya kwamba yu mwakilishi wa Mungu duniani, ambaye amepewa mamlaka makuu juu ya kanisana serikali pia._
*WAKATI NA SHERIA ZABADILISHWA*
_K**a kimekwisha kuondolewa kitu kilichoweza kuvumbua mambo ya uongo, basi Shetani aliweza kufanya apendavyo. Manenoya unabii yalisema dhahiri ya kwamba Kanisa la Kirumi litatumaini “kubadili majira na sheria.” Danieli 7:25. Tena halikukawia kujaribukufanya hivyo. Makusudi kuwavuta watu kutoka dini ya kipagani na kuwawezesha waongoke kwa urahisi katika dini ya Kikristo, badala ya kuabudu sanamu za kipagani likaingizwa kanisani tendo lakusujudu picha au sanamu zilizowekwa wakfu, pamoja na makumbusho ya watakatifu wa kale. Na mwishowe amri iliyotolewa nabaraza kuu ilithibitisha kawaida hii ya ibada ya sanamu katika Kanisa la Kirumi. Na kwao kutimiliza jambo hili la kukufuru na kumchukiza Mungu, Kanisa la Kirumi likathubutu kuondolea amri ya pili katika sheria ya Mungu, yaaniamri ile inayokataza tendo la kuziabudu sanamu. tena wakagawaamri ya kumi kuwa sehemu mbili, ili waidumishe hesabu yake yazamani. Lakini nia hii ya kutoa idhini kwa matendo k**a ya kipaganiili yafanywe kanisani, ilitengeneza njia ili mamlaka ya Munguipate kudharauliwa zaidi. Shetani aligeuza amri ya nne pia, akijaribu kuondoa Sabato ya zamani, yaani siku ile ambayo Mungualiibariki na kuitakasa; na mahali pake alitukuza siku ile iliyoshikwana wapagani kuwa k**a “siku kuu ya jua.” Mwanzoni badilisho hilihalikufanywa dhahiri. Katika karne chache baada ya Yesu, Wakristo wote wakaishika Sabato ile iliyo ya kweli. Wakawa na uangalifusana juu ya heshima iliyomhusu Mungu, wakaamini ya kwambasheria yake haibadiliki, wakafanya bidii katika kuutunza utakatifuwa maagizo yake. Lakini Shetani alitumia hila sana kwa mawakiliwake ili wapate kulitimiliza kusudi lake. Makusudi akawatazamisha watu siku kuu ile ya jua, siku ile ilifanywa kuwa siku kuu ya kukumbuka ufufuo wa Kristo. Ikathubutu kuondoaamri ya pili katika sheria ya Mungu, mikutano ya dini siku ile; hatahivyo ikahesabiwa kuwa siku ya mchezo na furaha, tena Sabatoikashikwa kuwa siku takatifu. Konstantine alipokuwa angali mpagani, alitoa amri akiamuru ili Jumapili iwe siku kuu kwa watu wote na mahali pote katika Ufalmewa Kirumi. Baada ya kuongoka kwake aliendelea kuishika siku ya Jumapili, tena amri ile aliyoitoa alipokuwa mpagani, ilitiliwanguvu kwa ajili ya dini yake mpya. Lakini kadiri siku ile ilivyotukuzwa haikutosha kuwazuia Wakristo wasiishike Sabato ya kweli kuwa sikutakatifu ya Bwana. Basi ilikuwa ni lazima jambo jingine lifanywe; sabato ile ya uongo lazima ipate kutukuzwa sawa na Sabato ile ya kweli. Miaka michache baada ya Konstantine kutoa amri yake,Askofu wa Rumi alitoa neno kwa kuiita Jumapili kuwa ni siku yaBwana. Kidogo kidogo hivi, watu waliongozwa mpaka kuihesabuhiyo kuwa ni siku takatifu. Lakini watu wakaendelea kuishika Sabato ya zamani. Lakini yule mdanganyifu mkuu alikuwa hajamaliza kazi yake. Aliazimia kukusanya jamii ya Wakristo wote chini ya uongozi wake,na kutumia nguvu zake kwa njia ya Askofu wa Rumi mwenyekujivuna na kujidai kuwa ni kaimu wa Kristo. Kwa njia ya watu waliojidai kuwa ni Wakristo lakini ni k**a nusu wapagani, na kwa maaskofu waliotaka makuu, na kwa washiriki wa kanisa waliopenda anasa za kidunia, basi Shetani alifikiliza kusudi lake. Mara kwamara zikakusanywa baraza zilizo kubwa, ambamo wakaitwa wakuuwa kanisa kutoka duniani pote. Na katika baraza karibu zote, Sabatoile iliyowekwa na Mungu ilikuwa ikizidi kuondolewa heshima na kutwezwa, na Jumapili ikazidi kutukuzwa. Kwa namna hiyo sikukuu ya kipagani ikapata kutukuzwa kuwa k**a jambo lililowekwana Mungu, na huku Sabato ya Biblia ikatangazwa kuwa ni msazo wadini ya Kiyahudi, tena wale waliotukuza siku ile wakanenwa kuwa wamelaaniwa.Sasa yule mwasi mkuu alikuwa amefaulu katika kujiinua nafsi“juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.” 2 The2:4. Alikuwaamethubutu kugeuza amri katika sheria ya Mungu iliyo amri ya pekee ambayo kwa dhahiri huwaonyesha wanadamu Mungu wa kwelialiye hai. Katika amri ya nne Mungu hudhihirishwa kuwa ni Muumbaji wa mbingu na nchi, na kwa hiyo ametofautishwa na miungumingine yote ya uongo. Siku ya Saba ilitakaswa kuwa pumziko kwawanadamu ili iwe kuna ukumbusho wa kazi za kuumba. Ilikusudiwa kuwa kitu cha kuwakumbusha wanadamu daima ya kwamba Mungualiye hai ndiye asili ya kuwako kwetu. tena yeye ndiye apaswaye kuheshimiwa na kusujudiwa. Shetani hujitahidi katika kuwavutawatu wasimche Mungu wala kuitii sheria yake; kwa hiyo hujitiakatika kushindana na amri ile hasa ambayo huwaonyesha watu jinsi Mungu alivyo Muumba. Sasa Waprotestanti walio wengi husema sana ya kwambaJumapili ndiyo Sabato ya Wakristo kwa ajili ya ufufuo wake Kristo. Lakini Biblia haishuhudii neno hilo. Wala Kristo mwenyewe walamitume wake hawakutukuza siku hiyo. Jambo la kuishika Jumapili kuwa k**a siku kuu ya Kikristo lilianzishwa na ile “siri ya kuasi” ambayo ilikuwa imeanza kutenda kazi yake hata zamani zile katika siku alipoishi Paulo. Basi siku gani, tena mahali gani ambapo Bwana alikubali jambo hili ambalo ni mzaliwa wa Kanisala Kirumi? Tena inaweza kutolewa sababu gani yenye nguvu kwa kuthibitisha badilisho hili ambalo haliwezi kamwe kuthibitishwa na Maandiko Matakatifu? Katika karne ya sita, mamlaka ya Papa yalikuwa yameimarishwazaidi. Kiti cha enzi yake kiliwekwa katika mji mkuu wa kifalme,naye Papa akatangazwa kuwa ni kichwa cha makanisa yote. Mamlaka ya zamani ya Upagani iliiondokea ile mamlaka ya Papa. Jokaalikuwa amempa mnyama “nguvu zake na kiti chake cha enzi nauwezo mwingi.” Ufunuo 13:2. Miaka 1260 ya mateso ya Kanisala Kirumi ambayo yalitabiriwa na Danieli na Yohana yalikuwayakianzishwa (Danieli 7:25; Ufu13:5-7). Wakristo walishurutishwa kuchagua, ili watupe uaminifu wao na kukubali urembowa dini na ibada za Kanisa la Kirumi, ama kumaliza maisha yaogerezani, kuunguzwa kwa moto, kushtushwa viungo katika mtambo,au kukatwa vichwa. Ndipo maneno haya ya Yesu yakatimia, “Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, narafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu. Nanyi mtachukiwa nawatu wote kwa ajili ya jina langu.” Luka 21:16.17. Mateso yaliwapata waaminifu kwa ukali usivyoonekana tangu awali, na duniayote ikawa k**a uwanja wa vita. Kwa miaka mia nyingi watu wakanisa la Kristo walikuwa wakijificha. Hivyo ndivyo asemavyonabii: “Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfuna mia mbili na sitini.” Ufunuo 12:6._
*ZAMA ZA GIZA*
_Mwanzo wa utawala wa Kanisa la Rumi ulikuwa mwanzo waZama za Giza. Kwa kadiri uwezo wa kanisa lile ulivyoongezeka, ndivyo na giza ilivyozidi kuwa nene. Imani ya watu ikatolewa kutokakwa Kristo aliye msingi wa kanisa wa haki, wakamwadhimisha papa. Badala ya kumtegemea Mwana wa Mungu kwa kuzisamehe dhambina kwa wokovu wa milele, watu wakamtazamia papa na maaskofuna makasisi ambao papa aliwapa mamlaka. Walifundishwa yakwamba papa ndiye aliyekuwa mpatanishi wao mbele za Mungu,na ya kwamba hakuna awezaye kumkaribia Mungu isipokuwa kwa papa, tena ya kwamba papa alikuwa mahali pa Mungu kwao, na kwa hiyo alistahili kuheshimiwa na kusikiwa kabisa. Kukosa kumtii nakuyafanya mapenzi yake papa kulikuwa sababu ya mkosaji kupataadhabu kali ajabu mwilini na rohoni. Hivi fikara za watu zikageuzwa toka kwa Mungu, ili wawaadhimishe wanadamu wakosaji na wakatili naam, wakamheshimumfalme wa giza mwenyewe, ambaye aliwaongoza na kuwatumiakwa kazi yake. Dhambi ilifunikwa na vazi la utakatifu. MaandikoMatakatifu yanapokataliwa, na mwanadamu anapoanza kujidhania kwamba yeye ndiye mkuu, hapo twaweza kutazamia ulagai,udanganyifu, na ufisadi. Kwa kuzikuza sana sheria na desturi za kibinadamu, ndipo ubaya wa kila namna ukatokea kwa ajili ya kuachilia kuzifuata amri za Mungu._
*SIKU ZA TAABU*
_Siku zile zilikuwa siku za taabu kwa kanisa la Kristo. Watuwaliokuwa thabiti kweli kweli walikuwa wachache sana. Ingawa mashahidi wengine walibaki ili kuutunza ukweli, lakini mara zingine ilionekana ya kwamba dhambi na ibada ya namna ya ushirikina llikaribia kushinda, na dini ya kweli ilikuwa karibu kutoweka kabisa duniani. Injili ilisahauliwa, lakini mifano mitupu ya dini ilizidishwa, na watu walilemewa kwa kutozwa fedha nyingi isivyo yahaki. Si kwamba walifundishwa tu kumtazamia papa kuwa mpatanishi wao, lakini pia walifundishwa wapate kuzitegemea kazi zaowenyewe kusudi waupate upatanisho wa dhambi. Safari ndefu adhabu za makosai, kuyaabudu makumbusho ya watakatifu wa kale, kuyajenga makanisa, mahali pa sanamu, na madhabahu, na kulipa pesa nyingi kwa kanisa haya yote na matendo mengine ya namna hayo yalishurutishwa kwa nguvu makusudi kuituliza ghadhabu yaMungu, au wapate kufadhiliwa na Mungu; kana kwamba Mungu,hufanana na wanadamu, tena hasira yake huwaka kwa mambo yaupuzi, au anaweza kutulizwa na sadaka au vitubio!Karne nyingi zilipoongezeka, ikaonekana ya kwamba makosaya mafundisho yaliyotolewa na Rumi yalikuwa yakiongezeka sana.Hata kabla ya kuimarishwa kwa mamlaka ya Papa, mafundisho yaWapagani wenye elimu yalikuwa yameingia kanisani. Wengi ambaowalijidai ya kwamba wameongoka moyo, walikuwa wakiyashikilia madhehebu ya elimu ya kipagani, tena hawakuendelea kujifunzamambo yao peke yao tu, bali waliwashurutisha wengine kuyapokea mafundisho yale, ili kwa njia ile wapate kuwa na nguvu na mvuto miangoni mwa wapagani. Hivi mafundisho makubwa ya uongoyalianza kuingia katika dini ya Kikristo. Mojawapo lililo kuu zaidi kati ya haya lilikuwa fundisho lililosema ya kwamba wanadamu wana hali ya kuishi milele, na ya kwamba wafu huwa na ufahamu wa nafsini. Fundisho hili la uongo ndilo lililokuwa asili ya kawaidaya Kirumi ya kuwaabudu watakatifu wa zamani na kumsujudu Mariamu. Tokea fundisho hili, uzushi mwingine ukatokea ya kwamba wale wasiogeuka mwishoni, watateketezwa milele; fundisho hilililipokewa na kuwa kanuni ya dini ya Kirumi wakati uasi ulipokuwaumeanzishwa karibuni.Ndipo njia ikatengenezwa tena kwa uvumbuzi wa namna nyingine ya upagani, ambao Warumi waliuita “Purgatory”, (yaani mahali pa kuwatakasa watu waliokufa); na njia hiyo ikatumiwakwa kuwaogofisha watu wengi waliokuwa wajinga na washirikina. Uzushi huu ndio unaosema ya kwamba pana mahali pa ahera pamaumivu makali, ambapo watu wasiostahili kuhukumiwa milelewataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, na baadaye wakisha kutakaswa na unajisi wao, ndipo watakapokubaliwa kuingia mbinguni.Lakini fundisho jingine lilikuwa lazima kubuniwa, kusudi kuiwezesha Rumi kujifaidia na hofu na makosa ya wafuasi wake. Likabuniwa fundisho juu ya jambo liitwalo “ Indulgence,” yaani ahadiya kuachiliwa dhambi, kwa ajili ya kufanya jambo fulani. Maondoleo kabisa ya dhambi, yaani dhambi zilizopita, za sasa na zitakazofanywa baadaye, na kuondolewa maumivu yote na adhabu zote zipasazo, mambo hayo yote yaliahidiwa kwa wale waliokubali kujitoa kwa kupiga vita vya papa kwa kuieneza milki yake ya dunia hii,kuwatesa adui zake, au kuwaharibu wale waliothubutu kuukanushaukuu wake. Watu walifundishwa pia ya kwamba kwa kulipa pesakwa kanisa, waliweza kuondolewa dhambi, na pia kuwaweka hururafiki zao waliokuwa wakiadhibika katika ndimi za moto. Hii ndiyonjia ambayo kwayo Rumi ilijaza masanduku yake ya pesa, na kuufululiza utajiri, fahari, na ufisadi wa wale waliojidai kuwa wajumbewa Yule asiyekuwa na mahali pa kulaza kichwa chake. Agizo la Biblia juu ya meza ya Bwana lilikuwa limeondolewa,na badala yake iliwekwa ibada ya Misa, ambayo ni k**a ibada yasanamu. Kwa njia ya kufanya mambo yasiyo na maana, makasisiwa Kanisa la Kirumi walijidai ya kwamba walikuwa na uwezo wakugeuza mkate na mvinyo kuwa mwili na damu ya Kristo kweli.Kwa ufidhuli na makufuru walijidai ya kwamba wana uwezo wa“Kumwumba Muumba wao.” Wakristo wote walishurutishwa kukirikwamba waliamini uzushi huu ambao kweli ulikuwa ukimtukana Mungu ama wapate adhabu ya kufa. Wale waliokataa kuufuata uzushi huo waliteketezwa kwa moto.Mamlaka ya Rumi yalipozidi kuenea, ndipo uovu waoukaongezeka duniani. Maandiko Matakatifu yalikaribia kupoteakabisa, si kwa watu peke yao, bali na kwa makasisi pia. K**a Mafarisayo wa zamani, watangulizi wa Kirumi waliuchukia nuru,isije ukazifunua dhambi zao. Baada ya kuiondoa sheria ya Mungu, ambayo ilikuwa kipimo cha ukamilifu, wakaanza kutumia nguvu bilakiasi, wakatenda mabaya bila kizuizi. Ulaghai, tamaa ya mali; nauasherati ukazidi. Watu hawakuepukana na tendo lo lote la uhalifu lililoweza kuwaletea mali au cheo. Majumba ya mapapa namaaskofu yalijaa zinaa na ulevi. Mapapa wengine wakuu walifanyamambo ya uhalifu na kuchukiza mno, hata watawala wa serikali yanchi walijaribu kuwauzulisha wale wakuu wa kanisa, wakiwaonakuwa ni watu wabaya kabisa wasiostahili kuyashika madaraka yaheshima. Kwa karne nyingi hayakuwa na maendeleo yo yote kwakuelimisha watu, kwa kazi ya ustadi, wala kwa ustaaarabu. Mambo ya kiroho na ya elimu yalizimishwa kabisa katika nchi zote zaKikristo._
🔚➖🔚➖🔚
🙏🙏🙏