07/05/2026
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini, Mch. Ezekiel Mwasamboma, amefungua kikao cha Kamati ya Miradi ya Kanisa hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Ileje Hotel, wilayani Ileje mkoani Songwe.
Kikao hicho cha kawaida cha Idara ya Miradi kimewashirikisha makatibu wa miradi kutoka wilaya mbalimbali za jimbo pamoja na wakuu wa taasisi za Kanisa, wakiwemo wakuu wa vyuo vya ufundi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mch. Mwasamboma amewasihi wajumbe kutumia kikao hicho kujadili na kutazama fursa mbalimbali za miradi ndani ya jimbo kwa lengo la kukuza uchumi wa Kanisa.
Aidha, amesisitiza kwa wakuu wa taasisi, hususan vyuo vya ufundi, kuwa wabunifu na kuongeza uzalishaji kupitia fani wanazozitoa katika vyuo vyao.
Kikao hicho kimeongozwa na Katibu wa Idara ya Miradi, Mch. Emmanuel Mwangata, ambaye pia amewashukuru wajumbe kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa idara. Part 10