Seba Sulle

Seba Sulle Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. 2 Timoth 2:15

Teacher β€œGrace and truth” (John 1:14).

  ya UdhaifuπŸ“Œ Mtume Paulo amekuwa akijisifu kuwa udhaifu wake wa kibinadamu ni mzuri ili uweza wa Kristo ukae juu yake "...
08/03/2025

ya Udhaifu

πŸ“Œ Mtume Paulo amekuwa akijisifu kuwa udhaifu wake wa kibinadamu ni mzuri ili uweza wa Kristo ukae juu yake

"Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu". 2 Wakorintho 12:9

πŸ“Œ Japokuwa udhaifu sio kitu cha kujivunia kwa akili ya kibinadamu kwa sababu unashusha hadhi ya mtu, lakini mimi sina budi kuungana na Paulo katika hili kuwa udhaifu wangu/wako unampa Yesu kukupa ukamilifu wake, yaana kupitia udhaifu wako yeye huja na huja na uweza wake juu yangu/ yako

πŸ“Œ Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya wanawake, niseme hili kwa wanawake wote kuwa, Mungu alipoumba mwanamke udhaifu uliokuwepo Yesu pamoja na uweza wake ukae juu yenu.
πŸ“Œ Kutambua nafasi ya mwanamke sio kuupoka nafasi ya mwanaume, Mungu aliweka kila kitu katika utaratibu, tuadhimishe siku hii njema tukikumbuka uumbaji mzuri wa mwanamke.

Barikiwa

07/03/2025
 πŸ“Œ Kila Mama yangu akitaka kupika maharage, lakini kabla ya kupika maharage, alichagua maharage mabaya na yasiyofaa na k...
20/09/2024



πŸ“Œ Kila Mama yangu akitaka kupika maharage, lakini kabla ya kupika maharage, alichagua maharage mabaya na yasiyofaa na kuyatupa nyuma ya nyumba iliko sehemu ya kuweka uchafu, huku akipika maharagwe mazuri.
πŸ“Œ Lakini mvua iliponyesha maharage hayo mabaya ambayo hayafai kupikwa yaliota na kuwa mbegu na kukua na kuonekana nzuri tena.
πŸ“Œ Baadaye mama akatushauri tuyapalilie vizuri na kwakuwa kwenye sehemu ya kutupia taka kuna mbolea maharage yalistawi na kutoa maua kisha mbegu ikakomaa

βœ… Katika maisha binadamu tunapitia mengi, wakati mwingine, yule mtu aliyetupwa na ndugu zake kwa kutokuona umuhimu wake wakati huo, Mungu humtunza kwa ajili ya wakati ambao thamani yake itarudi.
βœ… Kwenye pito huwa kuna kuchongwa na kuzongwazongwa, utalia machozi sana, utaona machungu mengi n.k lakini unatengenezwa ili thamani ya kuumbwa kwako ionekane.

βœ… Mama aliyatupa yale maharage kisha anatuagiza tuyapalilie, aliyezitupa anaanza kuzivuna. Anatambua kuwa maharage aliyoyatupa yana THAMANI.
βœ… Wakati Yusufu anatupwa shimoni na ndugu zake, wakati anauzwa na ndugu zake, hakuwa na thamani mbele zao, alikosa thamani alikuwa k**a maharage yasiyofaa kupikwa.

πŸ“Œ Usilie watu WAKIKUTUPA NYUMA, usilie watu WALIKUKATAA, usilie huku wanakutazama chini.
πŸ“Œ Yusufu alipitia mengi huko Misri, kufanya kazi kwa potifa,mke wa potifa kumtwenza, kufungwa gerezani, kutafsiri ndoto.......hadi kufikia cheo kikubwa kuaminiwa na Wamisri haikuwa kazi rahisi, ilihitaji Mungu kumchonga, ilihitaji uvumilivu, ilihitaji kujitunza kilichoko ndani.

πŸ“Œ MVUA inakuja na watu hao hao WANAOKUKATAA leo wataomba KUKUVUNA kesho.
πŸ“ŒNjaa ilipozuka ndugu zake Yusufu walimfuata Yusufu pasipo kujua k**a ndiye aliyeongeza thamani kubwa, yeye ndiye mwenye kutunza nafaka ya Misri na mataifa mengine yalihemea huko, siyo tena Yusufu waliyemuuza alikuwa tayari thamani yake imepanda sana hata kufikia kiwango cha kuogopwa sana, mtu mkubwa, mtu mwenye cheo kikubwa, mtu aliyebeba uhai wa watu, kumbuka chakula ni hitaji la msingi bila chakula hakuna uhai.

πŸ“Œ Hii ni yako wewe uliyekosa thamani kwako mwenyewe, mbele wa watu, umejichokea, umekata tamaa, Inuka umsifu Bwana kwenye mazingira yako, lipo kusudi juu yako, kesho yako inaandaliwa, thamani yako inatengenezwa, nyakati ya kutengenezwa ni nyakati ya utulivu, ongeza furaha yako kwa Mungu, kwakuwa hata ukinuna haisaidii, ni vizuri ufurahi kwenye chagamoto yako.
Paulo na Silla walipotupwa gerezani, tungetumia tamaduni zetu wangenuna, wangekasirika kuonyesha hisia zao, lakini wao walibadili gia hewani wakaanza kumsifu Mungu, Mungu akashuka na milango ya magereza yakunguka, kufuli zikadondoka. Haleluyah raha kuntumikia Mungu hakika πŸ› οΈ

Barikiwa

Mwebrania Sulle

Highlights

πŸ“Œ
29/08/2024

πŸ“Œ

πŸ“ŒπŸ› οΈ
28/08/2024

πŸ“ŒπŸ› οΈ

πŸ› οΈπŸ“Œ
28/08/2024

πŸ› οΈπŸ“Œ

Hii kwa watumishi vijana, mimi na wewe tudake kitu
25/08/2024

Hii kwa watumishi vijana, mimi na wewe tudake kitu

I want to express my deepest gratitude for being not just my wife but my best friend and confidante. Here's to many more...
18/08/2024

I want to express my deepest gratitude for being not just my wife but my best friend and confidante. Here's to many more years of laughter and love.
Happy birthday to you mama watoto

 πŸ’Ό "Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo, k**a kwa Bwana, wala si kwa wanadamu"Wakolosai 3:23  "Basi, ndugu zangu wapenzi, mw...
30/07/2024



πŸ’Ό
"Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo, k**a kwa Bwana, wala si kwa wanadamu"
Wakolosai 3:23

"Basi, ndugu zangu wapenzi, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, mkijua ya kuwa katika Bwana kazi yenu si bure." 1 Wakorintho 15:58

β€œ Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu ” Filipi 4:19

πŸ“Œ Saikolojia inatufundisha Motisha au hamasa ya aina mbili

1️⃣ Motisha ya ndani (Intrisic motivation) hutoka ndani

βœ… Unapokuwa na motisha ya ndani, unashiriki katika shughuli kwa sababu unaifurahia na kupata uradhi wa kibinafsi kutokana na kuifanya.
βœ… Msukumo wa ndani ni muhimu sana kuliko shauri linalotoka kwa rafiki au ndugu kwa sababu haitakuwa na msingi mzuri kwako maana ni wazo la kupandwa kutoka nje.
βœ… Ukisikiliza hamasa iliyoko ndani mwako na kujijenga huko ndio kupalilia kile Mungu ameumba ndani mwako.
βœ… Usiidharau hiyo sauti ya ndani mwako, ina hatima njema sana, ipalilie na kuijengea uwezo, utanishukuru baadaye.
βœ… Kila mtu Mungu amempa edeni yake, humo atafurahia ulimwengu wake bila kuwa na shida au kutumia nguvu kubwa kustruggle.
βœ… K**a bado hujajipata tafuta hamasa yako ya ndani ujipate na uishi humo.

2️⃣ Motisha ya nje (Extrinsic motivation) hutokana na mambo ya nje.
βœ… Unapohamasishwa kutoka nje, unafanya kitu ili kupata thawabu ya nje.
βœ… Motisha ya nje inaweza kukufaa pale ambapo unayemsikiliza ni mtangulizi wako katika kile una hamasa yako ya ndani
βœ…Si kila shauri inafaa kwako, na si kila neno la kuambiwa inaweza kufanya kazi kwako.
βœ… Haina maana maneno ya nje ni ya kupuuzwa hapana, pima, hakikisha ina mchango gani katika hamasa yako ya ndani
βœ… Kila mtu Mungu amempa marafiki na washauri wa kumfaa katika maisha usiwapuuze watakuongezea hatua mbele.

Barikiwa

Seba Sulle
@followers

πŸ“Œ Usikubali ufafanuzi wa maisha kutoka kwa watu wengine, maisha ni yako, jipe ufafanuzi wako mwenyeweπŸ‘Œ
22/07/2024

πŸ“Œ Usikubali ufafanuzi wa maisha kutoka kwa watu wengine, maisha ni yako, jipe ufafanuzi wako mwenyeweπŸ‘Œ

 βœ… Nami naungana na Daudi kuimba Zaburi hii🎷🎷🎢🎡🎼"Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya m...
14/07/2024



βœ… Nami naungana na Daudi kuimba Zaburi hii🎷🎷🎢🎡🎼

"Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele."
Zaburi 23:1-6

πŸ“Œ Ninamshukuru sana Mungu kwa namna amenipa uzima huu hata kuongeza miaka, wakati ninatafakari asubuhi hii, nimewaza sana nimelipa bili za umeme, nimelipa kodi za jyumba, nimelipia maji, n.k lakini sikuwahi kudaiwa bili ya pumzi, hakika Mungu alitupa pumzi ya uzima mtu akawa nafsi hai
πŸ“Œ Ninakushukuru na nitakushukuru jioni, nitakushukuru mchana na asubuhi kwa jinsi unanitunza na kunifanya kuwa mimi
πŸ“Œ Ninawashukuru na nitaendelea kuwashukuru wazazi wangu walionipa malezi ambay kwayo yananipa mwangaza wa kuona na kutafsiri maisha yangu na familia ya kwa mwelekeo ninaodhani ni sahihi (Input ya malezi yao ni mtaji wangu mkubwa sana)
πŸ“Œ Ninawashukuru familia yangu kipekee mke wangu kipenzi Sanura Sulle, hakika wewe ni rafiki, mshauri wangu mzuri, mama wa watoto wangu, libarikiwe akili hisia zako, watoto wangu Mungu awape kesho iliyo jema kwenu.
πŸ“Œ Mwisho kabisa niwashukuru ndugu zangu wote, marafiki zangu wote bila kuwataja kwa majina humu fesibuku, hakika ninyi ni watu wa thamani sana kwangu, input zeni mojamoja ina mchango mkubwa kwangu, ninawapenda na nitaendelea kuwapenda daima.

Heri ya kumbukizi

Kwa zawadi hii namba 0685000122 itakuwa hewani saa 24/7 hivyo ujumbe muamala unaweza kuitaπŸ₯€πŸ₯€

Barikiwa

🍷🍷
Mwebrania Sullee

Address

Manyara

Telephone

+255685000122

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Seba Sulle posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share