parokia ya Ekaristi Takatifu-lushoto

parokia ya Ekaristi Takatifu-lushoto Parokia ya Ekaristi Takatifu – Lushoto ni parokia ya Kanisa Katoliki chini ya Jimbo Katoliki la Tanga

Dominika ya 18 ya mwakaMungu wetu ni mkarimuTunaombwa kuwa wakarimu kwa tulichonacho kwa ajili ya wenzetu kwa kile tulic...
02/08/2026

Dominika ya 18 ya mwaka
Mungu wetu ni mkarimu

Tunaombwa kuwa wakarimu kwa tulichonacho kwa ajili ya wenzetu kwa kile tulichokirimiwa na mungu.

19/07/2026

MWANGAZA WA VIJANA ULIWAKA LEOLeo Parokia ya Ekaristi Takatifu ilishuhudia kitu cha pekee! Zaidi ya vijana 100+ kutoka P...
27/06/2026

MWANGAZA WA VIJANA ULIWAKA LEO
Leo Parokia ya Ekaristi Takatifu ilishuhudia kitu cha pekee! Zaidi ya vijana 100+ kutoka Parokia ya Ekaristi Takatifu na Parokia Tarajiwa ya Mhelo walijaza Ukumbi wa Kanisa kwa ajili ya Semina ya Vijana iliyokuwa na kichwa cha “Mwangaza wa Vijana”

Mungu alizungumza moja kwa moja na mioyo ya vijana kupitia mafundisho yenye nguvu, ushirikiano mkubwa, na furaha ya kiroho!

Hii si semina tu… ni mwanzo wa kizazi kipya cha vijana wenye mwanga na moto wa Kristo!
Asante sana kwa vijana wote waliojitokeza! Mungu awabariki na awape neema ya kuendelea kuwa nuru katika vizazi vyetu.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Baba Paroko Firmati Cosmas Tarimo!Kwa miaka 33 ya huduma ya uaminifu, upendo na kujitoa...
27/06/2026

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Baba Paroko Firmati Cosmas Tarimo!
Kwa miaka 33 ya huduma ya uaminifu, upendo na kujitoa katika ukuhani, Baba Paroko ameendelea kutufundisha, kutubariki na kutuongoza katika imani yetu.
“Wew ni kuhani hata milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” (Zaburi 110:4)
Asante sana Baba kwa mfano wako mzuri wa ukuhani! Mungu akubariki na akupatie afya na nguvu zaidi katika miaka mingine mingi. 🙏

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Baba Paroko Firmati Cosmas TarimoKwa miaka 33 ya huduma ya uaminifu, upendo na kujitoa ...
27/06/2026

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Baba Paroko Firmati Cosmas Tarimo
Kwa miaka 33 ya huduma ya uaminifu, upendo na kujitoa katika ukuhani, Baba Paroko ameendelea kutufundisha, kutubariki na kutuongoza katika imani yetu.
“Wew ni kuhani hata milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” (Zaburi 110:4)
Asante sana Baba kwa mfano wako mzuri wa ukuhani! Mungu akubariki na akupatie afya na nguvu zaidi katika miaka mingine mingi. 🙏

Katika unyenyekevu na imani kuu, tumetembea tukimshuhudia Kristo aliye hai ndani ya Ekaristi Takatifu.Si tukio la kawaid...
07/06/2026

Katika unyenyekevu na imani kuu, tumetembea tukimshuhudia Kristo aliye hai ndani ya Ekaristi Takatifu.
Si tukio la kawaida ni ushuhuda wa imani, ni agano la upendo, ni uwepo wa Mungu katikati yetu.

Leo tunakiri kwa matendo kuwa:
Mwili na Damu ya Kristo si ishara tu, bali ni uzima wetu, nguvu yetu, na tumaini letu.

Ekaristi Takatifu chanzo na kilele cha maisha ya Kikristo.
Tumebarikiwa kushiriki, kushuhudia, na kubeba uwepo huu mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku.

🎂 Heri ya kuzaliwa, Fr. Henry Mutune! 🎉Mungu akubariki na akujalie miaka mingi ya neema, afya na furaha tele katika utum...
01/06/2026

🎂 Heri ya kuzaliwa, Fr. Henry Mutune! 🎉

Mungu akubariki na akujalie miaka mingi ya neema, afya na furaha tele katika utumishi wako Baba Paroko Msaidizi. 🙏❤️

Heri ya Sherehe ya Utatu Mtakatifu! Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina! 🙏Leo tunashereheka Utatu...
31/05/2026

Heri ya Sherehe ya Utatu Mtakatifu!

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina! 🙏

Leo tunashereheka Utatu Mtakatifu siri kubwa ya upendo wa Mungu: Baba aliyetuumba, Mwana aliyetukomboa, na Roho Mtakatifu atutakasaye na kutuongoza.

Mungu mmoja katika Utatu Mtakatifu awabariki, awalinde na kuwaongoza nyinyi nyote katika maisha yenu. Mupate kuishi katika upendo na umoja k**a vile Utatu Mtakatifu.

Utatu Mtakatifu, utukufu kwako

💍📖 SEMINA YA SAKRAMENTI YA NDOAParokia ya Ekaristi Takatifu imeendelea kutoa malezi ya kiroho kwa waamini kupitia semina...
30/05/2026

💍📖 SEMINA YA SAKRAMENTI YA NDOA

Parokia ya Ekaristi Takatifu imeendelea kutoa malezi ya kiroho kwa waamini kupitia semina ya Sakramenti ya Ndoa yenye mada “Majukumu ya Wanandoa katika Familia.”

Semina hii imeongozwa na Sr. Theodora Tesha, Daniel Mayba na Severin Joseph, ikiwasaidia washiriki kutafakari nafasi ya wanandoa katika kujenga familia zinazomcha Mungu, zenye upendo, umoja na uwajibikaji.

Tunawashukuru waongozaji na washiriki wote kwa muda wao na ushiriki wao katika kuimarisha tunu za familia za Kikristo. Tuendelee kuziombea familia zetu ili ziwe makanisa madogo yanayoishi na kushuhudia Injili ya Kristo.

“Mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.” (Yos 24:15)

Siku ya Pentekoste imefika!Moto wa Roho Mtakatifu uendelee kuwaka mioyoni mwetu.Tupokee nguvu kutoka juu ili tuwe mashah...
24/05/2026

Siku ya Pentekoste imefika!

Moto wa Roho Mtakatifu uendelee kuwaka mioyoni mwetu.
Tupokee nguvu kutoka juu ili tuwe mashahidi wenye ujasiri wa Yesu Kristo.
Heri ya Pentekoste kwa Parokia yetu yote! 🙌

Address

Lushoto
Lushoto

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when parokia ya Ekaristi Takatifu-lushoto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share