29/06/2025
π€
Je, wewe ni *Mtakatifu* ?, Kwa nini?
ποΈ Em tulitazame hili katika Ufalme na Mamlaka ya Kiungu( *Mungu Wa Mbinguni* )
*TWENDE PAMOJA*
> Hadi Mwisho π
π§ββοΈ *UTAKATIFU* ni ile hali ya Mtu au Kitu kuwekwa wakfu kwaajili ya kazi ya MUNGU tu. Na Neno *Wakfu* linamaanisha *kujitolea* . Hivyo kuwa Mtakatifu ni ile hali ya *kujitolea kwaajili* ya MUNGU.
Pia hali ya *kujitolea* ni vile Mtu anafanya kitu kwa kuipenda tu pasipo kuangalia anapata kitu kwa ukubwa gani sasa lakini kwa *matumaini makubwa ya kupata kitu kikubwa* baadae.
π *SASA*
Kuwa *Mtakatifu* ni kujitolea kwa kazi ya MUNGU tu, yaani *kujitoa* ya kuwa wewe ni wa MUNGU na kila *ukifanyacho* au *kukiacha* ni kwaajili ya MUNGU tu na si vinginevyo.
π *Tuangalie*
Mlima Mtakatifu, Hekalu Takatifu, Mtaktifu Yohana *n.k* ( _oh kumbe hekalu ni kwaajili ya BWANA, Mlima nao Kwa kazi ya BWANA na Yohana nae kwaajili ya BWANA tu, wewe Je? Yule je?_ )
Hii inamaanisha kila ukifanyacho au ukiachacho ni kwaajili ya MUNGU.
> Kwa asilimia 100 zote bila hata kupunguka hata 1% kila akifanyacho au akiachacho Mtu huyo aitwaye Mtakatifu ni kwasababu ya MUNGU. Nayo katika mawazo, utayari wa moyo na matendo ya kujitoaπ
> Nabii na Mtume_Apolo *Nathubutu kusema* ya kuwa ukisema wewe au yule ni *Mtakatifu*, inamaana yeye ni Wa MUNGU, Kwaajili ya kazi ya MUNGU π
π *SIFA KUU YA MTAKATIFU*
> Kila Jambo analolifanya au kuliacha ni kwa ajili ya MUNGU tuπ
Na hii hali huthibitishwa na yeye mwenyewe *katika mawazo yake katika akili na utayari wa moyo pasipo huzuni* kisha huonekana kwa matendo ya kujitoa katika *mwili* kupitia macho ya *nyama* ambapo watu humuona.
πCHANZO KIKUU CHA MATENDO YA UTAKATIFU NI KATIKA *MAWAZO MEMA* NA *UTAYARI WA MOYO* PASIPO HUZUNI
π§ββοΈ *HALI YA MTU MTAKATIFU*
> MAWAZO MEMA, UTAYARI WA MOYO(pasipo huzuni) MATENDO YA KUJITOA
*Yaani*
1. Kutafuta kwake Pesa ili kutumika kwa kazi ya BWANA tu
2. Huzitazama Fursa au kazi kwa jicho la Kiungu tuπ yaani k**a hakutakuwa na nafasi ya MUNGU kutukuzwa au kazi ya MUNGU kutosonga mbele *kazi hiyo huiacha* hata k**a inafaida kubwa. Yaani MUNGU tu
3. Safari zake zote ni kwajili ya kazi ya MUNGU au kutimiza kusudi la MUNGU
3. Kutoa msaada kwaajili ya Utukufu wa MUNGU ( *Hakuna asilimia hata 1% ya kujitazama yeye bali 100 zote kwaajili ya BWANA MUNGU* )
4. Kula kwake ni kwaajili ya BWANA tu
5. Huduma yake ni kwaajili ya BWANA tu
6. Kusoma kwake ni kwaajili ya kutimiza kusudi la BWANA tu
7. Kutembea kwake hakuhariibu UTUKUFU wa BWANA tu
8. Kuvaa kwake hakuharibu Utukufu wa MUNGU tu
9. Mke au Mume ni kwaajili ya Kazi ya BWANA tu
10. Rafiki Kwaajili ya Kazi ya BWANA tu
11. Maombi yake ni kwaajili ya Kazi ya BWANA
12. Furaha yake au Huzuni yake juu ya kitu fulani ipo kwa jicho la kiungu tu( *liwe baya atafurahi k**a ni kwa Utukufu wa MUNGU, liwe zuri ataumia k**a linaharibu Utukufu Wa MUNGU*)
13. *YAANI NI MUNGU TU* πππ
Huyo ndiye *Mtakatifu*, yaani hana nafasi yake yeye k**a yeye katika Jambo lolote lile, bali yote kwaajili ya MUNGU.
π§ *KUMBUKA*
Inakubalika kuwa UTAKATIFU tu ndiyo ticketi ya kwenda Mbinguni.(Yaani *Walio watakatifu tu ndiyo warithi wa Nchi Mpya*)
β *MASWALI*
1. Je, wewe ni *Mtakatifu* ?
2. Ni kweli kila ukiwazacho ni kwajili ya MUNGU ?
3. Uhitaji wako ili ukamilishe kazi, kusudi au Utukufu wa MUNGU?
4. Ni kweli misaada unayotoa hautaki Kutambukika, umaarufu, uonekane unamoyo, umeguswa, haunashaka, hauna huzuni wala kutaka chochote??
5. Ni kweli umeacha kufanya Jambo fulani kwajili ya Utukufu wa MUNGU, na hakuna sababu zako binafsi k**a kuumia, au kupoteza pesa, au aibu au kudharaukika?
6. Ni kweli unaumia umekosa kitu fulani k**a pesa, au mke au ajira au kitu cha thamani kwa sababu kazi ya MUNGU itapunguka??
7. Ni kweli unamsifu mtu juu ya Jambo fulani kwasababu ya Utukufu wa MUNGU, *Pasipo kuangalia ni Rafiki, ndugu au anione* ?,
8. Je, Furaha na Huzuni yako iko katika MUNGU?
9. Je, ni una MAWAZO, UTAYARI WA KUFANYA JAMBO NA MATENDO YAKO YA KUJITOA *kwaajili ya MUNGU 100%*
10. N. Kadhalika
> πK**a ndivyo kwa 100% Basi wewe ni mmoja wa wale walionenwa yakuwa ni warithi wa nchi, na k**a unapunguka hata 1% basi hautaonja pepo wala hautakuwa mrithi wa Nchi. Kwakuwa warithi ni walio watakatifu tu . *Tafakari kuu ya Biblia na Nabii na Mtume_Apolo*
π₯² *Kweli kwa macho na tafakari ya kawaida ni vigumu kabisa kukamilisha Yote hayo ili kuwa Mtakatifu, lakini ni rahisi sana kuupata Utakatifu na Kudumu katika Utakatifu huo*
βοΈ *MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWEZE KUWA MTAKATIFU*
> ( _yaani kuweza kudumu katika utakatifu na kuweza *kufanya mambo yote* katika hali ya utakatifu_)
1. Kujisafisha kwa Toba iliyo ya kweli,π pale utakapanguka katika dhambi kwa bahati mbaya( *kuto kujua* )
2. Usifanye baadhi ya vitu kwa ugumu wa moyo
3. Usifanye kitu kwa huzuni, au kwa influence za mtu
4. Omba kabla ya kufanya
5. *K**A MOYO UNAKATAA ACHA HATA K**A NI JEMA, NA K**A MOYO UNAKUBALI FANYA HATA K**A BAYA*
> ilimradi tu Amani ya moyo iwepo, yaani sikiliza moyo tu, na si kwa kuangalia huruma ya mtu, au uhitaji wa mtu au utaonekanaje, au hadhi yako. Narudia tena k**a kukataa kataa hata k**a Jema, ilimradi moyo wako Amani haipungui
> π *Amesema Nabii na Mtume_Apolo*
π§βπ¦― *WITO*
Kuwa Mtakatifu ni Jambo linalohitaji kujitoa sana na si jambo la kuliepuka kwakuwa ndilo Tiketi ya kuwa Mrithi wa Nchi Mpya.
Hivyo, pasipo kuwa Mtakatifu huwezi kuwa Mrithi wa Nchi mpya. Jitahidi sana kudumu katika Utamatifu kwa Kuomba *Toba mara kwa mara* katika moyo ule unaohitaji msamaha wa kweli, na *mawazo ya kuchochea kiu* ya kuutafuta Utakatifu kwa Moyo wote. Nawe utadumu katika Utakatifu kwa Neema Ya BWANA YESU
> Amesema Nabii na Mtume_Apolo
π *MWISHO*
Utakatifu ni hali inayojengwa katika misingi hii
1. Mawazo mema
2. Utayari wa moyo
3. Matendo ya kujitoa
4. Kujikana kabisa
5. Toba, Sala na Maombi
6. Ibada takatifu
7. Na kadhalika
> Ameyasema: Nabii na Mtume_Apolo.
β *TAFUTA UTAKATIFU UWE MRITHI WA NCHI MPYA NA UFALME WA MUNGU UJAO ULIO WA MILELE*
π§ Hekima ya;
Nabii na *Mtume_Apolo*
> *_Nguvu Ya Mungu, Nuru Ya ulimwengu, Uamsho Wa Kiroho, Elimu Safi Ya Kimbingu, Na Ukombozi Wa Ulimwengu katika YESU_*
π *0613826135*
π§ββοΈ *TOBA, SALA NA IBADA TAKATIFU*
> ( _Misingi Ya Maisha Matakatifu_ )
*MATHAYO 5:3*
β
*ATUKUZWE MUNGU WA MBINGUNI, MUUMBA MBINGU NA NCHI NA ALIYE MTUKUFU KATIKA UTAKATIFU*
*AMINA!*
πππ
*__Soma na Mwenzako kwa kuwatumia wale uwezao kuwafikishia ujumbe huu_*_
π«π«π«π«π«π«π«π«π«π«π«π«
Facebook Nabii Apolo