31/03/2024
CHUKI
=====
Leo nahitaji kuwashirisha kuhusu .
Tukiangazia maana ya chuki ni hisia zinazohusisha kutopenda kitu, Jambo au mtu. Chuki ni kinyume cha upendo.
Historia ya chuki;
----------------------------
Chuki ina historia ndefu mno kwani Kwa mara ya kwanza imeonekana wakati dunia ikiwa na watu 4 Tu. Mwanzo 4:6-8
[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
[7]K**a ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
[8]Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani].
Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
Biblia inayoonyesha chuki ilianza lini na watu wakiwa wangapi, TAFAKARI KIDOGO walikuwa watu 4 Tu duniani yaani hata wangewana hii dunia kila mmoja angepata robo LAKINI bado chuki ikajipenyeza
Nini chanzo cha chuki
-------------------------------------
Chuki ina vyanzo vingi lakini kibali ni chanzo kikubwa maana hata chuki ilipoonekana Kwa mara ya kwanza chanzo Ilikuwa kibali. Chuki ya Esau Kwa Yakobo ni Kibali, chuki ya Wana wa Yakobo kwa Yusufu Ilikuwa ni KIBALI
Chuki ni kinyume cha upendo hivyo sababu zozote zinazosababisha upendo zikiondoka ndio sababu za chuki.
Hata ukiona watu wanachukiana sababu ya mapenzi ujue mmoja kapata kibali mwingine makosa.
Vyanzo vingine vya chuki ni kutofahamiana vema; usipomfahamu mtu vizuri ni rahisi kujenga chuki ikiwa atakuwa na matendo usiyoyapenda lakini ukimfahamu utatumia nafasi hiyo kubaini sababu ya matendo hayo
wivu; mtu kumwonea wivu mtu mwingine huzalisha chuki
Uzushi; hii hutokea pale mtu anasikiliza maneno ya uzushi juu ya mtu mfano anaambiwa Jenerali ni mwizi. Basi mtu atamchukia Jenerali Kwa sababu amesikia ni mwizi.
Itikadi Kali za kiimani; mtu atamchukia mtu Kwa sababu tu haamini juu ya kile anachokiamini mfano wazee wa Mila kuwachukia wakristo sababu T
tu hawashiriki sehemu ya Mila zao. Na mkristo anamchukia mzee wa Mila Kwa sababu zilezile.
PAmoja na vyanzo tajwa vya chuki pia chuki hutakuwa vizuri kwenye UNAFIKI Na hutekelezwa Kwa unahisi Kwa HILA
CHUKI HUFANYWA NA NANI?
-----------------------------------------------
Chuki hufanywa na binadamu yeyote; chuki haichagui kimo, unasaba, rangi, ushirika WA kazi n.k
WATU WENGI HUFIKIRI CHUKI INAPASWA KUFANYA NA MTU WA MBALI KWA MTU KINASABA, KIDINI, KIELIMU N.K huu ni upotoshaji mkubwa kwani tumeona chuki ilianzia Kwa binadamu wenye unasahau wa damu na walikuwa 4 Tu.
Chuki huweza kutokea katika familia, shuleni, mahali pa kazi, mahali pa ibada na kadhalika.
Chuki haichagui kitu chochote Bali yenyewe hufuata tu maandalio ya moyo.
Hivyo basi tufahamu chuki hutokea popote na mara nyingine bila sababu yoyote. Ukiona unachukiwa mshukuru Mungu kwamba kumbe wewe ni binadamu na umezungumwa na binadamu.
Watu wengi wanaweza kuvumia chuki bali wanaochukiwa na ndugu zao na marafiki wa karibu huumia mno. Hata biblia haijawa kimya juu ya chuki kwa watu wa nyumbani 1 Timotheo 5:8;
[8]Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Na ndio sababu nimeona tushirikishane.
Chuki ina athari mbaya na za kidumu. Kwanza Sigmund Freud anasema chanzo cha migogoro yote duniani ni mapenzi. Mapenzi hayawezi kuleta ugomvi isipokuwa inapozalishwa chuki.
Hata migogoro inayosababishwa na mivutano ya KIDINI bado dini imekuwa mwamvuli tu, kwani ikiwa Mimi ni mkristo nikahubiri Injili yangu Safi watu wasikubaliane nami kuna sababu gani ya kuwachukia hata kupigana??? Jibu ni chuki ni hulka ya binadamu. CHUKI ILIZALIWA KABLA YA UYAHUDI UKRISTO NA UISLAMU, CHUKI ILIZALIWA KABLA YA UWEPO WA MADOLA DUNIANI YAANI KABLA YA UWEPO WA MIPAKA YA NCHI NA WAFALME WAKE.
Ukiona rafiki yako anakuchukia mkumbuke Yesu akivyosalitiwa na Yuda
Ikiwa ndugu zako basi jua chuki Kwa ndugu ilianzia kwenye Eden.
Binadamu ndio sababu ya chuki hivyo tunalazimika kila mmoja kushinda chuki na uruhusu upendo utawale..
Mwl Kapagi