Free Anglican Church Kibondo

Free Anglican Church Kibondo Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Free Anglican Church Kibondo, Religious organisation, Stand mpya, Kibondo.

26/05/2026

Siku ya Pentekoste (Ujio wa Roho Mtakatifu)

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu (Wafilipi 4:13)
13/05/2026

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu (Wafilipi 4:13)

26/04/2026
26/04/2026

Hakika YESU alifufuka katika wafu- Free Anglican Kibondo Quire.

19/04/2026

Somo: YATUMIE MAARIFA ILI USIANGAMIE KIMWILI NA KIROHO.

Bwana YESU Asifiwe wapendwa katika Bwana!

Ninapenda kukaribisha kwa neema ya MUNGU tutafakari pamoja neno lake kutoka katika kitabu cha Nabii Hosea 4:6
"Watu wangu waangamia kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa Mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani wangu Mimi, kwa kuwa umeisahau Sheria ya MUNGU wako Mimi nami nitawasahau watoto wako"

Bwana apewe sifa, Kuna mambo 3 natamani tujifunze:
1. Maana ya maarifa.
2. Hasara/ madhara ya kukosa maarifa.
3. Faida ya kuwa na maarifa

1. Maarifa ni ujuzi, ufahamu au
uwezo wa kiakili wa kutatua
changamoto/ matatizo yako
na ya wengine.
Maarifa hayaji kwa kupata au
kufikia kiwango tu cha elimu
fula baali ni uwezi wa kutenda, hata k**a wewe hukusoma mpaka chuo kikuu. Hapa hatutazami vyeti tunatazama uwezo "competence" kwa hiyo, weka pembeni vyeti vyako, Fanya/ Tenda mambo yaende watu watoke kwenye mkwamo.

2. Hasara/ Madhara ya kukosa maarifa.
(a) Mambo yako yanakwama na kuharibika/ KUFA.
*Mfano; huduma haitasonga mbele.
*Mradi wako utakufa.
*Watoto wako hawawezi kufanikiwa.
* Mume/Mke wako hawawezi kusonga mbele kimaisha.

(b) Kukataliwa na Mungu.
Mungu akikukataa huwezi kusonga mbele katika maisha yako yote.
Mfano;
* Utajitahidi kuomba bila kujibiwa.
* Utafanya huduma mbalimbli k**a kuhubiri, kuomba na nafasi nyingine hapo kanisani kwako ukiwa peke yako yaani Mungu hatakuwa na wewe kwa unayoyafanya itakuwa sawa na kazi Bure.

3. Faida/ Umuhimu wa kutenda maarifa.
@ mambo yako hatakufa (Mithali 4:13)
@ Kutokulaumiwa na watu na kukuona hufai (Mithali 12:1)
@ Utapendwa na Mungu na kukutumia katika kazi yake (Hosea 4:6)

Mungu akubariki mpendwa.

Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Ameni.

Mt. Philbert Kazimoto- Kibondo.

Mtumikieni BWANA kwa furaha
17/04/2026

Mtumikieni BWANA kwa furaha

Address

Stand Mpya
Kibondo

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Free Anglican Church Kibondo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share