Mt Marko P. Kabanga

Mt Marko P. Kabanga Catholic church at the service of God's people

Kanisa Katoliki katika huduma ya watu wa Mungu

16/07/2026
26/04/2026

Shukrani baada ya watoto 266 kupewa kipaimara

Mambo ya Kipaimara Jumamosi 25/04/2026 katika adhimisho la Mt somo wa parokia
26/04/2026

Mambo ya Kipaimara Jumamosi 25/04/2026 katika adhimisho la Mt somo wa parokia

Maisha yanakuwa na maana na uzuri wa kweli pale tunapomfuata Kristo Yesu, kwani wito si mzigo bali ni mpango wake wa upe...
26/04/2026

Maisha yanakuwa na maana na uzuri wa kweli pale tunapomfuata Kristo Yesu, kwani wito si mzigo bali ni mpango wake wa upendo na furaha anaotushirikisha kila mmoja wetu. Katika Parokia, familia, na jumuiya za kitawa tunapaswa kuunda mazingira yanayoruhusu miito kuchanua, tukifahamu kuwa sote tunatembea pamoja k**a Jumuiya. Kuna umuhimu wa kusindikizana kidugu kwa sala kila mara ili kusaidia wale wanaopokea wito wa Mungu kuweza kuukubali kwa furaha na ujasiri. Dominka Njema!

Kristo Yesu anapoingia katikati yao anawauliza swali moja, “Ni maneno gani mnayosemezana hivi mnapotembea?” Yesu anawaul...
19/04/2026

Kristo Yesu anapoingia katikati yao anawauliza swali moja, “Ni maneno gani mnayosemezana hivi mnapotembea?” Yesu anawauliza Mnazungumza nini? Si kwa sababu hajui, bali ili kuwapa nafasi ya kutoa machungu, hofu, na majonzi yaliyokuwa yamejaa mioyoni mwao. Hii inatufundisha kuwa Kristo ni msikilizaji mkuu ambaye anataka tushiriki naye mahangaiko yetu ya kila siku. Kristo anakuja kwetu kila siku, anataka tumweleze yote yanayotusibu k**a hawa wanafunzi walivyomwelezea Yesu masikitiko, hofu, huzuni, kukata kwao tamaa. Kristo anakuja kwetu kila saa ya maisha yetu. Anatupa nafasi ya kumweleza yale yote tunayopitia katika maisha, huenda ni misiba, changamoto za maisha, migogoro ya familia, ni kukata tamaa, udhaifu wetu, mahangaiko yetu ya kila siku katika maisha nk. Ni kweli zipo nyakati tunapitia na hatuoni kabisa tumaini tena. Mara kwa mara katika misiba, katika changamoto kubwa tunaweza kuona namna huzuni inavyojaza mioyo yetu, wakati mwingine tunashindwa kuelewa Neno lolote. Kristo anataka tuseme naye, anatusikiliza. Dominika njema!

Address

Kabanga Mission
Kasulu
41

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mt Marko P. Kabanga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share