29/02/2024
NAMNA VIUNGO VINAWEZA KUKUFANIKISHA AU KUFUNGA MAFANIKIO YAKO.
Haleluya haleluya mtu wa Mungu, nakusalimu kwa jina la Yesu Kristo.
Karibu tujifunze neno la Mungu, leo Mungu ametupa kibali cha kujifunza kuhusu VIUNGO.
Adui anatumia viungo hivi hivi tulivyonavyo kuweza kuzuia hatima ya mtu, na Mungu anatumia viungo hivi hivi tulivyonavyo ili kuweza kumfanikisha mtu.
Viungo ambavyo tutaviangalia kwenye somo letu ni viungo vifuatavyo.
KICHWA, MIGUU NA MIKONO.
1. KICHWA.
Kichwa kinawakilisha hatima yako. Adui akitaka kushambulia hatima yako basi atashambulia kichwa chako.
Kichwa kimebeba viungo vingine k**a akili, macho, masikio na ulimi.
Kwahiyo ninaposema kichwa nimewakilisha na hivyo viungo vingine ambavyo vimeshikiliwa na kichwa.
Mhubiri 2:14 macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa.
Macho ya mwenye hekima yako kichwani mwake, macho ya mwenye hekima hakimbilii gizani, kichwa chenye akili nzuri hakikimbilii kutenda maovu, bali hukimbilia kwa Mungu mahali pa Nuru.
Zaburi 140:7 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu, Umenifunika kichwa changu siku ya vita.
Mungu asipokifunika kichwa , kichwa kinakosa nguvu, kichwa kinakosa kinga, kichwa kinavamiwa na kutumiwa na shetani atakavyo...
Mungu ni nguvu zetu sisi tulio katika Bwana, ametufunika vichwa vyetu tusienende katika Giza, ametufunika na nguvu za Roho Mtakatifu ili tuzidi kutulia nuruni na pendoni mwake...
Ndugu kichwa kikimkosa Mungu, kinampata shetani na mapepo yake, yaani muda wote kichwa kinawaza ulevi, kinawaza uzinzi na uasherati kwasababu hakijafunikwa na nguvu za Mungu bali kimefunikwa na giza (shetani) kwahiyo mawazo yatazunguka ya kishetani shetani tu, mawazo ya kumkosea Mungu na sio kumlingana Mungu wala kumsogelea Mungu.
Watu ambao vichwa vyao vimezungukwa na shetani muda wote wanawaza mambo ya gizani, ni tofauti kabisa na ambaye kichwa chake kimezungukwa na nguvu za Mungu, mtu aliyezungukwa na nguvu za Mungu atawaza muda wa MAOMBI, muda wa kusoma NENO LA BWANA, atawaza muda wa kukusanyika kumfanyia Mungu ibada. N.K.
MPENDWA KATIKA BWANA.
OMBA NGUVU ZA MUNGU ZIKIFUNIKE KICHWA CHAKO.
2. MIKONO
Mikono inawakilisha uwezo wa mtu kuzalisha (kuzaa)!
Kuna mikono ya aina mbili.
Kuna mikono ya baraka na mikono ya laana.
Mikono ya baraka ni mikono ambayo inauwezo wa kuzalisha.
Mikono ya laana ni mikono ambayo haina uwezo wa kuzalisha, ni mikono ya uharibifu.
Mikopo ya uharibifu huwa inategwa yaani mtu anategewa mikono ya uharibifu, kila anachogusa kinaharibiwa, au yaani hawezi kufanikisha jambo lolote zuri lazima tu ataliharibu.
Danieli 11:16 Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.
Na uharibifu utakuwa mkononi mwake, kwahiyo hii roho ya uharibifu ni mtu anasemewa na watu wengine kwamba uharibifu ukae katika mikono yake na hii ndio wengi wameangukiapo.
Mithali 3:16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
Shetani anajua siri iliyoko katika mikono, mikono inaweza kukupa maisha marefu au mafupi na mikono inaweza kukufanya masikini au tajiri.
Mkono wako wa kuume (kulia) kiroho unawakilisha wingi wa siku zako za kuishi na mkono wa kushoto unawakilisha utajiri na heshima.
Unaweza kukuta mtu anaota ndoto ameng'atwa na nyoka mkono wa kulia au kushoto, k**a umewahi kuota ndoto yoyote unang'atwa mkononi basi ujue shetani anawinda kati ya wingi wa siku zako za kuishi au utajiri na heshima unavyotakiwa kuvipata.
Katika mikono yako ndani yake kunaweza kukawa na mkono wa Mungu au mkono wa shetani, utajua kwa matokeo ya mikono yako.
Kutoka 17:11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
Mikono ya Musa iliwapa ushindi wana wa Israel, Musa akiinua mikono wana wa Israel wanashinda lakini akishusha mikono amaleki wanashinda, kwasababu ndani ya mikono ya Musa kulikuwa na mkono wa Mungu ambao uliwapa ushindi wana wa Israel.
Wachawi wanaweza kumloga mtu, badala ya kuwa na mkono wa baraka wa Mungu mtu anakuwa na mkono wa uharibifu na kutokufanikiwa.
Hii mikono ndio mikono ambayo Mungu anatumia pia kupitisha uzima, miujiza na uponyaji kwa watu wake.
Marko 16:18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Mikono ya watumishi wa MUNGU huwa imebeba mikono ya Mungu ndani yake.
Ndio maana watumishi wanaweza kuweka mikono yao kwa wagonjwa na wagonjwa wakapata afya.
K**a mtumishi wa Mungu amefungwa mikono yake hawezi kumuombea mtu akapona au kufunguka k**a amefungwa na pepo.
Mikono ya Musa ilitenda ajabu nyingi na ishara nyingi pale misri kwasababu ndani yake kulikuwa na mkono wa Mungu.
TORATI 34:11-12, KUTOKA 3;20.
OMBEA MIKONO YAKO IFUNGULIWE K**A IMEBEBA UHARIBIFU.
3. MIGUU.
MIGUU inawakilisha utawala au mamlaka yako.
Luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Tunakanyaga kwa miguu, maana miguu imebeba mamlaka.
Miguu inakupa kutawala, miguu inakupa mamlaka, nguvu zote za shetani NENO la Mungu linasema tutazikanyaga.
Maana yake ukikanyanga unakuwa juu yake, huwezi kukanyaga halafu ukawa chini ya ulichokikanyaga.
Warumi 16:20 Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.
Maana yake ni kwamba Mungu ametupa kumtawala shetani, shetani hawezi kuwa juu ya mtu aliyemuamini Mungu, hawezi kuwa juu ya mtu wa Mungu.
Zaburi 22:16 Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu.
Shetani akitaka kukuweza au akitaka kukuharibu atashughulika kwanza na kuizuia miguu yako, akiweza kuiongoza miguu yako basi shetani anakuwa amekushinda.
Ili akushinde anakufunga kwanza miguu, lakini Mungu naye akitaka kukuinua ataifungua kwanza miguu yako...
Naiamuru miguu yako ifunguliwe kwa jina la Yesu Kristo....
Kuna miguu mizuri na miguu mibaya pia.
MIGUU mizuri ni ipi???
Na
Miguu mibaya ni ipi???
Warumi 10:15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? K**a ilivyoandikwa, Ni mizuri k**a nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Miguu mizuri ni miguu inayopeleka habari njema kwa watu, miguu inapeleka habari za kufunguliwa kwa watu waliofungwa, habari za uponyaji kwa wagonjwa, Habari za kutuliwa mizigo ya dhambi.
Zaburi 8:6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
Mungu ameweka mamlaka ya vitu vyote katika miguu.
Kwahiyo Mungu akitaka kukupa kutawala anafungua miguu yako, miguu ikifunguka tayari umepewa vitu vyote chini yako.
MUAMBIE MUNGU AKUFUNGUE MIGUU YAKO UTAWALE....
Katika ulimwengu wa Roho unaweza kuwa na mguu unaoteleza, mguu ambao hauwezi kutunza vitu au watu.
Zaburi 17:5 Nyayo zangu zimeshik**ana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa.
Hold up my goings in thy paths, that my footsteps slip not.
2 Samweli 22:37 Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.
Thou hast enlarged my steps under me; so that my feet did not slip.
Nyayo zako zishik**ane na Mungu, zisiteleze kwa jina la Yesu Kristo.
Umebarikiwa.
Ev. Joseph Kidifu Jr
Kutoka Nyikani.