Pastor Ezekiel Jr

Pastor Ezekiel Jr The Christ's ambassador to all nation

19/12/2025

# Vijana wa Yesu kazini Pastor Ezekiel Jr

19/12/2025

Anarejesha kilichopotea wakati ule wa dhorubaaa

19/12/2025

ASANTE YESU KWA KUNIFIKISHA DESEMBA NIKIWA SALAMA NI KWA MKONO WAKO TU 🙏🙏🙏

19/12/2025

Wala hapana jina jingine tulilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa ni jina lake Yeau kristo Bwana wetu aliyepigwa msalabani

Oktoba 2 hadi 5 paleeee ISAGEHE-KAHAMA
14/09/2025

Oktoba 2 hadi 5 paleeee ISAGEHE-KAHAMA

1 Samweli 1:10-20 (KJV)   Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana. Akaweka nadhi...
24/04/2025

1 Samweli 1:10-20 (KJV) Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.
Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.
Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za Bwana, Eli akamwangalia kinywa chake.
Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana k**a anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana.
Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa.
Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka.
Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.

Bwana amekutia mafuta usijidharau hivyo ulivyo maana yeye haangalii k**a wanadamu waangaliavyo simama kwenye nafasi yako...
05/04/2025

Bwana amekutia mafuta usijidharau hivyo ulivyo maana yeye haangalii k**a wanadamu waangaliavyo simama kwenye nafasi yako na utumike k**a ipasavyo jifunze kuwa shujaa na hodari k**a Daudi

1 Samweli 16:1-13 (KJV) Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.
Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu.
Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako.
Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?
Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu.
Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.
Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii k**a binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.
Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu.
Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu.
Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.
Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

Twende tuhubiri pamoja watu waokolewe katika Jina la Yesu kristo aliye hai
27/01/2025

Twende tuhubiri pamoja watu waokolewe katika Jina la Yesu kristo aliye hai

26/01/2025

Address

472
Kahama

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pastor Ezekiel Jr posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share