TAG Betheli Deliverance Church-Sofi Kahama Tanzania

TAG Betheli Deliverance Church-Sofi Kahama Tanzania KWA SASA NATUMIKA KAGONGWA TAG VICTORY TEMPLE ,NABADILI PAGE HII KUTOKA ILIVYOKUWA MWANZO..

‎‎ SOMO:-   UWEZO‎ANDIKO:- ISAYA 43:2‎                   Upitapo katika maji mengi ‎                   nitakuwa pamoja n...
20/10/2025


‎ SOMO:- UWEZO
‎ANDIKO:- ISAYA 43:2
‎ Upitapo katika maji mengi
‎ nitakuwa pamoja nawe;
‎ na katika mito,
‎ haitakugharikisha;
‎ uendapo katika moto,
‎ hutateketea; wala mwali
‎ wa moto hautakuunguza.

‎ KIINI- UWEZO WA KUKABILIANA NA
‎ NYAKATI NGUMU

‎(I) UTANGULIZI
‎ Kila binadamu hupitia vipindi viwili
‎ maishani:

‎(a) KIPINDI CHA MAFANIKIO NA
‎ FURAHA

‎(b) KIPINDI CHA MAJARIBU NA
‎ MACHUNGU.

‎ONA:-
‎-Siri si kuepuka nyakati ngumu, bali kujua namna ya kuzishinda.

‎-Isaya anatukumbusha jambo kuu: Mungu hakusema hatutapitia majini, bali amesema “nitakuwa pamoja nawe unapopita.”

‎-Hii ndiyo nguvu ya waamini si kukosa misukosuko, bali kuwa na Mungu ndani yake.

‎(II) NYAKATI NGUMU SI ISHARA YA
‎ KUSHINDWA

‎-Watu wengi wanapopitia magumu hudhani Mungu amewaacha, kumbe Mungu yupo kazini.

‎-Ndugu wa Yusufu walitaka kuua ndoto yake , akauzwa utumwani lakini huko ndiko alipopandishwa cheo; Mwanzo 50:20 “Ninyi mlikusudia mabaya juu yangu, lakini Mungu alikusudia mema.”

‎-Danieli aliingia kwenye tundu la simba, si kwa sababu Mungu hakuwepo, bali ili ulimwengu ujue kwamba Mungu anaokoa.

‎Ukweli wa Kuchukua:-
‎Kila mtihani una nafasi ya ushuhuda. Mungu anatumia nyakati ngumu kutengeneza nguvu mpya ndani yako.

‎(III)- NAMNA YA KUKABILIANA NA
‎ NYAKATI NGUMU

‎1. KAA IMARA KWENYE NENO LA MUNGU
‎Mathayo 7:24–25 “Kila asikiaye maneno haya na kuyatenda ni k**a mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba juu ya mwamba.”

‎ONA:-
‎-Upepo unapovuma, Neno ndilo
‎ mwamba.
‎-Usijenge imani yako juu ya hisia,
‎ jenga juu ya ahadi za Mungu.

‎2. OMBA HATA K**A HAUONI MAJIBU MARA MOJA

‎ONA:-
‎-Maombi hayambadilishi Mungu, lakini yanambadilisha mtu anayeomba;
‎Luka 18:1 “Wapaswa kuomba siku zote wala wasikate tamaa.”

‎-Mungu anapochelewa, hajachelewa anakutayarisha.

‎3. USIRUHUSU HOFU ITAWALE
‎-Shetani hupenda kutumia hofu kukupofusha usione wokovu.
‎2 Timotheo 1:7 “Kwa maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.”

‎-Usikubali sauti ya hofu izime sauti ya matumaini.

‎4. ZUNGUKWA NA WATU WENYE
‎ IMANI
‎-Kuna nguvu katika ushirika sahihi.
‎Mhubiri 4:9–10 “Afadhali wawili kuliko mmoja; maana wakiporomoka, mmoja atamwinua mwenzake.”

‎-Wakati mwingine unahitaji tu mtu wa kukushika mkono na kukuambia, “Utafanikiwa!”

‎(IV)- KILA JARIBU LINA KUSUDI LA
‎ KIFALME

‎ONA:-
‎-Kabla ya taji, kuna vita.

‎-Kabla ya ushuhuda, kuna maumivu.
‎Warumi 8:28 “Tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao kwa mema.”

‎-Mungu anaweza kutumia magumu uliyonayo leo kuwa daraja la kukuinua kesho.

‎Note:-
‎-Kuna nyakati Mungu anaondoa dhoruba;
‎-lakini mara nyingine anamsaidia baharia aweze kuvuka mawimbi salama

‎(V)- KUMBUKA
‎-Nyakati ngumu si mwisho wako, ni mwanzo wa sura mpya ya ushindi.

‎-Mungu anasema leo: “Usiogope, nitakuwa pamoja nawe.”

‎-Uwezo wa kukabiliana na nyakati ngumu upo ndani yako kwa sababu Roho Mtakatifu anakaa ndani yako.
‎Zaburi 30:5.... “Kilio cha usiku ni cha muda mfupi, lakini furaha huja asubuhi.”
‎By.
‎Rev.Missionary Emmanuel F.Kitaly
‎(CHINI YA KANISA LA TAG VICTORY KAONGWA MJI MWEMA)
‎👇 Bonyeza viungo hapa chini kuungana nami moja kwa moja:
‎📺 YouTube:
‎👉 Rev. Missionary Emmanuel F. Kitaly
‎📘 Facebook (Page/Share):
‎👉 Jiunge / Share Posts
‎👉 Rev. Missionary Emmanuel F. Kitaly
‎💬 WhatsApp Group:
‎👉 Jiunge na Victory Mission Global
‎📞 Kwa Ushauri, Maombi na Maombezi
‎📲 +255 754 478 929
‎Kwa Ushuhuda,Sukrani,Sadaka,kuwezesha huduma.+255754478929
‎LIPA NAMBA VODA - 51260374
‎( JINA- EMMANUEL KITALY)

‎VICTORY MISSION GLOBAL (VGM)

10/10/2025

‎SHALOM,UCHAMBUZI NO.1 SOMO LA SIRI.

‎SOMO: SIRI
‎ANDIKO: Isaya 29:15

‎ “Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?”

‎📖 Tafsiri ya Kibiblia ya Neno “SIRI”

‎👉 Kiebrania: sôd
‎Maana yake ni eneo la faragha au mashauriano ya karibu kati ya Mungu na wale wanaomcha.
‎Hapa “siri” haimaanishi kitu cha uovu bali ushirikiano wa kipekee kati ya Mungu na mtu wake.

‎👉 Kigiriki: mystērion
‎Maana yake ni siri ya Mungu iliyofichuliwa kwa walio wake.
‎Yesu alisema:

‎NOTE:-
‎TAFSIRI YA KISWAHILI YA NENO “SIRI”
‎🔹 Asili: Neno “Siri” limetoka katika Kiarabu, likiwa na maana ya jambo ambalo mtu hatawi wengine wajue.
‎🔹 Maana ya kawaida: Ni jambo au habari inayofichwa kwa makusudi kwa sababu za usalama, heshima, au uhai.
‎🔹 Umuhimu: Kila mtu ana haki ya kuwa na siri zake — iwe katika maisha binafsi, kifamilia, au kijamii.

‎📌 KUMBUKA: Kuna siri njema (zinazolinda heshima na utu) na siri mbaya (zinazoficha uovu au dhambi).

‎👉"HIVYO ILI ULIELEWE SOMO HILI SHARTI UJUE AINA HIZO MBILI ZA TAFSIRI"

‎“Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.”
‎(Mathayo 13:11)

‎🔑 Hivyo basi:
‎Siri ya Mungu si kitu cha kufichwa kwa wacha Mungu, bali ni ufunuo wa kina anaoutoa kwa wale wanaomcha.

‎🔑 Yote tunayohitaji Kwa Bwana Yapo katika neno lake (Siri za Ufalme)Tukilifahamu Neno tutazijua siri zake na kupokea kila tunachoitaji, K**a kuhusu Ahadi, ulinzi,baraka,uponyaji,Neema,wokovu,
‎N.k

‎ “Siri ya BWANA iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake.”
‎(Zaburi 25:14)

‎💡Mungu hufunua siri zake kwa watu wanaokaa karibu naye — si kwa wanaotaka kwa maslahi yao binafsi wala kwa udadisi kisha wasiwe na kusudi la Mungu ndani, bali wanaotafuta utakatifu.
‎👉 Siri za Mungu hazipatikani kwa akili, bali kwa uhusiano wa kiroho.
‎Kila unapokaribia Mungu, unafunguliwa siri zaidi kuhusu maisha, huduma, na hatima yako.

‎🎯 Je, wewe unamkaribia Mungu kiasi cha kusikia siri zake?
‎Je,unapenda ibada,kumtolea,kumtii?
‎Maombi yako si ya kuuliza tu, bali ya kusikiliza yale anayotaka kukufunulia.

‎🕊️“Mungu hawezi kuficha siri zake kwa wampendaye; huzificha kwa wasiompenda/Wenye dhambi”
‎Tubu,Okoka,jiunge na kanisa lenye kukiri wokovu na Tafuta nafasi ya utulivu kila siku, kaa kimya mbele zake, na uanze kusikia kile macho hayajaona, wala masikio hayajasikia(Siri za Ufalme wa Mungu)

‎NOTE:-
‎ SIRI ya BWANA iko kwao wamchao!
‎Usitamani kujua mambo ya watu — tafuta kujua mambo ya Mungu!
‎Kadri unavyomkaribia Mungu, ndivyo anavyokufunulia siri za maisha yako.
‎📖 Zaburi 25:14 | Mathayo 13:11

‎By.
‎Rev.Missionary Emmanuel F.Kitaly
‎(CHINI YA KANISA LA TAG VICTORY KAGONGWA MJI MWEMA)
‎Kwa ushauri maombi na maombezi
‎+255754478929
‎Kwa Sadaka na kuwezesha huduma
‎+255754478929
‎LIPA NAMBA VODA - 51260374
‎( JINA- EMMANUEL KITALY)

‎VICTORY MISSION GLOBAL (VGM)

09/10/2025

‎🔑 Somo:- Siri
‎🔑 Andiko:- Isaya 29:15 Ole wao
‎ wanaojitahidi
‎ kumficha BWANA
‎ mashauri yao, na
‎ matendo yao yamo
‎ gizani, nao husema,
‎ Ni nani atuonaye?
‎ Nani atujuaye?
‎🔑 Kiini:- Siri-Ambazo Wanadamu
‎ Huwa Nazo na
‎ Huzificha

‎Utangulizi:-
‎Kila mwanadamu hubeba siri fulani moyoni mwake. Baadhi ya siri ni za faraja na heshima, nyingine ni za uchungu na maumivu, na nyingine ni za giza. Biblia, maisha ya kila siku, na hata sayansi ya nafsi (psychology) zinatufundisha kuwa siri ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.

‎{I} TAFSIRI YA KIBIBILIA YA NENO “SIRI”
‎ LINATUMIKA KWA MAANA TOFAUTI:-

‎(A)-Kiebrania: sôd – hufasiriwa k**a “mshauri wa karibu” au “eneo la faragha la kusikia mambo yaliyofichwa.”

‎(B)-Kigiriki: mystērion – maana yake “siri ya Mungu iliyofichuliwa kwa walio wake.”

‎Mathayo 13:10-12
‎Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
‎[11]
‎Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
‎[12]
‎Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

‎NOTE:-
‎HIVYO TAFSIRI YA KIBIBILIA MAANA YA NENO SIRI-
‎Ni mambo yaliyofichwa, yasiyo wazi kwa kila mtu (Kwa wasio Amini hayajulikani)
‎aIla Kwa wana wa ufalme hakuna cha kuwaficha yeye Bwana Huwafunulia
‎(Zab 25:14 Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.)

‎{II} TAFSIRI YA KISWAHILI YA NENO “SIRI”
‎ LINA MAANA TOFAUTI NA ILE YA
‎ BIBILIA:-
‎- SIRI (kutoka neno la Kiarabu)
‎ ni jambo lolote ambalo mtu analiona haifai kumshirikisha mtu yeyote yule, haijalishi ni nani, Pengine siri ni suala la uhai au kifo, Kila mmoja ana haki ya kuwa na siri zake ,Katika maisha ya jamii, siri ni muhimu, kiasi kwamba ni wajibu kuwa na siri katika nyanza zote n.k.

‎NOTE:-
‎KUMBUKA KUNA SIRI NZURI NA SIRI MBAYA.

‎ Hebu tuangalie makundi makuu ya siri ambazo wanadamu huwa nazo na huzificha:

‎1️⃣ Siri za Dhambi na Aibu

‎Mfano wa Kibiblia: Adamu na Hawa walipoanguka dhambini walijificha (Mwanzo 3:7-10).

‎Tabia yake: Watu hubeba siri za dhambi walizotenda, mapungufu yao, au mambo yanayowaletea aibu.

‎Sababu ya kuficha: Hofu ya kushutumiwa, kudharauliwa au kukataliwa.

‎Leo hii: Ni maisha ya “double life” – kuonekana wema hadharani lakini moyoni wakijua kuna uovu.

‎2️⃣ Siri za Maumivu na Majeraha ya Nafsi

‎Mfano wa Kibiblia: Hanna alipokuwa tasa alilia kwa uchungu moyoni mwake (1 Samweli 1:10-13).

‎Tabia yake: Watu hubeba siri za majeraha ya moyo, kukataliwa, unyanyasaji, au trauma walizopitia.

‎Sababu ya kuficha: Hofu ya kuchekwa au kutoeleweka.

‎Leo hii: Wengi wana depression, stress, au huzuni ya ndani wasiyoisemea.

‎3️⃣ Siri za Ndoto, Maono na Mipango

‎Mfano wa Kibiblia: Yosefu aliposhiriki ndoto zake ndugu zake walimchukia (Mwanzo 37:5-11).

‎Tabia yake: Watu mara nyingi huamua kuficha mipango yao ya baadaye kwa sababu ya wivu au hujuma.

‎Sababu ya kuficha: Kulinda maono yao yasiharibiwe au kukatishwa tamaa.

‎Leo hii: Mtu husema, “mpango wangu ataona tu matokeo, si maneno.”

‎4️⃣ Siri za Utambulisho na Hali Halisi

‎Mfano wa Kibiblia: Nikodemo alimwendea Yesu usiku (Yohana 3:1-2).

‎Tabia yake: Watu huficha historia zao, uhusiano wao, hali ya kifedha, au mapambano ya ndani.

‎Sababu ya kuficha: Heshima ya kijamii au hofu ya kupoteza cheo.

‎Leo hii: Wengine husema hadharani wanastahimili, kumbe moyoni wanapambana na madeni, magonjwa, au doa la kifamilia.

‎5️⃣ Siri za Nguvu, Karama na Uwezo

‎Mfano wa Kibiblia: Maria aliposikia maneno ya malaika aliyatunza moyoni na kuyatafakari (Luka 2:19).

‎Tabia yake: Watu hujua wamepewa kipaji au karama, lakini huamua kukaa kimya wakisubiri wakati wa Mungu.

‎Sababu ya kuficha: Hekima na kusubiri majira sahihi.

‎Leo hii: Kuna watu wana vipaji vikubwa lakini havionekani kwa sababu hawajavifunua.

‎6️⃣ Siri za Giza na Uovu
‎Mfano wa Kibiblia: Achan alificha vitu vilivyolaaniwa ndani ya hema yake (Yoshua 7:20-21).

‎Tabia yake: Watu wengine hubeba siri za uchawi, ushirikina, tamaa au maovu ya ndani.

‎Sababu ya kuficha: Hofu ya hukumu na matokeo ya kisheria au kijamii.

‎Leo hii: Kuna siri za uovu ambazo watu hufunika kwa jina la heshima, lakini huathiri familia na taifa.

‎✅ Hitimisho

‎Kwa ufupi, siri kubwa wanadamu huzificha mara nyingi ni:

‎1. Dhambi na aibu

‎2. Majeraha ya nafsi

‎3. Mipango na ndoto

‎4. Utambulisho au hali halisi

‎5. Nguvu na karama

‎6. Uovu na giza lililofichwa

‎Kila siri huathiri mwenendo wa mtu: zingine huchangia ukuaji na mafanikio (k**a siri za maono na karama), lakini zingine huumiza nafsi na jamii (k**a siri za dhambi na uovu).

‎NOTE:
‎(-Somo hili nitarudi kulichambua kila eneo kwa kina tena hivyo ukiwa na swali au kuhitaji maombo kwa yale Mungu amekugusa nipo tayari kukuhudumia katika jina la Yesu.
‎Usisite kuwasiliana nami kwa ushauri zaidi.)

‎By.
‎Rev.Missionary Emmanuel F.Kitaly
‎Kwa ushauri maombi na maombezi
‎+255754478929
‎Kwa Sadaka na kuwezesha huduma
‎+255754478929
‎LIPA NAMBA VODA - 51260374
‎( JINA- EMMANUEL KITALY)

‎VICTORY MISSION GLOBAL (VGM)

KARIBU SANA
08/05/2024

KARIBU SANA

14/03/2024

Address

Kahama
S.L.P576

Telephone

+255754478929

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TAG Betheli Deliverance Church-Sofi Kahama Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to TAG Betheli Deliverance Church-Sofi Kahama Tanzania:

Share