EAGT Gethsemane-Dodoma-Kahama

EAGT Gethsemane-Dodoma-Kahama Ni Kanisa la Mungu lenye lengo la kuwaleta watu kwa Yesu, na kuyaishi maisha matakatifu, lipo Kahama.

09/03/2024

KESHO NI SIKU YA IBADA, ANDAA MOYO WAKO KWAAJILI YA KUMTAFAKARI MUNGU JUU YA MATENDO YAKE MAKUU KWAKO USIKOSE IBADA!

  2:19
08/03/2024

2:19

21/09/2022

SOMO:-TAKA HATI YA MAKABIDHIANO HATA K**A UMEPEWA KITU BURE,USIJEJUTA SIKU MOJA.
Kutoka 1:8-11 & Esta 8:1-8

📜Bwana Yesu asifiwe sana mtumishi wa Mungu aliyehai,habari ya uzima.Naomba nikukaribishe katika somo letu linaloendelea lisemalo TAKA HATI YA MAKABIDHIANO HATA K**A UMEPEWA KITU BURE,USIJEJUTA SIKU MOJA.

✞︎Nikweli kabisaa katika maisha haya tunayoishi,watu wengi wamepateza nguvu zao kwa kunyang'anywa haki yake kisa tuu alipewa bila maandishi,utasikia "hapa palikuwa pakwetu wewe hauna haki,hata k**a umejenga nyumba wewe bomoa tuu sisi tunachokitaka ni ardhi yetu" na wakati huo unakumbuka wakati unapewa ile ardhi uliambiwa umepewa k**a sehemu ya familia.

✞︎Neno la Mungu linaeleza habari za Yusufu alivyoishi Misri k**a mwenyeji wa Misri na jinsi alivyokabidhiwa kila kitu na ndugu zake wakahamia kwenye ile ardhi na kugawiwa ardhi ya kukaa na kutunzia mifugo,lakini kwa bahati mbaya Yusufu hakukuwa na maandishi ya kuonesha siku ikitokea hitilafu itakuja kukusaidia ile hati ya umiliki wa ardhi.Neno linasema "akainuka mfalme mpya asiye mjua Yusufu,Kutoka 1:8 na hili ndilo linalowatesa wengi unakuta baba au mama alipoishi mahali fulani alipewa kila kitu pasipo maandishi,sasa changamoto inakuja kutokea ni pale ambapo wanaozaliwa hawayatambui makubaliano yenu,hapo ndipo kazi huanzia.
🔥 Kutoka 1:8-11
[8]Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
[9]Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.
[10]Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashik**ana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.
[11]Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

🔥Kuna watu walipewa viwanja ,magari,nk.pasipo maandishi,pasipo kutarajiwa walijikuta wananyang'anywa haki zao.

🔥Mtu mmoja alipewa shamba alime mpunga,akapewa na pori la kulisafisha ili kuongezea eneo la kilimo,na aliambiwa atalima bure kwa miaka kadhaa lakini siku alipoliandaa shamba vizuri ndio siku aliyempa shamba alipolihitaji.

🔥Esta 8:8
[8]Basi waandikieni Wayahudi pia vyo vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua.

🔨JIFUNZE KWA CHOCHOTE UNACHOAMBIWA UMEPEWA NA RAFIKI,JIRANI,NK.KASORO MZAZI HAO WENGINE WOTE AKITAKA KUKUPATIA KITU ,MSHAURI MUANDIKIANE.

🔥UKITAKA UAMINI HILI NENDA KAWAULIZE WALE WALINYANG'ANYWA HAKI ZAO, UTAGUNDUA SABABU KUU NI KWAMBA HAKUKUWA NA HATI YEYOTE NA KUTOKULIPA.

Yesu umempata rafiki wa kweli.

Mbarikiwe Sana na Bwana.

CREDIT BY Mwl.Lutango Mwilongo

06/07/2022

SOMO:-MUNGU AKIKUITA KATIKA HUDUMA UFANYE NINI?
(Hatua za kufuata) Kutoka 3:1-4

📜Bwana Yesu Kristo asifiwe sana,habari ya uzima mtumishi wa Mungu popote pale unapoendelea kujifunza maarifa haya,nasema hivi" MUNGU wa mbinguni akubariki sana.

📜Neno la Mungu linasema katika ile Luka 24:45"Ndipo akawafunulia akili zao wakapata kuelewa na maandiko"naomba ukiwa katika kujifunza somo hili mwombe sana Mungu akufunulie akili upate kile alichokikusudia ukipate katika somo hili.Nivema sana ukafuatilia toka mwanzo wa darasa letu ndipo utajua nini Roho wa Mungu anataka ujifunze.

📜Nakumbuka mwanzo wa somo letu tuliona yakuwa kuna utofauti kati ya KUITWA na KUTUMIKA,ukiitwa haimaanishi unatakiwa utumike,kabla ya kuambiwa yakupasayo unapaswa kusikiliza aliyekuita anasema nini? Yaani ni nini kusudi la kukuhitaji? Tuliona yakwamba mara nyingi watu wamepoteza mwelekeo wa huduma na wengine wameua huduma zao kwa sababu ya kutokuwa tayari kusikiliza na kufuata maelekezo ya aliyekuita.Jaribu kuwaza unafanya huduma ya uchungaji na umekabidhiwa ofisi ya kichungaji halafu Mungu kwenye orodha yake anaona unachokifanya sicho alichokuita na k**a hauamini naomba jifunze habari za Paulo katika ile Matendo ya mitume 13:1-3 unakuja kugundua kuwa kazi ya Mungu haifanywi kwa kufuata mkumbo bali hufanywa sawasawa na wito ulioitiwa katika utumishi inamaana k**a ni mchungaji unatakiwa ufanye katika ofisi ya kichungaji na k**a ni mwalimu tambua kuwa katika ofisi yako wapo watu wanakusubiri uwahudumie na kwenye orodha ya Mungu ujira wako unakuwa katika ofisi aliyokupangia na sio ile uliyojipangia.K**a unafikiri natania nenda kafungue huduma na uanze kuchunga na wakati huo Mungu kakuita kwenye uinjilisti,my friend ukiona watu wanabarikiwa utahisi sio bure kumbe tatizo ni ofisi sio yako,baraka zako zilipo na ndipo wito wako ulipo.

📜Naomba nisiendelee kuchambua sana naomba leo tuangalie kitu kingine cha kuzingatia ukiitwa kwenye huduma:-
📃MWOMBE MUNGU AJIFUNUE KWA UPYA K**A NI YEYE KWELI ALIYEKUITA.
Ndiyo katika huduma licha ya kujiridhisha kwa habari ya kuisikia sauti ya Mungu kupitia neno lake au maono,ndoto na mazingira,nk.ni vema umuombe Mungu akupe uthibitisho tena k**a niyeye aliyekuita au ni shetani anataka kukupoteza na kuua huduma yako.

✞︎Kuwa makini sana na majibu ya ndoto au maono,kumbuka hata shetani anauwezo wa kukupa mafunuo ili upotee,mfano unakuta unawito ndani yako ghafla moto wa Roho Mtakatifu unawaka ndani yako juu ya huduma,shetani huwa anauwezo kipindi k**a hicho kukupoteza kabisaa kwenye uso wa huduma na usijulikane kabisaaa.Naomba nikupe ushuhuda wa mtu mmoja aliyekuwa mchawi kabla hajampa Yesu maisha yake anasema alikuwa akigundua mtu fulani anahuduma kitu cha kwanza wanampa wazo la kuhama kanisa,kumbuka k**a maksai anayeongoza kwa ngumi kwenye kundi fulani siku akienda k***a jipya huwa anapigwa hata na ng'ombe wadogo tambua kuwa mafuta ya madhabahu hii ukiondoka k**a si Mungu aliyekuambia uondoke lazima upako utaondoka unaanza kutafuta mafuta mapya tena,sasa wakati unaaza kutafuta mafuta mapya na k**a si Mungu aliyekuambia uhame lazima utayumba tuu na ukishayumba wanafunga connection ya kukubalika na usipojiangalia mwisho wa siku unaamua kuwa mchungaji kumbe Mungu alikuita k**a mtume.

📜Na shetani akishagundua unataka kuvuka ng'ambo anauwezo wa kukuletea mafunuo kuwa fanya hiki,usipokuwa makini kujua nani kaongea hii sauti unaweza kujikuta umepoteza mwelekeo kabisaa.

🛠️NOTE:-NAOMBA NISEME SI KILA ALIYEHAMA KANISA AMEKOSEA HAPANA,NAOMBA NIELEWEKE VIZURI SANA PIA SIJASEMA KILA MTU ANAYEFUNGUA HUDUMA MPYA ANAKUWA KAKOSEA,HAPANA NAOMBA NIRUDIE TENA KUSEMA HIVI MUNGU AMETUPA MAARIFA TUJUE TUNAMSHINDAJE ADUI,BARIKIWA SANA🤝

📜Naomba nikwambie pia ukiwa katika kumuuliza Mungu ajifunue,kuwa makini sana na wale utakaowashirikisha kwa maana unaweza jikuta unapewa ufunuo usipokaa vizuri unatoka njee ya reli,tamani sana Mungu aseme nawewe zaidi kuliko mtu mwingine.

☕USHUHUDA,Mtumishi mmoja alikuwa anatakiwa kwenda kusuliluhisha kesi iliyodumu kwa miaka kadhaa kati ya mama mmoja na mtoto,ni kesi iliyokuwa haina suluhu miaka mingi.Sasa huyu mtumishi akawa amealikwa pia asaidie angalau mama na mtoto wapatane,nasi mtumishi kabla ya kwenda ilibidi awashirikishe watumishi wenzake kwamba wamkumbuke kwenye maombi maana siku inayofuata anatakiwa kwenda kutatua hilo tatizo basi wakakubaliana kumuombea,basi siku ilipofika asubuhi yake kabla hajaondoka mapema sana mtumishi mwenzake akamwambia" Mungu kaniambia usiende,amenionesha mambo mabaya sana yatakupata ukienda kwahiyo usiende maana Bwana amesema"lakini huyu mtumishi moyoni mwake akaona amani na anaruhusiwa kwenda basi akaenda.Kufika kule Mungu alijifunua kwa viwango vya juu na Mungu akawa amesaidia kurekebisha lile tatizo.USITAKE MAONO YA WATU YAKUPELEKE KWENYE HATMA YAKO,WENGINE NI WATAKUUZA USIPOANGALIA.

📜Naomba tusome habari hii ya Musa.Kutoka 3:1-4"
[1]Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
[2]Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
[3]Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
[4]BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa."

☕HONGERA SANA NAOMBA KWA LEO TUISHIE HAPA,TUONANE KIPINDI KIJACHO KWA SEHEMU YA 7 ,BARIKIWA SANA.

06/07/2022

JUHUDI ZA MAKUSUDI SHARTI ZIFANYWE DHIDI YA DHAMBI

Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima; bali maonyo hukosa. Mithali 10:17.

📚 Wengi wanaomba radhi kwa udhaifu wao wa kiroho, kwa mlipuko wa yeye aachaye shauku zao, kwa ukosefu wa upendo wanaouonesha kwa kaka na dada zao. Wanahisi hali ya kutengwa na Mungu, utambuzi wa utumwa wao kwa nafsi na dhambi; lakini shauku yao ya kufanya mapenzi ya Mungu inategemea mwelekeo wao wenyewe, sio katika usadikisho wa ndani na wa kina wa Roho Mtakatifu. Wanaamini kuwa sheria ya Mungu ni ya lazima kutiiwa; lakini wao, kwa nia ya shauku ya nafsi zilizofanya uamuzi thabiti hawatendi sawasawa na sheria hiyo. Wanakiri kuwa Mungu anapaswa kuabudiwa na kupendwa sana, lakini Mungu hayuko katika mawazo yao yote. Wanaamini kuwa kanuni zinazoamuru upendo kwa wengine zinapaswa kuzingatiwa; lakini wanawatendea rafiki zao kwa kutojali kabisa, na wakati mwingine kwa udhalimu. Kwa namna hiyo wanaiacha njia ya kupenda utiifu. Hawafanyi kazi ya kutubu inavyostahili. Hisia ya makosa yao inapaswa kuwaongoza kumtafuta Mungu kwa bidii zaidi kwa ajili ya uwezo wa kumfunua Kristo kwa wema na uvumilivu.

📚 Jitihada nyingi za matengenezo ya kushtukiza zinafanywa, lakini wale wanaofanya jitihada hizi hawajikani nafsi. Hawajitoi kikamilifu katika mikono ya Kristo, ili kutafuta nguvu ya uungu kuwawezesha kuyatenda mapenzi Yake. Hawako tayari kufinyangwa kwa mfano wa Mungu. Kwa ujumla wao wanakubali kutokukamilika kwao, lakini dhambi fulani fulani hazijaachwa. "Tumefanya mambo ambayo hatukupaswa kuyafanya," wanasema, "na tumeacha kuyafaya mambo tuliyopaswa kuwa tumeyafanya." Lakini matendo yao ya ubinafsi, yanayomchukiza sana Mungu, hayaonekani katika nuru ya sheria Yake. Toba kamili haioneshwi kwa ushindi ambao nafsi imeupata.

📚 Adui anapenda kuwa juhudi hizi za kushtukiza zifanywe; kwa wale ambao wanawafanya kujiingiza kwenye vita isiyopangwa dhidi ya uovu. Kana kwamba ulevi ubembelezao unawekwa katika akili zao, na katika kujitosheleza kwao wanafanya mwanzo mpya wa kufanya mapenzi ya Mungu.

🔘 Lakini sadikisho la jumla la dhambi halileti matengenezo. Tunaweza kuwa na hisia isiyoeleweka, na isiyokubalika ya kutokukamilika kwetu, lakini hii haitatusaidia chochote tusipofanya juhudi madhubuti ili kupata ushindi dhidi ya dhambi. Ikiwa tunatamani kushirikiana na Kristo, ili kushinda k**a Alivyoshinda, tunalazimika, kwa uweza Wake, kudhamiria kufanya upinzani zaidi dhidi ya nafsi na ubinafsi.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
📚📚

††††††††††††††††††††††††††††††

DECIDED EFFORTS MUST BE MADE AGAINST SIN

Whoever heeds instruction is on the path to life, but one who rejects a rebuke goes astray. Proverbs 10:17, NRSV.

📚 Many apologize for their spiritual weakness, for their outbursts of passion, for the lack of love they show their brethren and sisters. They feel a sense of estrangement from God, a realization of their bo***ge to self and sin; but their desire to do God's will is based upon their own inclination, not upon the deep, inward conviction of the Holy Spirit. They believe that the law of God is binding; but they do not, with the eager interest of judgment-bound souls, compare their actions with that law. They admit that God should be worshiped and loved supremely, but God is not in all their thoughts. They believe that the precepts which enjoin love to others should be observed; but they treat their associates with cold indifference, and sometimes with injustice. Thus they walk away from the path of willing obedience. They do not carry the work of repentance far enough. The sense of their wrong should lead them to seek God most earnestly for power to reveal Christ by kindness and forbearance.

📚 Many spasmodic efforts to reform are made, but those who make these efforts do not crucify self. They do not give themselves entirely into the hands of Christ, seeking for divine power to do His will. They are not willing to be molded after the divine similitude. In a general way they acknowledge their imperfections, but the particular sins are not given up. “We have done the things we ought not to have done,” they say, “and have left undone the things we ought to have done.” But their acts of selfishness, so offensive to God, are not seen in the light of His law. Full contrition is not expressed for the victories that self has gained.

📚 The enemy is willing that these spasmodic efforts should be made; for those who make them engage in no decided warfare against evil. A soothing plaster, as it were, is placed over their minds, and in self-sufficiency they make a fresh start to do the will of God.

🔘 But a general conviction of sin is not reformative. We may have a vague, disagreeable sense of imperfection, but this will avail us nothing unless we make a decided effort to obtain the victory over sin. If we wish to cooperate with Christ, to overcome as He overcame, we must, in His strength, make the most determined resistance against self and selfishness.

MAY GOD BLESS YOU ABUNDANTLY

BWANA YESU ASIFIWE.SWALI: Wana wa Asafu ni akina nani katika biblia? JIBU:Kabla ya kuwafahamu wana wa Asafu, ni vizuri k...
06/07/2022

BWANA YESU ASIFIWE.

SWALI: Wana wa Asafu ni akina nani katika biblia?

JIBU:Kabla ya kuwafahamu wana wa Asafu, ni vizuri kumfahamu Asafu mwenyewe alikuwa ni nani.

Asafu alikuwa ni mmoja wa walawi ambao, mfalme Daudi alimuweka k**a kiongozi wa mbele wa sifa, atakayesimama mbele ya sanduku la Mungu daima kumsifu Mungu. (Soma 1Nyakati 6:31-32, 39).

1 NYAKATI: MLANGO 16

1 Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana.

3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.

4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;

5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;

Kulingana na maandiko, biblia inasema huyu Asafu hakuwa tu mwimbaji, bali Mwonaji pia,

2Nyakati 29:30 “Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie Bwana sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu”.

Baadaye, uzao wake uliendeleza nyayo zake, na wote wakawa waimbaji katika hekalu la Mungu lililokuja kujengwa baadaye, na hata baada ya ule uhamisho wa Babeli, waliporudi bado waliweza kuwekwa katika kazi hiyo hiyo ya Sifa..

Soma, Ezra 2:41 “Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane”.,

Pia Nehemia 7:44

Halikadhalika kuna baadhi ya Zaburi zilijulikana k**a Zaburi za Asafu,Ambazo ni Zaburi 50 na ya 73-83. (Baadhi ya tafsiri zinaonyesha hivyo). Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu alimtumia yeye na uzao wake kwa njia ya uimbaji, kutoa nabii ambazo zinatusaidia hadi sasa.

Lakini kwasasa wana wa Asafu ni akina nani? Na tunapata funzo gani?

Wana wa Asafu ni watu wote wanaotumikia madhabahuni pa Bwana katika huduma ya kumsifu na kumwimbia Mungu. Watu hawa wanatenda kazi kubwa inayompendeza Mungu na kwa kupitia wao, Mungu huwa anapitisha, jumbe zake nyingi, na nabii nyingi zinazookoa na kuponya watu k**a ilivyokuwa kwa wana wa Asafu, hii ikiwa na maana, kwamba wakitumika vema katika kazi yao, basi ni utumishi mkubwa sana, hata Zaidi ya huduma nyingine zote.

Lakini, watu hawa walijua kanuni ya kumwimbia Mungu, walimwimbia Mungu katika “uzuri wa utakatifu”, sawasawa 1Nyakati 16:29. Tofauti na sasa, waimbaji wengi, wamekuwa wasanii, wanageuza uimbaji wa injili kuwa Sanaa na sio wito na huduma ya Kristo Yesu.

Wanasahau kuwa huduma yao ndio ya kwanza kabisa inayomkaribia Mungu Zaidi ya nyingine zote,..Huduma ya Maserafi na Makerubi malaika watakatifu wasimamao mbele ya Mungu daima

Lakini kinyuma chake, Mwimbaji wa injili, utamkuta anakata mauno, anavaa vimini, anapamba uso k**a Yezebeli, anaimba kwa staili za wasanii wa kidunia.. Twategemea vipi Mungu atasema au atawaponya, au atawafungua na watu wake kupitia uimbaji huo?, Haiwezekani..Inasikitisha kuona, kanisa la sasa, kundi kubwa la watu walioharibikiwa linatoka kwa wanakwaya na waimbaji.

Kumbuka Sababu iliyowafanya wana wa Israeli,wapelekwe utumwani haikuwa tu kuabudu maashera hapana, ilikuwa pia ni hiyo ya unafki katika kumwimbia.

Amosi 6:5 “ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, k**a vile Daudi;”

Bwana anatuonya vikali, na sisi pia atatuadhibu vikali k**a tutakuwa na tabia k**a za wao, anataka anapoimbiwa aimbiwe katika “uzuri wa utakatifu” (1Nyakati 16:29)..Maana yake ni kwamba wewe mwongoza sifa, wewe mwimbaji, wewe mpiga kinanda,wewe mpiga gitaa, uwe kielelezo kuanzia mavazi yako, usemi, hadi tabia, mbele za watu. Utakatifu ndio uwe leseni yako, ya kumwimbia Mungu.

K**a utashindwa utakatifu, ni heri uache tu, ukafanye kazi nyingine, kwasababu utakuwa unajizombea laana badala ya baraka.

Mahali Mungu anasifiwa na kuabudiwa ni kuwa makini sana.. wengine walipoteza Maisha walipojaribu kuvuruga utaratibu pindi Mungu anapokuwa anasifiwa (Soma 2Samweli 6:1-11 ), Vivyo hivyo na wewe mwimbishaji kanisani, usipokuwa siriazi na huduma yako, uwezekano wa kukutwa na hayo upo mkubwa sana.

Bwana anataka sote tuwe wana wa Asafu, ili atutumie kumtukuza yeye, Pamoja na kuzungumza na watu wake, ili aziponye roho za watu..

Bwana akubariki.

Asafu alikuwa ni mmoja wa walawi ambao, mfalme Daudi alimuweka k**a kiongozi wa mbele wa sifa, atakayesimama mbele ya sanduku la Mungu.Fungua.

01/07/2022

YOTE YAWEZEKANA KWA MUNGU
PAZA SAUTI, USIKAE KIMYA

"Hakika MUNGU AMESIKIA; Ameisikiliza SAUTI ya MAOMBI YANGU. *Na Ahimidiwe MUNGU ASIYEYAKATAA MAOMBI YANGU."
(Zaburi 66:20a)

Hili ni Neno la Ushuhuda wa Mfalme DAUDI Juu ya KUOMBA Kwake.

MAOMBI Yana Sifa Ya KUSIKIWA, KUSIKILIZWA na KUJIBIWA.

✍🏽Na MUNGU Daima........
-Hachoki Kusikia Maombi
-Hachoki Kujibu Maombi
-Hachoki Kusikiliza Sauti Zetu.

✍🏽DAUDI Anashuhudia Wazi Kuwa Alisikiwa na Kujibiwa.

✍🏽HEZEKIA Alipoomba Kwa Mungu Alisikiwa na Kujibiwa.

✍🏽HANA Alipoomba Mtoto Alisikiwa na Kujibiwa.

✍🏽ELIYA Alipoomba Mvua Isinye Alisikiwa na Kujibiwa.

✍🏽Hata JAMBAZI Msalabani Alipoomba Alisikiwa na Kujibiwa.

Mungu HAKATAI MAOMBI, Mwinulie MUNGU Sauti Yako ya MAOMBI.

-Usiinue Sauti ya Kulalamika.
-Usiinue Sauti ya Lawama.
-Usiinue Sauti ya Manung'uniko.

Mungu Husikiliza SAUTI ya MAOMBI, Usikae Kimya Mpazie SAUTI YAKO.

USIJIKATAE........

✍🏽Hata Wewe Unastahili Kujibiwa.
✍🏽Hata Wewe Unastahili Kupokea.
✍🏽Hata Wewe Unastahili Kupata.
✍🏽Hata Wewe Unastahili Kuona.
✍🏽Hata Wewe Unastahili Kupona.
✍🏽Hata Wewe Kubarikiwa.

MUNGU ni Mwaminifu Ukimuomba MKATE Hatakupa JIWE, Tena Ukimuomba SAMAKI hatakupa NYOKA

Ukimuomba Mungu Atakupa Sawa Sawa na HITAJI LAKO, PAZA SAUTI Usikae KIMYA.

✍🏽 "14 Na Huu Ndio UJASIRI Tulio Nao Kwake, Ya Kuwa, TUKIOMBA KITU Sawasawa na MAPENZI YAKE, ATUSIKIA."

✍🏽 "15 Na K**a Tukijua Kwamba ATUSIKIA, TUOMBACHO CHOTE, Twajua Kwamba Tunazo Zile HAJA TULIZOMWOMBA." (1 Yoh 5:14-15)

OMBA KITU Na MUNGU Atasikia na Kujibu, GOD ANSWER OUR PRAYER.

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

HAPPY NEW MONTH.

MUNGU KWANZA...

AHSANTE...!!!

05/06/2022

HERI YA SIKU YA PENTEKOSTE.

2:1-21

1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi k**a uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, k**a ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, k**a Roho alivyowajalia kutamka.

5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.

6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?

9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia,

10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,

11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.

12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?

13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;

16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.

19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.

20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.

21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.

MUNGU AWABARIKI NYOTE
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

04/06/2022

JIHADHARI NA "SIKU MOJA☝️"

☝️😢 SIKU MOJA, utafunga mlango wako, lakini sio wewe wa kuufungua.

☝️😢 SIKU MOJA, utafua hiyo nguo yako nzuri na hutaweza kuivaa.

☝️😢 SIKU MOJA, chakula ukipendacho kitatayarishwa na hautakuwepo kukila tena.

☝️😢 SIKU MOJA, utakula na kunywa usichowahi kukitoa.

☝️😢 SIKU MOJA, mtaala wa maisha (CV) na uzoefu wako wa miaka yote hautakuwa na umuhimu kwa mtu yeyote tena.

☝️😢 SIKU MOJA, mtu ambaye anaonekana kukupenda zaidi hatathubutu kamwe kusogea karibu na wewe.

☝️😢 SIKU MOJA, utafikiria yale ambayo huwezi kutimiza kamwe.

☝️😢 SIKU MOJA, utaonekana kuwa "maiti"

☝️😢 SIKU MOJA, utatengwa mahali panapoitwa "kaburi"

☝️😢 SIKU MOJA, hivyo vitu na watu unaowapenda sana watakuja kwako lakini hutaweza kuyatilia maanani.

☝️😢 SIKU MOJA, utashikilia pumzi yako na hutoweza kuitoa.

☝️😢 SIKU MOJA, utakuwa mshtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu (MUNGU).

☝️😢 SIKU MOJA nzi wa nyumbani/ mchwa watakuja kwako na utashindwa kuwakimbiza.

☝️😢 SIKU MOJA, utapokea simu ambayo huwezi kukataa kamwe.

☝️😢 SIKU MOJA, jina lako litaitwa, lakini hakuna atakayejibu.

☝️😢 SIKU MOJA, mali uliyothamini sana itachukuliwa na mtu mwingine.

☝️😢 SIKU MOJA, tendo lako Duniani litawasilishwa kwako k**a CD.

☝️😢 SIKU MOJA, jina litaongezwa kwa jina lako "Marehemu"

☝️😢 SIKU MOJA, Mgawaji Mkuu wa uhai atakutengea mahali panapofaa.

☝️😢 SIKU MOJA, ngozi yako nzuri itageuka kuwa asili yake - mchanga/vumbi.

☝️😢 SIKU MOJA, mwili wako wote utaacha kufanya kazi. Kitenzi kitabadilika kutoka kuwa mtu mwema hadi alikuwa mtu mwema.

☝️😢 SIKU MOJA, utapewa nyumba ya milele, iwe Peponi au kuzimu.

☝️😢 SIKU MOJA, hutaweza kushika wala kuandika chochote kwenye simu hii tena.

K**a unasoma hii sasa!!! Chukua dakika moja tu mwambie Mungu 'nisamehe dhambi zangu zote' kisha SHARE kwenye makundi 7, utasababisha watu wengi kumrudia Mungu.

15/05/2022

UTOSHELEVU WA MAISHA UPO KATIKA KUYAJUA NA KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU

~Na. Mwl. Francis M. Langula (+255754711247)

Mathayo 6:25 "...Maisha je! Si zaidi ya chakula..."

Chakula ni HITAJI la muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu, tunaweza kusema ni hitaji la kwanza baada ya mtu kuwa amepata hewa (oxygen) na maji safi...
Kwa mtazamo wa kawaida, mtu akikosa CHAKULA kwa muda fulani mrefu anaweza kupoteza MAISHA...

Lakini Yesu anasema, Maisha ni zaidi ya CHAKULA... yaani kuna kitu kingine kwenye maisha ambacho ni zaidi ya chakula, au kwa lugha nyingine, chakula pekee hata uwe nacho kingi kiasi gani HAKITALETA UTOSHELEVU WA (AU MAANA YA) MAISHA, *kuna kitu kingine ndio kina kamilisha huu mlinganyo wa maisha* na hicho kikiwepo ndipo maisha huleta maana...

Sasa hili neno "Chakula", linaweza kabisa kusimama badala ya MAHITAJI YA MWILI k**a vile Pesa, Nyumba, Magari, MKE, Mume, KAZI nk

Iko hivi, Wakati huna "CHAKULA" (kwa maana ya mahitaji k**a Pesa, Nyumba, Magari, MKE, Mume, KAZI nk) ni rahisi kufikiri "CHAKULA" ndio hitaji lako kuu kuliko kitu kingine chochote... Na kufikiri kwamba ukipata tu "CHAKULA" ule utoshelevu wa maisha ulioukosa utaupata wote...

Lakini Yesu anasema "...Maisha je! Si zaidi ya chakula..."

Kumbe si kweli kwamba ukipata "chakula" utakuwa umepata UTOSHELEVU WA MAISHA...

Kuna watu Wana "Chakula" namaanisha, wana pesa, wameolewa, wameoa, wana nyumba, wana magari, wana watoto na wana kila kitu tunachofikiri kina maana ya utoshelevu wa maisha lakini kitu wanachopungukiwa ni huo Utoshelevu WA MAISHA MIOYONI MWAO...

Na kuna watu wana upungufu wa "chakula" kwa maana ya mahitaji niliyotaja, lakini ndani ya mioyo yao wana utoshelevu wa maisha....

Kila aliye na hali ya utoshelevu wa maisha atakuambia huo utoshelevu haukutokana na "chakula" pekee, kwa sababu maisha ni zaidi ya "chakula"... K**a alivyosema Yesu, "Maisha je, si zaidi ya Chakula?"

KUNA KITU UKIKIPATA KWENYE MAISHA YAKO HICHO NI ZAIDI YA CHAKULA...

KITU HICHO, Ninaami, NI *KUYAJUA NA KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU, AMBACHO KITAZALIWA NA MAHUSIANO IMARA NA MUNGU (ROHO MTAKATIFU)*...

Sasa hapa Simaanishi Mahitaji sio muhimu, k**a vile msitari huo usivyomaanisha kwamba chakula si MUHIMU... lakini HIVI VITU VYOTE (CHAKULA) HAVIWEZI KULETA UTOSHELEVU IKIWA CHA MSINGI HAKIJAKAMILIKA... Na cha msingi ni nini? UHUSIANO IMARA NA ROHO MTAKATIFU AMBAO UTAZALISHA KUYAJUA NA KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU

💥 *Kwa nini nimefunganisha UTOSHELEVU WA MAISHA PAMOJA NA KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU NA KUYAISHI?*

Ukisoma maandiko utaona Yesu anaongea jambo kubwa sana katika kitabu cha Yohana 4:31-34
[31]Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule. [32]Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. [33]Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? [34]Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

Kwenye Msitari wa 34 wa maandiko hayo niliyonukuu, Yesu anawaambia, Utoshelevu wangu hauko kwenye chakula (vitu mbalimbali) bali KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU...

Ukisoma kuanzia mstari wa 31 unaona Yesu alikuwa hajala, hakuwa amepata "chakula" lakini hilo jambo la kutokula, halikumsumbua, halikumfanya ajihisi kupungukiwa (njaa)...

Pamoja na kwamba alikuwa hajala chakula, lakini wanafunzi walipomtaka ale, alisema "MIMI NINACHO CHAKULA" ... Halafu anakielezea hicho chakula chake ambacho kimemfanya ASILE CHAKULA ni KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU...

Kumbe, kuna kitu kina utoshelevu zaidi ya chakula... Kuna kitu kina maana ya maisha kuliko chakula... Kumbe maisha NI ZAIDI YA CHAKULA...

Mahusiano imara na Roho Mtakatifu ambayo yatazalisha KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU NA KUYAISHI ni MUHIMU KULIKO CHAKULA (MAHITAJI YOTE)

Umaana WA MAISHA NA VITU unakuja IKIWA MTU ANA MAHUSIANO HAYA NA MUNGU WAKE ambayo yatampelekea KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU...

Umaana wa "chakula" utakuwepo ikiwa hicho "CHAKULA" hakitamsababisha huyu mtu KUTOKA KWENYE MAPENZI YA MUNGU...

Unaweza ukadhani umewahi kupata LADHA ya MAISHA kwa sababu UMESHIKA FEDHA NYINGI, au umeishi maisha fulani ya kifahari, sasa hivyo vyote havina shida, LAKINI HAVIWEZI KUMPATIA MTU LADHA HALISI YA MAISHA.... Ninakuhakikishia K**A HUJAWAHI KUWA NA MAHUSIANO IMARA NA ROHO MTAKATIFU AMBAYO YATAPELEKEA KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO NA KUYATENDA, hujui LADHA YA MAISHA... HUJAWAHI KUUHISI HUU UTOSHELEVU WA MAISHA...

Ndugu yangu, MAISHA NI ZAIDI YA "CHAKULA"...

Kimaandiko, MAISHA ni kile ambacho unaweza kukipata au kuiishi hapa duniani na kisha kuvuka nacho kuingia nacho kwenye umilele wako... UHUSIANO HUU IMARA NA MUNGU UTAKAOKUPELEKEA KUYAJUA NA KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU DUNIANI, utakufanya ufurahie uzima wa umilele hapa na baadaye uzima wa milele Mbinguni...

Yohana 6:40
[40]Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

K**a huu uhusiano na Mungu, ambao utazalisha SHAUKU KUBWA YA KUYAJUA NA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU, haupo kwa mtu, HAKUNA KITU CHOCHOTE KITAMAANISHA MAISHA kwa huyu mtu, NA UTOSHELEVU HAUWEZI KUWEPO... Kwa sababu MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA...

Yesu anakazia kwa kusema katika Luka 12:15 "... uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."

Hii ni sawa na kusema "UTOSHELEVU WA MAISHA YA MTU haumo katika wingi wa vitu alivyo navyo"

K**a huu uhusiano haupo, wingi wa vitu unapoteza maana, kimsingi maisha yenyewe yanapoteza maana...

Hii ndio sababu ya watu wengi kutokuwa na hali ya utoshelevu wa maisha ndani ya mioyo yao, na shetani au mioyo yao inawadanganya kwamba ni kwasababu hawana chakula (yaani pesa, mume, mke, gari, watoto, nyumba, kazi nk)... Kumbe jibu sahihi ni kwamba HANA MAHUSIANO IMARA NA ROHO MTAKATIFU...

Utoshelevu wa kweli wa maisha uko KATIKA KUWA NA MAHUSIANO IMARA NA MUNGU AMBAYO YATAZALISHA KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU KWENYE maeneo mbalimbali ya maisha NA KUYAISHI...

HATUA YA KWANZA (LAKINI SIO YA MWISHO) YA KUYAJUA NA KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU NI KUMPOKEA YESU K**A BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO...

Yohana 6:47-48
[47]Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.
[48]Mimi ndimi chakula cha uzima.

Unamuhitaji YESU kuliko unavyohitaji kitu kingine chochote kwenye maisha kwa sababu Yesu NDIYE MAISHA YENYEWE....

Inawezekana una dini yako nzuri, lakini dini haina utoshelevu... YESU NDIYE CHAKULA CHA UZIMA, YEYE NDIO HATUA YA KWANZA KUELEKEA UTOSHELEVU na MAHUSIANO IMARA NA YA KUDUMU NA YESU NDIO UTOSHELEVU WA MAISHA...

Unahitaji Uhusiano IMARA NA YESU (Kupitia Roho Mtakatifu) kuliko hilo jambo unalofikiri unalihitaji kiasi cha KUKUKATISHA TAMAA YA MAISHA...

Geuzia shauku na vipaumbele vyako kwa kilicho muhimu kuliko chakula... Hamishia shauku yako kwenye kuyajua mapenzi ya Mungu na kuanza kuyaishi... Shift your desires and priorities to the REAL LIFE...

Hamishia SHAUKU yako iwe KATIKA KUHUSIANA NA MUNGU KUPITIA ROHO MTAKATIFU KWA KIWANGO CHA KUYAJUA NA KUYAISHI MAPENZI YA MUNGU KWENYE KILA ENEO LA MAISHA YAKO...

Wekeza katika ENEO HILI, FANYA HILI ENEO KUWA KIPAUMBELE CHAKO, UTAANZA KUONA UTOSHELEVU WA MAISHA...

Ukidaka Jambo hili ninalolizungumza hapa, na MAPENZI YA MUNGU YAKAWA KIPAUMBELE CHAKO, UTASHANGAA KUNA VITU VYA KIMAISHA VITAANZA KUSONGEA KWA NAMNA YA AJABU bila kutumia nguvu nyingi...

Utoshelevu UTAZALIWA UTAKAPOWEKA KIPAUMBELE KWA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU KIASI AMBACHO HAYO MAHUSIANO HAYATAWEZA KUINGILIWA NA JAMBO LOLOTE...

Matendo ya Mitume 17:28 "Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu."

💥 Ninakuombea Mungu akufungue macho yako ya rohoni na uione kweli hii muhimu itakayozalisha UTOSHELEVU WA MAISHA KWENYE KILA HATUA YA MAISHA YAKO YA SASA NA BAADAYE UZIMA WA MILELE MBINGUNI...




~Na Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
©May 2022

Address

Hongwa
Kahama

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EAGT Gethsemane-Dodoma-Kahama posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to EAGT Gethsemane-Dodoma-Kahama:

Share