14/07/2026
BADO LIPO TUMAINI.
Ayubu 14:7-9
7. Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.
8. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo;
9. Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi k**a mche.
Katika ulimwengu huu wenye kila aina ya maumivu, magonjwa,misiba, umasikini na mengine mengine......Watu hukata tamaa juu ya hatima ya maisha yao.
Wengine wameona yakua maisha hayana THAMANI tena, wamepoteza kila kitu na kubakia wapweke,watu wasio na tumaini.
Acha nikupe habari njema Kuwa Bado lipo TUMAINI, Tena tumaini lenye Baraka tele, Hili lipo mbele Yako.
Maisha na changamoto tupitiazo ni mfano WA mtu uliokatwa, lakini jua yakua haukung'olewa mizizi, japo hauna majani lakini kwa harufu ya maji mizizi huleta majani kuchanua upya, Hakika yake ni hii ipo siku yote yataisha na kua Historia.
Weka Imani Yako kwa Mungu yakwamba yu aweza yote, hakuna linalomshinda kwani yeye hushughulika saana na mambo yetu........
Biblia inasemaje juu ya kumtumaini na kumtegemea Mungu???
Zaburi 37:
5. Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
Na KITABU Cha mithali kinasema haya...
Mithali 16:
3. Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.
Nakushauri Ndugu na dada kuweka tumaini kwa YESU, yeye yu aweza yote na kwake hakuna lisilowezekana.
Bwana na akubariki na kukuongoza Katika njia zako zote, mkiri yeye nae atayanyoosha mapito Yako.
Mnyone The Advent Healing Ministry