Ufalme wa Mungu

Ufalme wa Mungu Bali utafuteni Kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo yote mtazidishiwa( mathayo 6:33)

12/04/2026
Pasaka
05/04/2026

Pasaka

Asante sana mtu wa Tabora usiache kufika siku ya kesho na Mungu akubariki 🙏🙏
20/03/2026

Asante sana mtu wa Tabora usiache kufika siku ya kesho na Mungu akubariki 🙏🙏

Yohana 3:12 Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?❤️❤️TUKUTAN...
20/03/2026

Yohana 3:12 Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?
❤️❤️TUKUTANE TABORA✅✅

MTUMISHI ZINGATIA HAYA KABLA HUJAANZA HUDUMA1. Huduma inahitaji Uvumilivu. Usiwe mwepesi kukata tamaa.2. Haijalishi umea...
11/12/2025

MTUMISHI ZINGATIA HAYA KABLA HUJAANZA HUDUMA

1. Huduma inahitaji Uvumilivu. Usiwe mwepesi kukata tamaa.

2. Haijalishi umeanzaje lakini jiandae kwa nyakati za kupimwa na kujaribiwa katika huduma yako.

3. Huduma itachanua kwa kuzingatia kutembea na Mungu, uaminifu, kutochoka mapema.

4. Kila hatua ya huduma ina watu wake na marafiki wake. Kuna wakati watu fulani watakuja au wataondoka. Usiwe mwepesi kujisahau kwa wanaokuja au kulaani wanaoondoka kipindi chao kinapoisha.

5. Hakikisha huduma yako ina mlezi au msimamizi wa kiroho anayeweza kukukemea na kukukosoa na ukanyenyekea na kusikiliza.

6. Unapopata fursa ya kutumika mahali tumika kwa moyo na nguvu zote maana huwezi kujua hiyo fursa moja itakufungulia milango gani.

7. Usikimbilie kuiga wanachofanya wengine na kikawasaidia kwenye huduma zao, kabla hujatulia na kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu k**a na wewe kitakufaa.

8. Kuna watumishi wengine wa Mungu kamwe hawatatambua wito wako wala kukukubali. Usipambane nao.

9. Kuna watumishi tena marafiki zako watabebea bango madhaifu yako na kamwe hawataangalia alichoweka Mungu ndani yako. Songa mbele.

10. Unahitaji kujijengea nidhamu ya hali ya juu katika Neno la Mungu na kujilinda na mawaa ili utumishi wako usiwe wa kulaumiwa.

11. Heshimu walio mbele yako kihuduma bila kujali umri wao.

12. Ushindani ni mkubwa. Kuwa na hekima, mbinu na shindana kwa msaada wa Mungu.

13. Katika huduma yako kitu kingine chochote kisiwe na thamani zaidi kuliko roho au nafsi ya mtu.

14. Ikimbie zinaa, pombe, tamaa (ya mwili, ya macho, ya mali), masengenyo, wivu na kiburi cha uzima.

15. Tunza sana siri zako na siri za waumini wako.

16. Kila mwaka kuna waumini wako unaowategemea sana wataondoka. Ila Roho Mtakatifu na vipawa alivyokupa havitaondoka.

17. Hakuna mjadala kuhusu Kufunga na Kuomba kila mara ili huduma yako ichanue.

18. Unyenyekevu utakuinua hata pale wengine wanapoona huna vigezo.

19. Usiendekeze sana kukaribishwa kwenda kuhudumia makusanyiko mengine kuliko kulihudumia kundi ambalo utalitolea hesabu.

20. Wapende na wajali washirika wako. Watie moyo, watembelee na ulizia maendeleo yao.

Address

Kisasa
Dodoma

Telephone

+255752407591

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufalme wa Mungu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ufalme wa Mungu:

Shortcuts

Share