16/07/2026
π₯ MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA KATIKATI YA MWAKA 2026
SIKU YA 2 | Jumanne, 14 Julai 2026
OMBI KUU: UAMSHO π₯
"Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie?" β Zaburi 85:6
Leo tumwombe Mungu alete uamsho wa kweli ndani ya maisha yetu, familia zetu, na Kanisa Lake.
π 1. Ombea Uamsho Ndani Yako na Ndani ya Kanisa
β’β β Uishi maisha ya utakatifu na kumcha Mungu (Matendo 10:1β2).
β’β β Uwe mtu wa maombi na ujitoe kikamilifu kwa Mungu na kazi Yake.
β’β β Umzalie Kristo matunda na ushiriki katika kulijenga Kanisa Lake (Matendo 9:31).
β’β β Uamsho wa kweli ulete ukuaji wa kiroho, umoja, na kuimarisha Kanisa la Kristo.
π 2. Ombea Uamsho wa Karama na Vipawa
β’β β Mungu achochee na kuhuisha karama zilizo ndani yako (2 Timotheo 1:6β7).
β’β β Akupe ujasiri mpya wa kumtumikia kwa uaminifu (Matendo 3:6).
β’β β Aachilie roho ya maombi ndani yako na ndani ya Kanisa (Matendo 12:5).
β’β β Aondoe kila uovu na kila kizuizi kinachopinga kazi Yake (Matendo 13:6β12).
π 3. Ombea DPC
β’β β Ombea moto mpya wa uamsho ushuke juu ya Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC), viongozi wake, watumishi, idara zote, vikundi vyote vya huduma, na washirika wote.
β’β β Mungu aliwezeshe Kanisa kutimiza kusudi Lake kwa nguvu za Roho Mtakatifu, umoja, na upendo.
"Ee Bwana, tuhuishe tena, ili jina Lako litukuzwe kupitia Kanisa Lako." π₯π