Christian Salvation Fellowship Church -csfc-Dodoma

Christian Salvation Fellowship Church -csfc-Dodoma CSFC is church with a vision to equiping university students with the knowledge of the word of God

A GOOD SAMARITAN (MSAMARIA MWEMA).Katika habari hiyo utagundua kuna watu wanne wametajwa.1. Kuhani.2. Mlawi.3. Msamaria....
24/05/2024

A GOOD SAMARITAN (MSAMARIA MWEMA).

Katika habari hiyo utagundua kuna watu wanne wametajwa.
1. Kuhani.
2. Mlawi.
3. Msamaria.
4. Mtu mmoja (Myahudi - aliyejeruhiwa na wanyang'anyi).

KUHANI NA MLAWI.
1. Wote ni wayahudi, wazao wa Abrahimu.
2. Wote ni watumishi wa Mungu hekaluni.
3. Wote ni Wacha Mungu.
4. Wote ni wanamjua Mungu na mafundisho ya torati kuhusu kuwatendea mema wasiojiweza.

JIRANI YANGU NI NANI?
1. Haikujalisha kuhani na mlawi mbali na kuwa wayahudi, watumishi wa madhabahu na wacha Mungu lakini bado hawakuweza kumsaidia Myahudi mwenzao.
2. Kwa kigezo cha torati au sheria, mtumishi wa Mungu na MKRISTO wa leo anaweza kushindwa kumsaidia mwenye dhambi walau mmoja.

MSAMARIA.
1. Ni mtu wa taifa lingine.
2. Hawachangamani na wayahudi (Yoh. 4:9).
3. Wasamaria hawana mahusiano mazuri ya kisiasa na kiuchumi pamoja na wayahudi.
4. Hawasaidiani maana ni maadui na wana uhasama.

GOLDEN RULE - SHERIA YA UFALME.
1. Usitafute kutendewa mema, bali tafuta kuwatendea mema wengine.
2. Usitafute kuonewa Huruma, bali amka na Anza kuwaonea Huruma wengine.
3. Usitafute kupewa vitu, bali Anza tabia ya kuwapa watu vitu (Luka 6:38).
4. Vile unavyowafanyia wengine ndio na wewe utakavyofanyiwa na kuzidi sana.
5. NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA (Mdo 20:35).

JIRANI YANGU NI NANI?
1. Anza kuwapenda wengine haswa wanaokuudhi.
2. Anza kuwajali wengine haswa masikini na wasiojiweza.
3. Anza kuwashuhudia wengine habari za Yesu haswa makahaba, wevi na walevi.
4. Anza kuwa support wengine haswa wasio na uwezo wa kukurudishia.
5. Anza kuwaombea wengine haswa wenye mahitaji makubwa na mazito kuliko yako.

UTUMISHI WA KWELI (UKRISTO HALISI) UKO KATIKA KUWATUMIKIA WENGINE KWA UPENDO, KUWAJALI WENGINE, KUWAONEA HURUMA WALIOSETWA NA ADUI, KUWAOMBEA NA KUSHIRIKI NAO VITU VYAKO. TUKIWATENDEA HAO TUMEMTENDEA MUNGU. THAWABU YAKO YADUMU MILELE.

BARIKIWA NA KRISTO.

04/02/2022
06/01/2022

Pendeza Channel itakuletea mafundisho mbalimbali kutoka kwa mchungaji na mmishenariDebora Kim. Usisahau kusubscribe katika channel hii ili uendelee kupata ta...

30/11/2021
16/11/2021

KARIBUNI..... Kanisa UDOM ng'ong'na. Tunawapenda... Ukiwa Dodoma usisite kuabudu pamoja na sisi..

05/10/2021

Thank

Address

NG'ONG'HONHA
Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Christian Salvation Fellowship Church -csfc-Dodoma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share