02/09/2024
IJAPOKAWIA INGOJEE, HAINA BUDI KUTIMIA (USIKATE TAMAA).
Bwana YESU KRISTO asifiwe sana mpendwa, leo mtumishi Apostle Rodrick Ndone anasema na wewe ambaye una ona ndoto yako ime chelewa kutimia. Nasema na wewe ambaye kila ukiangalia umri wako na muda ulio nao una ona ndoto zako zimeyeyuka!! Nasema na mtu mmoja ambaye amekata tamaa kwa sababu ya magonjwa nk!! Tumaini lipo, YESU KRISTO ni tumani letu, soma hapa,
Habakuki 2:2-3 neno la MUNGU linasema:
"BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma k**a maji.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia".
Katika neno hili tuna ambiwa itatimia kwa wakati ulioamriwa. Ukisoma kitabu cha Mhubiri 3:1 neno la MUNGU linasema:
"Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu".
Usikate tamaa, majira yako na muda wako wa kufurahi unakuja. Wewe umekusudiwa mema. MUNGU mwenyewe anasema katika
Yeremia 29:11:
"Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho".
Hapa ulipo sasa hivi unaona dunia haieleweki, unaona umefika mwisho, sasa mwisho wako ndiyo mwanzo wa MUNGU k**a hautakata tamaa. Huo unao uona ni mwisho wako ndiyo MUNGU anaona nwanzo na anaruhusu tumaini kuibuka.
MUNGU akikuinua, uwe na moyo wa shukurani.
Katika mapito yako yote usijinenee mabaya, usikiri kushindwa. Fahamu kwamba "kukata tamaa ndiyo silaha ya mwisho ya shetani na UVUMILIVU ndiyo kipimo cha kwanza cha MUNGU kwa mtu yeyote".
**********USIKATE TAMAA**********AMENI****************
Apostle Rodrick
0710111214