Christian Council of Tanzania (CCT)

Christian Council of Tanzania (CCT) The Christian Council of Tanzania (CCT) was established in January 1934 as a fellowship of Churches and Christians. The CCT has 12 National Churches

It was then named the Tanganyika Missionary Council until 1964 when it adopted its current name. The Christian Council of Tanzania (CCT) is an Ecumenical Church Organisation formed by twelve Protestant Churches and twelve Para-Churches Organisation/ministries. CCT Purposes include:1) to promote and sustain the spiritual unity of the Churches, 2) to serve as an instrument of the churches for monito

ring and expressing a common voice on issues of interest to the churches and those issues concerning the spiritual, moral, socio-economic and physical welfare of the people, 3). to promote and take an active role in the development and provision of welfare services for the communities of people served by the churches, 4).to sthrengthen and build capacity of the member churches to respond effectively to emergencies, human displacement, gender equity, good governance, justice and HIV/AIDS pandemic and orphans

Ibada maalum katika Chaplaincy ya Bunge leo kwa ajili ya kuombea bajeti ya serikali 2026/2027 katika kuhitimisha vikao v...
23/06/2026

Ibada maalum katika Chaplaincy ya Bunge leo kwa ajili ya kuombea bajeti ya serikali 2026/2027 katika kuhitimisha vikao vya Bunge la Bajeti, kuombea nchi, serikali pamoja na shughuli za bunge. Ibada imeongozwa na Baba Maaskofu na Chaplain wa Chaplaincy Mchg. Modest Pesha ikihusisha pia wachungaji kutoka CCT na CPCT pamoja na Kamati ya wanamaombi wa Bunge inayoundwa na umoja wa Makanisa, Dodoma. Kwaya ya watumishi CCT Ofisi Kuu pamoja na Kwaya ya Mt. Andrea ya Anglikana Msalato Dodoma zimehudumu. Bunge la Tanzania

Kongamano La wajane na Wagane linaendelea Mkoani Dodoma.Kongamano limeandaliwa na AACC kushirikiana na Kanisa la Anglika...
23/06/2026

Kongamano La wajane na Wagane linaendelea Mkoani Dodoma.

Kongamano limeandaliwa na AACC kushirikiana na Kanisa la Anglikana Tanzania, washiriki wa semina wakiwa wajane hasa toka makanisa wanachama CCT.

Katika ufunguzi wa Semina, neno kuu Luka 4:5 ambapo mhubiri wa Neno Baba Ask. Philipo Banji amewatia moyo washiriki kuwa Jasiri katika safari yao ya maisha wakiangalia ahadi ya kufika kilindini.

Katika mahubiri yake amesema“Nyinyi ni watu muhimu, mnapitia mambo mbalimbali ya kihisia, hasa mnapomkumbuka wenza, unapokutana na changamoto za kiuchumi, Mungu wetu ni mume wa wajane, na baba wa yatima.

Upendo wa Mungu ndio umetuleta mahali hapa kwenye kongamano, Petro alitii ahadi na kuzishusha nyavu na jambo kubwa na la ajabu likatokea, kwenye kongamano hili nawakaribisha kwenye safari ya matumaini ili mwende kilindini ambako ndiko kuna mafanikio, mafundisho ya leo yakawapeleke huko”

Naye Mratibu wa mafunzo hayo toka AACC Faustina Nillan amesisitiza washiriki kuwa tayari kupata kile wakufunzi wataenda kuwafundisha.

AACC(All Africa Conference of Churches) ni funganiko la makanisa ya kiprotestanti ndani ya bara la Afrika, moja ya malengo makuu ni kuimarisha umoja miongoni mwa makanisa wanachama ikiwemo Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) AACC - CETA Youth

Kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za utekelezwaji wa mradi wa kutetea haki za wakaazi wanaoishi maeneo ya migoni mkoani ...
09/06/2026

Kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za utekelezwaji wa mradi wa kutetea haki za wakaazi wanaoishi maeneo ya migoni mkoani Mara hususani wilayani Tarime kimefanyika leo tarime katika ukumbi wa Blue Sky Hotel.
Viongozi wa dini wamesisitiza kuiendelea kupaza sauti katika kutetea wakaazi hao wanaozungikwa na shuguuli za Migodi huku wakifuata mwongozo ambao umekabidhiwa kwao.

Kikao kimehusishwa na viongozi wa dini wilayani humo na wadau wa kusimamia mradi huo kupitia CCT ambao ni FECCLAHA , COS na SWEDWATCH.

Zingatia:
FECCLAHA kwa kirefu "Fellowship of Christian Councils and Churches in the Great Lakes Regon and the Horn of Africa"
Ni shirika ambalo jukumu lake ni kukuza ushirikiano thabiti wa Kikristo miongoni mwa wanachama wake 11 ili kuchukua umiliki na uwajibikaji kwa changamoto zinazoathiri Amani na Mshikamano wa Kijamii katika kanda na kuwawezesha kutafuta suluhu kwa vitendo sawa.

COS kwa kirefu "Church of Sweden" ni kanisa la Swideni linaloshirikiana na mashirika yanayohusiana na makanisa kwa ajili ya misaada ya maafa, maendeleo na utetezi.

SWEDWATCH ni shirika la utafiti linalojitegemea, lisilo la faida linalojitahidi kuwawezesha wenye haki na kukuza mazoea ya kuwajibika ya biashara AACC - CETA Youth FECCLAHA PROCMURA - Programme for Christian-Muslim Relations in Africa Norwegian Church Aid TanzaniaACT Alliance International Center for Peace, Human Rights and Development-IPHRD Africa

FECCLAHA, Swedwatch na ACT Church of Sweden, kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), wamezindua mwongozo ...
05/06/2026

FECCLAHA, Swedwatch na ACT Church of Sweden, kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), wamezindua mwongozo mpya unaoangazia nafasi muhimu ambayo viongozi wa dini mbalimbali wanaweza kutekeleza katika kusaidia jamii zilizoathiriwa na shughuli za uchimbaji madini kupata haki na suluhu stahiki.
Uzinduzi wa mwongozo huo umefanyika rasmi wakati wa Jukwaa la Mabadilishano ya Afrika Mashariki kuhusu Biashara na Haki za Binadamu lililofanyika jijini Arusha, Tanzania, tarehe 5 Juni 2026 katika Hoteli ya Meru.

Mwongozo huu unajibu changamoto zinazoongezeka katika ukanda wa Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika, ambako jamii nyingi zinaendelea kukumbwa na ukiukwaji wa haki za binadamu na madhara ya kimazingira yanayohusishwa na shughuli za uchimbaji madini, huku upatikanaji wa haki na suluhu ukiwa mdogo. Madhara hayo ni pamoja na kuhama kwa wananchi kutoka maeneo yao, uharibifu wa mazingira, hatari za kiafya, migogoro na vurugu, kupoteza maisha pamoja na ukiukwaji wa haki za ardhi. Aidha, mwongozo unaonyesha kuwa mifumo mingi ya malalamiko iliyopo kwa sasa haifahamiki vya kutosha, haifikiki kwa urahisi na mara nyingi haijajenga imani kwa jamii husika.

Katika mazingira hayo, mwongozo unasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya jamii, viongozi wa dini, serikali, makampuni na wawekezaji.

Baadhi ya maofisa wa CCT wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa FECCLAHA Bi, Jeannette Uwizeye  walipokutana leo jijini...
04/06/2026

Baadhi ya maofisa wa CCT wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa FECCLAHA Bi, Jeannette Uwizeye walipokutana leo jijini Arusha katika kikao cha Utetezi wa wakaazi wanaoishi maeneo yanayozungukwa na migodi hususani Mara na Geita.

Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Ask. Dkt. Stanley Hotay , Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa CCT, Ask. Nelson Kisare na Katibu Mkuu wa CCT Mchg.Dkt. Can. Moses Matonya.
Katibu Mkuu CCT ndiye mwenyekiti wa FECCLAHA kwa sasa
FECCLAHA AACC - CETA Youth

Ibada ya Maadhimisho ya CCT Day Kitaifa imefanyika leo hii katika viwanja vya Kanisa Kuu la Mt.Andrea(Anglikana)Njombe M...
31/05/2026

Ibada ya Maadhimisho ya CCT Day Kitaifa imefanyika leo hii katika viwanja vya Kanisa Kuu la Mt.Andrea(Anglikana)Njombe Mjini. Maadhimisho hayo yalitanguliwa na Maandamano yaliyoanzia Kanisa la Moravian Njombe mjini na maandamano hayo kupokelewa na Askofu.Dkt. Stanley Hotay Mwenyekiti wa CCT Taifa, Askofu Dkt.George Fihavango Mwenyekiti wa CCT Mkoa wa Njombe Pamoja na Maaskofu na viongozi mbalimbali wa CCT.

Askofu.Dkt.Abednego Keshomshahara Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa CCT amehubiri neno kuu la maadhimisho ya Mkutano Habakuki 3:2 akisisitiza wakristo wa CCT kuomba nguvu ya Mungu kufufua mambo mbalimbali katika Jamii ikiwemo uchumi,umoja na upendo.(picha ya Nne)

Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa njombe pia alishiriki katika maadhimisho hayo,akitoa salamu za serikali alisisitiza CCT na Makanisa wanachama yasiache wajibu wake wa kukemea mmong’onyoko wa maadili katika jamii,kusimamia Uchumi imara ,kujenga uchumi wa taasisi za kanisa na waumini.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano -CCT

Mhashamu Baba Askofu Dkt.Stanley Hotay Mwenyekiti CCT Taifa akiambatana na viongozi mbalimbali wa CCT Kitaifa na Mkoa wa...
30/05/2026

Mhashamu Baba Askofu Dkt.Stanley Hotay Mwenyekiti CCT Taifa akiambatana na viongozi mbalimbali wa CCT Kitaifa na Mkoa wa Njombe wametembelea Gereza la wilaya ya Njombe na kufanya huduma ya udiakonia kwa wafungwa na mahabusu. Akikabidhi mahitaji mbalimbali muhimu kwa ajili ya wafungwa Mwenyekiti wa CCT alisema huduma hiyo ni sehemu ya Maadhimisho ya CCT Day Kitaifa itakayofanyika Kesho haswa akisisitiza umuhimu wa jamii kuwakumbuka na kuwajali wenye uhitaji.
Katika hatua nyingine viongozi wa CCT Kitaifa ,Mkoa wa Njombe na Viongozi mbalimbali wa Makanisa wanachama ya CCT walishiriki kupanda miti ya katika viwanja vya Gereza la wilaya ya Njombe na Viwanja vya Kanisa Kuu la Mt.Andrea(Anglikana)Njombe Mjini,zoezi la upandaji wa miti limekumbusha umuhimu wa jamii kutunza Mazingira aidha limeonyesha moja ya Kazi kubwa inayofanywa na CCT katika Kukabiliana na Mabadiliko yatabia nchi.

Kaimu Mkuu wa Gereza la wilaya ya Njombe ASP. Ally Mdee amewashukuru uongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania-CCT kwa kutembelea gereza hilo Pamoja na kutoa mahitaji mbalimbali kwa wafungwa gerezani hapo,aidha amewasihi viongozi wa dini kuendelea kushirkiana na serikali katika kuhakikisha jamii inakuwa na maadili mema.

Maadhimisho ya Siku ya CCT ( CCT DAY) Mkoa wa Kilimanjaro yanaendelea leo Tar 30 Mei 2026, Mahali :-  KKKT Dayosisi ya P...
30/05/2026

Maadhimisho ya Siku ya CCT ( CCT DAY) Mkoa wa Kilimanjaro yanaendelea leo Tar 30 Mei 2026, Mahali :- KKKT Dayosisi ya Pare, wilayani Same, Neno Kuu Zaburi 3:2

Kitaifa maadhimisho yatafanyikia mkoani Njombe Tar 31 Mei 2026 katika kanisa Kuu la Anglikana la Mt. Andrea

11/05/2026

Address

P. O. Box 1454
Dodoma

Telephone

+255262324445

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Christian Council of Tanzania (CCT) posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Christian Council of Tanzania (CCT):

Share