06/06/2017
%KUTOKA KWENYE MAKTABA YA%
-------KITUME NA KINABII-------
SOMO:Lilifundishwa siku ya mwisho ya semina ya Ukombozi-Julai 2015
¶MAELEZO KUHUSU ROHO MTAKATIFU WA MUNGU÷
-Ana majeshi.-Yoh 14:16-31
*Andiko hili linathibitisha kuwa Roho Mtakatifu yupo.
-Roho wa Mungu ana Roho nyingi zitendazo kazi.
-Isaya anazungumzia Roho 7 ambazo Ufunuo unaziita macho 7 ya Mungu.
-Mithali16:4~wabaya pia wameumbwa kwa kusudi.
-Mwanzo 1:4~Mungu akatenga giza na nuru.
*Katika maisha yetu lazima tutenge kilicho cha nuru na kilicho cha giza;kilicho cha nuru hicho tufanye na cha giza tusifanye.
*Mwanzo 3:22-25~kujua mema na mabaya kulimpelekea mtu kufukuzwa,alichanganya mwanga na giza,kabla ya hapo alikuwa mtakatifu alivyokusudiwa.
*Giza lina kundi lake(utawala wa chini)
*Nuru ni utawala wa kati.
*Roho ni utawala wa juu.
¶WAKUU WA GIZA KAZI YAO NI÷
{Wakuu wa giza ni wachawi,waganga wa kienyeji,wapiga ramli,wanajimu,wenye mapepo ya utambuzi,wafanya mazingaombwe.}
i}Kukufanya usiwe na maamuzi yoyote kuhusu Mungu
-Waliokoka wanakuwa wapo wapo tu.
-Ukitangaza maombi kwa mfano,huyu hana maamuzi huyahusu au yupo mtaani muda wa ibada.
ii}Kufanya mapenzi ya Mungu kimwili.
-Wiki inaisha hajafanya ya Mungu.
¶MKUU WA ANGA KAZI YAKE NI÷
i}Kukuangalia kokote unakoenda na kutoa taarifa kwa wakuu wa giza na mapepo ili wakudhibiti.
-Walokole wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu huyu huwazuia wasifanye mapenzi ya Mungu.
-Lazima uuweke ufalme wa Mungu kwanza na haki yake utapewa+mengine uzidishiwe.
-Kumb la torati 28:1
*Lazima kusikia,kutunza kuyafanya maagizo yake naye atanitukuza duniani kote.
-Kituo kikuu cha Mungu duniani ni kanisa.
*Akisema mtmsh,lazima ufanye ni agizo.
-Baraka zitakujilia,hutazitafuta.
-Mambo hayaendi kwa kuwa umedhibitiwa.
ii}Anahakikisha umekufa kiroho.
-Kiroho wanaanza kufa alafu ndipo wanalala.
*Anakuua kiroho alafu anahakikisha umelala.
iii}Kukuchelewesha.
** #*** #** #** #** #** #** #** #** #*** #*
-Efeso 5:14~Amka,baada ya kuamka,Roho Mtakatifu anakufufua,alafu Yesu atakuangazia nuru yake alafu Rum 8:1{huna hukumu upo katika Kristo}alafu wanakuagiza ukaangaze{Isaya 60:1}
*Dan 12:3~Hawa hawakubali kufa kiroho ndiyo maana watang'aa.
-Efeso 2:13-Yesu alibomoa kiambaza ili ukaribie.
*Mkuu wa anga anakufuatilia kwa kuwa aliye na Kristo sio wa kawaida duniani.
-wakuu wa giza wanapewa taarifa na mkuu wa anga.
*mkuu wa anga anakuua kiroho alafu anawapa wakuu wa giza na mapepo taarifa ili wakushambulie kimwili.
hali hii Roho Mtakatifu na Bwana Yesu wanatuombea alafu Roho Mtakatifu anaingia mtumishi mmoja wa Mungu anaonyeshwa yanayokutesa afu anakupigania.
-Isaya 52:1~Amka Sayuni{mpendwa/mlokole}
-K**a hauna nguvu hauwezi kushinda
{Matendo 1:8}
*Nikiwa na nguvu nitashinda.
-Isaya 9:6
*Tunapewa Mungu mwenye Nguvu ili atusaidie.
*Yesu wetu sio wa show ni mwenye nguvu.
¶JINSI YA KUFANYA÷
i}Kuomba nguvu
-Usipowashinda hawa{mkuu wa anga na wakuu wa giza}huwezi kumpinga shetani.
-mkuu wa anga ni mfalme kwa hiyo ili kumshinda tunahitaji nguvu za kifalme.{Efeso 4:13}
-KAZI YA MUNGU INAENDA KWA MAJIRA NA NYAKATI.
-Lazima kuukomboa wakati ili÷
{i}Nimshinde,nikichelewa atanishinda.
{ii}Anajua majira ya Mungu kufanya kazi na mimi kwa hiyo baraka zangu atachukua.
-Mungu anaokoa na kukomboa,kukombolewa ni lazima usisikilize injili ya wainjilisti ya wokovu tu jua pia kuna Ukombozi.
-Usiwe mwepesi wa kutoa fedha yako kwa yeyote ambaye Roho wa Bwana hajakushuhudia umpe.
-Mtu anaweza kuwa anapigwa na Mungu hivyo na wewe ukimchangia pengine atibiwe hasira ya Bwana ikakuwakia.
-Usiwape wanaoombaomba mitaani bila ridhaa ya Roho Mtakatifu maana wengine ni mizimu kutoka kuzimu.
*Ukimpa mzimu hela yako ni zindiko kuzimu,unageuka mchawi au unakuwa kiloriti huelewi kwa nini.
-Hazina yako ilipo ndipo na moyo wako ulipo.
*Ukitoa kwa mchawi utapokea ya huko kwenye uchawi.
-Kila cha kwako kinafaa kumtumikia Mungu.
-Wafilipi 3:10-14
*Paulo anashughulikia yaliyopita.
*shetani anakukumbusha yaliyopita mfano huwezi wewe mjinga n.k.dawa ni KUSAHAU.
-Usiseme ulitukanwa siku ile sahau kaza mwendo fanya ulichoitiwa.
-mkuu wa anga haui mtu mpaka ajiue mwenyewe.
-Kufa au kuishi kuko katika ulimi wako.
-Efeso 3:16-17~Angalia Mungu katika upendo wake ndiyo uweze kusahau ya zamani.
¶SILAHA ZA MKUU WA GIZA KUKUMALIZA NI÷
i}Mwendo wako
2Tim 4:7
*Paulo alikuwa na mwendo.
*Paulo alikuwa na mwendo MZURI.
MWENDO MZURI ni pale mmoja anapoweza kuangalia majira na nyakati.
ii}Mwenendo~Kolosai 1:4-5
-Hapa maana yake ni jinsi unavyomaanisha,kujali na kuzingatia mambo ya Ufalme.
**-**-**-**-**AMINA-**-**-**-**-**-
I.C.T. EFATHA IHUMWA.
'share' tafadhali.....