EAGT Central Dodoma

EAGT Central Dodoma This is an OFFICIAL page of EAGT CENTRAL DODOMA|
Under pastor JOHN KASENGA. Join us for worship, prayer, and service.

Praise and worship 🙏🙏
22/03/2026

Praise and worship 🙏🙏



KANISA LA EAGT CENTRAL DODOMA, IBADA YA JUMAPILI TAREHE 22/03/2026MUHUBIRI: MCHUNGAJI  DONALD CHOGOSOMO: BARAKA ZINAZO B...
22/03/2026

KANISA LA EAGT CENTRAL DODOMA, IBADA YA JUMAPILI TAREHE 22/03/2026
MUHUBIRI: MCHUNGAJI DONALD CHOGO
SOMO: BARAKA ZINAZO BUBUJIKA.

BWANA anataka kuachilia baraka kwa watu wake jumapili ya leo.
Mwanzo 26:18-23
"Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika..."

Unaweza ukawa mtu wa thamani katika ulimwengu wa roho lakini bado kuna vitu atui anakunyang'anya.

Kila kitu lazima kibubujike
○Baraka isiyoisha
○Amani isiyoisha
○MUNGU atufanyie nafasi

K**a Mungu hajakubariki hata k**a uwe na upako wanamna gani ndoto ZAKO haziwezi kutumia.
Tamani Mungu akufanyie nafsi
MUNGU ni yule yule habadiliki aliye tenda kwa Ibrahim,Isaka na Yakobo anaweza Kutenda kwetu maana yeye ni Mungu wa maagano.
Kutoka 33:1
"BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii; "

Zaburi 26:7
"Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu."

Mwenye haki wa Mungu
●Haachwi na Mungu
●Analindwa na Mungu
●Anatetewa na Mungu
●Anapendwa na Mungu

MUNGU wetu habadiliki hata kidogo yeye ni Mungu wa maagano alitenda kwa wengine hata kwako anaweza Kutenda.
KUMBUKUMBU LA TORATI 7:9
"Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; "

Kunawakati huhitaji kuomba vitu ila vitu tu vinatokea ukiwa unatamka vitu vinatokea
VITU VYA KUZINGATIA ILI BARAKA ZAKO ZITOKEE.
1 . Endelea kuwaleta watu ndani ya Yesu
2 .Endelea kutembea katika mapenzi ya Mungu
3 .Linda utakatifu wako.

Ombi langu Bwana wanguPeke yangu sitowezaUwepo wako Beana uwe nami🙏🙏🙏
08/03/2026

Ombi langu
Bwana wangu
Peke yangu sitoweza
Uwepo wako Beana uwe nami🙏🙏🙏

Zaburi 1501 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.2 Msifuni kwa matendo yake...
08/02/2026

Zaburi 150
1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

38 Twende kwa Yesu Na furaha tutaiona,Mioyo ikitakata sana,Kwako, Mwokozi, kuonana,Na milele
08/02/2026

38 Twende kwa Yesu

Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako, Mwokozi, kuonana,
Na milele

"Abudu Mungu kwa roho na kweli, kujumuika pamoja katika ibada na upendo, na kushukuru kwa kila jambo 🌟        "
08/02/2026

"Abudu Mungu kwa roho na kweli, kujumuika pamoja katika ibada na upendo, na kushukuru kwa kila jambo 🌟

"

Nyumba ya Mungu, mahali pa amani na upendo 🌟
04/02/2026

Nyumba ya Mungu, mahali pa amani na upendo 🌟




Address

Dodoma Inn
Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EAGT Central Dodoma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share