Apostle Kamage Betheli Ministry Church of TANZANIA-Mwanzo 28:16-19

Apostle Kamage Betheli Ministry Church of TANZANIA-Mwanzo 28:16-19 GOD'S KINGDOM CHURCH

11/09/2017

KARIBU KWENYE GROUP LA WHATSAP KWA MASOMO MBALIMBALI YAHUSUYO NENO LA MUNGU NA MWENENDO UNAOFAA KUISHI KWA MKRISTO....

COMMENT NAMBA YAKO YA WHATSAP HAPA....

25/01/2017

Waefeso 3:20
Pia Ayoub 22:21
Wagalatia 4:1-3

NENO: MJUE SANA MUNGU.

Naomba nikupe sifa chache za Mungu, kabla sijakupeleka kwenye Somo lenyewe.....

Sifa ya kwanza ya Mungu ni Kusikia Maombi yako
yoote unayomuomba,
Sifa ya pili ya Mungu ni kutokujibu Maombi yote.
Sifa ya tatu ni kujibu kwa wakati wake sio kwa
Wakati wako

Na wakati Mwingine Mungu anakujibu
Leo maombi uliyoomba mwezi uliopita..

Na Biblia inasema Mungu Hawaii wala
Hakawii,utajifunza kitu hapo ikiwa tu
Utanisikiliza kwa msaada wa Roho Mt.

Kwanini uombe Vingi na Ajibu vichache?
Au uombe Vngi asikujibu kabisa?

Kwanini Unaomba Leo na Mungu akujibu
Keshokutwa? Mbona kachelewa na
Andiko linasema Hawaii wala hakawii?

Utaona Mwanadamu unapenda majibu yawahi
Lakini Mungu sio wakuwahi= Mwanadamu
Anapepishana sana na Mungu

Tujaribu kuelezana kwa mtiririko
Kwanza kabisa kinachomfanya Mungu
Asikie Maombi yako Mengii na kukujibu
Machache chanzo n wewe Mwenyewe,

Waefeso 3:20

Atukuzwe Yeye(Mungu) awezaye kufanya
Mambo ya Ajabu Mno(Ajabu ni kitu cha Ku
Shangaza, kilivyo ukutarajia, sasa unapoomb
A mambo mengi sana alafu Mungu akakuji
bu mambo machache, tayari inakupa maswa
ali inakushangaza "Mambo ya ajabu", umeo
MBA mengi na hajakupa hata moja tayari ni
mambo ya ajabu) ulitegemea Leo kakupa
K**a ulivyotaka lakini n kesho

Anaendelea ; kuliko yote tuombayo au tuwa
zayo(tunayofikiria) kwa kadri ya """NGUVU
itendayo ndani yetu""" hapa ndiyo pana
maliza kiu yetu


Kumbe Mungu anakujibu kwakutegemea
Nguvu itendayo kazi ndani yako
Unaomba Mambo Mengi sana lakin wkt
Mungu anataka akujibu anaangalia Capacity
Yako inaweza kubeba kiwango gani?

Hapa namaanisha kila Maombi unayoomba
Kuna Nguvu unabaki nayo itakayobeba Majibu yako
Na wakati Mwingne hiyo Nguvu ndiyo inayovuta
Majibu kutoka kwa Mungu kuja Kwako

Kapu la Maombi linakuwa kubwa sana lakini
Kapu lako la Majibu ulilobeba"NGUVU ITENDA
YO KAZI NDANI YAKO"" linakuwa n Dogo sana
na kiuwezo, ndio maana Mungu anakupa kuli
ngana na nguvu ya kubeba Majibu,

Yaani kwa "kwa kadri ya Nguvu itendayo kazi
ndani yako ndivyo Mungu atakavyokupa...

Mungu anaweza kukujibu yoote uliyoyaomba
Kwa wakati Mmoja lakini vitakuangamiza
Ni walokole wangapi Mungu kawabariki
na Wokovu wakaacha?

Na ili ujue Mungu ni Mtenda Mambo ya
ajabu, Kuna watu wanaomba kidogo tu
(Mahitaji) lakin Mungu uwapa zaidi ya
walivyoomba... Nini kimetokea hapo

Kapu lake la Maombi ni Dogo sana lakini
Kapu lake la majibu no kubwa sana
Mungu anasema aaah nikimpa na hiki vipi
anaona kapu lipo safi tu anaongeza tena
Lipo safi, ndio unakuta mpendwa anashuhudia

Aliomba apate Kazi lakini kapata kazi na gari
yakutembelea kapewa..
Na wewe uwe kundi hili katika Jina la Yesu..

Jifunze sana Kumjua Mungu kuliko kujifunza
Kuyajua Majibu ya Mungu(kupenda Miujiza)
Watu wanaojifunza kuyajua majibu ya Mungu
Ni rahisi sana Kuuacha Wokovu,Kuliko wale
Wanajifunza kumjua Mungu mwenyewe.

Ijue kweli nayo kweli itakuweka Huru, nahiyo
Kweli ni Neno la Mungu...

Neno la Mungu likae kwa Wingi Moyoni Mwenu
Mungu anapotambua unautafuta USO wake
Yeye ujifunua Kwako usema nawe kwa upole
na unyenyekevu,,

Kuna wakati MTU anaomba lakini hapati,
Tena upokea machungu badala ya furaha
Yesu akamwambia yule Mama Nitawezaje kuwap
APA mbwa chakula cha wanangu?

Kwahiyo shart la kwanza alilotakiwa kuli-
Fanya yule Mama ni Kutoka kwenye Nafasi
ya Mbwa na akae kwenye Nafasi ya Mwana
Automatically Yesu angemuhangaikia

Inachomaanisha hapa ni Kwamba Yule
Mama alitanguliza Mahitaji badala ya
Toba/Utakatifu, andiko linasema "Wale wasikiao
Neno la Mungu hao ndio wana wa Mungu"

Kuna wakati utaomba na usipate sababu
Ikawa ni Toba

Mathayo 15:25-26
Kilichomsaidia alionyesha Moyo wa Unyenye
kevu na Kujishusha, akasema ""Hakika sifai kuwa
mwana lakin naomba basi unipe kile wakibakisha
cho wanao maana ndio desturi ya Mbwa

Kuna vitu Utajibiwa na Mungu kwasababu tu
ya Moyo wako kuwa na Unyenyekevu mbele
zake hata k**a ukustahili kupata....

Andiko linasema kuomba kwake mwenye haki
kwafaa sana,hasa akiomba kwa Bidii..

Tafsiri ya andiko hili ni Kwamba
Mungu anapendezwa sana tena sana mwenye Haki
Anapomuomba yaani maombi ya mtu huyu kwa
Mungu ufanyika manukato mbele za Mungu..

Lakini anamalizia hapa ""Hasa akiomba kwa Bidii""
Yaani Mungu anapendezwa sana lakini unamchanga
nganya sana Mungu pale unapoomba kwa Bidii.

Ndiyo tafsri ya andiko hili...

WAGALATIA 4:1-3

Sababu nyingine ndio hii
Mungu akupi majibu yako sio kwa sababu
hajasikia ila Uchanga wa kiroho ulionayo
juu ya hitaji hilo umfanya Mungu akusikie
Lakini asikujibu,

Mungu ambariki MTU eti kwasababu ameok
oka na kukaa kanisani kwa Muda Mrefu sana
Mungu ufanya kazi na wale wanaomulewe
Mungu na mapenzi yake

Mathayo 5:3
Inasema MASKINI WA ROHO, UFalme wa
Mbingu ni wao..,,

Sasa wanaokaa kanisani Muda mrefu pasi
kumuelewa Mungu hao ni Matajiri wa kiroho
Walio ridhika na mambo ya Rohoni hawana
Uhitaji tena.

Lakini wale Maskini wa Roho ni wale wasikiapo
Neno la Mungu utetemeka na kusujudu mbele
zake maaana wana mahitaji ya rohoni..

Sasa anaposema mrithi hana tofauti na Mtumwa
ingawa ni Bwana wa yote(Ndiye Bosi wa zile Mali
alizoshikiwa na wakili hadi atakapokuwa MTU mzima
Kiakili na ufahamu) hadi Muda ulioamriwa na
Baba "MUNGU"

Nilipokuwa mtoto,Mara nyingi wageni walikuwa
wakija nyumba wakati wakuondoka wanatupa
sisi watoto hela, alafu punde unaona mama
anakuja anachukua ile hela anasema lete Niki
wekee,

Nikawa nakasirika sana k**a sio kulia kabisa
Lile tukio nikawa silielewi kabisa na lilikuwa
linanikwaza sana, imenichukua miaka mingi
kujua Tafsiri ya Mama kufanya vile
Leo nimejua kumbe alikuwa na nia njema kabisa

Mfano huu uhamishie kwenye mambo ya Rohoni
Utapata maana ya Wagalati 4:1-3 na
Utamtukuza Mungu kulielewa andiko linasemalo
""Mungu siku zote utuwazia Mema"

Naomba niishie hapa kwa Leo.

Call/Whatsap 0655301117
By Apostle K**age.

13/12/2016

ENDELEA MBELE,UTAMUONA MUNGU....

KITABU CHA KUTOKA 14:1-4, 10-14

INASEMA; BWANA akasema na Musa akamwambia,2 waambie wanawa Israel kwamba warudi na kupiga Kambi mbele ya Pi-hahirothi,kati ya migdoli na Bahari, kuikabili Baal-sefoni;mtapanga mbele yake karibu na Bahari. Naye farao atasema katika habari ya wana Wa Israel wametatanishwa katika nchi,ile jangwa imewazuia wasitoke. 4 nami nitaufanya uwe mngumu Moyo Wa farao,naye atafuata nyuma; nami nitajipatia utukufu kwa farao na kwa jeshi lake lote; na wamisri watajua ya kuwa Mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo...

Bwana yesu asifiwe mpendwa unayesoma Page hii,napenda nikuambie IPO sababu ya ki-MUNGU iliyokuleta hapa na MUNGU amekusudia jambo jipya juu yako Leo.

Unapoisoma habari hii ya Taifa teule LA Israel utagundua mambo haya:

(1)Kila jambo linalokutokea liwe baya au zuri katika ufahamu wako lina sababu katika kiti cha Enzi cha MUNGU, kuna wakati mambo yanakutokea ili MUNGU atangaze ukuu wake kupitia wewe katika eneo analokupitisha, sasa usipokuwa mtulivu katika eneo hilo una haribu Lengo LA MUNGU, na hapo ndipo laana inapoanzia..

Maana maandiko yanasema MUNGU Siku zote anakuwazia Mema,...

(2)MUNGU anaweza akampa Adui yako Nguvu ili akijiinu juu yako MUNGU naye asimame kwa ajili yako ikiwa tu utaendelea kuwa Muaminifu katika Majaribu, anasema "....NDIPO ADUI ZAKO WATAKUWA ADUI ZANGU....."

unapotoka hatua moja kwenda hatua ya mbele zaidi ni tafsiri kwamba unaacha hatua dhaifu zinazoyaongoza maisha yako na kuzielekea hatua zenye NGUVU zitakazo yaongoza maisha yako.

Hapa taifa LA Israel lilichoka kujenga uchumi Wa Misri, kubebeshwa na kufanyishwa kazi nzito, wakati huo hawakuwa na ufahamu walijionea sawa tu, tena waliongeza na bidii, lakini ukombozi Wa ufahamu ulipofanyika

Wakaumia sana na Kumlilia MUNGU, MUNGU akaleta Msaada..

Walipoianza safari walifurahi sanaa, waliambiwa wanaenda kanaani huko kuna maziwa na asali lakini njiani walikula na kusaza furaha yao ikawa inaongezeka,, hakika wakamtukuza MUNGU sana

Lakini ghafla ukisoma ;14:10-14
Mambo yanabadilika furaha inapotea,kiwango cha kumuamini MUNGU kinapungua, wanaona mbele Bahari wakti wasijue LA kufanya wanasikia nyuma yao Vishindo vya farasi na na magari ya vita

Ndipo wanakumbuka maneno yao ya nyodo waliomtamkia farao kwamba "tunaondoka kwako na watoto wetu na kila kitu chetu hata ukwato hatuach"

Wakashauriana wajitupe baharini lakini farao asiwaguse ,wakakubaliana lakin walipogeuka ilipo bahari wakashangaa kuona Bahari imesimama k**a ukuta tena imekasirika haswa wakaikumbuka Sala yao ya "lawama na mang'uniko"

Kutoka :14:11-12

Hii ni Sala ambayo wapendwa wengi wanaipenda wakiwa kwenye magumu,

Musa akawambia 14:13.(Soma)

MUNGU angeweza kuwaruhusu wavuke bahari kabla hata farao hajfika,
Hivyo tatzo LA bahari lingeisha lakin tatatzo LA farao kuwafuatilia wana Wa Israel lingeendelea maisha yao yote.

Sasa MUNGU akitaka tatzo lako liishe na likome kabisa uwa analiacha likue vizuri, wanaokudharau wajikusanye wote,k**a matusi wakutukane yote , ndipo anaichukua Aibu yako, mateso yako, anawrudishia adui zako Mara saba..

Muache MUNGU atengeneze utukufu kupitia hiyo shida yako.

Type AMENI utaona Mungu akitenda..

By Apostle K**age..
Kwa ushauri na huduma za kiroho
+255677593051 whatApp

03/12/2016
07/11/2015

MARA NYINGI UMEWAKARIBISHA WATU KWENYE MAISHA YAKO, SIKU YA MATESO YAKO HAWAKUKUSAIDIA, LEO MKARIBISHE YESU KWENYE MAISHA YAKO, NA AWEKE MAKAO MAISHA MWAKO.. WAPO WATU SIKU YA MATESO YAO WANAO WATU WANAWASAIDIA, SIKU YA MSIBA YAO WANAMFARIJI, WEWE NANI ATAKUFARIJI SIKU YA MATESO YAKO? NATAMANI KUOMBA NA WEWE LEO USOMAPO UJUMBE HUU shiriki ibada zangu nitumie namba yako ya whatsap nikuunge....BY PASTOR K**AGE

24/07/2015

''Walipo wawili watu wakakusanyika kwa ajili yangu, Nami ushuka kati yao''........ Ni maneno uliyoyazoea kuyatamka na kutamkiwa,
lakini nataka leo nikuambie kitu kilichojificha hapo. wakutanikapo watu wa Mungu kwa ajili ya Ufalme wake, kujadili iwe ni katika maombi, Kuhubiri, N.k Mungu utoa Upako wake katika jambo hilo
ili lifanikiwe na lazima mfanikiwe.. Watu wa MUngu kwa aliye Tayari
atume TXT yenye Jina lake,mahali alipo, kwenye namba 0655301117, nitakuwa nikituma meseji kwenye simu yako,yenye muongozo wa maombi, Neno, Hata kukuombea pia. MUNGU AKUBARIKI NA USIPUUZE K**A UMESOMA, MUNGU ANA KITU JUU YAKO, HIYO ROHO YA KUPUUZA NI SHETANI...

08/05/2015

BWANA YESU ASIFIWE, WAPENDWA KATIKA BWANA, WAKATI WA USIKU NI WAKATI MZURI KWA KUOMBA, TUMA MSG YENYE JINA LAKO, NA ULIPO PAMOJA NA NAMBA YAKO YA SIMU KWENYE 0655301117. NITAKUWA NIKIKUTUMIA MSG MUDA WA KUOMBA UKIFIKA NA MAMBO TUTAYOOMBA KWA SIKU HIYO... JINA LA BWANA LITUKUZWE MILELE.

30/06/2014

Kila jambo lina nguzo linazozitegemea, na kila utawala una nguzo unaotegemea.. vilevile utawala washetani umejengwa juu ya nguzo ziitwazo MAUTI na KUZIMU.. Ayubu 38:18 na nguzo hizi mbili ndizo ambazo zinashikilia utawala wa shetani na ndio maana maeneo mengi ambayo kuzimu inatajwa basin a mauti ipo pia.. mfano katika kitabu cha zaburi 116 :3 .. HAPA UTAONA kila mahali ambapo mauti imetajwa basi kuna mahusiano na kuzimu ..

MAANA YA MAUTI NA KUZIMU :

MAUTI ni roho ambayo kazi yake ni kuuondoa uhai ulio ndani ya mtu. Na KUZIMU ni roho ambayo kazi yake ni kuwahifazi wale waliokufa.. ufunuo 6: 9, Isaya 28 :15 ..

Mauti ni roho yenye akili na yenye kupanga.. ndio maana wanafunzi wa Yesu , walipomuona Yesu yuko juu ya maji, biblia inasema wanafunzi wa Yesu wakadhani wameona roho.. kumbe roho ina personality ina akili kili, inaweza kupanga na kutekeleza na pia yaweza kumpagaa mtu. Kwahiyo mauti ni roho yenye personslity hapo tunaweza sema mauti ni mtu.. Tunaweza sema mauti ni mtu ina “personality” ufunuo 20 : 13.. mauti inaweza kumeza watu..

ufunuo 20 : 14 kila mahali inapotajwa mauti kuzimu inafuata pale, hii inaonyesha kuwa mauti inaanza alafu kuzimu inafuata.. katika hiki kitabu cha ufunuo 20 : 14 tunaona kuwa “ mauti na kuzimu vikatupwa kwenye jehanamu” kumbe mauti unaweza uka ik**ata kabisa na kuitupa mahali.. k**a mauti na kuzimu vingekuwa ni matukio basi visingeweza kushikwa na kutupwa kwenye moto. Ndio maana Yesu alipokufa alishinda mauti na kuzimu. ( yohana 20 :3)

tuangalie hili andiko mwanzo 37:25 katika agano la kale kuzimu lilikuwa linatumika k**a mahali wafu walipokuwa wanakwenda, na palikuwa panaitwa “sheol” kwa lugha ya kingereza na huko wako wafu wote waliotenda haki na walitenda maovu walikuwa wanakwenda kule.. lakini palikuwa wamepagawa mahali pa watenda haki na mahali pa watenda maovu.. na mahali walipokuwa wanaenda watenda palikuwa panaitwa Kifuani pa Ibrahimu, ( yaani wale walioamua kuungana na imani ya Ibrahim) na sasa kunaitwa paradiso..

TOFAUTI YA JEHANAMU NA KUZIMU:

Jehanamu ni shimo la rohoni la moto watakapo angamizwa watu watendao dhambi, kwasasa jehanamu hakuna mtu ndani maana hukumu bado haijatolewa lakini watu wanaokufa kwa sasa wanaenda kuzimu (bottomless pit) hii ni roho iliyojifunua k**a shimo. Isaya 14:11,15 . tunaona shetani alipoasi akatupwa kwenye hilo shimo ndio maana ya maneno yaliyo katika kitabu cha ufunuo 12:7-9 kumbe kuzimu ipo hapa katika nchi, hapaonekani kwa kuwa lipo katika ulimwengu wa roho. Ufunuo 9:15 , KUZIMU ndio kwenye makao makuu ya shetani , wanakofanyia kazi zao.. (operation centre) ufunuo 17:8 .. kwa hiyo ni muhimu kujua kuzimo ipo angani, baharini na hata kwenye nchi.. ndio maana biblia inataja mara nyingu neon hili wakuu wa anga’

KAZI ZA KUZIMU NA MAUTI.

Kuzimu ndio inayo achilia uovu duniani, inaachilia magonjwa, tabu, dhambi, mateso, balaa,mikosi, ukimwi, kuchanganyikiwa, kuchukiwa na watu, inadhoofisha, inatesa na inaleta uhalibifu.. kwahiyo kuzimu inaleta roho ya uzinzi na uasherati, uovu na dhambi na hizi zote zinamfanya mtu kudhoofika na kuishiwa nguvu. Hapo sasa mauti ndo inakuja pale mtu anapokuwa kwenye comma. KWAHIYO kuzimu kazi yake ni kudhoofisha kwanza.. na ndio maana unaweza muona mtu anaumwa hadi kudhoofika sana lakini huyo mtu hafi.. hii ni kwasababu mashetani ya mauti hayajaanza kufanya kazi..

Hapo mgonjwa anapokuwa dhaifu ndipo sasa mauti inakuja na kufanya kazi yake, ya kumuua . na mauti ikifanikiwa kuutoa uhai basi sasa mauti inatuma mapepo wa kuja kumchukua Yule mtu k**a alikuwa mtenda dhambi.. na ndio maana utaona kuwa mtu anapotaka kufa waliowengi utawasikia wanasema maneno k**a ‘naona giza’ au msinichukue’ basi ujue wakati huo.

Kuzimu inaleta duniani hata mitindo ya kuvaa.. ili kuingiza tamaa za uzinzi na uasherati.. na unapoona tamaa ya dhambi inaongezeka basi jua unakaribia kufa.. k**a ulipangiwa kuishi miaka 80 utajikuta unaishi miaka 40.. kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.
Marko 16 :19-22.. Mtu anapokata roho anachukuliwa na malaika kwenda mbinguni au anachukuliwa na malaika kwenda kuzimu..

NGUZO MBILI ZA KIPINDI CHA SAMSON

SAMSON alikuwa mnadhiri alikuwa na jukumu la kuangamiza wafilisti, lakini wafilisti walimnasa baada ya kudanganywa na mkewe, ILI kutoa siri ya nguvu zake, baada ya kujua wafilisti wakmnyoa nywele , wakamtoboa macho na kumweka asage ngano, mfano huu wa Samson unaonyesha hali ya kanisa ya sasa baada ya kanisa kukosa nguvu, na kudharauriwa Mungu ameanza kulipa nguvu kanisa k**a nywele za samason zilipoanza kuota.. Samson alipopata nguvu akajitegemeza kwenye nguzo mbili ambazo jingo linazitegemea. Na akazitikisa hadi jingo lote likaanguka kabisa. Ndivyo kanisa linavyotakiwa kuwaangamiza nguzo za mauti na kuzimu.. ili liweze kurudi kwenye uweza wake na ndio maana ushindi wa Yesu msalabani kimsingi ni ushindi dhidi ya mauti…

MAUTI NA KUZIMU HAZINA NGUVU JUU YETU..

Address

Dar Es Salam

Telephone

+255655301117

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Apostle Kamage Betheli Ministry Church of TANZANIA-Mwanzo 28:16-19 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share