Jofrey Kaigarula Ministries

Jofrey Kaigarula Ministries NATIONS ALTAR CHURCH (NAC).

A prophetic and apostolic revival ministry transforming lives, restoring destinies, and igniting nations through the teaching of the Word, and the fire and power of God. The Working Altar Rhema Church [WARC] is the ministry owned by God Himself.Our assignment is to preach and teach the truth of the Word of God to people of all nations so that we can allow the Spirit of God Almighty to bring forth

Salvation and Deliverance through the blood of Jesus Christ,Healing,Restoration and all Spiritual Blessings that God kept for those whom He loved.

"Mwezi wa Urejesho wa Neema na Utukufu"Katika mwezi huu, tunatangaza kwa imani kwamba Mungu anarejesha kile kilichopotea...
01/05/2025

"Mwezi wa Urejesho wa Neema na Utukufu"

Katika mwezi huu, tunatangaza kwa imani kwamba Mungu anarejesha kile kilichopotea—neema yake ya wokovu, uponyaji, baraka, na utukufu wake unaotujaza tena kwa nguvu mpya. Ni wakati wa kuinuliwa tena, kufufuliwa kiroho, na kuona mkono wa Bwana ukitenda kwa wingi kuliko hapo awali.

““Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.”
— Hagai 2:9

Prophet Jofrey Kaigarula

https://youtube.com/?si=v3P5wP-wbrPIiZPcBwana Yesu asifiwe,  tunahitaji subscribers 50 tu ili kuweza kuanza kurusha vipi...
01/05/2025

https://youtube.com/?si=v3P5wP-wbrPIiZPc

Bwana Yesu asifiwe, tunahitaji subscribers 50 tu ili kuweza kuanza kurusha vipindi mubashara katika chanel yetu hii mpya, tunaomba mkono wako wa shirika kwa ku-subscribe na kubofya alama ya notification bell 🔔 . Ili leo leo tuweza kuanza kutumia account hii.

Asante sana

Welcome to the Official YouTube Channel of Prophet Jofrey Kaigarula! This is a God-ordained platform where Jesus Christ is touching lives through powerful teachings, prophecies, prayers, and divine wisdom from His servant, Prophet Jofrey Kaigarula. Prophet Kaigarula is the lead pastor of The Nations...

I give all glory to God for each of you—those who know me, love me, and follow my ministry, receiving the anointing and ...
16/02/2025

I give all glory to God for each of you—those who know me, love me, and follow my ministry, receiving the anointing and grace of God upon my life.

To my beloved wife, my parents, our pastors, evangelists, church leaders, workers, and every member of Nations Altar Church (NAC)—as well as my sons, daughters, friends, and partners across the world—your love and support through the years have been a great blessing.

Today, As I celebrate my birthday,I take this moment to speak blessings upon your lives. May God’s grace abound in all you do, and may His favor continue to lift you higher in Jesus Name.

With love and gratitude,

Prophet Jofrey Kaigarula
Nations Altar Church

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANAMAOMBI YA MFUNGO,JUMANNE, 28 JANUARI, 2025SIKU YA 23: KASI YA AJABUANDIKO LA MSINGI: “Anga...
28/01/2025

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANA
MAOMBI YA MFUNGO,
JUMANNE, 28 JANUARI, 2025
SIKU YA 23: KASI YA AJABU

ANDIKO LA MSINGI: “Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.”
— Amosi 9:13

UTANGULIZI:

Mstari huu unazungumzia wakati ambapo mchakato wa kawaida wa kilimo unavurugwa na kuingiliwa na Mungu kwa njia ya kipekee, ya kutisha na yenye kustaajabisha. Kawaida, kilimo kinafuata mchakato maalum: kulima, kupanda, kukuza, kuvuna, kisha kupumzika kabla ya kuanza tena. Lakini hapa, mvunaji anamfikia aliyelima, na mpandaji anamfikia anayekamua zabibu. Hii inaonyesha kuwa mavuno na baraka ni nyingi na za haraka sana kiasi kwamba muda wa kusubiri kati ya kupanda na kuvuna haupo.

Bwana anapohusika kwenye jambo akiwa na mukusudi ya kulifanikisha kwa haraka, kile ambacho kawaida huchukua muda—maendeleo, ukuaji, au ustawi—kinatimizwa haraka zaidi kwa uwezo wa Mungu. Hakika, Mungu akihusika, anaweza kuharakisha mchakato, kuondoa vikwazo, na kuleta baraka kwa kiwango cha ajabu sana.

Kwa kawaida, kilimo kinahitaji kazi ngumu, uvumilivu, na kusubiri matokeo. Hata hivyo, mstari huu unatufunulia wakati au kipindi ambacho mapambano na kuchelewa kunabadilishwa na urahisi kwa nguvu na hekima ya Mungu. Kuingiliana kwa kupanda na kuvuna kunaonyesha kuwa baraka zitakuja kwa haraka sana na kwa wingi kiasi kwamba hakutakuwa na muda wa kawaida wa kusubiri au changamoto. Unaweza kuona kwamba katika ufalme wa Mungu, hatuwaangushi wala kuwaza wengine washindwe ili tufanikiwe. Wakati Bwana anakufanikisha wewe kwa haraka, wale aliowafanikisha mwanzo ambao wapo katika kipindi cha kila mavuno wanaendelea na kipindi cha mavuno kwa muda mrefu. Wakati kanisa moja linakuwa na kuongezeka, lingine linaendelea kukusanya maelfu ya waamini na kuwafundisha njia za Bwana.

Nabii Amosi anaendelea kuona divai mpya ikitiririka kutoka milimani na kutoka kwenye vilima vyote. Kawaida tunajua kwamba milimani na kwenye vilima kilimo hakifanyi vizuri sana k**a sehemu za mabondeni na tambalale, lakini kwa mkono wa Bwana tunaona maeneo yasiyotarajiwa kuwa na uzalishaji yakizalisha, maeneo ambayo uzalishaji ni mdogo yanazalisha sana . Mungu anaweza kuwafanya wasio na elimu wawe wakuu na hata kuwatumikisha wenye elimu, Mungu anaweza kuwafanya watu wanyonge kabisa katika jamii kubwa waokozi wa hiyo jamii.

MAARIFA YA KUSHIKA : Baraka za Mungu zinaweza kutoka mahali tusipotarajia au tusipodhani panaweza kuzaa matunda. Mungu akihusika jumla katika jambo, ustawi utakuwa mwingi sana kiasi cha kufurika, zaidi ya uwezo wa mwanadamu kuhimili au kudhibiti. Hata maeneo kame au yasiyozaa matunda katika maisha yako yanaweza kubadilishwa na kuwa vyanzo vya baraka na ustawi mkubwa.

Ni vema unapotafuta ustawi na mafanikio kwa Bwana uwe na picha ya Mungu anavyotaka uwe kuliko picha ya umasikini, unyonge, changamoto na masumbufu yako. Sara kwa kuangalia umri wake aliicheka ahadi ya Mungu lakini Bwana alimwonyesha kwamba kinachompa mtu ujauzito sio mzunguko wa siku zake bali ni mzunguko wa mawazo na hukumu za Mungu kwenye maisha yake.

ANDIKO LA HEKIMA: “Mkono wa Bwana ulikuwa juu ya Eliya; akajikaza viuno, akapiga mbio mbele ya Ahabu mpaka kuiingia Yezreeli.” — 1 Wafalme 18:46

MWONGOZO WA MAOMBI: Leo utaomba Mungu aingilie maisha yako kwa namna ya tofauti, hususani katika maeneo ambayo unaona umecheleweshwa, maeneo ambayo unajua Bwana anapaswa kuwa mbali lakini huoni mabadiliko, maeneo ambayo kwa akili zako umejaribu kuvuka lakini ni k**a jitihada zako hazikusaidii kwa lolote.

MISHALE YA MAOMBI:

• “Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.” — Amosi 9:13

1. i) Baba wa mbinguni, ninakuomba uniletee kasi ya kiungu katika kila eneo la maisha yangu, ili mavuno yangu yawe tele na ya haraka kwa jina la Yesu.

ii) Ee Bwana, ninatangaza kwamba kila kuchelewa au kusimama kwa maendeleo yangu kunavunjwa sasa kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Kila giza lililosimama kuzuia mafanikio yangu, ligeuke kuwa nuru kwa jina la Yesu.

iii) Mungu wangu, badilisha maeneo yote tasa au yasiyo na matunda katika maisha yangu kuwa vyanzo vya baraka nyingi na za haraka kwa jina la Yesu.

• ²⁵ Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.²⁶ Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
— Yoeli 2:25-26

2. i) Ee Mungu wa urejesho, nirejeshee miaka yote ambayo nilipoteza kwa kuchelewa, matatizo, na changamoto.

ii) Baba, harakisha urejesho wangu na uniletee ushindi wa kipekee katika maisha yangu kwa jina la Yesu.

iii) Bwana, ninatangaza kwamba nitakula na kushiba, na nitashuhudia baraka zako haraka zaidi kuliko matarajio yangu.

• “Mdogo atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, Bwana, nitayahimiza hayo wakati wake.” —Isaya 60:22

3. i) Bwana, niharakishe kufanikisha maono y angu, na nikue kutoka udogo hadi ukuu kwa uwezo wako wa kiungu.

ii) Mungu wangu nakuomba, fanya mambo makubwa yanipate kwa kasi, na jina lako litukuzwe kupitia ushuhuda wangu.
iii) Ee Bwana, kila baraka iliyocheleweshwa katika maisha yangu iharakishwe kwa jina la Yesu!

• “Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.” — Zaburi 18:29

4. i) Baba, nipe nguvu na kasi ya kushinda kila jeshi linalosimama kinyume na maendeleo na ustawi wangu kwa jina la Yesu.

ii) Ee Bwana, niongezee kasi ya kiungu ili nivuke vizuizi vyote vya adui kwa nguvu zako za ajabu.

iii) Mungu wangu, kila ukuta wa kuchelewa katika maisha yangu uanguke sasa kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

• Isaya 41:18

“Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji.” — Isaya 41:18

5 . i) Ee Mungu, nifanyie njia katika kila jangwa la maisha yangu, na uniletee kasi ya kiungu kuelekea mafanikio na hata yangu.
ii) Baba, badilisha kila ukame wa kiroho, kifedha, na kihisia kuwa misimu ya tele na ustawi.

iii) Bwana, achilia baraka zako kwa haraka hata mahali ambapo hakujawahi kuwa na matumaini ya kufanikiwa.

MAELEKEZO:

• Maombi ni ya siku 42, tutafunga masaa 12 kila siku bila kunywa maji wala chakula. Tutafungua saa 12 jioni, mwisho wa kula chakula ni kabla ya saa 03:00 usiku. Usile tena chakula baada ya hapo. • Masaa ya kuomba na kusoma maandiko yaliyomo kwenye kila mwongozo ni kati ya 12:00 Asubuhi, 03:00 Asubuhi, 06:00 Mchana, 09:00 Alasiri, 12:00 Jioni, 03:00 Usiku, 06:00 Usiku, 09:00 Usiku. • Watu wote tulioko Dar es Salaam tunakutana kujifunza Neno na kuomba kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa saa 10:30 Jioni mpaka saa 12:30 Jioni hapa kanisani Nations Altar Church (NAC) - Mbezi kwa MSUGURI. Unaweza kupiga simu 0716298890 ili kuweza kufika. • Siku za Jumamosi na Jumapili tunakutana kuanzia saa 03:00 Asubuhi mpaka saa 08:00 Mchana kwa ajili ya Mafundisho Na Maombi.

Prophet Jofrey Kaigarula
Nations Altar Church (NAC)
Mbezi Msuguri, Dar es Salaam, Tanzania.

23/01/2025

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANA
MAOMBI YA MFUNGO,
ALHAMISI, 23 JANUARI, 2025
SIKU YA 18: KUMTUKUZA MUNGU KATIKA MWILI

ANDIKO LA MSINGI:
“Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
— 1 Wakorintho 6:20

---

UTANGULIZI:

Neno "MTUKUZENI" lililotumika katika 1 Wakorintho 6:20 limetokana na neno la Kigiriki "doxazō," linalomaanisha "kuheshimu; kutambua kwa namna chanya, au kuthamini tabia, asili, au sifa za mtu." Paulo anawasisitiza Wakristo kuheshimu na kutambua kila kitu wanachojua kuhusu tabia takatifu ya Mungu kwa kutumia miili yao ya kibinadamu. Sio tu kutambua kwa ufahamu, bali kutambua kunakohusisha kuhamisha ufahamu na heshima hiyo kwenye miili yao. Mungu anataka matendo na tabia zetu kuwa na mfanano wa utakatifu Wake katika kila tunachofanya.

Ufahamu huu unaanza kutambua jinsi Mungu anavyoheshimu mwili wa mwamini. Paulo anatoa ufunuo kwamba miili yetu ni hekalu la Roho wa Mungu, na anasema hivi ili kutufundisha tumtukuze Mungu katika miili yetu na kuwa na ufahamu kwamba tunatukuza hekalu takatifu la Mungu.

“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;”
— 1 Wakorintho 6:19

Muktadha wa andiko hili ulilenga katika kuliheshimu hekalu la Mungu kwa kutoruhusu uchafu kuingia. Hapa alilenga zaidi kuhusu usafi kingono. Unaweza kuona maneno ya mtume Paulo,

1 Wakorintho 6:14-20
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.
¹⁵ Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
¹⁶ Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
¹⁷ Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
¹⁸ Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
¹⁹ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
²⁰ maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Kuwa safi katika mambo ya zinaa ndiko kunaweza kutufanya tuheshimu miili yetu. Usafi wa kingono unaanzia katika kutofanya, kutowaza wala kutojiweka katika mazingira ya kushawishi wengine kutamani kufanya. Ni kweli kuna tamaa iliyokithiri kwenye mioyo ya watu inayoweza kuwafanya watu watamani hata k**a wanaowatamani hawajajiweka katika mazingira au hali ya kutamaniwa, hayo ni makosa yao. Lakini wewe k**a Mkristo hupaswi kujiweka katika mazingira au hali ya kuwafanya wengine wasio na mawazo machafu kukuwazia uchafu ndani au nje ya kanisa. Ukiwa na ufahamu huu hutahitaji mtu akufundishe namna ya kusitiri mwili wako. Utajua jinsi ya kujiweka katika hali ya kumwonyesha Mungu katika mwili wako pia.

Wale wote wanaosema Mungu huangalia moyo, wako sahihi. Lakini ni lazima wajue kuwa yote ya nje ambayo mtu anafanya ni kwa sababu ya taarifa zilizopo moyoni mwake; tabia za watu na matendo yao ni matokeo ya mambo yaliyomo mioyoni mwao. Kabla mtu hajatukana matusi, tayari moyoni mwake ana kifurushi cha matusi; kabla mtu hajaamua kuanika maungo yake, anakuwa uchi kwanza kwenye moyo wake. Mungu anaangalia moyo ndiyo, ila hawezi kukuta chochote kilicho tofauti na kile anachofanya mtu nje (Luka 6:45).

---

MAARIFA YA KUSHIKA:

Ingawa ulimwengu unaenenda katika uchafu na uasi mwingi, nataka nikwambie kwamba unaweza kuwa msafi katika ulimwengu uliiooza na kunuka. Wengi wetu tunahisi aibu kwa sababu tumekosea mara kadhaa katika uchafu huu kwa muda mrefu. Lakini, kuna msamaha kwa Kristo Yesu kwa ajili yetu k**a tukiamini na kupokea. Ikiwa unajikuta ukiishi na aibu, hukumu, na kusutwa ndani yako kutokana na dhambi ya uasherati au uzinzi ya zamani au labda unashiriki katika hiyo katika kipindi hiki cha maisha yako, unaweza kufunguliwa kabisa kutoka katika hali hiyo ngumu. Kiri mbele za Mungu na omba msamaha Wake. Kisha, acha mambo hayo yabaki kuwa historia iliyosahauliwa katika maisha yako maana wewe ni kiumbe kipya katika Bwana, ishi katika upya wa utukufu Wake kila siku.

“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”
— 1 Yohana 1:9

Tunamuheshimu Mungu kwa kuamua kubaki safi kimaadili, hata tuache kabisa kushiriki ngono nje ya ndoa au kabla ya ndoa na ibaki kuwa zawadi kwetu katika ndoa pekee. Tunaweza kufanya hivi kwa sababu Mungu ametupa neema ya kufanya hivyo. Ujue mwili wako, uheshimu, na uuweze katika Bwana. Kumbuka kwamba, hutaweza kabisa kumtukuza Mungu katika mwili wako bila kuwa na tunda la Roho Mtakatifu.

---

ANDIKO LA HEKIMA:

1 Wathesalonike 4:2-5
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
³ Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
⁴ kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
⁵ si katika hali ya tamaa mbaya, k**a Mataifa wasiomjua Mungu.

---

MWONGOZO WA MAOMBI:
Mkabidhi Bwana mwili wako, mwambie akufundishe kuishi maisha ya kumpendeza. Na akupe nguvu za kushindana na mwili wako hata uwe kiongozi wake na sio mwili wako ukutawale. Sulibisha mawazo yote mabaya ndani yako na kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kukutawala.

---

MISHALE YA MAOMBI:

• “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, k**a iwastahilivyo watakatifu;”
— Waefeso 5:3 (Biblia Takatifu)

1. i) Kwa uaminifu na haki yako, unitakase na kunifanya kuwa safi Ee Bwana. Unisamehe na kuniondolea udhalimu wote ulionijia kwa sababu ya dhambi.
ii) Hakuna kinywa kitainuka na kutaja habari za uchafu wa kingono kwangu na iwe kweli, Bwana, utaniepusha na uchafu wote.
iii) Bwana, neno lako likaweke mpaka kati ya baraka na laana kwenye maisha yangu, mpaka kati ya furaha na huzuni, nguvu na udhaifu, haki na dhuluma, nimechagua kukufuata naomba unipe neema ya kukutukuza katika mwili wangu.

• “Jitengeni na ubaya wa kila namna.”
— 1 Wathesalonike 5:22

2. i) Ubaya nifanyao ambao umekuja k**a wema hata nisiweze kutambua, Ee Bwana, nipe macho nione.
ii) “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]” — Mathayo 6:13
iii) Bwana nipe hekima ya kutambua hila za adui na kumshinda katika jina la Yesu.

• “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.”
— 1 Wakorintho 10:31

3. i) Roho Mtakatifu, nifundishe kukutukuza katika kila jambo. Ongoza hatua za matendo yangu ili nisiifanye neema yako kutukanwa kwa jina la Yesu
ii) Nirejeshee furaha ya wokovu wangu Ee Bwana, nipe neema ya kuleta utukufu kwako kupitia kila ninachofanya kwa jina la Yesu
iii) Moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisikutende dhambi, neno lako Bwana liwe hai na katazo kuu la uasi ndani yangu.

---

Wagalatia 5:24-25
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁴ Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
²⁵ Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

---

4. i) Ninapokea nguvu za kuishi na kuenenda kwa roho, kila chembe ya uovu ndani yangu, mawazo mabaya na tamaa mbaya na vinyamaze kwa damu ya Yesu
ii) Ninasulibisha kila nguvu ya tamaa za mwili ndani yangu, Mimi ni mshindi dhidi ya dhambi kwa sababu ya neema ya Mungu ndani yangu.
iii) Malango ya neema na kibali yafunguke katika maisha yangu kwa jina la Yesu.

---

“Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.”
— Yakobo 1:14

---

5. i) Kila mlango wa fahamu ambao adui anatumia kupitisha uovu katika mwili wangu, Ee Bwana, Roho Mtakatifu uwe mwalimu na mlinzi katika malango ya fahamu zangu na mwili wangu
ii) Ee Bwana, unilinde na kila hila za adui kuniweka katika hali ya utumwa wa dhambi, sitarudi nilipotoka kwa jina la Yesu.
iii) Nakataa kusikia sauti za udanganyifu kunivuta katika uovu. Mimi ni mtakatifu wa Mungu, sitatamani hata tone la tamaa ndani yangu kamwe.

MAELEKEZO:
• Maombi ni ya siku 42, tutafunga masaa 12 kila siku bila kunywa maji wala chakula. Tutafungua saa 12 jioni, na mwisho wa kula chakula ni kabla ya saa 03:00 usiku. Usile tena chakula baada ya hapo.
• Masaa ya kuomba na kusoma maandiko yaliyomo kwenye kila mwongozo ni kati ya 12:00 Asubuhi, 03:00 Asubuhi, 06:00 Mchana, 09:00 Alasiri, 12:00 Jioni, 03:00 Usiku, 06:00 Usiku, 09:00 Usiku.
• Watu wote tulioko Dar es Salaam tunakutana kujifunza Neno na kuomba kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa saa 10:30 Jioni mpaka saa 12:30 Jioni hapa kanisani Nations Altar Church (NAC) - Mbezi kwa MSUGURI. Unaweza kupiga simu 0716298890 ili kuweza kufika.
• Siku za Jumamosi na Jumapili tunakutana kuanzia saa 03:00 Asubuhi mpaka saa 08:00 Mchana kwa ajili ya Mafundisho na Maombi.

Prophet Jofrey Kaigarula
Nations Altar Church (NAC)
Mbezi Msuguri, Dar es Salaam, Tanzania.

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANAMAOMBI YA MFUNGO,JUMATANO, 22 JANUARI, 2025SIKU YA 17: UPAKO WA ENHAKOREANDIKO LA MSINGI:“...
22/01/2025

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANA
MAOMBI YA MFUNGO,
JUMATANO, 22 JANUARI, 2025
SIKU YA 17: UPAKO WA ENHAKORE

ANDIKO LA MSINGI:
“Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, nalo lipo katika Lehi hata hivi leo.” — Waamuzi 15:19

UTANGULIZI:
Mungu akiingilia jambo la mtu, ushindi siyo jambo la kuuliza. Nimewafundisha watu jinsi ya kumfanya Mungu ahusike na mambo yao na kuwapa ushindi katika nyakati zote ngumu au nyakati za mashindano na majaribu. Biblia inazifunua kanuni nyingi k**a sadaka ya dhabihu, sadaka za kiagano k**a zaka na malimbuko, sadaka kwa ajili ya wahitaji, unyenyekevu kwa watumishi wa Mungu na watu wenye mamlaka, heshima kwa wazazi, shukurani, sifa kwa Mungu, na mambo mengine mengi. Lakini katika yote, hakuna njia inayofanya kazi haraka katika kumleta Mungu kwenye maisha yako k**a maombi na utii katika neno lake.

Maombi ni silaha kubwa sana ya mwamini, na lazima ifahamike kwamba mwamini hawezi kamwe kuishi maisha ya ushindi katika ulimwengu huu bila kuishi maisha ya maombi. Hatupaswi kuwa na maisha ya maombi k**a kitu cha ziada; maombi lazima yawe sehemu ya maisha yetu k**a vile kula chakula, kuoga, kulala, kujisaidia na mambo mengine ya lazima. Hakuna mtu ambaye anasema ana maisha ya kula, maisha ya kulala; kwa nini iwe na maisha ya maombi? K**a mtu atalala mara moja kwa siku au masaa matatu au kumi, haitapoteza ukweli kwamba hawezi kuishi bila kulala. Huu ndio mtazamo ambao mwamini anapaswa kuwa nao—kwamba hawezi kuishi kabisa, hawezi kamwe kuishi bila maombi.

Tuangalie jinsi Mungu alivyomsaidia Samsoni kuwapiga wanajeshi wa Wafilisti 1000 kwa utaya wa punda.

Waamuzi 15:14-17
¹⁴ Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa k**a kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. ¹⁵ Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa huo; ¹⁶ Samsoni akasema, “Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, kwa taya ya punda nimepiga watu elfu.” ¹⁷ Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena, akautupa ule mfupa wa taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi.

Siri ya ushindi wa Samsoni ilikuwa ni ujio wa roho ya Bwana juu yake. Asingeweza kuyafanya haya kwa nguvu zake mwenyewe. Lakini baada ya ushindi huu, angalia kile anachosema; hamtukuzi Mungu. Anasema, “Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, kwa taya ya punda nimepiga watu elfu.” Samsoni alijua kuwa aliyemsaidia kufanya hayo ni Bwana, lakini hakumtaja kabisa; alijisemea yeye mwenyewe. Tunaweza kugundua kwamba Samsoni alijua kuwa ni Bwana aliyempa ushindi, kwa kuangalia maombi yake baada ya hapo.

Waamuzi 15:17-19
¹⁷ Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena, akautupa ule mfupa wa taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi. ¹⁸ Kisha akaona kiu sana, akamwita Bwana akasema, “Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa mtumishi wako; na sasa nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu wasiotahiriwa.” ¹⁹ Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.

MAARIFA YA KUSHIKA:
Kuna hakikisho katika Bwana kwamba anaweza kukushindia vita zako zote. Mungu anaweza kuja kwako kwa sababu ya agano lake na wewe, k**a tunavyoona alivyoacha roho yake ije juu ya Samsoni. Hatuoni Samsoni akiomba maombi yoyote ili Bwana ampe msaada kuwapiga Wafilisti, lakini tunaona kuwa Bwana alimtetea Samsoni kwa sababu alikuwa mkananishi wake, alikuwa na agano naye. Ndio, kuna baadhi ya mambo ambayo unaona Mungu anafanya kwako bila kuomba, lakini isikupe kiburi kwamba utafanya mengine bila maombi. Mtu ambaye haombi ili kupata fedha na mahitaji fahamu kuwa kuna kitu pia anapata kwa kuomba; usijilinganishe na mwingine. Unachopata wewe bila kuomba, mwingine anapata kwa maombi. Kuna watu wanapata watoto bila maombi, sadaka wala kuhangaika, lakini wengine watapata watoto kwa sadaka, maombi, na kulia mbele za Bwana. Kubwa katika yote ni kwamba yote hufanywa kwa utukufu wa Mungu na kwa hekima yake mwenyewe. Usiingie katika mtego wa kuiga maisha ya mtu; k**a mtu anaomba saa moja kwa siku na mambo yake yanaenda, haina maana wewe ukifanya k**a yeye mambo yataenda pia. Acha Roho Mtakatifu akupimie kipimo chako.

Samsoni anapobanwa na kiu, hasubiri tena roho wa Bwana aje juu yake na kumsaidia k**a ilivyotokea kwa Wafilisti. Anaamua kumwalika Mungu katika jambo lake. Nilikwambia kwamba tunaweza kuona kuwa Samsoni alijua wazi kuwa msaada wa kwanza alipata kwa Mungu, na tunaweza kuthibitisha hilo kwa kuangalia maombi yake.

“Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa mtumishi wako; na sasa nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu wasiotahiriwa.”

Maombi haya yalikuwa ni ya kumchoza au kumsuta Mungu; hayana tofauti na maombi ya Musa wakati Mungu anataka kuwaua Waisraeli wote na kumwacha Musa na uzao wake. Musa aliongea maneno k**a haya.

Unachoweza kujifunza hapo ni kwamba tunapoomba, Mungu anahusika nasi moja kwa moja. Kwa mara nyingine, tunaona Mungu akifanya jambo na kumpa matokeo Samsoni. Hakuitwa mara ya kwanza, lakini alipoitwa hapa, alikuja na kufanya jambo.

“Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.”
— Waamuzi 15:19

Maana ya neno Enhakore ni KISIMA CHA MTU ALIYELIA, AU CHEMCHEM YA MTU ALIYEPAZA SAUTI YAKE.

Na kweli, Samsoni baada ya kumlilia Bwana, Bwana anapasua mahali penye shimo na kinachotoka hapo siyo tu maji, bali maji ya uzima, yenye uwezo wa kurejesha nguvu, kuleta burudani na kumfanya mtu apate nafasi na kuheshimiwa.

Katika yote unayopitia, umemwita Bwana? Umemlilia Bwana? Jibu likiwa hapana, basi mwite Bwana. Jibu likiwa ndiyo, basi mwite tena ukiwa na ufahamu huu mpya. Mungu atakupa majibu yenye uzito.

MWONGOZO WA MAOMBI:
Leo tutaomba k**a jana. Ni suala la mahitaji yetu. Hata hivyo, kutokana na ufahamu huu mpya, naamini utaomba kwa nguvu zaidi. Paza sauti yako k**a vile na Bwana atakutiririshia maji ya faraja na ushindi.

MISHALE YA MAOMBI:

• “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” — Warumi 8:32

1. i) Ee Bwana, ninayo mahitaji mengi kwenye maisha yangu, naamini huwezi kushindwa kunisaidia na kunivusha. Nivushe Bwana.
ii) Achilia wasaidizi wa hatma yangu kwa wingi, kutoka kila pande za ulimwengu waje na kuwa msaada kwangu.
iii) Ee Bwana, shughulika na maisha yangu, niondolee kila vikwazo vinavyojijia na kunisumbua kwa jina la Yesu.

• “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”
— Warumi 8:26

2. i) Roho Mtakatifu, bado sijui kuomba inipasavyo kuomba, k**ata kinywa changu, akili, mwili, roho na nafsi yangu unifundishe kuomba.
ii) Bwana, nisaidie maisha yangu ya maombi, natamani kuomba bila kukoma, kuomba kwa usahihi na kuomba kwa muda mrefu. Rekebisha maisha yangu ya maombi.
iii) Roho wa Mungu, niombee mapenzi ya Mungu yatimizwe kwangu, niombee kwa kuugua, Bwana anayasikia maombi yako mno. Nisaidie kuomba.

• “Kwa kuwa k**a katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.” — 1 Wakorintho 15:22

Pata muda leo kuomba kwa ajili yako, unajua mahitaji yako, mwambie Bwana kwa imani atakupa.

MAELEKEZO:
• Maombi ni ya siku 42, tutafunga masaa 12 kila siku bila kunywa maji wala chakula. Tutafungua saa 12 jioni, na mwisho wa kula chakula ni kabla ya saa 03:00 usiku. Usile tena chakula baada ya hapo.
• Masaa ya kuomba na kusoma maandiko yaliyomo kwenye kila mwongozo ni kati ya 12:00 Asubuhi, 03:00 Asubuhi, 06:00 Mchana, 09:00 Alasiri, 12:00 Jioni, 03:00 Usiku, 06:00 Usiku, 09:00 Usiku.
• Watu wote tulioko Dar es Salaam tunakutana kujifunza Neno na kuomba kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa saa 10:30 Jioni mpaka saa 12:30 Jioni hapa kanisani Nations Altar Church (NAC) - Mbezi kwa MSUGURI. Unaweza kupiga simu 0716298890 ili kuweza kufika.
• Siku za Jumamosi na Jumapili tunakutana kuanzia saa 03:00 Asubuhi mpaka saa 08:00 Mchana kwa ajili ya Mafundisho na Maombi.

Prophet Jofrey Kaigarula
Nations Altar Church (NAC)
Mbezi Msuguri, Dar es Salaam, Tanzania.

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANA MAOMBI YA MFUNGO,JUMATATU, 20 , JANUARI, 2025SIKU YA 15 : ROHO YENYE KUHUISHAANDIKO LA MS...
20/01/2025

SIKU 42 ZA UTUKUFU UNAOONEKANA
MAOMBI YA MFUNGO,
JUMATATU, 20 , JANUARI, 2025
SIKU YA 15 : ROHO YENYE KUHUISHA

ANDIKO LA MSINGI: “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.” — 1 Wakorintho 15:45

UTANGULIZI: Maisha ya utukufu katika ulimwengu huu hutegemea chanzo cha utukufu. Kuna watu wanazo sifa kuu lakini utukufu walionao wamepewa na shetani. Ndio, kuna watu ni mashuhuri, watu maarufu, matajiri na wenye sifa mno, lakini ukweli ni kwamba chanzo cha utukufu wao ni shetani, udanganyifu, uovu, kuua na kutoa kafara wengine, ngono, na mambo mengine yaliyo machafu ya ulimwengu huu. Hata hivyo, katika ulimwengu ulioharibika mno,wapo watu ambao ni raia wa mbinguni, watu ambao uchumi wao hauangalii uchumi wa dunia bali utukutu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Paulo mtume, anapowabariki Wafilipi anaonyesha chanzo cha kubarikiwa kwao sio cha ulimwengu huu.

“Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”
— Wafilipi 4:19

Mungu bado anabariki, Mungu bado anaweza kuhusika na maisha yetu ya kila siku yenye kujaa ushindi, mafanikio, shuhuda na utukufu mwingi mno.

Wakati asili yetu ya mwanzo inawaza kukata tamaa, asili yetu mpya inapiga kelele kutuambia tusonge mbele. Wakati Adamu wa kwanza anaachilia mauti, Adamu wa pili anaachili uzima. Adamu wa kwanza aliyekuja kwa njia ya uumbaji alituachia urithi wa mauti kwasababu ya dhambi, wakati Adamu wa pili aliyezaliwa kwa roho alituachia urithi wa uzima kwa haki yake na kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

MAARIFA YA KUSHIKA : Mungu hawezi kututukuza bila Yesu Kristo na Kristo hawezi kututukuza bila Roho Mtakatifu. Maandiko yanasema wao ni umoja, na kwasababu hiyo Kristo anapoachilia utukufu aliopewa na Mungu kwetu lengo kuu ni kutufanya kuwa wamoja.

“Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja k**a sisi tulivyo umoja.”
— Yohana 17:22

Kupitia Neno la Mungu, Roho Mtakatifu anaachiliwa na kutuimarisha katika hali ya uzima kila siku.

“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”
— Yohana 6:63

Mtu anayelisikia Neno la Mungu kila siku na kilishika, maisha yake yote yatatawaliwa na uzima, utukufu wa Mungu utafunuliwa na kuwa dhahiri kila siku maana Roho wa Mungu ni roho mwenye kuhuisha

ANDIKO LA HEKIMA : “Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.” — Warumi 8:11

MWONGOZO WA MAOMBI: Leo maombi yako yaelekezwe kwenye kuboresha mahusiano yako na Roho Mtakatifu, Roho ahuishaye. Mungu akusaidie kumsikia na kumtii na kuenenda katika uzima wa nuru yake ili utukufu wa Mungu ufunuliwe kwa ukubwa katika maisha yako. Lakini tutafanya maombolezo na maombezi kwa ajili ya watu ambao hawajamjua Kristo aliye Bwana wa utukufu bado, ili nuru hii ya utukufu ikawazukie wapate kuamini na kuokoka waupate uzima wa milele.

MISHALE YA MAOMBI :

• “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.”
— Yohana 3:5

• 1 Timotheo 2:3-4
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³ Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
⁴ ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.

“Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”
— Isaya 55:11

“ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”— 2 Wakorintho 4:4

1. i ) Bwana Yesu, k**a ulivyonipa uzima na wokovu kupitia kukuamini wewe, naiachilia nuru yako kwao wasiokujua kwa jina la Yesu. Jifunue kwao na kuwajalia kuiamini injili kwa kina la Yesu

ii ) Kila nguvu za ulimwengu huu, nguvu za giza zinazowapofusha watu wako wasiuone upendo wako na kuiamini injili, nalikemea, acha wa Mungu wa Mungu waokoke kuanzia leo kwa jina la Yesu.

iii ) Ninalituma neno lako la ukombozi na wokovu, neno lako la faraja na upendo, neno lako la uzima na amani kwenye mioyo ya watu ninaowafahamu na nisiowafahamu, waokoke na kuyaacha maasi ya ulimwengu huu kwa jina la Yesu.

• “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.”— Obadia 1:17

• “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”— Yohana 3:6

2. i ) Katika jamii yangu watakuwepo wenye kuokoka, katika familia yangu watakuwepo wengi wenye kuokoka, ninatabiri, katika kanisa letu watakuja maelfu na kuokoka kwa jina la Yesu.

ii ) Kila madhabahu za giza zilizoshikilia watu wasiokoke katika familia yangu, katika mtaa wangu, katika kitongoji changu, katika tarafa yangu, katika mji wangu, katika nchi yangu, katika bara langu na katika ulimwengu mzima, damu ya Yesu shughulika nazo, Roho Mtakatifu shughulika nazo, watu wa Mungu waachiliwe na kuipata nuru ya wokovu.

iii ) Ee Bwana, kwa Neno lako na kwa Roho wako jikusanyie maelfu, jikusanyie mataifa, nawaachilia malaika wa mavuno wakatende kazi na watendakazi shambani mwako, okoa watu kwa mkono wako hodari.

• “Kwa kuwa k**a katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.” — 1 Wakorintho 15:22

3. i) Ninapokea nguvu ya kuhuishwa ndani yangu, kila ambacho nilikuwa nimepoteza nguvu ya kufanya, napata nguvu upya.

ii ) Kila miaka niliyopoteza katika ujinga, katika dhambi, katika tabia za mwilini Ee Bwana kwa Roho Mtakatifu wako unirejeshee

iii ) Unitie nguvu ee Bwana, unihuishe sawa sawa na neno lako.

• Wagalatia 5:16-17
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.¹⁷ Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

Wagalatia 5:24-25
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁴ Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. ²⁵ Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

4. i ) Ninapokea nguvu za kuishi na kuenenda kwa roho, sitayatimiza mapenzi ya mwili kuanzia sasa, Roho Mtakatifu nisaidie

ii ) Kila mashindano ya mwili na roho ndani yangu, naamua kwamba roho na ishinde ndani yangu kwa jina la Yesu.

iii ) Kila mlango wa utukufu, uliokuwa umefungwa kwenye maisha yangu, naufungua kwa jina la Yesu

• “Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.” — Waefeso 1:12

5. i ) Kila kilichowekwa chini ya mamlaka yangu na kigeuke kuwa utukufu wa Mungu kuanzia sasa kwa jina la Yesu

ii ) Utukufu wa Mungu na uzidi kuonekana na kuongezeka katika maisha yangu kwa jina la Yesu

iii ) Baraka za Mungu za rohoni , mwaka huu zitathibitishwa katika mwili na utukufu wa Mungu utaonekana kwa jina la Yesu.

MAELEKEZO :

•Maombi ni ya siku 42, tutafunga masaa 12 kila siku bila kunywa maji wala chakula. Tutafungua saa 12 jioni, mwisho wa kula chakula ni kabla ya saa 03: 00 usiku. Usile tena chakula baada ya hapo.
• Masaa ya kuomba na kusoma maandiko yaliyomo kwenye kila mwongozo ni kati ya 12:00 Asubuhi, 03:00 Asubuhi, 06:00 Mchana, 09:00 Alasiri, 12:00 Jioni, 03:00 Usiku , 06:00 Usiku, 09:00 Usiku.
• Watu wote tulioko Dar es salaam tunakutana kujifunza Neno na kuomba kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa saa 10:30 Jioni mpaka saa 12:30 Jioni hapa kanisani Nations Altar Church ( NAC) - Mbezi kwa MSUGURI. Unaweza kupiga simu 0716298890 ili kuweza kufika.
• Siku za Jumamosi na Jumapili tunakutana kuanzia saa 03:00 Asubuhi mpaka saa 08:00 Mchana kwa ajili ya Mafundisho Na Maombi.

Prophet Jofrey Kaigarula
Nations Altar Church ( NAC)
Mbezi Msuguri, Dar es salaam, Tanzania.

Address

NATIONS ALTAR CHURCH, MBEZI MSUGURI, MSINGWA, NEAR HEBRON PRIMARY SCHOOL
Dar Es Salam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
17:00 - 22:00

Telephone

+255713474790

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jofrey Kaigarula Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Jofrey Kaigarula Ministries:

Share