Ark of Salvation Ministries

Ark of Salvation Ministries Huduma ya Injili ya kweli, kuwafundisha watu wokovu, toba, na maisha ya utakatifu kwa maandalizi ya kuja kwa YAHUSHA HAMASHIACH.

Shalom family welcome let's take another edifying lesson that the Spirit of YAH has lead me to share with you.THE REVELA...
15/07/2026

Shalom family welcome let's take another edifying lesson that the Spirit of YAH has lead me to share with you.

THE REVELATION OF GRACE AND THE TIME OF SALVATION

Main Scripture

2 Corinthians 6:1–2 (NKJV)

"We then, as workers together with Him also plead with you not to receive the grace of God in vain. For He says: 'In an acceptable time I have heard you, and in the day of salvation I have helped you.' Behold, now is the accepted time; behold, now is the day of salvation."

Scripture Explanation

The Apostle Paul teaches that God's grace is not something to be treated lightly. The right time to receive His grace is now, not tomorrow. Grace is God's opportunity for mankind to be saved and to begin a life of holiness. God desires that we embrace this opportunity while it is still available.

---

Introduction

Shalom, beloved family of God.

Today we will study one of the most important subjects in the Christian faith: The Grace of God—His undeserved favor and His divine power that enables us to live a righteous life.

Grace is the foundation of salvation, the power to overcome sin, and the basis of our service to God.

Today we shall study:

✅ 1. The Meaning of Grace

✅ 2. The Different Types of Grace

✅ 3. The Time of Grace and the Opportunity for Salvation

✅ 4. Lessons for Believers

---

LESSON OUTLINE

1. The Meaning of Grace

Grace is the undeserved favor of God.

Grace is not a license to continue in sin; rather, it is God's power that transforms us.

Titus 2:11–12

"For the grace of God that brings salvation has appeared to all men, teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly in the present age."

Grace teaches us to say NO to sin and YES to holy living.

---

2. Types of Grace

1. Saving Grace

This is the grace that brings salvation.

It does not depend on our works but upon the finished work of YAHUSHA HAMASHIACH.

Ephesians 2:8–9

---

2. Enabling Grace

This grace gives believers the strength to overcome temptation, weakness, and sin.

2 Corinthians 12:9

---

3. Teaching Grace

This grace instructs believers to live righteous and holy lives.

Titus 2:11–12

---

4. Ministerial Grace

This grace empowers believers to serve God effectively through their spiritual gifts.

Romans 12:6

---

5. Sustaining Grace

This grace preserves and strengthens believers during trials, suffering, and persecution.

1 Peter 5:10

---

6. Common Grace

These are God's blessings that are given to all humanity, both the righteous and the unrighteous.

Matthew 5:45

---

3. The Revelation of 2 Corinthians 6:1–2

Spiritual Analysis

Grace is for today, not tomorrow.

Failing to respond to God's grace is losing the opportunity for salvation.

"Do not receive the grace of God in vain" means that God's grace must produce visible results:

- Holy living
- Righteousness
- Obedience
- Fruitfulness in ministry

The phrase "the acceptable time" refers to God's appointed season of mercy.

The phrase "the day of salvation" means that today is God's opportunity for repentance and transformation.

Grace gives every believer a spiritual responsibility:

- To receive grace
- To live by grace
- To share grace with others

---

4. Lessons for the Church

Grace is the first step toward spiritual growth and maturity.

Each type of grace takes us through God's divine process:

✅ Salvation

✅ Spiritual instruction

✅ Spiritual empowerment

✅ Preservation

✅ Ministry

God's season of grace is NOW.

No one should delay responding to His call.

---

5. Practical Applications

1. Recognize God's grace in your life.

2. Receive the salvation of YAHUSHA today without delay.

3. Let grace produce visible transformation in your character.

4. Extend God's grace to others through ministry.

5. Depend upon God's grace every day.

---

PRAYER POINTS:

PRAYING FOR DIFFERENT TYPES OF GRACE

1. Saving Grace

Ephesians 2:8

Father, I thank You for the grace of salvation through Your Son, YAHUSHA HAMASHIACH.

Open my eyes to appreciate the value of my salvation.

If there is any part of my life that is not fully surrendered to You, save me completely.

Place within me a hunger for genuine salvation.

---

2. Teaching Grace

Titus 2:11–12

Father, let Your grace teach me to reject sin.

Give me understanding to live a holy life.

Remove worldly desires from my heart.

Help me to love righteousness and hate sin.

---

3. Enabling Grace

2 Corinthians 12:9

Father, let Your grace be sufficient for me in my weakness.

Give me strength to overcome every temptation.

Help me never again to be defeated by sin.

Enable me to stand firm in difficult circumstances.

---

4. Sustaining Grace

1 Peter 5:10

Father, sustain me so that I will not fall along the way.

Grant me endurance through every trial.

Strengthen me to remain faithful until the end.

Help me continue even when I become weary.

---

5. Ministerial Grace

Romans 12:6

Father, reveal my spiritual gifts.

Grant me grace to serve You faithfully.

Make me a blessing to others.

Let my ministry bear lasting fruit.

---

6. Common Grace

Matthew 5:45

Father, thank You for life and every breath I take.

Continue to cover me with Your mercy.

Grant me favor in my daily life.

Open doors for me through Your grace.

---

7. Grace Not to Abuse Grace

Jude 1:4

Father, remove every attitude that misuses Your grace.

Give me a heart of genuine repentance.

Help me live in the fear of the Lord.

Teach me to use Your grace righteously.

---

8. Grace for Spiritual Growth

2 Peter 3:18

Father, help me grow continually in Your grace.

Increase my hunger for Your Word and prayer.

Transform me day by day.

Bring me into spiritual maturity.

---

9. Grace Not to Receive Grace in Vain

2 Corinthians 6:1–2

Father, help me never to receive Your grace in vain.

May my life demonstrate the evidence of Your grace.

Help me use this present season of salvation wisely.

Teach me never to delay responding to Your calling.

---

Practical Exhortation

Do not pray these prayer points as mere words.

Take time with each point.

Pray deeply and allow the Holy Spirit to minister to your heart.

Listen carefully as He teaches and transforms you through His grace.

---

Conclusion / Challenge

Behold, now is the accepted time; behold, now is the day of salvation!

Do not receive the grace of God in vain.

Live it.

Demonstrate it.

Overcome sin through it.

Beloved family of God, if we embrace God's grace today, we shall become true witnesses of His glory and faithful servants of His Kingdom.

Prepared by

Pastor Stephen Odhiambo Muruayi

KISWAHILI VERSION 👇

SOMO:
‎UFUNUO WA NEEMA NA WAKATI WA WOKOVU.

‎Andiko Kuu:
‎2 Wakorintho 6:1-2 (NKJV)
‎“Nasi tukitenda kazi Pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. ( Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusikia, SIKU ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio Sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa).”

‎📜Tafsiri ya maandiko:
‎Paulo anatufundisha kwamba neema ya Mungu si kitu cha kuchezea. Wakati wa kuikubali neema ni sasa, sio kesho. Ni fursa ya kuokolewa na kuanza maisha ya utakatifu, na Mungu anataka tuichangamkie hii fursa sasa.

‎Utangulizi.
‎Shalom familia ya Bwana. Leo tunajadili somo muhimu sana: Neema ya Mungu—upendeleo wake usiostahiliwa na nguvu ya kuishi maisha ya haki. Neema ni kiini cha wokovu, nguvu ya kushinda dhambi, na msingi wa huduma yetu kwa Mungu.

‎Tutaangalia:
‎✅ 1. Maana ya neema
‎✅ 2. Aina zake
‎✅ 3. Wakati wa neema na fursa ya wokovu
‎✅ 4. Changamoto na matokeo kwa waamini.

‎Vipengele Vya Somo.

‎1. Maana ya Neema.
‎Neema ni upendeleo wa Mungu usiostahiliwa.( undeserved favor of God).

‎🌾 Neema ya Mungu Si leseni ya kuendelea na dhambi; bali ni nguvu ya kubadilika.

‎Tito 2:11-12:
‎[11] Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

‎[12] nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

‎👉 Neema inatufundisha kusema hapana kwa ubaya na kuishi maisha matakatifu.

‎2. Aina za Neema.

‎🌱 1. Saving Grace (Neema ya Wokovu)
‎Hii ndiyo mwanzo wa wokovu.
‎Haitegemei matendo yako, inategemea kazi ya YAHUSHA.
‎Warumi 2:8-9

‎💪 2. Enabling Grace (Neema ya Uwezo)
‎Inakupa nguvu ya kushinda dhambi na majaribu.
‎2 Wakorintho 12:9

‎👩‍🏫 3. Teaching Grace (Neema ya Kufundisha)
‎Inakuongoza kuishi kwa haki.
‎Tito 2:11-12

‎⛪ 4. Ministerial Grace (Neema ya Huduma)
‎Inakuwezesha kutumia vipawa vyako katika utumishi.
‎Warumi 12:6

‎💪 5. Sustaining Grace (Neema ya Kudumisha)
‎Inakushikilia wakati wa mateso na changamoto.
‎1 Petro 5:10

‎🌾 6. Common Grace (Neema ya Jumla)
‎Baraka za Mungu zinazopatikana kwa wote, wema na ovyo.
‎Mathayo 5:45

‎3. Ufunuo wa 2 Wakorintho 6:1-2
‎Uchambuzi:

‎🌾Neema ni sasa, si kesho.
‎Kukosa kuitumia neema ni kupoteza fursa ya wokovu.

‎“Usipokee neema ya Mungu bure” = neema inapaswa kuishia matendo: maisha matakatifu, haki, na huduma.
‎Wakati wa kusikia vs. siku ya wokovu:
‎Sasa ndio fursa ya kubadilika na kuanza maisha ya kiroho.
‎Neema inatupa ofisi ya kiroho: kupokea, kuishi, na kushirikisha neema.

‎4. Mafunzo kwa Kanisa.

‎🌾 Neema ni hatua ya kwanza ya kuukulia wokovu.

‎🌱 Kila aina ya neema inatupa mchakato:
‎✅ 1. kuokolewa.
‎✅ 2. kufundishwa.
‎✅ 3. kupewa nguvu.
‎✅ 4. kudumishwa.
‎✅ 5. kuhudumu.

‎👉 Wakati wa Mungu wa neema ni sasa; hakuna kuchelewa.

‎5. Hatua za Kivitendo.

‎1. Tambua neema ya Mungu katika maisha yako.

‎2. Kubali wokovu wa YAHUSHA sasa, bila kuchelewa.

‎3. Itaisha neema kwa mabadiliko ya tabia yako.

‎4. Tumia neema kwa wengine katika huduma.

‎5. Ishi kwa kutegemea neema kila siku.

‎PRAYER POINTS: KUOMBA AINA MBALIMBALI ZA NEEMA

‎🔥1. KUOMBA SAVING GRACE (Neema ya Wokovu)

‎📖 Waefeso 2:8
‎Baba, nashukuru kwa neema ya wokovu kupitia mwanao Yesu Kristo.
‎Nifungue macho nione thamani ya wokovu wangu
‎K**a kuna sehemu haijaokoka ndani yangu, niokoe kikamilifu
‎Nitie ndani yangu njaa ya kuishi maisha ya wokovu wa kweli

‎🔥 2. KUOMBA TEACHING GRACE (Neema ya Kufundisha)

‎📖 Tito 2:11-12
‎Baba, neema yako inifundishe kukataa dhambi
‎Nipe ufahamu wa kuishi maisha matakatifu
‎Niondolee tamaa za dunia ndani yangu
‎Nifanye nipende haki na kuichukia dhambi

‎🔥 3. KUOMBA ENABLING GRACE (Neema ya Uwezo)

‎📖 2 Wakorintho 12:9
‎Baba, neema yako initoshe katika udhaifu wangu.
‎Nipe nguvu ya kushinda kila jaribu.
‎Nisiwe dhaifu mbele ya dhambi tena.
‎Nifanye nisimame imara hata katika mazingira magumu.

‎🔥 4. KUOMBA SUSTAINING GRACE (Neema ya Kudumisha)

‎📖 1 Petro 5:10
‎Baba, nidumishe nisije nikaanguka njiani.
‎Nipe uvumilivu wa kustahimili majaribu. Nisimame mpaka mwisho wa wokovu wangu.
‎Nipe nguvu ya kuendelea hata ninapochoka.

‎🔥 5. KUOMBA MINISTERIAL GRACE (Neema ya Huduma)

‎📖 Warumi 12:6
‎Baba, nifunulie kipawa changu
‎Nipe neema ya kutumika kwa uaminifu
‎Nifanye niwe chombo cha baraka kwa wengine
‎Nipe matokeo katika huduma yangu

‎🔥 6. KUOMBA COMMON GRACE (Neema ya Jumla)

‎📖 Mathayo 5:45
‎Baba, nakushukuru kwa uhai na pumzi
‎Endelea kunisitiri kwa rehema zako kila siku
‎Nipe kibali katika maisha yangu ya kila siku
‎Nifungulie milango kwa neema yako

‎🔥 7. KUOMBA NEEMA YA KUTOKUITUMIA VIBAYA

‎📖 Yuda 1:4
‎Baba, niondolee roho ya kutumia neema vibaya
‎Nipe moyo wa toba ya kweli
‎Nisaidie kuishi kwa hofu yako
‎Nifanye niitumie neema kwa haki

‎🔥 8. KUOMBA NEEMA YA KUKUA (GROWTH IN GRACE)

‎📖 2 Petro 3:18
‎Baba, nisaidie kukua katika neema yako
‎Niongezee njaa ya Neno na maombi
‎Nifanye nibadilike kila siku
‎Nifikishe katika ukomavu wa kiroho

‎🔥 9. KUOMBA NEEMA YA KUTOTUMIA NEEMA BURE

‎📖 2 Wakorintho 6:1-2
‎Baba, nisipokee neema yako bure
‎Nifanye niishi matokeo ya neema ndani yangu
‎Nitumie neema yako kwa wakati huu wa wokovu
‎Nisaidie nisichelewe kuitikia wito wako


‎🔥 Ushauri wa kiutendaji (muhimu sana):
‎Usiombe hizi prayer points k**a maneno tu—

‎👉 chukua kila kipengele, kaa nacho, omba kwa muda

‎👉 ruhusu Roho Mtakatifu akufundishe ndani yake.

‎Hitimisho / Changamoto.
‎Tazama, sasa ndio wakati wa wokovu!
‎Usipokee neema ya Mungu bure; iishi, ipe matokeo, ushinde dhambi.
‎Familia ya Bwana, tukitumia neema sasa, tutakuwa mashuhuda wa kweli wa utukufu wa Mungu.

‎Imeandaliwa na Pastor Stephen Odhiambo Muruayi.

20/06/2026
Shalom watumishi wa Mungu 🙏‎Hii ndiyo Sehemu ya 5 (ya mwisho) ya series—kilele cha mafundisho, kinacholeta njia ya ukomb...
24/05/2026

Shalom watumishi wa Mungu 🙏
‎Hii ndiyo Sehemu ya 5 (ya mwisho) ya series—kilele cha mafundisho, kinacholeta njia ya ukombozi na urejesho wa utakatifu.

‎MWALIMU: SENIOR PASTOR, STEPHEN ODHIAMBO MURUAYI

‎Kichwa cha Somo:
‎NJIA YA UKOMBOZI: KURUDI KWENYE UTAKATIFU WA KWELI

‎Ibada ya Mafundisho / Ukombozi na Urejesho wa Utakatifu

‎Andiko Kuu:
‎Warumi 12:1-2 (SUV)
‎“Basi ndugu zangu, nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

‎Utangulizi
‎Baada ya kuona:
‎asili ya tatizo (Sehemu ya 1)
‎sanamu ya siri (Sehemu ya 2)
‎mlango wa tamaa (Sehemu ya 3)
‎kiburi kilichojificha (Sehemu ya 4)

‎Sasa swali kubwa ni:
‎Mwamini anatokaje hapa?

‎Habari njema ni kwamba:
‎👉 Kuna njia ya ukombozi
‎👉 Kuna njia ya kurejeshwa
‎👉 Kuna njia ya kurudi kwenye utakatifu wa kweli

‎Vipengele vya Somo

‎1. Tambua Utambulisho Wako Ndani ya Kristo

‎Tatizo kubwa la beauty obsession ni:
‎kutafuta thamani nje

‎Lakini ukweli ni huu:
‎✅ Thamani yako iko ndani ya Kristo
‎✅ Wewe ni wa thamani bila kujali mwonekano

‎Unapojitambua:
‎➡️ unavunja utegemezi wa mwonekano

‎2. Toa Mwili Wako Kuwa Dhabihu

‎Biblia inasema:
‎mwili utolewe kwa Mungu

‎Hii ina maana:
‎✅ hutumii mwili kwa tamaa
‎✅ hutumii mwili kwa kujionyesha
‎✅ hutumii mwili kwa kuvutia

‎Bali:
‎➡️ unautumia kwa utakatifu

‎3. Fanya Upya Nia Yako (Renew Your Mind)

‎Mabadiliko ya kweli huanza:
‎kwenye mawazo

‎Lazima:
‎✅ ubadilishe namna unavyojiona
‎✅ ubadilishe vigezo vya thamani
‎✅ uache mfumo wa dunia

‎4. Jifunze Kujikana (Self-Denial)

‎Yesu alisema:
‎mtu ajikane nafsi yake

‎Hii inahusisha:
‎✅ kusema “hapana” kwa tamaa ya kuonekana
‎✅ kupunguza obsession ya mwonekano
‎✅ kuweka mipaka ya kiroho

‎5. Jenga Maisha ya Ndani

‎Utakatifu wa kweli unatoka:
‎✅ kwenye maombi
‎✅ kwenye Neno la Mungu
‎✅ kwenye ushirika na Roho Mtakatifu
‎Kadiri ndani inavyojengwa:
‎➡️ nje inapoteza nguvu ya kutawala

‎6. Kuishi Maisha ya Heshima na Kiasi

‎Mwamini anapaswa:
‎✅ kujisitiri kwa heshima
‎✅ kuwa na mipaka
‎✅ kuonyesha utakatifu hata kwa mwonekano

‎Sio kukataa urembo—
‎bali:
‎➡️ kuuweka chini ya utawala wa Mungu

‎Mafunzo Tunayopata K**a Kanisa

‎1️⃣ Kuna njia ya kutoka kwenye beauty obsession

‎2️⃣ Utambulisho wa kweli uko ndani ya Kristo

‎3️⃣ Mwili ni hekalu, si chombo cha maonesho

‎4️⃣ Mabadiliko huanzia kwenye mawazo

‎5️⃣ Utakatifu ni maisha ya kila siku

‎Hatua za Kivitendo

‎1️⃣ Jikumbushe kila siku wewe ni nani ndani ya Kristo

‎2️⃣ Tumia muda mwingi kujenga maisha ya kiroho

‎3️⃣ Punguza vitu vinavyochochea obsession (media, comparisons)

‎4️⃣ Chagua mavazi ya heshima na kiasi
‎Ishi kwa kusudi la kumpendeza Mungu

‎Maombi ya Pamoja
‎Ee Baba wa mbinguni,
‎Katika jina la YAHUSHA HAMASHIACH,
‎Tunakushukuru kwa Neno lako lililotufundisha na kutuonya.

‎Leo tunachagua:
‎kuacha njia za dunia
‎kuacha kutegemea mwonekano
‎kurudi kwako kwa moyo wote
‎Bwana:
‎fanya upya nia zetu
‎safisha mioyo yetu
‎rejesha utakatifu ndani yetu
‎Tunatoa miili yetu kuwa dhabihu iliyo hai mbele zako.
‎Tusaidie kuishi maisha yanayokupendeza Wewe.
‎Tufanye kuwa kanisa safi, lililo tayari kwa ujio wako.
‎Katika jina la YAHUSHA HAMASHIACH,
‎Amina.

‎Hitimisho / Changamoto
‎Utakatifu si wazo—ni uamuzi wa kila siku.
‎Jiulize:

‎Je, ninaishi kwa ajili ya kumpendeza Mungu au watu?
‎Neno la Mwisho kwa Kanisa
‎Kanisa la mwisho halitakuwa:
‎la kuvutia macho ya watu

‎Bali litakuwa:
‎takatifu
‎safi
‎limejaa utukufu wa Mungu

‎Imeandaliwa na Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi,
‎Ark Of Salvation Ministries (ASM),
‎Simu: 0762168594.

Shalom watumishi wa Mungu 🙏‎Ni matumaini u Hali njema mahali ulipo na BWANA anaendelea kukuneemesha katika mwema yote.‎‎...
23/05/2026

Shalom watumishi wa Mungu 🙏
‎Ni matumaini u Hali njema mahali ulipo na BWANA anaendelea kukuneemesha katika mwema yote.

‎Nichukue nafasi hii nikukaribishe Tena katika mfulizo wa SOMO LETU BEATY OBSESSION.

‎Naendelea sasa na Sehemu ya 4, tukiingia kwenye eneo la ndani zaidi—kiburi kinachojificha ndani ya beauty obsession.

‎MWL: SENIOR PASTOR, STEPHEN ODHIAMBO MURUAYI

‎Kichwa cha Somo:

‎KIBURI KILICHOJIFICHA: UZURI UNAOINUA NAFSI BADALA YA MUNGU

‎Andiko Kuu:
‎Mithali 16:18 (SUV)
‎“Kiburi hutangulia uharibifu, na roho ya majivuno hutangulia maanguko.”

‎Utangulizi
‎Moja ya hatari kubwa inayojificha ndani ya beauty obsession si tamaa tu—bali kiburi.

‎Kiburi hiki si cha wazi kila wakati. Mara nyingi:

‎🔵 hujificha ndani ya uzuri
‎🔵 hujificha ndani ya kujipenda
‎🔵 hujificha ndani ya kutaka kuonekana

‎Na mtu anaweza kuwa:

‎🔴 anaonekana mtakatifu nje
‎🔴 lakini ndani amejaa kujiona na kujitukuza.

‎Vipengele vya Somo letu.

‎1. Kiburi ni nini kwa mtazamo wa kiroho?

‎Kiburi ni:

‎1️⃣ kujiona zaidi kuliko ulivyo
‎2️⃣ kujipa nafasi ambayo ni ya Mungu
‎3️⃣ kutafuta kujitukuza badala ya kumtukuza Mungu

‎👉 Ni hali ya moyo inayosema: “Ninatosha kwa sababu ya mimi mwenyewe.”

‎2. Beauty Obsession Inavyozalisha Kiburi

‎Mtu anapoanza:

‎🔵 kupokea sifa nyingi kuhusu mwonekano
‎🔵 kujilinganisha na wengine
‎🔵 kuona uzuri wake k**a faida

‎Anaweza kuingia taratibu kwenye:
‎➡️ kujiona bora
‎➡️ kujitenga na wengine
‎➡️ kutafuta attention
‎Hapo ndipo kiburi kinapoota.

‎3. Dalili za Kiburi Kinachotokana na Mwonekano

‎🔴 Unapenda kusifiwa na kuonekana
‎🔴 Unajilinganisha na wengine mara kwa mara
‎🔴 Unajiona bora kimwonekano
‎🔴 Unatafuta attention hata bila kusema
‎🔴 Unachukia kupuuzwa au kutotambuliwa

‎Hizi ni ishara kuwa: moyo umeanza kuinuka juu ya nafasi yake.

‎4. Hatari ya Kiburi kwa Maisha ya Kiroho

‎(a) Kinamfanya Mungu akupinge

‎Biblia inasema:
‎Mungu humpinga mwenye kiburi
‎humpa neema mnyenyekevu

‎(b) Kinazuia uwepo wa Mungu

‎Mahali palipo na kiburi:
‎uwepo wa Mungu hupungua
‎neema inapungua

‎(c) Kinaandaa anguko

‎Kiburi ni mwanzo wa:
‎kuanguka kiroho
‎kupoteza mwelekeo
‎kupoteza neema

‎5. Mfano wa Kiroho (Kanuni ya Mbingu)

‎Kila kinachojiinua:
‎➡️ kitapunguzwa

‎Kila kinachojinyenyekeza:
‎➡️ kitainuliwa

‎Hii ni sheria ya Mungu isiyobadilika.

‎6. Wito wa Kurudi Kwenye Unyenyekevu

‎Mwamini anaitwa:
‎✅ kuishi kwa unyenyekevu
‎✅ kutambua kila kitu ni neema
‎✅ kumpa Mungu utukufu wote

‎👉 Uzuri si tatizo—
‎lakini kujivunia uzuri ndicho tatizo.

‎Mafunzo Tunayopata K**a Kanisa

‎1️⃣ Kiburi kinaweza kujificha ndani ya uzuri
‎2️⃣ Sifa za watu zinaweza kuharibu moyo usipojilinda
‎3️⃣ Mungu humpinga mwenye kiburi
‎4️⃣ Unyenyekevu ni msingi wa utakatifu
‎5️⃣ Kila tulicho nacho ni kwa neema ya Mungu

‎Hatua za Kivitendo

‎1️⃣ Jifunze kumpa Mungu utukufu kwa kila sifa unayopokea
‎2️⃣ Epuka kujilinganisha na wengine
‎3️⃣ Jikumbushe kila mara kuwa yote ni neema
‎4️⃣ Jifunze kukaa mahali pa unyenyekevu
‎5️⃣ Tafuta zaidi kukua ndani kuliko kuonekana nje

‎Hitimisho / Changamoto
‎Kila unapojisikia juu kuliko wengine,
‎chunguza moyo wako.

‎Jiulize:
‎Je, ninamtukuza Mungu au ninajitukuza mimi?
‎Neno la Mwisho kwa Kanisa
‎Mungu hatumii wenye kiburi—
‎Anatumia wale waliovunjika na wanyenyekevu.

‎Asanteni sana Kwa kufuatilia mfululizo huu wa mafundisho haya ya kulijenga mwili wa Kristo. Baba Mungu wa BWANA wetu YAHUSHA HAMMASHIACH, awabarikie na kuwajazeni kila mlichopungukiwa Kwa utukufu wa jina lake.... Amein.

‎Sehemu ya 5 (ya mwisho):
‎🔥 “Njia ya Ukombozi – Kurudi Kwenye Utakatifu wa Kweli”

‎Imeandaliwa na Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi,
‎Ark Of Salvation Ministries (ASM),
‎Simu: 0762168594.

SOMO BEATY OBSESSION AND HOLINESS ‎( Urembo na Utakatifu)‎‎MH. Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi.‎‎Sahemu ya 3;‎‎ML...
15/05/2026

SOMO BEATY OBSESSION AND HOLINESS
‎( Urembo na Utakatifu)

‎MH. Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi.

‎Sahemu ya 3;

‎MLANGO WA TAMAA: BEAUTY OBSESSION NA DHAMBI YA NDANI

‎Andiko Kuu:
‎Mathayo 5:28 (SUV)
‎“Lakini mimi nawaambia, kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”

‎Utangulizi
‎Katika ulimwengu wa leo, urembo hauishii tu kuwa kitu cha kupendeza macho, bali umegeuzwa kuwa chombo cha kuvuta tamaa.

‎Hii imeleta hatari kubwa sana hata ndani ya kanisa, ambapo:

‎🔴 watu wanajipamba ili kuvutia
‎⚪ mwili unatumika kuamsha hisia
‎🔵 utakatifu unapungua kimya kimya

‎Hapa ndipo tunapoona kuwa beauty obsession inaweza kuwa mlango wa dhambi ya ndani.

‎Somo kamili;

‎1. Tamaa ni nini kwa mtazamo wa kiroho?
‎Tamaa si tendo tu—ni hali ya moyo.

‎Yesu anaonyesha wazi kuwa:

‎dhambi huanzia moyoni
‎kabla haijatokea nje

‎Tamaa ni:

‎🔴 hamu isiyo safi
‎⚪ inayochochewa na macho
‎🔵 inayompeleka mtu kwenye dhambi

‎2. Beauty Obsession Inavyofungua Mlango wa Tamaa

‎Mtu anapozingatia sana mwonekano:

‎✅ anaanza kujionyesha
‎✅ anatafuta kuvutia macho ya watu
‎✅ anajenga taswira inayochochea hisia

‎Hapo:
‎➡️ anakuwa sio tu mhanga
‎➡️ bali pia chanzo cha majaribu

‎3. Kuwajibika kwa Mwonekano Wetu
‎Hili ni eneo ambalo wengi hawataki kulisikia, lakini ni kweli ya kiroho:
‎Mwonekano wetu unaweza:

‎⚪ kusaidia utakatifu
‎au
‎🔵 kuharibu utakatifu

‎Biblia inatuita:

‎✅ kuwa watu wa heshima
‎✅ wenye mipaka
‎✅ wasioamsha tamaa

‎4. Mazingira ya Dhambi Ndani ya Kanisa
‎Beauty obsession imezalisha:

‎☑️ mavazi yasiyo na staha
‎☑️ kujionyesha kupita kiasi
‎☑️ ushindani wa mvuto

‎Matokeo yake:

‎🔴 tamaa inaongezeka
‎⚫ mawazo machafu yanaingia
‎⚪ utakatifu unaharibika

‎Hii ni hatari kubwa sana kiroho.

‎5. Ukweli Mgumu kwa Kanisa
‎Ni lazima tuseme ukweli:

‎Kujionyesha kwa lengo la kuvutia:
‎🔵 ni mtego
‎🔴 ni mlango wa tamaa
‎⚫ ni kushiriki kwa namna fulani katika dhambi

‎Mungu anaita kanisa:
‎➡️ si tu liwe safi
‎➡️ bali pia liwe chanzo cha usafi kwa wengine

‎6. Wito wa Utakatifu wa Kweli
‎Utakatifu si:
‎✅ maneno
‎✅ ibada za nje

‎Ni:
‎☑️ maisha
‎☑️ maamuzi

‎namna unavyoishi hata kwa mwonekano

‎Mafunzo Tunayopata K**a Kanisa

‎1️⃣ Dhambi huanzia moyoni kabla ya kuonekana nje

‎2️⃣ Tamaa ni hatari na lazima idhibitiwe

‎3️⃣ Mwonekano wetu una athari kwa wengine

‎4️⃣ Hatupaswi kuwa chanzo cha majaribu

‎5️⃣ Utakatifu ni jukumu la kila mwamini

‎Hatua za Kivitendo

‎🔴 Chunguza namna unavyovaa na kujionyesha

‎🔵 Epuka mavazi au mitindo inayochochea tamaa

‎⚪ Linda macho yako na mawazo yako

‎🔴 Jifunze heshima ya mwili k**a hekalu la Mungu

‎🔵 Tafuta maisha ya ndani yenye nguvu kuliko ya nje.

‎Hitimisho / Changamoto
‎Usiangalie tu unavyoonekana—
‎angalia unavyoathiri wengine kiroho.

‎Jiulize:
‎Je, maisha yangu yanajenga utakatifu au yanachochea tamaa?

‎Neno la Mwisho kwa Kanisa
‎Kanisa la kweli halitakuwa chanzo cha majaribu,
‎bali litakuwa chanzo cha utakatifu.

‎Mungu akubariki endelea kunifuatilia katika Sehemu ya 4:
‎🔥 “Kiburi Kilichojificha – Uzuri Unaoinua Nafsi Badala ya Mungu”

‎Imeandaliwa na Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi,
‎Ark Of Salvation Ministries (ASM),
‎Simu: 0762168594.

SOMO BEATY OBSESSION AND HOLINESS ( Urembo na Utakatifu)‎‎Sehemu ya 2:‎‎SANAMU ISIYOONEKANA: KUABUDU MWONEKANO (BEAUTY A...
04/05/2026

SOMO BEATY OBSESSION AND HOLINESS ( Urembo na Utakatifu)

‎Sehemu ya 2:

‎SANAMU ISIYOONEKANA: KUABUDU MWONEKANO (BEAUTY AS AN IDOL)

‎Mafundisho / Uchunguzi wa Moyo na Utakatifu

‎Andiko Kuu:
‎Ezekieli 14:3 (SUV)
‎“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu zao mioyoni mwao, na kuweka kikwazo cha uovu wao mbele ya nyuso zao; je! niulizwe neno kwao?”

‎Utangulizi
‎Katika nyakati hizi za mwisho, hatari kubwa si tu sanamu zinazoonekana kwa macho, bali zile zinazojificha ndani ya moyo wa mwanadamu.

‎Watu wengi wameacha kuabudu sanamu za kuchonga, lakini wameanza kuabudu:

‎🔵 mwonekano wao
‎⚪ miili yao
‎🔴 uzuri wao

‎Hii ndiyo tunaita sanamu ya siri — beauty obsession.

‎Somo kamili:

‎1. Sanamu ni nini kwa mtazamo wa kiroho?

‎Sanamu si lazima iwe:
‎🔴 jiwe
‎🔵 mti
‎⚪ sanamu ya kuchongwa

‎Sanamu ni: Kitu chochote kinachochukua nafasi ya Mungu moyoni mwa mtu.

‎Inaweza kuwa:

‎🔵 pesa
‎🔴 cheo
‎⚪ au hata mwonekano (beauty)

‎2. Beauty Obsession Inapokuwa Ibada

‎Mtu anapoanza:

‎☑️ kujifikiria sana kuhusu mwonekano wake.

‎☑️ kutumia muda mwingi kulinda sura yake.

‎☑️ kutegemea compliments ili kujisikia vizuri.

‎Hapo urembo: unakuwa chanzo cha utambulisho na thamani
‎Na hapo ndipo: ➡️ inageuka kuwa sanamu.

‎3. Dalili za Mtu Aliye na Sanamu ya Mwonekano.

‎✅ Unajali sana watu wanakuonaje kuliko Mungu anavyokuona.

‎✅ Mood yako inabadilika kulingana na ulivyopokelewa na watu.

‎✅ Unatumia muda mwingi sana kwenye mwonekano kuliko kwenye maombi.

‎✅ Unajisikia huna thamani bila kusifiwa.

‎✅ Unajilinganisha na wengine kila mara.

‎Hizi ni ishara kuwa: moyo umeanza kutawaliwa na sanamu.

‎4. Kwa Nini Hii ni Hatari?

‎(a) Inachukua nafasi ya Mungu.

‎Moyo unapotawaliwa na mwonekano:

‎🔵 Mungu anakuwa wa pili
‎🔴 Nje inakuwa ya kwanza

‎(b) Inaharibu ushirika na Mungu

‎Mungu hutaka:

‎⚪ moyo wote
‎🔵 ibada ya kweli

‎Lakini sanamu:
‎inagawanya moyo

‎(c) Inazuia ukuaji wa kiroho

‎Mtu anakuwa:
‎🔴 busy na mwonekano
‎🔵 lakini maskini kiroho.

‎5. Mungu Anavyoshughulika na Sanamu

‎Biblia inaonyesha wazi:

‎☑️ Mungu hapendi sanamu
‎☑️ Mungu hushughulika nazo kwa nguvu

‎Kwa nini?

‎Kwa sababu: sanamu huiba utukufu unaostahili Mungu.

‎6. Wito wa Toba kwa Kanisa.

‎Kanisa linahitaji:

‎✅ kujichunguza
‎✅ kutambua sanamu zilizojificha
‎✅ kuzirudisha chini ya mamlaka ya Mungu.

‎Hii ni vita ya ndani—lakini lazima ishindwe.

‎📜 Mafunzo Tunayopata K**a Kanisa

‎1️⃣ Sio kila sanamu inaonekana—nyingine ziko moyoni.

‎2️⃣ Urembo unaweza kuwa sanamu k**a haujadhibitiwa.

‎3️⃣ Mungu anataka moyo wote, sio sehemu.

‎4️⃣ Hatupaswi kutafuta utambulisho wetu kwenye mwonekano.

‎5️⃣ Lazima tuvunje kila kitu kinachochukua nafasi ya Mungu.

‎Hatua za Kivitendo.

‎1️⃣ Fanya uchunguzi wa moyo wako kwa uaminifu.

‎2️⃣ Jiulize: “Ninathamini nini zaidi?"

‎3️⃣ Punguza utegemezi wa sifa za watu.

‎4️⃣ Weka Mungu kuwa kipaumbele cha kwanza.

‎5️⃣ Tenga muda wa kujenga maisha ya ndani kuliko taswira ya nje

‎Maombi ya Pamoja
‎Ee Baba wa mbinguni,
‎Katika jina la YAHUSHA HAMASHIACH,
‎Tunakuja mbele zako kwa unyenyekevu, tukikiri kwamba kuna nyakati tumekuwa na sanamu zilizojificha mioyoni mwetu.
‎Bwana, k**a mwonekano umechukua nafasi yako ndani yetu,
‎tunaomba utusamehe.
‎Leo tunavunja kila sanamu ya siri:
‎sanamu ya mwonekano
‎sanamu ya kujipendeza kwa watu
‎sanamu ya kutafuta sifa
‎Tunakutawaza tena uwe Bwana wa mioyo yetu.
‎Tujaze njaa ya haki, utakatifu, na uwepo wako.
‎Katika jina la YAHUSHA HAMASHIACH,
‎Amina.

‎Hitimisho / Changamoto

‎Kila kitu unachokithamini zaidi ya Mungu,
‎hicho ndicho sanamu yako.

‎Jiulize leo:

‎Je, kuna kitu kimechukua nafasi ya Mungu ndani yangu?

‎Neno la Mwisho kwa Kanisa
‎Mungu hatashindana na sanamu moyoni mwako.

‎Ama Yeye awe wa kwanza—au ameondoka.

‎Chagua leo.

‎Imeandaliwa na Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi,
‎Ark Of Salvation Ministries (ASM),
‎Simu: 0762168594.

Shalom wapendwa wangu katika Bwana,Welcome again to my new sermon, BEAUTY OBSESSION AND HOLINESS SERIES.ARK OF SALVATION...
30/04/2026

Shalom wapendwa wangu katika Bwana,
Welcome again to my new sermon,
BEAUTY OBSESSION AND HOLINESS SERIES.

ARK OF SALVATION MISSION MINISTRIES TANZANIA
‎(Huduma ya Safina ya Wokovu, UBUNGO - MAKOKA, DAR ES SALAAM)

‎MHUDUMU: SENIOR PASTOR, STEPHEN ODHIAMBO MURUAYI.

‎SOMO LA IBADA

‎Kichwa cha Somo:
‎UREMBO WA NJE DHIDI YA UREMBO WA NDANI
‎(Asili ya Beauty Obsession na Athari Zake kwa Utakatifu)

‎Tarehe: 30/04/2026.

‎Ibada ya Mafundisho / Mafundisho ya Utakatifu.

‎Andiko Kuu:
‎1 Samweli 16:7 (SUV)
‎“Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usiangalie uso wake, wala urefu wa kimo chake, kwa maana nimemkataa; kwa kuwa BWANA haangalii k**a mwanadamu aangaliavyo; maana mwanadamu huangalia sura ya nje, bali BWANA huangalia moyo.”

‎Utangulizi
‎Katika nyakati hizi za mwisho, kanisa linakabiliwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya thamani. Kile ambacho Mungu anakithamini si kile ambacho dunia inakitukuza.

‎Dunia imeinua sana:
‎☑️ mwonekano wa nje
‎☑️ mvuto wa macho
‎☑️ uzuri wa kimwili.

‎Lakini Mungu anatazama:
‎✅ moyo wa mtu
‎✅ hali ya ndani
‎✅ utakatifu wa maisha
‎Hapa ndipo tunapoona mgongano mkubwa kati ya mfumo wa Mungu na mfumo wa dunia.

‎Somo kamili.

‎1. Mfumo wa Dunia: Kuinua Mwonekano kuliko Moyo.

‎Dunia inafundisha kwamba:
‎🔴 Ukiwa mzuri, una thamani
‎🔵Ukiwa na mvuto, una nguvu
‎🔴Ukiwa na sura nzuri, unapendwa

‎Hii imesababisha watu wengi—including waamini:
‎🔵 kuanza kuishi kwa ajili ya kuonekana
‎kujilinganisha.

‎🔴 kutafuta kukubalika kwa watu.

‎Lakini huu si mfumo wa Mungu.

‎2. Mfumo wa Mungu: Moyo Ndiyo Kipimo
‎Mungu hachunguzwi na:
‎☑️ rangi ya ngozi
‎☑️ muundo wa mwili
‎☑️ urembo wa nje

‎Bali huangalia:
‎✅ usafi wa moyo..
‎✅ unyenyekevu.
‎✅ hofu ya Mungu.
‎Utakatifu huanzia ndani, sio nje.

‎3. Vita ya Kiroho: Ndani dhidi ya Nje
‎Kuna vita halisi:
‎🔴 Roho inataka utakatifu
‎🔵 Mwili unataka kuonekana

‎Beauty obsession inaanza pale:
‎🔵 mtu anapoanza kujali nje kuliko ndani.

‎🔴 muda mwingi unaenda kwenye mwonekano kuliko maombi.

‎🔵 thamani ya mtu inahusishwa na sura
‎Hii ni ishara ya kupoteza mwelekeo wa kiroho.

‎4. Hatari ya Kuishi Kwa Ajili ya Kuonekana
‎Mtu anapoingia kwenye mfumo huu:

‎🔵 Anakuwa mtumwa wa maoni ya watu.
‎🔴 Anapoteza uhuru wa kiroho.
‎🔵 Anaanza kuigiza badala ya kuishi kweli.
‎🔴 Yesu hakuitwa tuonekane—aliwaita watu wabadilike ndani.

‎5. Urembo wa Ndani Ndio Wa Kudumu
‎Biblia inasisitiza:

‎🔵 upole wa roho
‎🔴 utulivu wa moyo
‎🔵 tabia njema

‎Huu ndio urembo:
‎☑️ Usioharibika.
‎☑️ Unaompendeza Mungu.
‎☑️ Unaodumu milele.

‎Mafunzo Tunayopata K**a Kanisa.
‎1️⃣Thamani yetu haitokani na mwonekano, bali kwa Mungu.

‎2️⃣ Utakatifu ni wa ndani kabla ya kuwa wa nje.

‎3️⃣ Hatupaswi kuishi kwa ajili ya kukubalika na watu.

‎4️⃣ Lazima turudi kwenye msingi wa moyo safi.

‎5️⃣Urembo wa kweli ni ule unaotoka ndani.

‎Hatua za Kivitendo.
‎1️⃣ Punguza muda unaotumika kujishughulisha na mwonekano kupita kiasi.

‎2️⃣ Ongeza muda wa maombi na Neno la Mungu.

‎3️⃣ Jifunze kujitazama kwa macho ya Mungu, si ya watu.

‎4️⃣ Epuka kujilinganisha na wengine
‎Jenga tabia ya ndani kuliko taswira ya nje.

‎Maombi ya Pamoja.
‎Ee Baba wa mbinguni,
‎Katika jina la YAHUSHA HAMASHIACH,
‎Tunakuja mbele zako tukitambua ya kwamba mara nyingi tumetazama mambo ya nje kuliko ya ndani.
‎Bwana utusamehe kwa kila namna tuliyoweka thamani kwenye mwonekano kuliko moyo.
‎Leo tunaomba:
‎utupe macho ya kuona k**a unavyoona
‎utupe moyo safi
‎utujaze hofu yako
‎Vunja ndani yetu kila roho ya kutafuta kukubalika na wanadamu.
‎Tufundishe kuishi kwa ajili ya kumpendeza Wewe peke yako.
‎Tufanye kuwa kanisa safi, takatifu, na lenye moyo ulio sawa mbele zako.
‎Katika jina la YAHUSHA HAMASHIACH,
‎Amina.

‎Hitimisho / Changamoto
‎Mungu hatatafuta watu wazuri kwa nje,
‎Atatafuta watu safi kwa ndani.
‎Jiulize leo:
‎🔵 Je, ninajenga zaidi sura yangu au moyo wangu?
‎Neno la Mwisho kwa Kanisa
‎🔴 Kanisa la kweli halitambuliki kwa uzuri wa nje,
‎bali kwa utukufu wa Mungu unaoishi ndani yake.

‎Imeandaliwa na Senior Pastor Stephen Odhiambo Muruayi,
‎Ark Of Salvation Ministries (ASM),
‎Simu: +255762168594.

Address

P. O. Box 7012
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ark of Salvation Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share