EL-Can Revival Network

EL-Can Revival Network EL-CAN Revival Network
A Ministry committed to revival, healing, deliverance, and transforming lives

Karibu katika Ibada ya Baraka JUMAPILI hii tarehe 4/1/2026. Ibada ya kwanza mwaka 2026,Usipange kukosa na mkaribishe mwe...
03/01/2026

Karibu katika Ibada ya Baraka JUMAPILI hii tarehe 4/1/2026. Ibada ya kwanza mwaka 2026,Usipange kukosa na mkaribishe mwengine.
Mawasiliano : 0659474300

Eternal Life Church For All Nations MWAKA WA UAMSHO NA UREJESHO 2026
31/12/2025

Eternal Life Church For All Nations
MWAKA WA UAMSHO NA UREJESHO 2026

USIKU WA KUVUKA KWA MAMLAKA Ibada ya Mkesha wa Mwaka Mpya,Kuvuka Kuingia 2026Karibu kwenye ibada maalum ya mwisho wa mwa...
30/12/2025

USIKU WA KUVUKA KWA MAMLAKA

Ibada ya Mkesha wa Mwaka Mpya,Kuvuka Kuingia 2026
Karibu kwenye ibada maalum ya mwisho wa mwaka, mahali pa kuvunja mipaka, kufunga mwaka kwa mamlaka na kuvuka kwa nguvu ya Mungu.

“Tazama nimekupa mamlaka…” (Luka 10:19)
Mtumishi wa Mungu:
Ev. SHADRACK MWAKIBINGA

Jumatano, 31.12.2025
Saa 2:00 Usiku
Tabata Kisukuru – Migombani

Ni usiku wa:
Kuvunja vifungo vya mwaka uliopita
Kufunga milango ya giza
Kuingia 2026 kwa mamlaka, ufunuo na ushindi

Mawasiliano: 0659 474 300
Usikose. Karibu wewe na walio wako.
Shiriki tangazo hili, mwalike mwingine.

BARAKA HAIPANGIWI MAHALI, INAKAA KWA MTU" Baraka haikukaa kwa Labani,ilihama ikamfuata Yakobo.Kwa nini?Kwa sababu baraka...
24/12/2025

BARAKA HAIPANGIWI MAHALI, INAKAA KWA MTU

" Baraka haikukaa kwa Labani,ilihama ikamfuata Yakobo.
Kwa nini?
Kwa sababu baraka haipangwi kwenye eneo, kampuni, au familia.Baraka inakaa juu ya mtu mwenye agano.Popote ulipo, baraka itakutengenezea mazingira mapya.

Ninatangaza;

Waliokuja na fimbo,watarudi na makundi.
2026 si mwaka wa kupambana ni mwaka wa ushuhuda wa kiuchumi. "

Apostle Mathew George Kihiyo

Kutoka: PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE II, 20 December 2025. EL-CAN TABATA KISUKURU MIGOMBANI.

USHUHUDA MWINGINE - Kutoka PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE.MUNGU ANATIMIZA AHADI KWA WAKATI WAKE Shebene alikuwa ...
24/12/2025

USHUHUDA MWINGINE - Kutoka PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE.
MUNGU ANATIMIZA AHADI KWA WAKATI WAKE

Shebene alikuwa na ahadi ya muda mrefu kutoka kwa ndugu yake mmoja, ambaye alikuwa ameahidi kumpa bajaji kwa ajili ya biashara. Hata hivyo, ahadi hiyo ilikuwa imechukua muda mrefu bila kutimizwa, na hali ya kusubiri ikaendelea.

Katika Ibada ya PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE I (Oktoba 2025), Shebene aliweka hitaji hilo mbele za Mungu kwa maombi na imani. Ndani ya ibada hiyo, matamko ya kinabii yalitolewa yakithibitisha kuwa Mungu angeharakisha jambo hilo na kulitimizia kwa wakati uliopangwa.

Utukufu kwa Mungu!
Baada ya ibada hiyo, ndani ya mwezi mmoja tu, ahadi ile ilitimia kikamilifu. Ndugu yake alitimiza alichoahidi na Shebene akapokea bajaji, sawasawa na matamko ya kinabii yaliyotolewa juu yake.

Hakika, Mungu wa EL-CAN ni Mungu anayesikia maombi na kutimiza ahadi ambazo kwa macho ya kibinadamu huonekana kuchelewa.

Kutoka:
PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE I
Oktoba 2025
EL-CAN, Tabata Kisukuru Migombani
Mungu akitenda, hakuna ahadi inayochelewa.
K**a alivyomtendea Shebene, anaweza kukutimiza na wewe pia.

22/12/2025

USIKU WA KUVUKA KWA MAMLAKA

Ibada ya Mkesha wa Mwaka Mpya
Unakaribishwa kwenye ibada maalum ya mkesha wa kuuvuka mwaka kwa nguvu, maombi na matamko ya kinabii, tukiuacha mwaka 2025 na kuingia mwaka 2026 kwa mamlaka ya Roho Mtakatifu.

Ni usiku wa:

Maombi ya kina
Matamko ya kinabii
Kuvunja vifungo
Kuweka mwelekeo wa mwaka mpya

Jumatano, 31.12.2025
Saa 2:00 Usiku
Tabata Kisukuru, Migombani
Mawasiliano: 0659 474 300
Usiukose usiku huu wa neema.

Njoo uvuke mwaka kwa ushindi, mamlaka na uamsho.

DHULUMA HAIZUII BARAKA YA MUNGU" Yakobo alidhulumiwa mshahara mara kumi, lakini hakutoroka, hakulaani, hakuiba.Kwa nini?...
22/12/2025

DHULUMA HAIZUII BARAKA YA MUNGU

" Yakobo alidhulumiwa mshahara mara kumi, lakini hakutoroka, hakulaani, hakuiba.Kwa nini?
Kwa sababu alijua:
Baraka ya Mungu haitegemei haki ya mwanadamu.
K**a uko kazini au kwenye biashara na unaona umeonewa, usikate tamaa.Dhuluma haikukwamishi bali inakuzalisha kiwango kipya cha baraka.Mungu atatumia uaminifu wako kukuinua. "

Apostle Mathew George Kihiyo

Kutoka: PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE II, 20 December 2025. EL-CAN TABATA KISUKURU MIGOMBANI.

USHUHUDA MWENGINEMUNGU ANAFUNGUA MILANGO YA UCHUMIEunice aliingia katika Ibada ya PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE...
22/12/2025

USHUHUDA MWENGINE
MUNGU ANAFUNGUA MILANGO YA UCHUMI

Eunice aliingia katika Ibada ya PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE I (Oktoba 2025) akiwa hana biashara kabisa.

Biashara aliyokuwa akiifanya hapo awali ilikuwa imesimama, kutokana na kukatika kwa mtaji.

Katika ibada hiyo, Eunice aliweka hali yake mbele za Mungu kwa imani.
Mara tu baada ya kutoka ibadani siku hiyo hiyo, alipigiwa simu na mtu aliyekuwa akishirikiana naye kibiashara, ambaye alimpatia fedha ya mtaji ili aanze tena biashara yake.

Akiwa na shukrani na hofu ya Mungu, Eunice aliweka agano moyoni kuwa atakapofanikiwa kuanza upya biashara yake, hataacha kutoa zaka kwa uaminifu.

Utukufu kwa Mungu!
Katika Ibada ya PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE II (Desemba 2025), Eunice anashuhudia kuwa:
Biashara yake inakua kila siku
Mapato yanaongezeka kwa kasi
Biashara moja imezaa biashara nyingine tena

Hakika, Mungu anayeamsha uchumi wa watu wake ni hai, na agano linalofungwa mbele zake huzaa matunda.

Kutoka:
PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE II . Desemba 2025
EL-CAN, Tabata Kisukuru Migombani

Mwaka wa Uamsho wa Kiuchumi unaendelea!
K**a alivyomtendea Eunice, Mungu anaweza kukufungua na wewe.

SIRI YA KUANZA KIDOGO NA KUTOKA NA KIKUBWA" Yakobo aliingia kwa Labani bila mtaji, bila fedha, bila watu, lakini hakuwah...
21/12/2025

SIRI YA KUANZA KIDOGO NA KUTOKA NA KIKUBWA

" Yakobo aliingia kwa Labani bila mtaji, bila fedha, bila watu, lakini hakuwahi kuwa bila Mungu. Mungu alikuwa juu yake,hivyo alimbariki.Kwa labani aliingia na fimbo, lakini zaidi ya fimbo kulikuwa na AGANO.

Ufunuo huu ni wa muhimu sana
Huanzi na ulicho nacho mkononi, unaanza na ulicho nacho moyoni. Je moyoni Kuna nini ? Kuna nani ? . Wengi wanangoja mtaji, lakini Mungu anangoja mtu atakayeingia Agano na yeye la kimahusiano na ushirikiano. Anza na Mungu matokeo yatakufuata tu "

Apostle Mathew George Kihiyo

Kutoka: PROPHETIC ECONOMIC EMPOWERMENT SERVICE II, 20 December 2025. EL-CAN TABATA KISUKURU MIGOMBANI.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EL-Can Revival Network posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share