Efatha Church YOMBO

Efatha Church YOMBO Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Church YOMBO, Pentecostal Church, Yombo Kipera, Dar es Salaam.

31/08/2026
30/08/2026

Ni furaha Kwa Mungu wetu

Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye as...
30/08/2026

Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”
Furaha ya Bwana inapokuja ndani yako inakupa nguvu, inakupa kuwa hodari na shujaa kwa nini? Kwa sababu kile ulichokula ndicho kinachokupa furaha, kipi hicho? Neno la Mungu linakupa furaha, na ni nguvu yako. Unapopata hiyo furaha inakupa nguvu na wepesi.
Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.”
Nini maana ya furaha ya wokovu? Unapokula Neno la Mungu ambalo ni mkate wa uzima linakupa furaha. Roho ya wepesi ni nini? Ni kujua namna ya kufanya mambo kwa haraka na kwa wakati pasipo kupoteza majira yaliyowekwa. Kwa maana kuna muda wako wa kuanzisha biashara, kujenga au kuanziasha jambo fulani sasa kwa wewe kulijua Neno litakupa furaha na hiyo furaha itakusaidia kufanya mambo kwa wepesi na kwa wakati sahihi.
Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”
Kwa kulifahamu Neno unakuwa unatenda katika haki na ukamilifu, kwa nini Neno lina nguvu namna hii? Neno lina nguvu ili kukufanya wewe uwe mshindi katika kila eneo la maisha yako.
Neno la Mungu lina maeneo saba ya muhimu sana:-
1. Ukilielewa Neno kamwe hauwezi kuwa masikini,
2. Neno ni mkate wa uzima: linatupa nguvu,
3. Neno ni mwanga wa miguu yetu;
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”
Soma Neno, tafakari neno, kula neno, tamka Neno, kwa namna unavyofanya hivyo ndivyo unaruhusu neno likae ndani yako, namna unavyotenda na kukiri neno ndivyo linakaa ndani yako na kuanzia hapo kila utakachokitenda kitakaa kwa nini? Kwa sababu neno linakuwa ndani yako.
©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira See less

30/08/2026
IBADA YA PAMOJA YA SIKU YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE |TAREHE 30.08.2026Mathayo 11:28-30 “Njoni kwangu, ninyi nyot...
30/08/2026

IBADA YA PAMOJA YA SIKU YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE |TAREHE 30.08.2026
Mathayo 11:28-30 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.’’
Siku ya leo mtu asikie mualiko wa Bwana Yesu, maana anawaita wale wote wanaoelemewa na mizigo na kusumbuka nayo. Ukipokea mualiko huu amini kila mzigo uliokuwa unakusumbua, Yesu yupo tayari kupokea na kukuweka huru kwenye maisha yako na hutalia tena maana anaondoa hiyo mizigo na anakupa mzigo wake ambao ni mwepesi na ambao ni pendo lake.
© Mtume Betson Kikoti

Somo Ibada Ibada Yako inamaandalizi ukiandaa ibada utaandaa nguo Hadi Sadaka ibada inaandaliwa jumamosi ,Mungu anaangali...
16/08/2026

Somo Ibada
Ibada Yako inamaandalizi ukiandaa ibada utaandaa nguo Hadi Sadaka ibada inaandaliwa jumamosi ,Mungu anaangalia ibada Yako ,ibada Yako iandae mapema ili uwahi mahali pa ibada ,ibada ni mahusisno Binafsi kati ya mtu na Mungu ni ushirika Binafsi ibada Haina harambee ukiandaa ibada mapema ni rahisi Mungu kujibu maombi Yako Mungu ni wakwako sio wa wawatu wote ,adui shetani analenga kukuibia ibada ndomana imefika mahali huna furaha na ibada Yako Leo angalia ibada Yako uko sawa na yeye au Kuna mahali umepungua

Mch Kiongozi Ibrahimu Mwansasu

UFUNGUZI WA IBADAWamtumainio Bwana ni k**a mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Zaburi 125:12 K**a milima in...
16/08/2026

UFUNGUZI WA IBADA
Wamtumainio Bwana ni k**a mlima Sayuni, Ambao hautatikisika,
wakaa milele.
Zaburi 125:1

2 K**a milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.
Zaburi 125:2

3 Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Zaburi 125:3

16/8,2026
Askofu Edison Amon
Efatha Church YOMBO

Address

Yombo Kipera
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 15:00
Sunday 08:00 - 13:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church YOMBO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share