08/06/2025
MUDA MFUPI WA CHANGAMOTO AMA MAZURI YA KIPINDI KIREFU CHA KUDUMU
*MH:AMOS MUHEMBA*
Je wajua kitu kidogo kinaweza kuharibu kabisa maisha yako?,lakini ili uweze kushuhudia mambo makubwa unahitaji kua na vitu vifuatavyo;_
1 .Nguvu ya Roho mtakatifu ;wakati unapopita katika kipindi cha shida unatakiwa kumgonja BWANA,Zaburi 37:34 inatuambia kwamba "Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kushika njia yake, naye atakukuza uimiliki nchi, na kuwaona waovu wakiangamizwa".katika kipindi cha changamoto ukimtumaini MUNGU na kua na nguvu za roho mtakatifu utafanikiwa.
3. Nyenzo)
Ni Nyenzo gani unayotumia ili uweze kuvuka katika kukiendea kipindi cha kudumu?zaburi 102:25,Nyenzo unayotumia katika vipindi hivi viwili vinaweza kukuangusha au kukuinua,unatumia Nyenzo gani katika shida/Raha yako katika kipindi kifupi au kirefu.Mshikilie Yesu.Usikitazame kipindi kigumu kwa uoga ili uweze kufikia ushindi wako.
Waefeso 3:14-21 inasema
"Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya MUNGU Baba, aliye baba wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. Namwomba MUNGU awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa MUNGU, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo; na mpate kufahamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe. Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu. Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina."
4. Kua na uhakika; MUNGU ni wa uhakika,unae mtumaini ni mkuu kuliko shida zako,kuliko changamoto zako,akisema ndio ni ndio,Luka 12:29-30"Wala msihangaike mtakula nini au mtakunywa nini.msiwe na wasiwasi juu ya haya.Kwa maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wote wasiomjua Mungu.Ishikilie hekima ya MUNGU ili kipindi chako cha kudumu kiwe na uwakika.
5. Maarifa;Kua na maarifa ya ki MUNGU,kaa kwenye shule ya Mungu ufundishwe,1 wakorintho 13:8.kua na maarifa katika utendaji,usipoteze mda wako kuangalia mambo ya kusogola tu,Yaone mambo katika ubora, angalia kipindi kigumu katika ubora utashinda
6. Kua dhahili-; Kua wewe kamwe usikubali kipindi kifupi kikuletee mauzauza,k**ata Yesu na roho mtakatifu ndani yako awe amejaa,achana na kipindi kidogo tu.Maana mwili ni k**a majani na majani yanachakaa,unapopitia changamoto za muda mfupi watu wanaweza kukukimbia wote,lakini Neno la MUNGU lidumu milele kwenye maisha yako.
Tuambie unatutazama kutokea wapi na jinsi gani unabarikiwa na huduma yetu popote pale ulipo.Mtumishi wa Mungu Bishop Amosi Muhemba atakuhudumia popote pale ulipo kwa mawasiliano piga 0764994295/0782487686/0687566647.
KARIBU CCCI DAR ES SALAAM
Joy Mk**a Majaliwa Amosi Method Ratory Wa Ratory