06/12/2024
UJUMBE WA LEO UNASEMA KILA KITU NI MAANDALIZI
📌Maandalizi ni hali ya kufanya matayarisho kwa ajili ya jambo fulani.
Katika maisha mambo mazuri huandaliwa, kila jambo kinalotokea bahati mbaya bila maandalizi hupotea bila taarifa. Yani ambacho hakikupitia mchakato wa kuandaliwa hupotea ghafla
Mchakato wowote unaokutana na maandalizi sahihi huwa unaleta muendelezo wa uhakika,
Mtu mwenye maandalizi ana taarifa sahihi za kuelezea mafanikio yake hatua kwa hatua na tunaweza kujifunza kutoka kwake,
✅Maandalizi ya jambo fulani huweza kuwa katika namna mbalimbali kulingana na aina ya jambo linatakiwa kufanyika.
💥Maeneo mbalimbali ya maisha yanahitaji maandalizi, mfano
-biashara
-ndoa
-elimu
-huduma
-safari
-kuanza siku yenye mafanikio pia ni maandalizi
Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwa mtu ywyote mwenye akili timamu katika maisha yake yote hakuna mahali ambapo hapahitaji maandalizi
HEBU TUGUSIE MAANDALIZI ENEO LA UWEZO
Yapo maono makubwa ndani yetu, zipo ahadi za Mungu maishani mwetu ni kubwa sana pengine kuliko uwezo wetu,
Tumwangalie mtu k**a Yusufu, anaota ndoto kubwa kuliko uwezo wake na kwa kuwa uwezo hauruhusu kufikia ile ndoto anaanza kuandaliwa kwa kujengewa uwezo, Yeye hakuwa anaendana na ile ndoto lakini alianza kupitia mitihani inayoendana na ndoto yake ili Yusufu sasa awe na uwezo unaoendana na kile anachokwenda kukifanya/ile ahadi ya Mungu/ndoto yake
Ili ndoto isiishie kuwa ndoto inahitaji maandalizi sahihi
Mungu huachilia rasilimali mahali penye uwezo kwa sababu hapendi hasara, Mungu hapendi na haendani na wazembe,
Tunaweza kujiuliza mbona kuna watu walipewa rasilimali na Mungu na wakafeli, hawa ni wale ambao walikuwa na uwezo na Mungu akawaamini lakini wakabweteka
Lakini unapaswa kujua kuwa Mungu anaachilia rasilimali kulingana na uwezo ulio nao na ndio utaamua kwa kiasi kipi ulete faida
Matthew 9:17
[17]Neither do men put new wine into old bottles: else the bottles break, and the wine runneth out, and the bottles perish: but they put new wine into new bottles, and both are preserved.
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na k**a wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote. Msichana Arejeshewa Uhai na Mwanamke Kuponywa
Katika andiko hili tunaona ya kuwa kwa akili za kibinadamu tu hakuna mtu anaweza kuweka divai mpya katika viriba vikuukuu, ni kwa sababu viriba vitapasuka na divai itamwagika na ni hasara
Mungu anazo rasilimali zote za kutufanya tufikie hatima/mafanikio lakini lazima tulitie mchakato wa kuongeza uwezo ili kukwepa hasara.
Ni wazi kuwa tunapokwepa maandalizi kuna vitu tunakosa na vitu hvyo kukosekana maana yake tunaenenda kwa akili zetu na ndipo anguko hutokea
📌Lazima ujue kuwa tunashirikiana na Mungu kuelekea mchakato, Mungu ana nafasi yake nasi tuna nafasi yetu,
💥Nafasi ya Mungu ilishaachiliwa tayari kwa kiasi kikubwa maamuzi yapo mikononi mwetu
2 Peter 1:3-4
[3]According as his divine power hath given unto us all things that pertain unto life and godliness, through the knowledge of him that hath called us to glory and virtue:
Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
[4]Whereby are given unto us exceeding great and precious promises: that by these ye might be partakers of the divine nature, having escaped the corruption that is in the world through lust.
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Hapa tunaona kuwa uweza wa Mungu umetukirimia vitu vyote na Mungu ameachilia sehemu ya uungu ndani yetu, kwa kujua hivyo lazima k**a mwana wa Mungu utambue iko nguvu ya ndani inayokupa uwezo wa kuanzisha jambo na likafanikiwa

HAYA NI KUHUSU YUSUF, KWA TAARIFA ZAIDI UTASOMA MWANZO 39 NA KUENDELEA
HEBU TUMWANGALIE DAUDI NAYE 1samwel 16
Daudi maandalizi yake ya kuwa mfalme hayaanzii ikulu, hayaanzii kwenye mifumo ya kisiasa au ya uongozi,
Maandalizi ya daudi yanaanzia nyikani, yaani mtu anayetakiwa aongoze watu anapimwa uwezo wake kwenye kuchunga wanyama, huyu daudi uwezo wake wa kuweza kuokoa kondoo wasiliwe na simba ndio maandalizi ya kuuendea ufalme imagine,
Kumbe wakati mwingine kuna mazingira ambayo ni tofauti na kusudi letu lakini ni njia ya kutuandaa kiuwezo kuendea kusudi,
Daudi kumuua simba na dubu hakuwa anaandaliwa kuwa mchunga kondoo mzuri, ilikua ni maandalizi ya kuwa mfalme,
Inawezekana hicho unachokifanya sasa sicho mwisho wako bali ni maandalizi na kuwekewa uwezo wa kufikia mambo makubwa zaidi, lazima ukae hapo kwa uaminifu na ushinde kila mtihani

UWEZO
ni kitu cha kuonekana si kiti cha kuzungumza tu, daudi mbele za mfalme alikuwa na cha kuzungumza kuhusu simba na dubu, k**a hatupitii kipindi cha maandalizi hatuwezi kujua nguvu yetu ilo wapi
K**a Yusuf hakutafsiri ndoto kule gerezani angejulikanaje kwa mfalme? Kumbe kipindi cha maandalizi ni kizuri kutuandaa kujua uwwzo wetu, kupata cha kutufanya tuzungumzwe kwa wakuu, kwa wakuu hatujipeleki tunaitwa, Kinachotuitisha kwa wakuu sio kwa sababu tunatia huruma ni taarifa, k**a hakuna maandalizi na mchakato ambao ulikwisha kufanyika je ni taarifa zipi zinaweza kutubeba?
LAZIMA KUBORESHA UWEZO
UWEZO NDIO UNALETA KUAMINIWA,,
KWA NINI NI LAZIMA KUJIANDAA?
-Kuleta ufanisi, maandalizi yanaleta ufanisi katika utendaji kwa sababu hutoa nafasi kwa mtu kujifunza kabla ya kuamua kufanya jambo lakini inamtengenezea mtu utulivu
-Kuepuka mabadiliko yasiyotarajiwa, kuna watu ni wataalam wa kuanzisha vitu na kuacha kwa sababu ya changamoto ambazo hazikutarajiwa. kunapokuwa na maandalizi basi mchakato mzima huwa katika namna ambayo kila kinachohitajika kinafahamika lakini pia kwa kasoro zinazojitokeza huweza kushughulikiwa kwa usahihi
-Kutokurudia makosa, maandalizi hutupa muda wa kujifunza kwa wengine lakini kuboresha eneo la ufahamu ili kuepuka makosa ya kujirudia rudia
-Kufanya maamuzi sahihi, tofauti na mtu anayekurupuka ambaye anaweza kubadilisha maamuzi au kufanya maamuzi yasiyo sahihi kwa sababu ya pressurw, lakini mwenye maandalizi anajua dira hivyo hufanya maamuzi kwa kuzingatia maono, hawezi kuamua maamuzi ya kuumiza malengo yake
Kujiandaa humuwezesha mtu kuwa na muda wa kufanya tathmini na kujua mahitaji anayohitaji kukamilisha mpango kazi wake na kujua namna gani rasilimali zinahitajika
- Kuniamini, maandalizi yanatufanya tuwe na kujiamini na kutokuwa na hofu kwa sababu tuna uhakika
Mtu aliyesoma vizuri ana uhakika wa kufaulu mtihani, kadhalika ukijiandaa kwa lolote una uhakika wa kufaulu
Jiulize k**a tunaweza kuweka mikono juu ya wagonjwa wasipone na wengine wapone, vipi daudi angepata hofu kuwa lile jiwe lisipomuua goliath itakuwaje? Lakini utaona kuwa daudi hakuwa na hofu sababu ameshazoea ndio shughuli zake tangu kipindi anaandaliwa
Kwa maana hiyo hakuna kisichohitaji maandalizi na katika kujiandaa lazima kuwa na uwezo, uwezo huu tunao kutoka juu lakini ni lazima sisi wenyewe tujue kuwa uwezo wa Mungu unamhitaji mtu
Mungu anapoachilia nguvu yake lazima ikutane na mtu sahihi anayeweza kuifanyia kazi na kukubali io nguvu imuendeshe
KWA KUHITIMISHA NI KUWA TUNAISHI KULINGANA NA UWEZO TULIORUHUSU UFANYE KAZI NDANI YETU, K**A TUNAHITAJI KWENDA ZAIDI TUNAHITAJI KUONGEZA UWEZO NA NI MCHAKATO TUSIKWEPE MCHAKATO
WANAOKWEPA MCHAKATO HAWANA SHUHUDA, HAWANA CHA KUSIMULIA JUU YA MAFANIKIO YAO NA MAFANIKIO HAYO HUWA HAYADUMU
YESU ATUJALIE UWEZO,
KIRIBA KIKUUKUU KIKIWEKWA DIVAI KINAPASUKA
HAKIKISHA UNAKUA MPYA KILA SIKU, JENGA UWEZO UNAOFANANIA KESHO YAKO, KESHO NJEMA ITAKUFUATA KWA SABABU UNA MVUTO
BARIKIWA SANA NA BWANA YESU
HADI WAKATI MWINGINE
Ireen❤