π”π“π”πŠπ”π…π” π‡πŽπ’π’π€ππ€ 𝐉𝐔𝐔 πŒππˆππ†π”ππˆ

  • Home
  • Tanzania
  • Dar es Salaam
  • π”π“π”πŠπ”π…π” π‡πŽπ’π’π€ππ€ 𝐉𝐔𝐔 πŒππˆππ†π”ππˆ

π”π“π”πŠπ”π…π” π‡πŽπ’π’π€ππ€ 𝐉𝐔𝐔 πŒππˆππ†π”ππˆ ππ„ππŽ 𝐋𝐀 πŒπ”ππ†π” 𝐍𝐈 π”π‡π€πˆ

18/10/2024

Vijana rafiki wapendwa, kila mnachopanda mtakivuna pia.sasa ni wakati wenu wa kupanda. Mavuno yatakuwaje? mwapanda nini? Kila neno msemalo, kila tendo mtendalo ni mbegu ambayo itazaa matunda mema au mabaya, nayo italeta furaha au huzuni kwa mpandaji. K**a ilivyo mbegu iliyopandwa.Ndivyo yatakavyokuwa mavuno. MUNGU amewapa nuru kubwa na mibaraka mingi. Baada ya nuru hiyo kutolewa baada ya hatari kuonyeshwa dhahiri mbele yenu, mambo yanabaki juu yenu. Namna mnavyofaya na nuru ambayo mnapewa na MUNGU italeta furaha ama huzuni. Ninyi wenyewe mnajitayarishaia mwisho wenu wenyewe”. EG White- 1 kutayarisha njia sura ya 35:1 uk.212.

Kila neno msemalo kila tendo mtendalo ni mbegu ambayo itazaa matunda mema au mabaya. Nayo italeta furaha au huzuni kwa mpandaji. Nataka uelewe kuwa kutowaza sahihi tu kwa dakika moja, kutenda jambo dogo tu ambalo si la haki, kunaweza kubadiri mkondo wa maisha yako yote; Ninyi wenyewe mnajitayarishia mwisho wenu.

Muda mfupi unaotumika katika kupiga maisha ujanani, rafiki zangu vijana wapendwa, utatoa mazao ambayo yatafanya maisha yako yote yawe machungu, saa moja ya kutowaza sahihi, mara unapokubali kuingia katika jaribu, waweza kubadilisha mkondo mzima wa maisha kwenda mwelekeo usio sahihi. Unao ujana mmoja tu, hebu ufanye kuwa wenye manufaa. Upitapo katika eneo moja huwezi kurejea na kurekebisha makosa yako. Shetani huwa anajigeuza na kuwa mfano wa malaika wa nuru ajapo kwa vijana na majaribu yake yanayohadaa na huwa anafanikiwa kuwashinda, hatua kwa hatua kutoka katika wajibu wao”

Ni kweli shetani ajapo kwa vijana na majaribu yake tena yanayohadaa anafanikiwa kuwashinda. Ni wengi ambao shetani amewashinda kwa tamaa za mwili, kwa ulevi wa pombe, ulafi, na kwa kutowatii wazazi wao. Vijana hawa ambao ndio hufanya familia, taifa na kisha mataifa, wengi wao wamearibika kiasi kikubwa. Katika Mataifa mbalimbali hata vijana wanavyoongea tu ushuhudia jambo hili na wengine wanaongea k**a mazezeta, wenyewe wakijiita kuwa ni masela; huu wote ni upotevu wa maadili.

MUNGU anahitaji maisha ya ujana juu ya vijana tulio nao katika nyumba zetu na kanisani, maisha yao yawe kielelezo: - Kielelezo katika usemi

usemi

- Kielelezo katika mwenendo

- Kielelezo katika upendo

- Kielelezo katika imani

- Kielelezo katika mavazi, uvae kwa kujistiri. Maandiko yanaendelea kuonya ifuatavyo:-

β€œMtu awaye yote asiudharau ujana wako,bali uwe kielelezo kwao waaminio,katika usemi na mwenendo na katika upendo na imani na usafi”. 1 Timotheo 4:12.

Ili ujana wako usidharauliwe uwe kielelezo katika mwenendo, usemi, upendo, kielelezo katika imani, utakuwa na ujana wenye manufaa. Lakini k**a mwenendo wako ni wa ovyo, usemi ni waovyo, watu hawataacha kukudharau. Je wewe kijana unaesoma kitabu hiki ulichonacho mkononi mwako, mwenendo wako ukoje? Je, watu wanavyo kutazama wanaona kielelezo katika imani na usafi? Habari gani juu ya usemi wako, Maana katika siku hizi za mwisho kuna lugha zinazotumika mitaani ambazo zinaonyesha upotovu wa maadili. Zifuatazo ni baadhi ya lugha zinazotumiwa na vijana lakini ni upotofu wa maadili cha ajabu hata vijana Wakristo nao wamepotoka.

18/10/2024

VIJANA NA HATARI INAYOWAKABILI.

Katika somo hili tutajifunza mambo yafuatayo:-

1. Wito wa MUNGU kwa vijana

2. Ni nini kinachoweza kuwafanya vijana wamshinde shetani?

3. Maovu na makosa katika siku za ujana

Katika siku hizi za mwisho ni vijana wachache sana waliojitoa kikamilifu kumtumikia MUNGU. Wengi wa vijana hata wale walio makanisani wanaishi kwa unafiki, machoni pa watu wakionekana k**a watu wa dini, lakini machoni pa MUNGU wakiwa wameoza na kunuka, sababu ya matendo na tabia zao chafu, ingawa si wote. Ningali kijana mdogo niliwahi kuwasikia watu wakidai kuwa dini ni ya wazee. Usemi huu ulimaanisha kuwa,hakuna kijana anaeweza kuwa mcha MUNGU katika siku za ujana,kwamba amewahi kushika dini mno na lazima ataasi tu. Huu ni usemi unaotoka katika kinywa cha shetani mwenyewe. Na kwa ajili hiyo vijana wengi wanaamua kuishi kwa tamaa za mwili wakifanya zinaa wapendavyo na kudhani kuwa wataweza kubadili mielekeo yao pale watakapotaka, maskini watu hawa wamenaswa wavuni mwa shetani na shetani amewamiliki kikamilifu.

Yafuatayo ni baadhi ya matendo mabaya ya vijana wa kizazi hiki.

1. Utumiaji wa madawa ya kulevya

2. Tamaa za uasherati

3. Kuiga na kuvaa nguo na mitindo ya ajabu ya kidunia (vimini,vibode,modo)

4. Kutowaheshimu wazazi wao.

5. Kunyoa denge

6. Kutazama picha chafu

7. Kula vyakula na vinywaji vya ovyo.

8. Kupenda miziki na mpira kana kwamba wanashindania uzima wa milele nk.

Vijana wengi wanaishi kana kwamba hakuna MUNGU, na kwa wengi hawamjui MUNGU wala na madai yake kwao. Lakini MUNGU anawaita Vijana;

1 Wito wa MUNGU kwa Vijana.

β€œMkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,kabla hazijaja siku zilizo mbaya,wala haijakaribia miaka utakaposema,mimi sina furaha katika hiyo” Mhubiri 12:1.

MUNGU muumbaji anawataka vijana wajitoe kumtumikia; anataka aabudiwe, akumbukwe, ajaliwe, katika siku za ujana, bado una nguvu. Lakini pia fungu hili linataka tuelewe kuwa, baada ya ujana kuna siku zinakuja zilizo mbaya, siku za kukosa furaha.

β€œWewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako , na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote MUNGU atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uondoe ubaya mwilini mwako,kwa maana ujana ni ubatili na utu uzima pia”. Mhubiri 11:9

MUNGU muumbaji anataka kila kijana afurahie ujana wake. Lakini ili ujana upite vizuri-ondoa ubaya mwilini mwako, je ni ubaya gani ulionao? Na utambue ujana ni k**a maji ya moto ujana ni ubatili. Na ya kwamba mambo yote ya ujana na utu uzima pia yataletwa hukumuni. Ufanye unalotaka lakini usisahau kuwa katika hayo yote ipo hukumu ya MUNGU inakuja, Jiandae.

Usisahu kuhudhulia WhatsApp ibada online
02/09/2024

Usisahu kuhudhulia WhatsApp ibada online

Sababu Zinazosababisha Watu Wahame Hame Makanisa:-Ukiachilia mbali kwamba siku hizi watu wamekuwa na masikio ya utafiti,...
08/08/2024

Sababu Zinazosababisha Watu Wahame Hame Makanisa:-
Ukiachilia mbali kwamba siku hizi watu wamekuwa na masikio ya utafiti, yaani hawawezi kutulia sehemu moja, ni wazi kwamba kuna sababu zinazosababisha hayo yote yatokee! Kwa ujumla katika utafiti wangu nilioufanya tangu mwaka 2014 mpaka hivi leo. Hebu ngoja tuzitalii sababu hizi

1.Inawezekana kutokana na watu kukosa majibu ya ahadi walizoahidiwa kabla ya kuokoka
Tangu zamani ni watu wachache sana wanaoenda kanisani pasipo kupitia changamoto nyingi katika maisha yao. Watu wengi wanaposikiliza mikutano ya injili na jinsi watumishi wa Mungu wanavyowaahidi kwamba ukimpokea Yesu kristo mambo yako yatakuwa safi. Sasa mara wanapokaa kanisani kwa muda wa mwaka mmoja wanaona hali zao zinazidi kuwa mbaya, basi huamua kuondoka.

Tumesikia mara kwa mara katika mikutano ya Injili nyimbo k**a vile β€œkwa Yesu ni tambarare” au k**a ukimwamini Yesu leo β€œmagonjwa yako yatapona yote kabisa, hutaugua tena kwa Jina la Yesu” umaskini wako utaondoka leo hii, leo Bwana anaenda kufanya muujiza wa kuokota hela, leo kuna mtu atakuja kukulipia kodi, leo mchumba wako atakuja jioni kukusalimia, leo mumeo k**a alikuwa hatoi hela ya matumizi anaenda kukuachia laki moja, leo maadui wako wote wanaena kuwa marafiki wako kabisa, ndani ya wiki hii unaenda kununua kiwanja na mwakani majira k**a haya utaenda kujenga, mwakani majira k**a haya wewe mama utakumbatia mtoto, hata k**a huna mume Mungu anaenda kukupa mume muda huu” pamoja na ahadi nyingine lukuki!

Ahadi hizo hapo juu siyo kwamba Mungu hawezi kuzitimiza kwa makusudi yake. Hakuna jambo linamloshinda Mungu, katika kubadilisha historia ya binadamu. Lakini wakati wa kuzitoa ahadi hizi lazima tuangalie kwanza hitaji la mwanadamu ni nini? Naamini kwamba hitaji la mwanadamu la kwanza ni kuwa na uhusiano wake na Mungu zaidi na zaidi. Kutokuwa na mali za hapa duniani haimaanishi kwamba uhusiano wetu na Mungu pia umeharibika. Tatizo kubwa la mwanadamu ni dhambi inayomsumbua usiku na mchana, hilo tatizo likitibiwa vizuri mambo mengine anaweza kuvumilia hata pale yanapokuwa magumu.

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba kwa sababu ahadi hizo zinaweza kushindikana kutimizwa mapema kwa majira ambayo mtumishi alisema, lakini pia kwa majira ambayo huyo aliyeahidiwa aliyapanga, na kwa kusahau majira ya Mungu; watu k**a hawa hujikuta wakihamia sehemu nyingine ili kusaka ahadi zao, labda pengine Mungu wa mahali hapo hajatimiza haja za mioyo yao.

Watu kadha wa kadha walipohamia kanisani kwetu niliweza kuwadadisi ni kwa vipi wamehama sehemu walizokuwa wanasali na kuamua kujiunga na huduma yetu. Mara kwa mara walinijibu sababu tofauti k**a vile; kanisa lile liko hivi na hivi, lakini baada ya muda kupita waliondoka pia kanisani, kwa sababu hiyo niligundua shida yao nini hasa. Nilikugundua kwamba wanatafuta majibu ya maisha yao ya kimwili, lakini kwa sababu hawakuwa wawazi zaidi ndiyo maana wameondoka tena na kuelekea sehemu nyingine ili wakajaribu upya wa huko.

Hivyo basi, mtumishi wa Mungu unapoona watu wanaanza kuondoka kanisani na kuelekea kanisa lingine, haijalishi wewe uko katika kiwango gani, hao bado hawajapata majibu ya maswali yao au zile ahadi walizoahidiwa siku ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao. Hili nalo wewe k**a mtumishi wa Mungu liweke kwenye kumbukumbu kwamba lazima ugundue hitaji la mioyo yao na ahadi walizoahidiwa mara ya kwanza ni zipi.

4.Nia Ya Kutafuta Uongozi Ndani ya Makanisa            K**a tujuavyo kwamba kanisa linakuwa na uongozi, na ule uongozi n...
08/08/2024

4.Nia Ya Kutafuta Uongozi Ndani ya Makanisa
K**a tujuavyo kwamba kanisa linakuwa na uongozi, na ule uongozi ni watu ndio wanaowachagua. k**a mtu alienda kwenye kanisa fulani kwa nia ya kupata uongozi, anapokuwa hajapewa uongozi alioutaka, ni dhahiri kwamba atahama tu. Tangu zamani hata tunaposoma historia tunaona kwamba watu mbalimbali walipokosa uongozi mahali fulani waliamua kuhamia makanisa mengine.

Kwamba, nia ya watu wa namna hii ni kuongoza na wala siyo kuongozwa, kwa kifupi wao hawana karama ya kuongozwa (k**a ipo) na wala hawajawahi kuota ndoto ya kuongozwa hata siku moja. Wao wakikaa katika kanisa kazi yao kubwa ni kukosoa uongozi uliopo madarakani na kutaka wao ndio wachaguliwe kuwa viongozi.

Hoja yangu hapa sipindi nia ya kuwa kiongozi. Biblia inasema kwamba β€œatakaye kazi ya askofu atamani kazi njema”. Hakuna tatizo kabisa. Ninachokisema mahali hapa ni kwamba nakutahadharisha wewe mchungaji unapokuwa unachunga kanisa lazima ujue kwamba kuna watu wengine wanataka uongozi. Ama kwa hakika kuna wengine kweli kwa sababu ya hiyana ya watu fulani fulani wamepoteza uongozi ndani ya makanisa lakini ni viongozi wazuri sana.

Nimewahi kushuhudia kanisa moja ambalo uongozi wake ulikuwa ni wa kindugu tu. Kuanzia mchungaji wa kanisa lile mpaka wazee wa kanisa ni wa ukoo mmoja. Sasa kila mtu mwingine anapotaka kutafuta uongozi katika kanisa lile wale viongozi wengine wanapiga majungu mpaka akome. Na mara kwa walikuwa wanasingiziwa kesi zisizowahusu na matokeo yake watu hao walikuwa wanaamua kuhamia makanisa mengine. Jambo la kushangaza ni kwamba wanapohamia makanisa mengine wanafanya kazi vizuri mno kuliko wale waliowaacha kwenye kanisa hilo.

Hivyo basi, mchungaji unapaswa kuiangalia hii hoja kwa pande mbili; kwa uzuri wake na ubaya wake. Hata hivyo, mchungaji usijaribu kumpa mtu uongozi kwa sababu amekuja anataka uongozi kwako. Atakuwa mwiba baadaye kwako.

Nakumbuka kipindi nilipoanza huduma, kuna mchungaji mmoja alikuwa kwangu akanieleza kuwa amehama kanisa fulani kwa sababu alikuwa hapewi nafasi ya kuhubiri kabisa. Alieleza mambo mengi sana. Nikaona kwamba huyu mtu pengine kweli anafaa kuwa mchungaji pamoja katika kanisa letu; sasa mimi nikamwambia asubiri angalau asali pamoja nasi miezi miwili tu, halafu nitampa mibari siku moja tuone namna anavyopiga gombo! Kilichotokea hapo siwezi kusimulia kwa undani ila aliniambia maneno mabaya sana huku akidai kwamba yeye ni mtumishi wa siku nyingi kwa hiyo sina haja ya kuanza kumwangalia tena! Sasa hapo kwa akili ya haraka haraka nani anayeweza kumpa uongozi wa namna ile? Nafikiri hakuna!

Lakini namkumbuka ndugu mmoja zamani kidogo alihamia kanisa fulani kwa sababu katika kanisa alilokuwa anasali alikuwa hapewi uongozi wowote na nia yake ilikuwa ni kutumika. Alipohamia kanisa lingine na kupewa nafasi aliweza kutumika vizuri sana. Na mpaka leo ingawa sina taarifa naye nafikiri bado anatumika mahali pale.

Katika kuamua watu walio katika kundi hili lazima hekima na maarifa ya Roho Mtakatifu itumike kwa sababu bila hivyo unaweza kujikuta unaharibu huduma, na pia kusababisha hata watu ambao walikuwa wametulia ndani ya kanisa wanaanza kuyumba kwa sababu ya mtu mmoja tu. Kumbuka pia kuna wengine wanapotaka kuhama kwa kawaida huhama na watu au kundi la watu.

Mchungaji lazima uwe makini na hawa wanaotafuta uongozi kwako. Hasa wenye karama fulani fulani kanisani, kwa sababu mwishowe huamua kuhama na kundi la watu wengi. Nimewahi kuwashuhudia vijana wengi wenye huduma ya kuimba, wanapohamia makanisa mengine huwa wazuri kwa mara ya kwanza, lakini baada ya kufundisha kwaya nyimbo mbili tatu, hutaka kulipwa zaidi, na ukikataa kuwalipa huamua kuondoka-wakiondoka,hawaondoki peke yao bali hushawishi vijana wengine pia. Kutafuta kiki ni sawa lakini kwa njia gani ni muhimu sana.

Tumwogope Mungu kwa matendo yetu kila siku na kila wakati!HIZI NI SIKU ZA MWISHO?Hili ni swali wengi hujiuliza na kukosa...
07/08/2024

Tumwogope Mungu kwa matendo yetu kila siku na kila wakati!

HIZI NI SIKU ZA MWISHO?

Hili ni swali wengi hujiuliza na kukosa Majibu zaidi

Nabii Daniel alizungumza juu ya β€œWAKATI WA MWISHO.” Mtume Petro alisema, β€œkatika SIKU ZA MWISHO watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki.” Paulo alisema, β€œSIKU ZA MWISHO kutakuwako nyakati za hatari.” Wanafunzi wa Kristo walimwuliza juu ya β€œMWISHO WA ULIMWENGU.” Je, wakati huo umefika? Unaweza kuwa na uhakika?

Mpaka lini Kristo atarudi? Kabla tukio hili kubwa kuliko yote halijatokea, Biblia huongelea juu ya kipindi kinachoitwa β€œsiku za mwishoβ€β€”β€œwakati wa mwishoβ€β€”Β­β€œmwisho wa ulimwengu [zama]β€β€”β€œmwisho wa mambo hayaβ€β€”β€œmwisho wa siku”—na ya wakati ambapo historia ya mwanadamu, k**a tuijuavyo, β€œitakapomalizika.”

Bila shaka, wengi wanaojidai kuwa Wakristo hawaamini katika tukio halisi la kurudi kwa Yesu Kristo duniani. Miongoni mwa wanaoamini, wengi wao huamini kwamba inaweza kutokea baada ya miaka mamia ijayo. Baadhi wanaamini inaweza kuwa β€œmiaka maelfu ijayo.” Wengine kwa namna fulani wanafikiria juu ya β€œHar-Magedoni.” Wanahisi kwamba wakati unaweza kuwa mfupi lakini hawana uwezo wa namna ya KUJUA.

Wewe unaamini nini?

MITUME WA AWALI πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mitume wa awali walifikiri kwamba Kristo angerudi wakati wa maisha yao. Paulo katika 1 Wakorintho 15:51 na 1 Wathesalonike 4:15, alipokuwa akiongelea ufufuo wa wafu utakaotokea Kristo anaporudi mara ya pili, alitumia neno β€œsisi” akitegemea kuwa mmoja wa wale ambao wangekuwa β€œhai, [tutakao] salia hata wakati wa kuja kwake Bwana.”

Katika waraka wake wa pili kwa Wathesalonike, Paulo alikuwa amegundua kwamba hapo awali alikuwa ameelewa vibaya muda wa kutokea matukio maalumu ambayo ni lazima yatangulie Kurudi kwa Kristo. Alienda mbele na kuonya dhidi ya wale ambao wangedanganya wengine juu ya lini tukio hili lingetokea. Aliandika juu ya β€œkuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo” na ndugu wanapaswa wawe waangalifu kwamba β€œMtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu” (2 Wathesalonike 2:1, 3).

KURUDI KWA KRISTO MARA YA PILI

Je, tuko kwenye siku za mwisho? K**a ndivyo, unaweza kujua kwa hakika kwamba hii ni kweli? Yesu alisema kwa wanafunzi wake, β€œNitarudi tena” (Yohana 14:3). Siku arobaini baada ya kufufuka kwake, wanaume wawili (malaika) waliwaambia wanafunzi wake wakati anapaa mbinguni, β€œHuyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni” (Matendo 1:11). Mathayo anaandika maneno ya Kristo: β€œMaana k**a vile umeme uonekanavyo…ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu” (Math. 24:27, 30, 37, 39, 42, 44, 46). Je, karibu ulimwengu utalifikia tukio hili la upeo wa juu kabisa? Tena, je, tunaweza kujua?

Usifanye kosa! Biblia iko wazi kuhusu Kurudi kwa Yesu Kristo. Mafungu mengi zaidi yanayoongelea Kurudi Kwake Mara ya Pili duniani yanaweza kunukuliwa. Kutatokeaβ€”na haitegemei juu ya mapendekezo ya wanadamu. Hata hivyo, kabla tukio hili la juu kabisa halijatokea, mambo mengine mengi zaidi yalisemwa yatatokea katika kipindi cha kuelekea matukio ya kutisha yanayotangulia kurudi kwake!

Dhana ya mwisho wa ulimwengu limekuwa ni somo lenye hisia, kejeli, mjadala, kusisimua na linalowafanya watu wafikiri kwa miaka 2,000. Bado, ni wachache wanaofahamu kiasi gani Biblia inaonyesha juu ya kile kinachoweza kueleweka kuhusu wakati huu.

β€œSIKU NA SAA”

Katika unabii maarufu wa Mlima wa Mizeituni kwenye Mathayo 24, wanafunzi walimwuliza Kristo, β€œTuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja Kwako, na ya mwisho wa dunia?” (fu. 3). Baada ya kujibu swali hili kwa kirefu, mafungu thelethini-na-tatu baadaye Kristo aliongeza, β€œWalakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake” (fu. 36).

Je, hii inamaanisha kwamba hatuwezi kujua kiujumla wakati wa Kuja kwa Yesu Mara ya Pili? Baadhi wanaamini hiviβ€”na watu hawa hutupilia mbali hitaji lolote la kujishughulisha ili kujua lini kutakuwa Kurudi kwa Kristo.

Mathayo 24:50-51 humaanisha nini inaposema, β€œbwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki”? Ni wazi kwamba karibu kila mmoja hategemei Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili katika wakati sahihi. Ukweli ni kwamba atarudi wakati ambapo wengi hawamtazamii kabisa. Kitu gani kitawafanya wengi wasitambue mwanzo wa tukio hili kubwa?

Litaendelea..............

1⃣ KUMTII MUME WAKE KATIKA BWANA1 petro 31 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Nen...
06/08/2024

1⃣ KUMTII MUME WAKE KATIKA BWANA

1 petro 3

1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

PIA SOMA(KOLOSAI 3:18)

➑ Kwa Tafsiri nyingine ni kuwa mwanamke anapokuwa MTII hiyo ni injili tosha kabisa kwa mume wake na hata ikiwa mume hajamwamini Yesu, ule utii unamvuta aweze kuamini. Utii anaouzungumza hapo siyo ule wa kukubali kila kitu. Katika Waefeso anasema k**a ipendezavyo katika Bwana.

➑ Mwanamume siku zote anapendezwa na utii ndani ya mke na siyo vinginevyo.

Unaweza jipamba ukawa na nywele k**a mzungu, kope k**a mdoli, midomo myekundu k**a damu, uso mweupe k**a mwarabu, kucha ndefu k**a za tai, n. K nguo zinazovutia hata wanaume wa mtaani n. K, lakini k**a hauna UTII, atakuchukulia tu k**a mwanamume mwenzake. Ndio maana Mtume Paulo katika 1TIMOTHEO 2:9 pia 1Petro 3:3 anasisitiza kuto kuweka kipaumbele katika mapambo ya nje bali ndani ya moyo.

➑Wanawake qengi wamekuwa wakilia kuachwa na wachumba wengi lakini hawajiulizi kwanini yeye tu ndo aachwe na watu wengi, mbona mwenzio kaolewa??.

Usihangaike dada yangu, kujirudia rudia kujiangalia kwenye KIOO sura yako ukidhani ni mbaya ndo maana unachukiwa. WEWE NI MZURI SANA TENA MREMBO MNO. Ila unaweza kuwa na tatizo moja linalokusumbua. UTII wako upoje kwa mchumba au mumeo.???

➑ Wapo wanawake wengine kwenye ndoa wanasababisha uchungu kwa waume zao kwa sababu wanakosa utii. Mwanaume anafikia wakati anapoteza HISIA za kuwa na wewe(affection) wengine akikosa uvumilivu anaanza kutoka nje ya ndoa.

🌸 NIKUPE SIRI HII MAMA;

➑Kugombana kwenu au kupishana kwenu katika Mazungumzo kusiwe sababu ya kutomuwekea maji ya kuoga, kutompikia chakula ama kutompokea mzigo atokapo kazini. Hili ni bomu kubwa sana usipokuwa makini. UKITAKA USHINDE; wewe mpikie chakula, mpe maji ya kuoga tena ikiwezekana omba hata umsindikize bafuni, mpokee mzigo atokapo kazini na kumwambia pole mume wangu/mpenzi wangu/sweetheart wangu/darling wangu/honey wangu/tomato sauce wangu, n. K nakuambia lazima hasira zake sishuke tuuu… Halleluyah!!!!!!!!!

NDOA ni mapatano ya kiroho(spiritual)  na kimwili(physical) kati ya mwanamke na mwanaume ya kuishi pamoja k**a mke na mu...
06/08/2024

NDOA ni mapatano ya kiroho(spiritual) na kimwili(physical) kati ya mwanamke na mwanaume ya kuishi pamoja k**a mke na mume.

πŸ”…Kiroho ni kwa sababu yanamhusisha Mungu pia. Na hapo haijalishi wanandoa /hao watu wanamjua Mungu au lah.

MWANZO 2:

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

HAPA anasema watakuwa MWILI MMOJA maana yake huu ni muunganiko wa kimwili katika namna ya kiroho na ndiyo maana Mungu anahusika.

Huu muunganiko unahusisha mwanaume(ADAMU) na mwanamke(EVA) ambaye lazima kiungo (ubavu wake) uwe umetolewa kwa huyo huyo mwanamume(ADAMU) katika namna ya kiroho, hivyo kwa mwilini ni vigumu kutambua kuwa nani ambaye umeumbiwa.

➑ Mtu asikudanganye kuwa mtu yeyote aweza kuwa Mume/mke wako. Lazima sehemu ya EVA(UBAVU) iwe imetoka kwa Adamu fulani uliyeumbiwa na Mungu.

➑ Wewe dada, kuna mtu pekee ambaye katika ulimwengu wa roho wewe umetwaliwa kwa huyo,, na huyo ndiye pekee Mungu anataka uishi naye k**a mume wako. Suala siyo tu kwa vile mnapendana na mtu basi ndo useme huyu ndiye kusudi la Mungu, no no no.

MITHALI 19 :14

14 Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.

Ndiyo maana biblia inasema mambo ya rohoni hutambulikana kwa jinsi ya rohoni na watu wa rohoni

Kwa hiyo kwa watu wasio wa rohoni ataona kuwa mtu yeyote ilimradi wanapendana basi anastahili kuwa mume/mke wake. K**a ni hivyo mbona mimi ninapendana na wadada zaidi ya mia moja ambao hawajaolewa? Je, niseme kuwa yeyote kati yao anastahili kuwa mke wangu??? LA HASHA.

➑Kusudi la Mungu kumuumba mwanaume na mwanamke na kuwafanya waishi pamoja siyo tu ili wawe mume na mke, bali PIA wawe MTU NA MSAIDIZI wake katika kutimiza kusudi la Mungu ambalo kwalo mwanadamu aliumbwa.

Mungu hajakuumba na kukuweka duniani uje UOANE, Mungu amekuleta duniani kwa kazi ya KUILIMA NA KUITUNZA bustani ya Edeni( kulifanya/kulitimiza kusudi la Mungu la wewe kuletwa duniani). Na kwa kutambua UZITO wa kazi aliyoiweka ndani yako akaamua awaweke muqe wawili ili kurahisisha utendaji wa hilo jukumu kwa namna ya kiroho.

MHUBIRI 4:

9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Njoo watsApp somo litamalizika huko Mungu Akubariki sana

Roho mtakatifu ndiye chanzo cha kweli. Imeandikwa Yohana 14:16-17 "Nami nitamwomba Baba naye atawapa msaidizi mwingine i...
06/08/2024

Roho mtakatifu ndiye chanzo cha kweli. Imeandikwa Yohana 14:16-17 "Nami nitamwomba Baba naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele ndiye roho wa kweli amabaye ulimwengu hauwezi kumpokea kwa kuwa haumwoni wala haumtambuibali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu naye atakuwa ndani yenu."

Kupokea Roho mtakatifu ni kuzaliwa upya. Imeandikwa, Yohana3:5-7 "Yesu akajibu amin amin, nakwambia mtu asipo zaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika ufalme wa Munngu kilicho zaliwa kwa mwili ni mwili na kilicho zaliwa kwa roho ni roho usistaaajabu kwa kuwa nilikwambia hamna budi kuzaliwa mara ya pili."

Kupata Roho mtakatifu uliza kisha amini naye atakushukia na kukuongoza. Imeandikwa, luka 11:13 "Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyemaje! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa roho mtakatifu hao wamwombao?." Matendo ya mitume 5:32 "Na sisi tumashahidi wa mambo haya pamoja na Roho mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio."

Roho mtakatifu ni oja wapo ya ungu yani ungu Baba, mwana naye Roho mtakatifu. Imeandikwa Matendo ya mitume 5:3, 4 "Petro aksea, Anania kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya dhamani ya kiwanja kilipokuwa kwako hakikuwa mali yako na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, dhamani yake haikuwa katika uwezo wako? ili kuwaje hata ukaweka neno hilo mwonyoni mwako? haukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu."

Roho takatifu ni Mungu anaye ishi nadani ya waqle wanao mwamini. Imeandikwa, Mathayo 18:19-20 "Amin nawaambieni yo yote takayofunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni na yo yote mtakayoyafungua duniani yatafunguliwa mbinguni... tena nawaambia ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba watafanyiwa na Baba yangu aliye mbiguni kwa kuwa walipo wawili watatu waekusanyika kwa jina langu nami nipo papo hapo katikati yao."

Roho mtakatifu yupo nasi wakati wataabu, Imeandikwa, Mathayo 10:19-20 Lakini hapo watakapo wapeleka msifikiri -fikiri jinsi mtakavyosema maana mtapewa saa ile takayosema kwa kuwa ninyi msemao bali ni Roho wa Baba asemaye ndani yenu."

Roho mtakatifu hutu saidia kumwabunu Mungu. Imeandikwa Yohana 4:23-24 "lakini saa inakuja, nayo saa ipo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu Mungu ni Roho nao wamwabudu katika roho na kweli."

Roho hutupa uwezo wa kunena mambo ya kiroho na uwezo. Imeandikwa, Matendo ya mitume 1:8 "Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi ktika Yeresalemu na katika uyahudi wote na Samaria na mwisho wa nchi."

Dhana ya kumwabudu Bwana "kwa roho na kweli" inatoka kwenye mazungumzo ya Yesu na mwanamke kwenye kisima katika Yohana 4...
06/08/2024

Dhana ya kumwabudu Bwana "kwa roho na kweli" inatoka kwenye mazungumzo ya Yesu na mwanamke kwenye kisima katika Yohana 4: 6-30. Katika mazungumzo, mwanamke alikuwa anazungumzia mahali pa ibada na Yesu, akisema kuwa Wayahudi waliabudu huko Yerusalemu, na Waasamaria waliabudu kwenye Mlima Gerizimu. Yesu alikuwa ameshuhudia kwamba alijua kuhusu wanaume wake wengi, pamoja na ukweli kwamba mwanamme ayeishi naye wakati huo hakuwa mume wake. Hii ilimtia wasiwasi, kwa hiyo alijaribu kupotosha mawazo Yake kutoka kwa maisha yake binafsi na kuzungumzia mambo ya dini. Yesu alikataa kupotoshwa kutoka kwa somo lake kuhusu ibada ya kweli na akalizungumzia kwa kina: " Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu. "(Yohana 4:23).

Somo la jumla juu ya kumwabudu Bwana kwa roho na kweli ni kwamba ibada ya Mungu haifai iwe kwenye sehemu moja ya kijiografia na sio lazima iwe chini ya sheria za Agano la Kale. Kwa kuja kwa Kristo, utengano kati ya Myahudi na Mataifa haukukuwa muhimu tena, wala ukumbi wa hekalu katika ibada. Kwa kuja kwa Kristo, watoto wote wa Mungu walipata fursa sawia kwa Mungu kupitia kwake. Kuabudu ikawa suala la moyo, sio vitendo vya nje, na kuongozwa na ukweli badala ya sherehe.

Katika Kumbukumbu la Torati 6: 5, Musa anawaelezea Waisraeli jinsi wanapaswa kumpenda Mungu wao: "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa uwezo wako wote". Kumwabudu kwetu kunachochewa na upendo wetu kwake ; k**a tunavyopenda, basi tunamwabudu. Kwa sababu dhana ya "nguvu" kwa Kiebrania linaonyesha kwa ukamilifu, Yesu aliongeza maana ya neno hili kuwa "akili" na "nguvu" (Marko 12:30; Luka 10:27). Kumwabudu Mungu kwa roho na kweli kunahusisha kumpenda kwa moyo, roho, akili na nguvu.

Kuabudu kweli lazima iwe "kwa roho," yaani, kushirikisha moyo wote. Pasipokuwa kuna shauku halisi kwa Mungu, basi hamna ibada katika roho. Wakati huo huo, ibada lazima iwe "kwa kweli," ambayo ni sahihi. Isipokuwa tunajua Mungu tunayeabudu, hakuna ibada kwa kweli. Yote ni muhimu katika ibada ya kuridhisha na ya heshima kwa Mungu. Roho bila ukweli husababisha hisia isiyo ya kina ambayo inaweza kulinganishwa na kuasi. Mara baada ya hisia kukamilika, wakati shauku inapotea, pia ibada inapotea. Ukweli bila roho unaweza kusababisha ushujaa kavu, usio na shauku ambayo sio halali. Mchanganyiko bora wa mambo yote mawili ya ibada husababisha shukrani ya furaha kwa Mungu iliyochochewa na Maandiko.Tunavyojua zaidi kuhusu Mungu, tunamthamini zaidi. Tunaposhukuru zaidi, ihaina budi kuwa na ibada kwa kina. Tunapozidi kuabudu, Mungu hutukuzwa zaidi.

Mchanganyiko huu wa roho na kweli katika ibada umeelezewa kwa kina na Jonathan Edwards, mchungaji wa karne ya 18 wa Marekani na mwanateolojia. Alisema, "Ni lazima nidhani nafsi yangu kwa njia ya wajibu wangu kuinua [hisia] za wasikilizaji wangu kwa kadiri iwezekanavyo , isipokuwa wanaathiriwa na chochote isipokuwa ukweli." Edwards alitambua kwamba ni ukweli pekee unao shawishi vizuri hisia kwa njia inayoleta heshima kwa Mungu. Ukweli wa Mungu, kuwa na thamani isiyo na kipimo, unastahiki shauku isiyo na mwisho.

Somo hili litamalizikia watsApp njoo jiunge moja kwa moja kupata Elimu hii ya kiroho Amen

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when π”π“π”πŠπ”π…π” π‡πŽπ’π’π€ππ€ 𝐉𝐔𝐔 πŒππˆππ†π”ππˆ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share