30/09/2018
KIVULE-DAR ES SALAAM -TANZANIA
TAREHE: 23/09/2018
UJUMBE: DHAMBI NO.1
UTANGULIZI
• Miongoni mwa vitu vikubwa ambavyo mtu anayemuamini YESU KRISTO anatakiwa kufurahia na ni:
- Kukemewa kuhusu dhambi.
- Kukaripiwa na kuonywa juu ya dhambi.
- Kufundishwa na kuelekezwa namna ya kushinda dhambi.
Kwanini?
Dhambi inayomtenganisha mtu na Yesu Kristo.
(TIMOTHEO 4:13)
(Baraka za mwamini zinakuja pale anapoamua kumtii Yesu Kristo).
Tabia ya dhambi inamuotea mtu: na inamtamani mtu.
• Roho Mtakatifu umfunulia na kumfundisha mtu kuhusu dhambi na kumpa mtu nguvu ya kushinda dhambi.
• Maswali ya kujiuliza:
Dhambi ni nani?
Na ni nani anayempa nguvu huyu dhambi.
Jibu: ni ibilisi
• Dhambi ni nini?
Dhambi ni roho chafu ya ibilisi inayodhihirisha matendo yake kwa kutumia vitu na tabia mbalimbali za kibinadamu.
• Dhambi kwa maana nyingine ni tunda la roho chafu (ibilisi) ambalo linazaliwa ndani ya mtu pale anapoach akuitii Sauti ya Mungu (NENO LA MUNGU).
• ZINGATIA
• Makosa yangu yasinifanye niukimbie Uso wa Mungu, lakini yanifanye nione sababu ya kumsogelea Mungu Zaidi.
• Makosa yasinitoe kwenye uwepo wa Mungu bali yawe sababu ya kunipeleka Zaidi kwenye uwepo wa Mungu.
• Dhambi ni roho ya giza ndio maana utakuta mtu anapambana dhidi ya dhambi leo, ila kesho yupo kwenye dhambi tena, kwa sababu hajatoa nafasi ya kutii Neno la Mungu.
• Ibilisi anajua mtu anashinda dhambi kwa kutii Neno la Mungu, (ndio maana anaweza kutumia pia Neno la Mungu kumjaribu mtu ili akosee pale anapojua mtu anatii Neno La Mungu).
• Dhambi ni roho chafu ya ibilisi inayofanya kazi kwa kutumia watu na vitu vinavyoonekana.
• Dhambi ni roho, nitaweza kupambana na roho hiyo kwa kuamua kuingia rohoni.(Roho upambana na roho)
• Mtu anakuwa roho pale anapolijaza Neno la Mungu ndani mwake ma kuwa k**a Roho Mtakatifu anavyotaka, kwa kuomba, kwa kufunga na kwa kujinyenyekesha kwa Mungu.
• Yesu Kristo alituonyesha mfano wa wazi wa kufunga, kuomba, na kuskesha ili kumtafuta Mungu na kuishinda dhambi.
• Ndio maana Yesu Kristo ingawa alikuwa katika mwili huu wa dhambi, hakutenda dhambi.
• Watumishi wote wa Mungu adui wao mkubwa ni dhambi (ibilisi)., sababu wanajua kitendo wakikosea tu, wanapoteza mamlaka yao kwa ibilisi, hawataweza kumtiisha tena/ kumkemea.
• Dhambi wakati mwingine utumia udhaifu wa mtu au mawazo ya mut kumshambulia mtu.
• Ufahamu na maarifa juu ya Neno la Mungu vina nguvu ya ajabu ya kuweza kumpiga ibilisi k**a nimeamua kuruhusu Neno la Mungu likae ndani mwangu.
• Hata k**a naomba kwa juhudi kiasi gani k**a sina maarifa ya Nneo la Mungu na mahusiano mazuri na Mungu nijue wazi tayari ibilisi ameshanishinda.
• Biblia inasema mpingeni ibilisi katika uthabiti wa Imani.
• Imani haiwezi kuwa thabiti k**a sina maarifa ya Neno la Mungu ndani mwangu.
• Inahitaji maarifa ya NENO LA MUNGU ndani ya mwamini kuamuru vitu na vikatokea.
• Bila maarifa ya Neno la Mungu watu uangamia.
• MWANZO 4:5-…..
• Dhambi ni roho giza inafanya kazi katika ulimwengu wa giza na sio wa nuru.
• ZINGATIA:
K**a wewe una roho giza, inakuwaje ukemee ufalme wa giza? MATENDO 19:11-16
• Dhambi uondoa mamlaka ya Mungu katika maisha ya mwamini.
• Ndio maana mtume Yohana akasema aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi bali ujilinda asitende dhambi.
• 1YOHANA 3:9
• Katika suala la dhambi mtu hujilinda, yaani, ana uchaguzi aidha afanye au akatae dhambi.
• Na mtu uwa mtumwa wa yule aliyeamua kumtumikia, ikiwa ni utumwa wa dhambi kwa uangamivu wake mwenyewe, ama ukiw autumwa wa haki kwa wokovu wa roho yake mwenyewe.
• Dhambi ikimvaa mtu uondoa aibu na hofu ya Mungu ndani ya mtu.
• Dhambi (roho chafu ya giza) ina uwezo wa kupofusha ufahamu wa mtu asione k**a anakosea.
• Dhambi ikimvaa mtu umtawala mtu, anakuwa hana maamuzi yake tena, kwa kuwa dhambi umuongoza
• WARUMI 7:14-25
• Mimi nina maamuzi ya roho chafu kukaa mbali na mimi kwa kuamua kutii Neno la Mungu.
• Vilevile nina maamuzi ya roho chafu iniingie na kukaa ndani yangu kwa kuacha kutii Neno la Mungu.
• MWANZO 4:5-10
• Mara nyingi tunaisikia Sauti ya Mungu lakini moja ya changamoto kubwa tuliyonayo ni katika kutii maelekezo ya Sauti ya Mungu.
• Inahitaji Imani na utii wa Neno la Mungu ndani ya mtu ili aweze kutii Sauti ya maelekezo ya Mungu.
• Yesu Kristo akiona maamuzi ya mtu ya kukataa dhambi, ndipo umpa nguvu ndani yake ya kuishinda dhambi.
• (MITHALI 7:7-…)
• Roho ya dhambi ikishaingia ndani ya mtu, mtu uwa na tabia hizi:
- Hakubali kuonywa
- Ujiona yuko sahihi na anajua kila kitu.
- Ujihesabia haki.
• Ila kwa mtu mtiifu na mnyenyekevu akigundua tu amekosea papo hapo uingia magotini kumsihi Mungu rehema, uwa aanzi kujitetea.
• Mfano: Mfalme Daudi (Soma 2 SAMWELI Sura ya 11 na 12
• (Nisitumie udhaifu nilionao kuruhusu au kuhalalisha roho chafu ya dhambi initawale).
• Roho chafu ula katika tabia mbaya za watu ( tabia mbaya ni chakula cha roho chafu)
• Kile ambcho ndani mwako umekusudia kukifanya ikiwa ni cha Kimungu, Roho Mtakatifu atakithibitisha (kwa kupitia Neno lake).
• K**a ilivyo kwa matunda ya Roho Mtakatifu dhambi pia ina matunda ya roho chafu, ambazo ni:
- Ghadhabu
- Wivu
- Chuki
- Dharau
- Kutokutii
- Uchoyo
- Matukano/matusi
- Kiburi cha uzima
- Tamaa mbaya za mwili
- Utovu wa nidhamu
- uongo
- Kutokuamini n.k
• Miongoni mwa vitu ibilisi amewafunga watu in kuwazuia wasipate maarifa ya Neno la Mungu.
• WARUMI 1(Soma yote)
TAREHE: 30/09/2018
Mahusiano yangu na Mungu yakiimarika mahusiano yangu na Mungu pia yataimarika.
Kwanini?
Kwasababu mtu uanza kumpenda Mungu kwanza ndipo atapenda na wenzake pia
Mahusiano yangu na Mungu ni ya muhimu kuliko mahusiano yangu na mwanadamu yoyote yule.
UJUMBE: DHAMBI- SEHEMU YA .2
• DHAMBI NI UASI.
• Nini maana ya uasi?
• Hauwezi kuacha kitu ambacho haukijua,lakini pia hauwezi kuchukia kitu ambacho haukijui.
• Ibilisi hahitaji mtu anahitajiroho ya mtu, ukimkubali tu akak**ata fikira zako atakuongoza kufanya kile anachotaka ukifanye.
• Ibilisi uja kwa njia ya ushawishi ndio maana uitwa mjaribu.
• Ibilisi anaweza kukujaribu kwa kutumia au kupitia uhitaji ulionao.
• Ibilisi pia anaweza kukujaribu kwa kukuonyesha maono feki.
• Ibilisi utumia vitu na tabia za kibinadamu kumsahwishi mtu.
• YAKOBO Biblia inasema mtu ujaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe uku akivutwa na uongo.
• Ibilisi umdanganya mtu kwa kutumia tamaa yake mwenyewe.
• Inahitaji maarifa ya Neno la Mungu na maongozi ya Roho Mtakatifu kutambua kwamba uyu ni ibilisi.
• Biblia inasema watu wangu wanangamia si kwa kukosa upako, bali kwa kukosa maarifa.
• K**a ambavyo Mungu anahitaji maamuzi yako kwa kutoa muda wako kufanya anachotaka ili
• Vivyo hivyo ibilisi anasubiri utoe maamuzi kwa kutoa muda wako kufanya anachotaka ili akuletee uharibifu.
• *DHAMBI NI UKUTA KATI YA MTU NA MUNGU, hii ina maana nikitenda dhambi katika fikra zangu, moyo wangu, na mwili wangu, nimejiwekea ukuta kati yangu na Mungu.
• (ndio maana Yesu Kristo ni Mpatinishi kati yetu na Mungu.)
• Nikitenda dhambi ninajiondolea haki ya kusikiwa na kujibiwa maombi yangu na Mungu.
• ISAYA 59:1
• *KUASI maana yake ni kukana wenzako na kuacha utaratibu mliojiwekea na kuingia upande wa adui., kwa hiyo unapoingia kule umepoteza haki ya kundi uliloliacha, na kundi uliloliacha haliwezi kukuacha ubaki salama sababu linajua wazi unafahamu siri za kundi husika kwahiyo unaweza kuzitumia kuleta uharibifu kwenye kundi lako uliloasi.
• Hali ya uharibifu ikishaingia ndani ya ufahamu wa mtu aliyemuasi Mungu hata akiambiwa ujumbe wa Mungu hawezi kuuelewa au kuukubali kwa sababu ya hali ya mazoea.
• (Mungu ana njia nyingi za kuzungumza na mtu)
• Unapotenda dhambi unajiletea mwenyewe uharibifu kwenye maisha yako.
• (Changamoto tulizonazo si sababu ya sisi kutenda dhambi, bali ziwe chanzo cha kumsogelea Mungu Zaidi).
• *Dhambi inapofusha macho ya mtu ya rohoni asione k**a ambavyo Mungu anaona; masikio ya rohoni asisikie k**a Mungu anavyosikia.
• *Dhambi inapofusha ufahamu wa mtu wa rohoni asiwe na uwezo wa kupambanua, kwamba hiki ni sahihi, na hiki si sahihi.
• (Mungu ametoa nafasi ya mimi kuchagua kati yay eye na ibilisi, ni nani nitamtumikia).
• Kitu cha kwanza ambacho natakiwa kuogopa sana ni mahusiano yangu na Mungu, natakiwa niwe makini sana yasiharibike, ni hatari.
• Biblia haisemi Mungu atakulinda na dhambi, bali inasema aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi bali hujilinda mwenyewe asitende dhambi.
• 1 YOHANA 2:15-………
• Yohana 8:41
• Moja ya adui mkubwa wa mtu anayeamini, si jirani yake au mtu mwezake, bali ni roho chafu ya dhambi ndani ya mtu.
• Zingatia:
• Ni rahisi sana kumkaribisha ibilisi ndani mwako, ila ni vigumu sana kumtoa, inahitaji neema.
• DHAMB NI UASI:
UASI ni kukimbia ufalme mmoja au ufalme wangu ambao nilizaliwa ( sisi tumezaliwa kwa Neno katika roho) na kuingia ufalme wa pili ambao unapingana n aufalme wangu.
Zingatia:
Kuna kukimbia ufalme na kuna kutekwa.
Mfano: roho chafu zinakuvizia wakati wa kulala, ama wakati ambao haujaomba, ama wakati ambao nimeacha kusoma Neno, ama kwa njia ya ndoto.
Mtu mara nyingi amuachi Mungu haraka, balia uanza kidogo kidogo, kwa kuanza kulipuuzia Neno la Mungu.
• Wengi wetu tunaishi maisha ya kinafiki tukijifanya tumeokoka wakati tayari rohoni tumeharibu mahusiano yetu na Mungu. Hapo hatumdanganyi mtu bali tunajidanganya wenyewe na kujiletea uharibifu wenyewe.
• Watumishi wa Mungu wameamriwa kukemea, kukaripia na kuonya na kurejesha kwa upole pale mtu anapoanguka dhambini, na si kuwahukumu au kuwatenga pale wanapokosea.
ZINGATIA
“Ogopa kukaa mahali hatari bila kuchukua tahadhari”.
Unapokuwa mkristo anayeishi maisha ya kawaida tu k**a mtu mwingine asiyeamini, ni hatari kwake, anaweza kupigwa.
• ISAYA 1:15-……
• Unapoingia katika kuomba hakikisha ndani mwako umeweka dhambi zako mbali nawe, yaani unaacha.
• Dhambi ni dhambi, hakuna tofauti ya dhambi na dhambi wala hakuna dhambi ndogo na kubwa.
• Mfano: anayesema uongo ni sawa sawa tu na anayezini.
• *kitendo cha kutenda dhambi maana yake umemtii ibilisi.
• *dhambi ni mujumuiko ya matendo yote yasiyo ya haki, yasiyo halali.
• *DHAMBI NI UHALALI WA ADUI (IBILISI) KUMKALIA MTU. (ni leseni ya makazi kwa mtu).
• Wajibu wa watumishi wa Mungu ni kufundisha watu yaliyo kweli, ila maamuzi ya kukaa katika kweli hiyo no maamuzi ya mtu.
MAMBO YA KUJIFUNZA
NAMNA GANI ROHO YA DHAMBI INAMUINGIA MTU;
NI NAMNA GANI MTU ANAWEZA KUPINGANA NA ROHO YA DHAMBI.
• LAZIMA UJUE SILAHA ZA ADUI NA MBINU ANAZOZITUMIA ADUI NDIPO UWEZE KUPIGANA NA ADUI
• UKIINGIA KUPINGANA NA ADUI KABLA YA KUJUA SILAHA NA MBINU ANAZOTUMIA ADUI LAZIMA UTAPIGWA.
HAUWEZI KUIJARIBU ROHO K**A WEWE SI ROHO.
NINAKUWA ROHO KWA KUPATA MUUNGANIKO NA ROHO MTAKATIFU
•
• WOTE WALIOUNGWA NA BWANA NI ROHO MOJA NAYE.