Phares Sedekia

Phares Sedekia HOLY Spirit Church,
Spirit Driven Church,
spiritual movement,

10/12/2025

U P A K O

Upako ni kufunikwa na Mungu. Kuwa na Mungu au kuzungukwa na Mungu pande zote mahali popote ulipo. Ni kutembea Mungu au Mungu kukutangulia k**a ilivyokuwa kwa wana wa Israeli jangwani. Upako ni ishara ya Mungu kukutenga kwa kazi yake MAALUM.

Upako siyo mafuta AU maji ya upako. Upako hauuzwi kwa fedha. Wala siyo zana za rohoni.

Upako wa kibiblia ni ishara ya uwepo na nguvu ya Roho Mtakatifu, uliotolewa kwa watu walioteuliwa na Mungu ili kutekeleza majukumu maalum k**a makuhani, manabii, na wafalme.

Neno la Mungu ni upanga wa ROHO (Waefeso 6:17), hii ndiyo zana ya rohoni. Utakosea ukisema kuwa mafuta ni zana.
Watu wasome neno la Mungu, wajifunze kusoma Biblia kwa bidii. Wakisoma wataijua njia sahihi ya Mungu. Watayajua mawazo ya Mungu juu yetu. Wataijua mipango ya Mungu juu yetu. Wataijua nafasi yao katika Ufalme wa Mungu. Wataijua NGUVU iliyo ndani yao na jinsi Mungu alivyowaficha ndani ya Kristo ( wakolosai 3:3)

Mungu kanipa mafunuo haya niwaambie watu waache kujichanganya AU kujihadaa na kujidanganya.

Watu wasije wakajikuta wanamwacha Mungu kwa kuyafanya mafuta au maji kuwa miungu. Wasije wakasema mafuta yanaponya au maji yanaponya. Kumbe Neno la Mungu ndilo linaloponya (Zaburi 107:20).

Kibiblia mara nyingi mafuta yalitumika k**a ishara ya kuwasimika viongozi kuwa Mungu ameridhia awe kiongozi. Nabii Samweli alimpaka mafuta Sauli awe mfalme wa Israeli ( 1Sam 9:15-16, 1Sam 10:1). Nabii Samweli alimpaka mafuta DAUDI awe mfalme baada ya Sauli kukataliwa au kutenguliwa (1Sam 16:13).

Na Barnaba na Paulo Mungu alipowachagua kwa kazi ya MITUME, waliwekewa Mikono k**a ishara ya Upako badala ya mafuta ( Mdo 15:1-3).

Lakini Yakobo 5:14 inasema k**a mtu hawezi, aombewe na kupakwa mafuta KWA jina la Bwana.
Hapa haimaanishi kuyafanya mafuta k**a miungu. Mafuta ni ishara ya uwepo wa Mungu. Mafuta hayakai badala ya Mungu, ukifanya hivyo unamaanisha KUABUDU sanamu. MAFUTA siyo Mungu, usiyaabudu au kuyasifia au kuyachukulia kuwa ya maana sana katika ibada. Yametumika ukapona, mshukuru Mungu, na SIFA zote umpe Mungu na siyo kusema, mafuta mafuta mafuta mafuta mafuta mafuta.

Natumaini umenielewa vizuri.

ILI KUJIFUNZA ZAIDI
SOMA

Waebrania 1:9
Waebrania 4:12
1Yohana 2:20
Marko 6:13
Yakobo 5:14

Mafuta yametumika KWA NAMNA nyingi katika Biblia. Nakutahadharisha usiyafanye miungu. Soma NENO, jifunze KWA bidii na kuomba.

HITIMISHO
Upako wa kibiblia ni zawadi ya Roho Mtakatifu inayomsaidia mtu kutekeleza kazi ya Mungu kwa nguvu na ufanisi. Ni ishara ya kuwekwa kando au kutengwa na ni ishara ya uthibitisho wa Mungu. Katika Agano Jipya, upako unahusiana moja kwa moja na maisha ya utii kwa Kristo na kujaa Roho Mtakatifu.

UBARIKIWE SANA.

KARIBU LEO KATIKA BIBLE STUDY.

TUPIGIE SIMU / SADAKA
0755288412
0783157766
0769407195
0793004323

02/12/2025

Mawazo ya Haki ni Matakatifu.

20/07/2025
Kesho Jumapili Usikose Ibada Hii.
14/06/2025

Kesho Jumapili Usikose Ibada Hii.

Address

Kwembe
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Phares Sedekia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share