Yesu Kwanza

Yesu Kwanza It's all about Jesus

14/08/2025
14/08/2025

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Emmanuel Kuguru, Nzala Tweve

14/08/2025
03/03/2025
08/12/2024

NAMNA YA KUUSHINDA MWILI WAKO.{USIUHURUMIE}
Na Dennis Davis.

“Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” 1 Wakorintho 9:27.

Shalom…
Mwili wako Ni jukumu lako.
Kwenye mstari wetu mkuu, huyo ni mtume Paulo. Mtu mkuu, aliyeijua neema vizuri, aliyekuwa na nguvu za Mungu ndani yake, aliyekua na maarifa yakutosha, lakini pia ni mtu aliyepelekwa mpaka mbingu ya tatu, aliyesema ananena kwa lugha kuliko kanisa lote la Korintho(1Kor 14:18), Alikutana na Yesu mwenyewe, hakufundishwa na mwanadamu bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo(Gal 1:12).

Kwanini nakuonesha yote hayo? Nataka nikuoneshe kuwa pamoja na yote hayo, Mtume Paulo anatueleza kuwa bado anautesa mwili wake na anautumikisha ili asije akawa mtu wa kukataliwa pamajo na kuwa amefanya kazi kubwa ya injili. Wewe na mimi mpendwa imetupasa kufanya hivyo hivyo pasipo kupungua. Mchezaji wa mpira wa miguu hujuzuia kwenye mambo mengi sana kwa ajili ya afya yake(fitness), sisi tulio ndani ya Kristo Yesu ni lazima tujizuie mambo mengi hasa ya mwilini maana mwili hushindana siku zote na Roho, mwili ni wa duniani na nia yake ni mauti.(Rum 8:6).

Kataa kuufuata mwili wako, jizuie, jizoeze kupata utauwa katika mambo yote, Warumi 8:13 “kwa maana k**a tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali k**a mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi”. Watu wengi wanasubiri Mungu ndo azuie hali za miili yao wakati Neno la Mungu liko wazi kuwa inatupasa kila mtu ajue namna ya kuuweza mwili wake mwenyewe. 1 Thes 4:4 “kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;”

Mwili wako ni jukumu lako. (YOUR BODY IS YOUR RESPONSIBILTY)

Matendo yapi ya kujizuia?
Ni haya, “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, k**a nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”

Usione kuwa ni ngumu na haiwezekani kwa kuwa na jibu la kuyashinda haya yote lipo ndani yako. JIBU NI HILI.

“ENENDENI kwa ROHO, wala hamtazitimiza KAMWE tamaa za mwili” . Gal 5:16.

Tendea kazi Neno la Bwana.

24/11/2024

These verses from the Bible offer timeless wisdom on when to keep our mouths shut, encouraging us to speak thoughtfully, avoid destructive speech, and strive for words that promote peace, understanding, and righteousness in our interactions with others. 🥹

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255762050072

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Yesu Kwanza posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share