Mwalimu Wa Kiroho

Mwalimu Wa Kiroho Mwalimu Wa Kiroho. Amen

Tuhimizane juu ya Upendo wa Kristo kwa kanisa la Leo, wokovu katika maisha, tuepuke matendo yasiyo faa na tujitahidi kutenda yaliyo ya upendo wa Mungu, hifadhi hazina yako katika Kristo na furahia matunda ya kazi yako.

18/07/2026

Kwanini ni muhimu kutoa sadaka?

Sadaka nimatoleo ya ibada, yanayo tolewa na waumini kwa lengo la kuonyesha utiivu na utekelezaji wa maandiko katika eneo hili la matoleo.

Katika maandiko Matakatifu, kwaeneo kubwa zaidi, Biblia inamtaka muumini kuwa mwaminivu na muadilivu katika kutekeleza maagizo ya Mungu katika maandiko haya matakatifu.

Moja ya maagizo ya Mungu kwa wanadamu, ni pamoja na kushika Amri 10 za Mungu, mfano, usiue. Hii nimoja ya onyo ambalo Mungu amemuonya mwanadamu duniani, hasa mwanadamu anae mwamini.

Kadhalika Sadaka ni matoleo ya ibada, ambayo Muumini atamtolea Mungu mbele ya kiongozi wa dini ama madhabahu ya anapo abudia.

Sadaka hii hutumika kununua chakula na maendeleo mengine ya nyumba ya ibada pamoja na wanao husika kusimamia mahali hapo, ambao ni watumishi wa Mungu mahali hapo.

Swali sadaka hii itakusaidia nini?

Sadaka inaruhusu kupokea baraka toka kwa mtu aliye barikiwa, yaani kupata sehemu ya baraka toka kwa mtu ambae Mungu amesha m'bariki.

Hivyo kwakutoa sadaka kanisani, mfano kanisa la RC, sadaka itakuruhusu kupokea baraka katika mfumo wa kanisa hilo, kuanzia parokia uliyo toa matoleo yako na kuenda hadhi shinani.

Kadhalika katika makanisa mengine, na hata kwa watumishi unao wajua na ukapata kibali machoni mwao, ikiwa utatoa matoleo yako kwao piya, utapokea sehemu ya baraka toka kwa watu hao ambao unaamini Mungu amewababriki katika nafasi yao.

Hii ni kwawatoaji.

Kadhalika kunawapokeaji wa sadaka.

Mtu anaye pokea sadaka ama unataka kupokea sadaka, kunamambo kadhaa unapaswa kusimamia.

Kwanza ama ujiunge na mtandao wa kanisa fulani, ama ufwate namna Roho wa Bwana anavyo kuongoza, ili utambue mahali utakapo simama ili kuwaonyesha wengine ile karama Mungu amekukarimia, ili kwakazi zako wapendwa wa Mungu wakutunze kwa matoleo yao.

Hivyo nakusihi kutokumuone wivu mtumishi wa Mungu yoyote yule kwa sadaka anayo pewa, kwani hakuna anaye toka sadaka ya bure, kila anaye toa sadaka anajua kwanini ametoa, hasa wanao toa sadaka kubwa wanajua uzito wa sadaka zao.

Badala ya kumuonea wivu ama chuki, nivyema ukasoma elimu ya Roho pengibe ukatambua kuwa hakuna ujira wabure, na k**a ukitambua wala hakuna siku utatamani sadaka kubwa kushindwa nguvu ya kharama uliyo karimiwa.

Barikiwa sana kwa kusoma nakuelewa mafundisho ya wa kiroho

14/07/2026

Upendo wa Mungu ni kiini cha upendo kwa wanadamu. Kabla sijajua maana ya kuwa rafiki wa Mungu, nilichukulia uwepo wa Mungu k**a tegemeo la wanadamu la kawaida na lisilokuwa na ulazima, kwani maisha yalionekana kuwepo k**a yalivyo na hakuna mwenye kuyafanya kuwa mazuri ama mabaya. Ilionekana ni hali yakawaida iliyopo ulimwenguni. Hivi ndivyo nilivyo amani.

Siku moja katika maisha nikaona umuhimu wa kuwa karibu zaidi na Mungu, hapo ndipo nilipojuwa kumbe Mungu ni rafiki mzuri, wapekee na aliye tumaini la kweli.

Pengine na wewe unaishi wakati wangu ulio pita, acha kuchelewa, amua sasa, Mungu ni Uhai kamili. By mwalimu wa kiriho

14/07/2026

Sauti Ya Bwana

Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;

Mwanzo
Mlango 12
Mstari 1

10/07/2026

Ni wangapi wanashangaa hali ya mwalimu wa Kitoho kutotoa masomo mara kwamara? Je umejua ni kwanini? Hii inatokana na madaraja tofauti ya wanao fwatilia masomo yetu, nakusababisha kuunda madarasa tofauti tofauti kutokana na madaraja ya mafundisho kwa wapokeaji. Chagua kuwa mmoja wa wafwatiliaji wa masomo yetu nawe hautajutia kujiunga Elimu bora ya roho, elimu itakayo kufaa maishani 2026

02/07/2026

Shalom wana wa Mungu

11/06/2026

Wakati wa Bwana unaamua sawa kila wakati

10/06/2026

Mungu ni mwema kila wakati.

28/05/2026

Tito 1
9 Maana imempasa askofu awe mtu asiyesh*takiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa MUNGU; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu.
8 bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;

Bwana Yesu apewe sifa.
Neno la Mungu ni elimu kwa wenye kumuamini, Neno linaelekeza mambo ambayo mkuu wa dini anapaswa kusingatia, na kanisa liweze kufahamu sifa hizo ili kuweka kiasi kati ya mkuu wa dini k**a mwakilishi wa Mungu, na waumini ambao niwenye kumuamini Mungu.

Hayahitajiki mabishano yamtu na mtu, kufikiri wema wa mkuu wa dini kwa majina tambuka, katika wadhifa wanao usimamia na vile tunavyo weza kufikiri kwaile imani na kusema "kwani huyo askofu sio binadamu" hii nikukosa unyenyekevu, kwani kwa kumpuuza mtumishi wa Mungu katika nafasi yako ni kudumaza kazi ya Mungu.

Ni kweli watu wengi wanahitaji ushetani kushinda wanavyo weza kumhitaji Mungu katika maisha. Hii inawezekana kutoka katika imani ya wajinga, kwamba shetani anagawa mali ikiwa watamuasi Mungu na kumuamini yeye.

Basi kipimo cha laana ni matezo, mapito magumy na mahangaiko mengi, na mali ni sehemu ya mwili wa mwenye kuasi, hivyo wawezaje kujitukuza juu ya mwili wako mwenyewe hali ukiiangamiza roho yako?

03/05/2026

Pongezi kubwa kwa mashabiki wangu bora kwenye mfululizo🔥! Bernard Werner

Shukrani nyingi kwa Bernard Wernerkwa msaada wenu mkubwa! Hongera kwa kuwa mashabiki bora kwenye mfululizo 🔥!
03/05/2026

Shukrani nyingi kwa Bernard Werner

kwa msaada wenu mkubwa! Hongera kwa kuwa mashabiki bora kwenye mfululizo 🔥!

Address

Online Church
Dar Es Salaam
27220

Opening Hours

Wednesday 11:00 - 13:00
Friday 22:00 - 04:30
Saturday 16:00 - 18:30
Sunday 08:30 - 12:30

Telephone

+255755636363

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwalimu Wa Kiroho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mwalimu Wa Kiroho:

Shortcuts

Share