23/03/2026
Kitabu kipya: *MAFUNZO YA BIBLIA: INJILI YA YOHANA*
Jumapili tarehe 22/03/2026 katika ibada KKKT Kundichi Dar es Salaam tulizindua kitabu kipya: *_MAFUNZO YA BIBLIA: INJILI alivyoiandika YOHANA MTAKATIFU_* .
Kitabu kimeandikwa na Prof. David Ngassapa na kuchapwa na kusambazwa na Soma Biblia .
Ibada hiyo iliongozwa na Baba Mchungaji Jacob Mwangomola, Mkuu wa Jimbo la Kasakazini DMP, akisaidiwa na Mchungaji Kiongozi Janeth Mwambungu pamoja na Wainjilisti Stella na Monica.
*_Ofa maalumu: Katika mwezi huu wa Machi na mwezi Aprili, kuna punguzo la bei kwa 20% kwa kitabu hiki._*
Kitabu hiki ni mwongozo wa kipekee kwa kila msomaji wa Injili ya Yohana: Kuna
• Maelezo – hutoa ufafanuzi wa Neno
• Fundisho – hujumlisha ujumbe wa msingi
• Maswali – hukusaidia kujihakikishia uelewa
• Tafakuri – hufanya Neno libadilishe maisha yako.
Biblia ni hazina isiyoisha kwa imani na maisha yetu yote. Kitabu hiki kimeandaliwa kwa mtazamo huo, kikikusaidia kusoma Injili k**a alivyoiandika Yohana Mtakatifu, hatua kwa hatua.
Kinafaa kwa mtu binafsi na zaidi kusoma katika kikundi. Karibu ujiunge na ushirika wa kujifunza Biblia.
Pata nakala yako dukani Soma Biblia. Tunapatikana Soma Biblia: Dar es Salaam, Iringa, Makambako, Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza
+255 754 292 995
www.somabiblia.or.tz