20/01/2025
MWAKA 2025 NI MSIMU MPYA.
Mwanzo 8:11
[11]njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
Mwanzoni mwa mwaka huu niliwashirikisha ujumbe wa mwaka huu kutoka mwanzo 8:13 Ambapo tunaona Nuhu anatoka ndani ya safina baada ya mwaka mzima kupita.
Kuna mambo kadhaa nataka uyafahamu kwa uhakika kuhusu msimu mpya, na tutajifunza mambo hayo kwa kujibu maswali haya mawili;
1. Kwanini Nuhu, alimtoa njiwa kwenye dirisha ilhali yeye mwenyewe alikuwa nauwezo wa kuona nje ya safina kwa kutumia dirisha hilohilo?
Njiwa katika agano jipya ametumika k**a ishara ya Roho mtakatifu, pia katika mazingira ya Nuhu, ni wazi kuwa njiwa aliweza kuona umbali mrefu na eneo kubwa kuliko ambavyo Nuhu angeona.
Jambo la kujifunza hapa ni hili; Mwanzo wa msimu mpya unahitaji zaidi msaada wa Roho mtakatifu kuona zaidi ya pale uwezo wako unaishia. inawezekana Nuhu alikuwa anaona aridhi imekwisha kauka, lkn ili kujiridhisha akaamua kumtumia njiwa. Macho yetu ya kimwili na uwezo wetu wa kiakili unamipaka katika ulimwengu huu uliofungwa kwenye muda, lkn Tunaingia Rohoni na kuamua kushirikiana na Mungu na kumsikia yeye anachotuambia, tunafunguliwa kwenye mipaka ya kiulimwengu na hiyo inatusaidia kuepuka hasara.
Kwakuwa ni msimu mpya kwako, unapaswa kutazama kila fursa inayoonekana mbele yako kwa sura ya Mungu, weka matamanio yako pembeni na lenga zaidi kutafuta shauri la Bwana kwenye jambo husika. Unaweza kuelewa mtu kukaa ndani ya safina mwaka mzima! alikuwa na shauku kubwa sana ya kutoka nje, lkn alijidhibiti na kutafuta uhakika wa usalama wake akiwa huko nje anakotaka kwenda.
Unaweza kuwa ni msimu mpya kwako kwenye mahusiano, kwenye biashara, kwenye kazi yako, kwenye elimu yako, lkn ili ufanikiwe katika kiwango bora, unapaswa kushik**ana na mashauri ya Mungu.
2. Kwanini njiwa alikuja na jani la mzeituni?
Biblia inataja aina ya jani ambalo njiwa alirudi nalo sio kwa bahati mbaya, ukumbuke kuwa njiwa ni ishara ya Roho mtakatifu katika agano jipya.
Vile vile mti wa mzeituni, unamaana kubwa ya kinabii ndani ya biblia.
Kumbukumbu la Torati 28:40
[40]Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.
Hapa Biblia inatuambia k**a mzeituni ukipukutisha majani yake maana yake mafuta hayatakuwepo, na kitu kinachoweza kupelekea mizeituni ya nchi kupukutisha majani yake ni k**a Mungu hajairidhia nchi kwa sababu ya kutotii kwao. Hivyo, Njiwa alipokuja na jani la mzeituni ishara ya kwanza ilikuwa ni Mungu kuiridhia au kuikubali nchi. Hili ni jambo muhimu sana kujua mwanzo wa msimu mpya ni kitu gani unapaswa kufanya ambacho Mungu anakiridhia.
Vile vile Ubichi wa jani la mzeituni ni ishara kwamba kuna uwezesho wa kiMungu juu yako unapoanza msimu mpya, kumbuka hatuna mafuta ya mzeituni k**a zeituni itapukutisha majani yake, mafuta ya zeituni ni ishara ya uwezesho wa kiMungu (Upako).
Majani ya zeituni ni dawa, hii inatuashiria kuwa Mungu atakupa neno la uponyaji ili uponywe kutoka kwenye madhara yaliyoletwa na gharika kwa msimu uliopita.
Nuhu na familia yake walisaziwa maisha tuu, lkn walipoteza vitu vingi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Haijalishi umepoteza nini, lkn tarajia neno la uponyaji kwa Bwana ndani ya msimu huu mpya.
Neno la Mungu analolituma kwako linakuja kukupa wazo la kufanya, kukupa uhakika wa mapenzi ya Mungu, kukupa upako utakao amsha Ari ya kulitekeleza ndani yako na zaidi sana litakuponya kutoka kwenye madhara uliyoyapata ya mwaka uliopita. Umebarikwa.
-2025
+255746283923