23/12/2025
Kuoa ama kuolewa ni jambo zuri tena jema na kila mmoja anatamani kuona ama kuolewa k**a hana tatizo lolote.Na wazazi nao wanapenda na kufurahia mtoto wao akioa ama akiolewa na hilo jambo la kuona ama kuolewa huwa ni la heshima kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
Lakini Leo mi nakuletea ujumbe wa muhimu na tena wa kutafakarisha.Mara nyingi watu wanapokutana na kupendana na kuamua kuoana taarifa hufika kwa wazazi,na viongozi wa kiroho ambao wao nao wanahusika kufungisha ndoa na pia wakati mwingine serikalini.Sasa hoja yangu ni hii mara nyingi wanaambiwa wakapime afya ili mambo mengine yaendelee cha ajabu ni kwamba wanapia tu HIV. Sasa hoja ni ni vyema Hawa watu wakikutana wanapoenda kupimwa HIV wapimwe pia akili na wanaohusika wanatakiwa kutambua kuwa kwa kadri wanavyoenda kushangilia wakati wa kufunga ndoa ndivyo pia inalazimu wazazi,ndugu na jamaa kushughulikia changamoto zao pale wanapochokana na kutaka kupeana talaka. Vikao vianze k**a ilivyokuwa vikao vya harusi,vikao vya kuanza hatua za kwenda kudai talaka vianze na siku ikitolewa hiyo talaka bado tufanye k**a tulivyofanya siku ya harusi.Japo sio furisho kwa Imani ya Kikristo kuachana,Yesu alisema haikuwa hivyo toka mwanzo.
Marko 10:4-8
Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Ndiyo maana hoja yangu wanapotaka kuoana wapimwa kila kitu mpaka akili.
Ni namna nilikuwa nawaza juu ya namna watu wanapokutana na kupendana na kuoana kwa shangwe na nderemo lakini baada ya muda hao wapendanao wanaanza kuchokana.