AYUBU 22:21

AYUBU 22:21 Karibu kwenye Neno Hai – Sehemu ya kusikia Neno safi la Mungu, lenye kuponya, kufundisha na kuimarisha maisha ya kiroho.

Tunatangaza ukweli wa Kristo kila siku!"*

26/04/2026

Isaya 43:4
‎Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.

‎Kuna ujumbe mzito sana juu ya andiko hili,.

‎Mungu anatuthibitishia kuwa anaweza kutumia watu kumbariki mtu. ukweli ni kwamba Kuna aina ya baraka, msaada au hitaji ulilo nalo Mungu hatashuka mwenyewe kuja kukusaidia Bali atakutumia watu sawa sawa na ahadi yake Katika Isaya 43:4.

‎Tatizo la kazi ulilonalo, Mungu anaweza kutumia mtu akakupa hitaji la kazi.

‎Shida ya pesa uliyonayo Mungu anaweza kutumia mtu kukamilisha hitaji lako.

‎Hali uliyonayo, dhiki, shida magonjwa na mahangaiko yako Mungu anaweza kutumia mtu kukusaidia kuubeba msalaba wako, Je unakumbuka juu ya habari ya Simon wa krene aliyemsaidia Yesu kuubeba msalaba? kwenye maombi yako mwambie Mungu akupe Simon wa krene wa kwako😥.

‎Sikiliza siyo biashara yako inayokupa utajiri Bali ni watu/wateja walio kwenye biashara yako.

‎Elimu uliyonayo si chochote k**a kusipokuwa na watu ambao watakufanya wewe uitwe mtumishi wao.

‎Huwezi kuwa mfalme k**a hakuna watu wakukufanya wewe uwe mfalme (ufalme ni watu ndiyo maana vita kubwa Katika ulimwengu wa Roho ni vita ya ufalme).

‎Je, umewahi kusoma habari za Yusufu akiwa gerezani? jambo la kwanza alianza kutengeneza watu, kutengeneza connection ya watu kumtoa pale akiwepo Mkuu wa wawanyeshaji na waokaji. Mungu atatumia watu kukutoa kwenye gereza lako.

‎unapoingia kwenye maombi yako kumbuka kumuomba Mungu akupe watu kwenye maisha yako k**a Isaya 43:4 alivyo ahidi.

‎Somo lijalo nitazungumza juu ya aina Saba za watu ambao unapaswa kumuomba Mungu akupe kwenye maisha yako.

‎Follow usipitwe na somo hili. link https://www.facebook.com/share/18DQcJ3TQ5/

24/04/2026

MATENDO YA MITUME 16:25-40, TAFAKARI NA

‎Kuna wakati maisha yanatufikisha mahali ambapo tunahisi tumefungwa kabisa hakuna njia ya kutoka, hakuna tumaini, hakuna msaada. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Paulo na Sila walipokuwa gerezani. Walifungwa minyororo, wakapigwa viboko, na kuwekwa sehemu ya ndani kabisa ya gereza. Kwa macho ya kibinadamu, kila kitu kilionekana kimekwisha.

‎Lakini usiku ule wa manane, badala ya kulalamika, waliinua sauti zao wakamwimbia Mungu na kumwomba. Walichagua kuabudu katikati ya maumivu. Walichagua kumtumaini Mungu hata pale ambapo haikuwa rahisi.

‎Ghafla, kulitokea tetemeko kubwa la ardhi, milango ya gereza ikafunguka, na minyororo yao ikaanguka! Mungu aligeuza hali yao kwa namna ambayo hakuna mwanadamu angeweza kufanya. Si wao tu waliopata uhuru, bali hata mkuu wa gereza alipokea wokovu pamoja na familia yake.

‎Mpendwa Katika Kristo Yesu naomba nizungumze na wewe Leo! wakati unaopitia Sasa haimaanishi ndiyo mwisho wako. Giza unaloliona Sasa mbele ya maisha yako tambua Kuna mwanga wa kweli ambaye ni Yesu Kristo atakuangazia nuru yake. utashinda, nakuombea Kwa Jina la Yesu Kristo 🙏

‎USIKU WAKO UNAWEZA KUWA NDIO MWANZO WA MUUJIZA WAKO. USIKATE TAMAA KWA SABABU YA HALI UNAYOPITIA. MUNGU BADO ANAFANYA KAZI, HATA PALE AMBAPO HUONI DALILI ZAKE.

‎WALE MNAOPITIA KIPINDI KIGUMU NAOMBA TUOMBE PAMOJA 🙏

‎Ee Baba wa mbinguni, tunakuja mbele zako kwa unyenyekevu, tukikushukuru kwa kuwa wewe ni Mungu wa nyakati zote katika furaha na hata katika majaribu.

‎Bwana, tunawaombea wote wanaopitia kipindi kigumu k**a Paulo na Sila. Wengine wamefungwa na changamoto za maisha k**a kiuchumi, kiafya, kifamilia, au kiroho. Wapo wanaolia kimya kimya, wapo waliokata tamaa, na wengine hawaoni tena njia ya kutoka.

‎Ee Mungu mwenye nguvu, ingia katikati ya hali zao sasa. K**a ulivyotikisa gereza la Paulo na Sila, tikisa kila kifungo kinachowazuia watu wako. Fungua milango iliyofungwa, vunja minyororo ya hofu, mashaka, na kukata tamaa.

‎Bwana Yesu, wape nguvu ya kukuabudu hata wakiwa kwenye “usiku wa manane” wa maisha yao. Wajaze amani isiyoelezeka, na tumaini jipya litokalo kwako. Badilisha huzuni zao kuwa furaha, na machozi yao yawe ushuhuda wa ushindi.

‎Roho Mtakatifu, wasimame pamoja nao, uwatie nguvu pale walipo dhaifu, uwakumbushe kuwa hawako peke yao. Na kupitia hali wanazopitia, jina lako litukuzwe.

‎Tunaamini, Ee Bwana, kuwa kila anayesoma maombi haya atapata mguso wako, na ushuhuda utafuata.

‎Katika jina la Yesu Kristo, tumeomba na kuamini,
‎Amina. 🙏

‎👉 Leo, uko kwenye “gereza” gani la maisha yako?
‎👉 Ni jambo gani unahitaji Mungu akufungulie milango?

Andika “Amina” k**a unaamini Mungu anakutendea muujiza wako, au taja hitaji lako tuombe pamoja.


19/04/2026

Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako."
‎Yoshua 1:9

Mpendwa,
‎Wakati mwingine maisha yanakuja na upepo mkali wa kushindwa, hofu, shinikizo, au hata hali ambapo unahisi umeachwa peke yako. Moyo unapungukiwa, akili inachanganyikiwa, na sauti ndani yako inaanza kusema “huwezi, umechelewa, huwezi kufanikiwa.”
‎Lakini leo Mungu anakukumbusha kile alichomwambia Yoshua:
‎"Si mimi niliyekuamuru?"
‎Huyo Mungu ambaye alimwamuru Yoshua kuingia katika ahadi ambayo ilikuwa na vita na changamoto kubwa, ndiye huyohuyo anayekuamuru wewe leo: Uwe hodari. Uwe na moyo wa ushujaa. Usiogope. Usifadhaike.
‎Si kwa sababu wewe una nguvu zako mwenyewe.
‎Bali kwa sababu Yeye yu pamoja nawe kila uendako katika biashara yako, katika ndoa yako, katika masomo yako, katika afya yako, katika machozi yako, na hata katika mahali ambapo unahisi umepotea kabisa.
‎Mungu hakukupigia kelele tu.
‎Alikupa ahadi: Mimi nipo pamoja nawe.
‎Kwa hivyo simama kidete leo.
‎Chukua hatua hiyo unayoogopa.
‎Sema neno hilo unalohofia.
‎Anza tena hata k**a ulianguka mara nyingi.
‎Wewe si peke yako. Mungu yuko pamoja nawe.
‎Unapomwamini Yeye, hofu inabadilika kuwa imani, na udhaifu wako unageuka kuwa nguvu yake.
‎Mungu akubariki na akupatie moyo mpya wa ushujaa leo. 🙏

31/01/2026

Mke wa Potifa akamtamani Yusufu na kumwambia:
“Lala nami.”

Yusufu alikataa kwa hekima akasema:

“Nifanyaje uovu huu mkubwa nimkosee Mungu?”

Siku moja mwanamke huyo akamshika vazi.
Yusufu akakimbia akaacha vazi mikononi mwake.
Uaminifu wake ukamgharimu.

Ukweli ukageuzwa uongo.
Yusufu akatuhumiwa kwa kosa ambalo hajafanya.

Hapo ndipo Yusufu akaingia gerezani, si kwa dhambi, bali kwa utii Kwa Mungu wake.

Lakini hata gerezani,
Biblia inasema: “Bwana alikuwa pamoja na Yusufu.”

Gereza halikumfanya Yusufu apoteze maono.
Hapo ndipo Mungu akaanza kuandaa ngazi ya ikulu.

Akatumika gerezani.
Akatumika kwa tafsiri za ndoto.
Akasahaulika kwa muda wa miaka miwili gerezani ila hakukata tamaa.

Mpaka siku moja,
Mfalme Farao akaota ndoto.
Hakuna aliyeweza kuitafsiri.
Ndipo jina la Yusufu likatajwa.
Kutoka gerezani hadi mbele ya mfalme.
Kutoka mavazi ya wafungwa hadi mavazi ya heshima.
Kutoka minyororo hadi pete ya mamlaka.
Farao akasema:

“Je, tupate wapi mtu k**a huyu aliye na Roho wa Mungu?”
(Mwanzo 41:38)

Na siku hiyo hiyo,
Yusufu akafanywa mtawala wa pili baada ya Farao.

MPENDWA WA
Usifikiri uaminifu wako unapotea.
Huenda unaumia kwa sababu ulichagua haki badala ya raha.
Lakini Mungu huandika historia kwa wale wanaomcha.

Kukataa dhambi leo, kunaweza kukupeleka gerezani, lakini kesho kutakupeleka ikulu.

Je, umechoka na Hali unayopitia Sasa kwenye uchumi, ndoa, kazi, masomo, Afya na mengine?

Usikate tamaa, Mungu aliyetenda Kwa Yusuph yupo atatenda na kwako pia.

✍️ Andika kwenye comment: “Wakati wangu wa Mungu unakuja” k**a tamko la imani.

04/01/2026

OMBA MAOMBI HAYA UNAPOKUTANA NA VITA ZA KIROHO

Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja kila kitu ambacho kinazuia kutimizwa kwa mipango yako kamili katika maisha yangu.

Ninaamuru na kutangaza kwamba kila mnyororo, kamba, gereza, pingu kwamba zimefunguliwa, zimekatwa, na kuondolewa kutoka kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.

Baba, Bwana Nakushukuru, kwamba wewe pekee ndiye hakimu wa maisha yetu, kwa mujibu wa Yeremia 17:9-10 "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.

Baba naomba katika jina la Yesu, kwa mujibu wa Zaburi 22:19 Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Baba naomba kwamba utusaidie, na kutupa uvumilivu wa kusubiri mapenzi yako kutimizwa.

Baba katika jina la Yesu, neno lako linasema katika Isaya 41:10-12 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa k**a kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.

Baba, ninakubaliana na neno lako lenye nguvu, uweza, uhakika, na la kujiamini, kwamba utawalinda watu wako dhidi ya maadui. Umetuambia kwamba kisasi ni chako asema Bwana, na utawalipa waovu.

Bwana Ninakushukuru, kwa ajili ya ulinzi wako, na neno lako la nguvu na la ukombozi. Katika jina la Yesu.
Baba tunakushukuru kwa neno lako linalosema katika Ayubu 5:12 Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.

Baba wa Mbinguni, ninachukua mamlaka ya neno lako kufunga, kufuta na kung’oa mipango yote miovu ya adui, nakuifanya kuwa utupu, batili, na kuifuta kwa jina la Yesu kristo.

Baba neno lako linasema nami katika Luka 10:19 kwamba “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Bwana natumia uwezo wako na mamlaka yako, ili kuvunja, kubamiza, kuponda, kung’oa, kutawanya vipande vipande, kila mipango ambayo shetani ameandaa dhidi ya maisha yangu, familia yangu, huduma yangu, nyumba yangu, uhusiano, fedha, na vitu vyote vilivyo vyangu. Nakushukuru Bwana, na ninadai ushindi kamili katika jina la Yesu kristo.

Baba nasimama sawa sawa na neno lako katika Ayubu 6: 8 linalosema “Laiti ningepewa haja yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!” Bwana Naomba katika jina la Yesu kwamba ombi letu utalijibu kulingana na mapenzi yako na kwa wakati, na utatupa vitu vilivyomo katika mapenzi yako kwa ajili yetu.

Baba katika jina la Yesu Kristo kulingana na Wafilipi 4:6 unatuambia “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Bwana nakushukuru, kwamba tunaweza kuja kwako wakati wowote kwa maombi ili haja zetu zijulikane kwako.

Baba k**a ulivyosema katika Zaburi 23:1 Wewe ni mchungaji wangu, sitapungukiwa au kukosa vitu vyovyote vizuri katika maisha yangu. Wewe ni Mungu ambaye unatupatia mahitaji yetu yote. Nakiri k**a ulivyosema, kwamba huwezi kuzuia mambo yoyote mazuri kwa watoto wako. Baba nadai faida zako zote za kiroho, na za kimwili. Katika Jina la Yesu Kristo.

Baba umetuambia katika neno lako, katika Luka 17:6 kwamba “Bwana akasema, K**a mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” Baba nachukua mamlaka ya neno lako leo, na kung’oa madeni yote ya kifedha, kila mapambano, kila misiba, kila ukosefu, uhitaji, na roho zote zinazoshambulia fedha zetu, afya, ndoa, nyumba, watoto, huduma, kazi zetu, na yote yaliyo yetu. Nazifunga, nakuzing’oa toka kwenye maisha yetu, na kuzitupa katika bahari. Katika jina la Yesu Kristo.

Baba umeniambia katika 2 Tim. 4:18 kwamba “Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.” Baba nakushukuru kwa kuwa umeniokoa na kila matendo maovu ya adui, na kunihifadhi kwa ajili ya ufalme wako wa mbinguni.

Baba ninasimama sawa sawa na neno lako na kuyafunga kila matendo maovu, yaliyofanywa maishani kwangu, watoto wangu, familia yangu, nyumbani kwangu, huduma yangu, afya yangu, fedha zangu, mustakabali wangu na vitu vyote tunavyomiliki. Ninayafunga toka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini, mbingu ya pili, katika maji, kwenye moto, katika hewa, katika ardhi, katika maeneo, katika mazingira, na kila maeneo chini ya jua, mwezi, nyota, na sehemu nyingine zote za siri yanakojificha. Ninaachilia neno lako, damu ya Yesu Kristo, na jina lako dhidi yao, katika maeneo hayo yote, kwamba yatakuwa yamefungwa milele na milele amina.

Baba natumia funguo muhimu katika Mathayo 18:18 kwamba “na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Ninajifungua, pamoja na kila kitu changu, toka kila mnyororo, vifungo, pingu, na kamba katika jina la Yesu Kristo.

Baba k**a ulivyosema katika kitabu cha Hesabu 11:1. Nasimama kwenye mamlaka ya neno lako, na amrisha moto ushuke kutoka mbinguni na kuharibu kila roho ya kurudi nyuma ambayo imewekwa na adui katika maisha yetu. Katika jina la Yesu Kristo.

Baba, Bwana nasimama sawasawa na neno lako katika Joshua 1:8. Naomba maneno yako yasindoke vinywani mwetu wala mioyoni mwetu, bali tuyatafakari mchana na usiku, ndipo tutakapoifanikisha njia yetu.

Bwana ninaomba mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, niyatafakari hayo sawasawa na neno lako, katika Wafilipi 4: 8.

Baba umeniambia katika 2 Timotheo 1:7 kwamba Mungu hakunipa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Baba napinga roho ya woga, nakataa kuwa na wasiwasi, au kukatishwa tamaa. Nautumia nguvu yako na mamlaka juu ya kila mipango na miradi ya adui. Nadai ushindi kamili juu ya nguvu zote za giza, katika jina la Yesu Kristo.

Baba neno lako linasema katika Yer 23:29 " Je! Neno langu si k**a moto? Asema Bwana; na k**a nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? Baba katika jina la Yesu, natumia moto wa Mungu kuteketeza kila uovu dhidi yangu, na wapendwa wangu, toka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. Natumia nyundo ya neno la Mungu kuvunja kila uovu wa vifungo vya nafsi, uhusiano wa damu, uchawi na laana zote mababu, uliopitia kwa uzao wetu. Najifunika, pamoja na kizazi cha pili, cha tatu na cha nne, kwa damu ya Yesu Kristo.

Naachilia baraka za Bwana juu yetu, baraka za kizazi hadi kizazi, baraka za Ibrahimu, na baraka zote. Katika jina la Yesu Kristo.

Baba katika jina la Yesu. Navaa silaha zote za Mungu, napokea chapeo ya wokovu, navaa dirii ya haki kifuani, natwaa ngao ya imani, najifunga kweli kiunoni, nafungiwa miguu yangu utayari niupatao kwa injili ya amani na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu kwa sala zote na maombi nikisali kila wakati katika Roho kwa mujibu wa Efeso 6: 10-18

Baba kwa mujibu wa neno lako katika Yer 30:17 Ulisema “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.” Nakushukuru kwa kutuponya machungu yetu, majeraha, makovu, na maumivu. Nakushukuru kwa ajili ya kuturejesha tena. Katika Jina la Yesu Kristo.

Baba katika Isa 53: 4-5, Ulisema “Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona." Bwana nakushukuru kwa neno lako, lina nguvu, linatupatia nguvu, ujasiri, ulinzi, na uponyaji katika jina la Yesu Kristo.

Baba nakushukuru, k**a ulivyosema katika Zaburi 46:1 kwamba wewe ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Nakushukuru kwa kuwa tunaweza kukuita wakati wa shida.
Baba nasimama sawa sawa na neno lako katika Marko 3:27. Namfunga huyo mtu mwenye nguvu, nakuvunja kila vizuizi, kamba, vifungo, pingu, minyororo, minyororo ya utumwa, kutoka katika maisha yangu, wapendwa wangu, na yote yaliyo yangu. Ninaamrisha mali za mwenye nguvu kuharibiwa, sasa na hata milele. Katika jina la Yesu Kristo.

Baba nakushukuru kwa ulinzi wako, ulisema katika neno lako katika Kutoka 23:27 " Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao na kukimbia. Namshukuru wewe Bwana, kwa nguvu iliyopo katika neno lako ambayo husababisha maadui kuonyesha maungo yao na kukimbia. Katika jina la Yesu Kristo.

Baba katika jina la Yesu ninafungua machafuko na upofu wa mungu wa dunia hii, kutoka kwenye akili zetu, ambazo zinatuzuia kuona mwanga wa injili ya Kristo. Ninaita kila neno la Mungu linaloingia kwenye akili zetu, na moyo liinuke kwa nguvu ndani yetu.

Baba wa Mbinguni, asante ninakushukuru wewe, ninakutukuza wewe, ninakuabudu wewe, nakushukuru kwa neno lako katika Kumbukumbu 28:7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Asante kwa nguvu yako, ulinzi, na usalama ambao umetoa kwa watoto wako, tukitumia neno, maadui si tu watakimbia, bali watakimbia kwa njia saba kutoka kwetu, katika jina la Yesu Kristo.

Baba nakushukuru, kwa mikono yako imara, na mkono wako wa haki wa kulia. Umetuambia, katika 1 Petro 5: 7 Tumtwike yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. Bwana nakushukuru kwa kujishughulisha na mambo yetu, nakushukuru kwa kuwa tayari kwa ajili yetu wakati tunakuhitaji.
Baba katika jina la Yesu ninaliadhimisha jina lako; nakupa heshima na utukufu wote unaotoka kwenye jina lako takatifu. Neno lako linaniambia katika Joshua 1:5 “Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; k**a nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia kamwe wala sitakuacha.” Asante Bwana kwa ulinzi wako, na baraka.

Baba nakushukuru kwa neno lako katika 3 Yohana 1:2 linasema kwamba mipango yako kwa ajili yetu ni ya kutufanikisha, na kuwa na afya njema k**a vile roho zetu zifanikiwavyo. Natumia mamlaka ya neno lako, na kudai ustawi, afya, furaha, mafanikio, amani ya akili, baraka, na kila mambo mema ambayo umepanga tupate, juu ya maisha yangu, wapendwa wangu, mali na vitu vyote nilivyonavyo, katika jina la Yesu Kristo.

Baba wa mbinguni neno lako katika Luke 8:11 linatuambia kwamba neno lako ni mbegu, na mioyo yetu ni ardhi.

Bwana ninakuomba utayarishe mioyo yetu kupokea neno lako na kulificha katika mioyo yetu, tusitende dhambi dhidi yako, kwa jina la Yesu Kristo.

🙏🙏🙏🙏🙏

18/12/2025

Hagai 1:8
Neno la Bwana linasema:
“Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.”

Watu wa Mungu walikuwa wamesahau nyumba ya Bwana, kila mmoja akijishughulisha na mambo yake binafsi. Ndipo Mungu akaita watu wake wachukue hatua. Hakusema angalia, hakusema fikiria alisema pandeni, mkalete, mjenge.

Hili neno lina ujumbe mkubwa kwetu leo, hasa katika huduma za kiroho k**a ukurasa wa Neno Hai.

1. PANDENI MILIMANI – CHUKUA HATUA

Kupanda milimani ni ishara ya jitihada na kujitoa. Kazi ya Mungu haisongi kwa kutazama pembeni.

KUSUPPORT UKURASA WA NENO HAI NI KUPANDA MLIMA:

Kufuatilia (follow)

Kushare neno

Kutoa maoni (comment) ya kuhamasisha

Kuomba kwa ajili ya huduma

Hakuna mlima usiopandika kwa mwenye moyo wa kumtumikia Mungu.

2. Mkalete miti – Toa ulicho nacho

Mungu hakutaka watu walete dhahabu, aliwaambia walete miti kitu walichoweza kupata.

WEWE UNA KITU CHA KULETA:

Muda wako

Ushuhuda wako

Like moja

Share moja

Invite rafiki mmoja

Usiseme sina, Mungu hutumia kilicho kidogo kutengeneza jambo kubwa.

3. MKAIJENGE NYUMBA – SHIRIKI KATIKA UJENZI

Nyumba ya Bwana inajengwa kwa ushirika. Hakuna mtu mmoja anayejenga peke yake.

UKURASA WA NENO HAI NI JUKWAA LA KUJENGA ROHO, KUPONYA MIOYO, NA KUOKOA WALIOPOTEA.
UNAPOUNGA MKONO UKURASA HUU, UNAJENGA MAISHA YA WATU USIOWAJUA, LAKINI MUNGU ANAWAONA.

4. NAMI NITAIFURAHIA, NAMI NITATUKUZWA – Ahadi Ya Mungu

Mungu mwenyewe anaahidi:

Atapendezwa na kazi hiyo

Jina lake litatukuzwa

Kila support yako kwa Neno Hai si bure. Mungu anaifurahia na anaandikisha mbinguni.

Follow ukurasa wa Neno Hai🙏
Shiriki ujumbe huu kwa wengine🙏
Kuwa sehemu ya ujenzi wa ufalme wa Mungu🙏

UKIJENGA NYUMBA YA BWANA, BWANA ATAJENGA MAISHA YAKO.
ASEMA BWANA.

18/12/2025

SOMA HADI MWISHO UJUMBE HUU NAKUSIHI MPENDWA 🙏

Kulikuwa na mtu mmoja katika Biblia aliyeitwa Ayubu.
Alikuwa tajiri, mwenye familia yenye upendo, na aliishi kwa kumcha Mungu.
Lakini siku moja, kila kitu kilibadilika.

Alipoteza mali zake zote.
Akapoteza watoto wake.
Mwili wake ukaanza kujaa vidonda.
Marafiki wakamlaumu, wakamwambia: “Lazima kuna dhambi umefanya.”

Lakini katikati ya maumivu yote, Ayubu hakumkataa Mungu.
Badala yake alisema:

“Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe.”
(Ayubu 1:21)

Mwishowe, Mungu alimrejeshea Yobu mara mbili ya yote aliyopoteza.

Usimlaumu Mungu kwa kile ulichopoteza.
Usikate tamaa kwa sababu ya mateso ya sasa.
Mungu anayekupa leo, ndiye anayekujaribu kesho, na ndiye atakayekuinua kesho kutwa.

👉 MAUMIVU SIYO MWISHO WA SAFARI.
👉 SUBIRA NI DARAJA LA BARAKA.
👉 MUNGU HAJAKUSAHAU JINA LAKO.

UKIPITIA MAJARIBU, JUA BADO MUNGU YUKO KAZINI.

Je, wewe leo unapitia jaribu gani linalokufanya uone k**a Mungu amekaa kimya?
✍️ Andika kwenye comment: “Bado namwamini Mungu” k**a ishara ya imani yako.

🙏 Tuombeane, maana ushuhuda wako unaweza kuwa nguvu kwa mtu mwingine.

• •
Uwe baraka kwa mwingine 💙

19/11/2025

TUREJEE MBELE ZA MUNGU KWA TOBA🙏

Bwana Mungu wangu,
Nanyenyekea mbele zako usiku huu.
K**a kuna neno, wazo, au tendo lolote lililokuhuzunisha,
Uniongoe, unisamehe, na unitakase kwa damu ya Yesu Kristo.

Nirejeshee moyo msafi na roho iliyo thabiti mbele zako.

1 YOHANA 1:9
“Tukiungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atusamehe dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”

BWANA, NIPE NEEMA YA KUKAA KATIKA NJIA ZAKO.

AMINA.

08/10/2025

Ile Nguvu Iliyomfufua Yesu Toka Katika Mauti, Ikafufue Kila Mipango Yako Iliyokufa Kwa Jina La Yesu Kristo Aliye Hai 🙏

02/10/2025

KWA UNYENYEKEVU MKUBWA TUPIGE GOTI MBELE ZA MUNGU TUOMBE 🙏

Baba wa rehema, tunakuja mbele zako leo tukiyakabidhi maisha ya ndugu zetu wote wanaopitia changamoto mbalimbali.

WENYE MAGONJWA 🙏
Uwape Uponyaji Na Nguvu Mpya.

WALIOKATA TAMAA 🙏
Uwatie Moyo Na Matumaini Mapya.

WALIOPUNGUKIWA NA MAHITAJI 🙏
Uwafungulie Milango Ya Riziki.

WALIO NA HUZUNI 🙏
Uwafariji Na Kuwapa Amani Ya Moyo.

WALIOFUNGWA NA MATATIZO 🙏
uwaachilie na kuwapa ushindi.

Ee Mungu wa huruma, tunawaweka mikononi mwako wote wenye shida. Tunaamini kuwa mkono wako si mfupi kushindwa kuokoa, wala sikio lako si zito kushindwa kusikia kilio cha watu wako.

Tunaomba kwa jina la Yesu Kristo. Amina.

13/09/2025

BWANA, NAKUOMBA🙏

1. Niongoze Katika Maamuzi Yangu Yote Leo.
2. Nijalie Neema Ya Kufanikisha Kazi Zangu na Mipango Yangu.

3. Nilinde Dhidi Ya Hila Za Adui Na Majaribu.

4. Nijalie Upendo, Uvumilivu, Na Amani Moyoni.

Tunaomba Haya Kwa Njia Ya Yesu Kristo Bwana Wetu, Amina. 🙏

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255743198476

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AYUBU 22:21 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to AYUBU 22:21:

Share