08/07/2024
Sala ya Peter; “Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu unapitia mateso, roho yangu ina faraja. Ningewezaje kutosifu hekima Yako na matendo Yako? Hata k**a nitafa baada ya kuja kukujua, daima nitakuwa tayari. Ee, Mwenyezi! Hakika si kwamba Wewe kweli hutaki kuniruhusu nikuone? Hakika si kwamba sistahili kweli kupokea hukumu Yako? Inaweza labda kuwa kwamba kuna kitu ndani yangu usichotaka kuona?”