Tag Amani

Tag Amani Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tag Amani, Religious organisation, Tabata Amani, Dar es Salaam.

13/12/2019

MWANGAZA WA SIKU
Friday 13th of December 2019

*JIANDAYE KWA MAVUNO*

MATHAYO 9:35-38
36.*Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika k**a kondoo wasio na mchungaji.*

37.*Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. *

Matthew 9:37-38 NIV
[37] Then he said to his disciples, “The harvest is plentiful but the workers are few. [38] Ask the Lord of the harvest, therefore, to send out workers into his harvest field.”

Nyuma ya kila mafanikio hutanguliwa na maandalizi na mipango mahususi kuhusiana na mafanikio hayo.

Katika tafakari yetu leo Yesu anatukumbusha na kutupa changaMoto kwa habari ya kumvunia Bwana mavuno ambayo yapo tayari lakini wavunaji au watendaji ni wachache.

Ili tuweze kufanikiwa kumvunia Bwana,tunajitaji kumuomba Mungu atupe moyo wa Yesu aliokuwa nao kwa mavuno(watu walioko dhambini na waliotayari kupokea injili na kugeuka).

🔹*Tunahitaji Kuona K**a Yesu alivyoona.*
-Wakati wanafunzi wake wanaliona kusanyiko tu la watu,lakini Yesu aliona HITAJI KUBWA ndani ya mioyo ya hao watu
•Walichoka nakutawanyika k**a kondoo wasio na Mchungaji)
•Aliona utayari wao wakutubu na kuziacha njia zao mbaya lakini hakuona au walikuwepo watumishi wa chache waliokuwa tayari Kuwasaidia na kuwaongoza katika nia yao hiyo.
-Mungu anatutaka sisi tuliokwisha kuokoka tuwe sababu ya wengine kumjua Kristo.

🔹*Tunahitaji kuguswa au kujisikia ndani mioyo yetu kuhusu wenye dhambi K**a Yesu alivyojisikia*
-Alipowaona makutano ALIWAHURUMIA
•Hatuwezi kuifanya kazi ya kumvunia Bwana Mavuno bila kusukumwa na UPENDO wa Mungu ndani yetu ambapo ndani yake kunakuwahurumia maana si wao Bali wamefungwa na shetani na kutumikishwa bila ridhaa yao.

🔹*Tunapaswa kuchukua hatua K**a Yesu alivyochukua hatua*
-Aliamua kuwahudumia kiroho na kimwili(uponyaji wa magonjwa yote na mafundisho pia)

Katika Utumishi huu wakumvunia Bwana mavuno yaliyotayari huwa hatujipeleki au kujituma wenyewe K**a sehemu pengine ya moja ya ajira k**a ajira zingine HAPANA,bali ni lazima Mungu ahusike kututuma ndio maana tunatakiwa KUMUOMBA MUNGU ili awapeleke wavunaji ili katika Utumishi huu wasiwepo watumishi WAMISHAHARA bali wenye kujitoa kwa moyo hata bila posho lakini Wawe tayari kulitimiza kusudi la Bwana katika Mwito wao.Maranatha

Karibisha na wengine...
12/12/2019

Karibisha na wengine...

MWANGAZA WA SIKU Tuesday 29th of October 2019*NGUVU YA UMOJA KATIKA KANISA*Waefeso 4:1-61. *Kwahiyo nawasihi,Mimi niliye...
29/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Tuesday 29th of October 2019

*NGUVU YA UMOJA KATIKA KANISA*

Waefeso 4:1-6
1. *Kwahiyo nawasihi,Mimi niliye mfungwa katika Bwana,mwenende k**a inavyoustahili Wito wenu mlioitiwa,2.kwa unyenyekevu wote na upole,kwa uvumilivu,mkichukuliana katika Upendo 3.na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha Amani.*

Ephesians 4:3 NIV
[3] Make every effort to keep the unity of the Spirit through the bond of peace.

Kuwa pamoja haimaanishi mpo kwa umoja,kwahiyo kuna uwezekano mkubwa Mkawa mahala pamoja lakini mkiwa mmetofautiana.

Mtume Paul Anaanza kujenga msingi katika kutuonyesha Umuhimu K**a kanisa Kuwa na umoja ni kutokana na kwamba Mungu ametuokoa na kumpatia kila mtu Wito au Karama ambazo Kila zinapotumika kwakusudi la kuufaa mwili wa Kristo na kumtukuza Mungu zitakuwa sababu ya umoja katika kanisa.

Palipo na umoja ndipo Mungu alipoamuru kuzikalisha baraka zake,ndio maana nimuhimu sana katika kanisa Kuwa na Umoja

Kuna mambo muhimu au sifa muhimu zinazopaswa kudhihirishwa na wakristo ili kuleta nakudumisha umoja katika kanisa:-
🔹 *Unyenyekevu* ,si kwasababu sisi ni hafifu kwa watu wengine Bali hatujihesabu kuwa bora kuliko wengine.
-Unyenyekevu ndo msingi wa Utumishi
heshima,staha na Upendo kwa wengine.

🔹 *Upole* na Uungwana,Unahusika nakuwafikiria wengine na si kutaka kuwakalia k**a watawala
-Hii inahusika na kuepuka tamaa yakujilipiza kisasi au kukimbia wakati watu wametuudhi.

🔹 *Wavumilivu*,uvumilivu wetu ndio unaotuwezesha Kustahimili tabia,mienendo na makosa ya wengine.

🔹 *Kutendeana Mema* Yaani kukutana na uhitaji wa mwingine,Haya yakifanyika katika kanisa, huhifandhi umoja Miongoni mwetu,Mungu atupe Neema katika hili.*(Wafil.2:3-8*)Maranatha!

MWANGAZA WA SIKU Monday 28th of October 2019*NGUVU YA UPENDO WA MUNGU KWETU*1Yohana 3:1-31.  *Tazameni, ni pendo la namn...
28/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Monday 28th of October 2019

*NGUVU YA UPENDO WA MUNGU KWETU*

1Yohana 3:1-3
1. *Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.......*

1 John 3:1 NIV
[1] See what great love the Father has lavished on us, that we should be called children of God! And that is what we are! The reason the world does not know us is that it did not know him.

Yohana ni mtu sahihi wakutufundisha kwa habari ya Upendo wa Mungu maana alikuwa mtu wakaribu sana wa Yesu(Akipendwa sana)

Kupendwa wakati wote huongeza hamasa na motisha(motivation )na kichocheo chanya kinachoweza Kusababisha Matokeo chanya pia katika maisha ya mtu.

Bilashaka linaweza likawa ndo lengo la tafakari yetu kwamba kupitia kujua nguvu na matekeo ya Upendo wa Mungu katika maisha yetu, *itatutia Moyo,hamasa na motisha utakao tusaidia kudumu katika imani na kuwa na ushindi endelevu.*

Katika mistari hii tunajifunza kwamba:-
♦Upendo wa Mungu *umekuwa ni sababu ya sisi kuokolewa toka dhambini na kufanywa watoto wa Mungu.*

🔹Kuwa mtoto wa Mungu *ndio msingi wa Imani tegemeo letu kwa Mungu*
🔹Kuwa mtoto wa Mungu ni *Heshima na Upendeleo wa Hali ya juu mbele za Mungu*(tunapaswa kutunza na kuudhamini) pamoja na Kukirimiwa Ahadi zote kubwa na za thanani.(2pet.1:4)

🔹Kule kuwa watoto wa Mungu *kumetutofautisha na Dunia*
🔹Kuwa mtoto wa Mungu kunatupa *tumaini la kuuridhi uzima wa milele * pamoja na utukufu utakao fanana na utukufu alionao Mungu Baba yetu na *hii inatujukumisha Kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wetu kwakujitenga mbali na dhambi.*(utakatifu)

♦Mwisho Upendo wa Mungu hutupa *wajibu endelevu wakumpenda Mungu(kumtii) na Kuwa na mahusiano Mema na watu wengine.* Waeff.5:1-2,Mungu atusaidie.Maranatha!

MWANGAZA WA SIKUSaturday 26th of October 2019*TOA SADAKA INAYO MGUSA MUNGU*LUKA 21:1-43.**Akasema, Hakika nawaambia, huy...
26/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Saturday 26th of October 2019

*TOA SADAKA INAYO MGUSA MUNGU*

LUKA 21:1-4
3.**Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote ** *4.Maana hao wote walitia sadaka katika mali iliyo wazidi bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.*

Luke 21:3-4 NIV
[3] “Truly I tell you,” he said, “this poor widow has put in more than all the others. [4] All these people gave their gifts out of their wealth; but she out of her poverty put in all she had to live on.”

Mara zote sadaka isiyo kuuma na Kukugusa wewe mtoaji,kamwe haiwezi kumgusa wala Kumpendeza Mungu unaye mtolea.

Utoaji wakati wote huonyesha na kuwakilisha vile tunavyoweza KUITIKIA Upendo mkuu wa Mungu aliouonyesha katika Maisha yetu.

Katika tafakari hii tunajifunza mambo kadhaa toka kwa mjane na Yesu:-

♦ *Bwana Yesu huangalia,hudadisi na kuchunguza Utoaji wetu*.(Mith.15:3)
-Huona na kumdadisi mtoaji
-Huona na kudadisi kiwango au kiasi kilichotolewa

♦ *Bwana Yesu hufanya TATHMINI ya utoaji wetu* (2Sam.24:24)
-Hutathmini thamani ya sadaka iliyotolewa
-Hutathimini NIA ya mtoaji

♦ *Utoaji unamhusu kila mtu*
-Uwe maskini au Tajiri
-Uwe mtumishi au Mwamini wakawaida.n.k

Kweli hizo zinatuelekeza kwamba ili tumtolee Mungu sadaka inayomgusa,lazima kila tunapotoa tutoe:-
•Kwa Moyo wakupenda
•Kwa uaminifu bila kujali mazingira
•Kwa imani
•Tutoe Kalingana na Baraka yetu, na hakika tutaziona Baraka za Bwana katika Maisha yetu.Maranatha!

MWANGAZA WA SIKU Friday 25th of October 2019 *HEKIMA YA KI-UNGU IWE ULINZI WAKO* DANIEL 2:2323 *_Nakushukuru, nakuhimidi...
25/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Friday 25th of October 2019

*HEKIMA YA KI-UNGU IWE ULINZI WAKO*

DANIEL 2:23
23 *_Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.Danieli Afasiri Ndoto*_

Daniel 2:23
[23 _]I thank You and praise You, O God of my fathers, Who has given me wisdom and might and has made known to me now what we desired of You, for You have made known to us the solution to the king's problem._

Haya ni maneno ya Shukrani toka kwa Daniel baada ya Mungu kumjalia Yeye na wenzake hekima iliyotafisiri ndoto ya mfalme.

Ukisoma hapo juu utagundua kwamba zoezi la kutafisiri ndoto ya mfalme ilikuwa mtego na jaribu toka kwa Shetani ili kukatisha uhai wa Daniel na wenzake *,lakini ashukuriwe Mungu kwa hekima yake na uweza wake uliosababisha wokovu na ulinzi kwa watu wake.*

*Katika Mhubiri 7:12* inasema _kwa maana hekima ni ULINZI,k**a vile fedha ilivyo ulinzi na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humuhifadhi yeye aliye nayo._ hiki ndicho kilichotokea kwa Daniel na wenzake.

Neno la Mungu ndio HEKIMA YA MUNGU kwetu leo,k**a tutakuwa wabobezi katika maneno ya Mungu, *tutajikuta tumehekimishwa na kupata maarifa kuzidi wenye hekima na wenye maarifa ya kidunia* na hayo yatasababisha baraka na kibali katika Maisha yetu. *Mith.4:7-8*

Ni maombi yangu kwako leo,Mungu akujalie hekima na maarifa katika mambo yote ili ulindwe na kuhifadhiwa hatimaye Mungu ajipatie UTUKUFU wote.Maranatha!

24/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Thursday 24th of October 2019

*BWANA NA AKUONYESHE WOKOVU WAKE.*

KUTOKA 14:13
13 *_Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.*_*

Exodus 14:13
[13 _]Moses told the people, Fear not; stand still (firm, confident, undismayed) and see the salvation of the Lord which He will work for you today. For the Egyptians you have seen today you shall never see again._

Haya ni maneno ya mtumishi wa Mungu M***a akiwaambia kundi la watu wa Mungu wairael waliokuwa wakifuatiwa na maadui na mbele yao kulikuwa na kizuizi cha habari ya shamu na kulia na kushoto kulikuwa na milima mikubwa.

Ukiatazama mazingira hayo utaweza kujiridhisha kwamba yalikuwa mazingira magumu na yakukatisha tamaa k**a mwanadamu,

Lakini kupitia mazingira k**a hayo Mungu huyatumia kutuonyesha ukuu na uweza wake na kujipatia UTUKUFU WOOTE,lakini ili hilo litokee tuna wajibu wakufanya mambo yafuatayo:-

*●TUSIOGOPE*
-Hofu ni hisia inayotokana na kile ulichokisikia au kukiona kinachokuaminisha kwamba mbele yako au kesho yako kutatokea mambo mabaya na ya hatari yenye kuangamiza maisha yako.
- *Hofu hukupotezea Uwezo wakupambana na tatizo* kwahiyo tunapaswa tuipinge na kuikataa maana hatukupokea roho ya hofu bali ya Nguvu.

*●TUWE NA IMANI*
-Tukatae kunyenyekezwa na kuwezwa na mazingira bali katika hayo mazingira tuione na kuiamini ahadi ya Mungu iliyo kinyume na hayo mazingira.
-IMANI ndani yetu ndiyo inayotengeneza mazingira mazuri ya Mungu kuingilia kati vita vyetu, na tunazo sababu za kutosha kumwamini Mungu katika mazingira yeyote:-
-Ana uweza wote(haishindwi na jambo)
-Hana njia moja katika kututoa na kutuokoa taabuni.
-Anatupenda upeo n.k

Nimalize kwakusema hivi,Mara zote Mungu *anapotuambia tusimame tuu tukauone wokovu wake,* ni kiashirio tosha kwamba *anakwenda kupigana kwa niaba yetu* na vita vinakuwa si vyetu bali nivya Bwana na ndivyo itakavyokuwa kwako k**a ukifanya wajibu wako.Maranatha!

20/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Sunday 20th of October 2019

*ROHO MTAKATIFU NI ROHO WAMABADILIKO.*

Warumi 8:9-11
11* *_Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliye mfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu,yeye aliye mfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika Hali ya kufa,Kwa Roho wake anayekaa ndani yenu._**

11 _.But if the Spirit of him that raised up Jesus from the dead dwell in you, He that raised up Christ from the dead shall also quicken your mortal bodies by his Spirit that dwelleth in you._ [Romans 8]

Kwa tafakari hii,tunaona ukweli huu:-

♦ *Tunapookoka,miili yetu inakuwa makao ya Roho mtakatifu yule yule aliyekuwepo ndani ya Yesu.*
-Tunabeba uungu mtakatifu,basi lazima miili hii pia,iwe mitakatifu wakati wote.
- *Hututia muhuri* unaobeba utambulisho kuwa sisi ni mali ya Mungu na tu watoto wake.
- *Hutuongoza* katika njia za haki kwaajili yake (Mungu)
- *Hubadilisha mfumo* wetu wamaisha ya kale(Dhambi ) na kutupa mfumo Mpya wa Maisha ya haki.

♦ *Roho huyo hubeba uweza na Nguvu yamabadiloko* yatakayo athiri kwa uzuri miili roho na maisha yetu kwaujumla,athari hizo ni:-
•Kutupa Uzima wamilele
•Husababisha uponyaji wamagonjwa yetu
•Hurejesha nguvu ktk miili nakuifanya upya tena

Kwa ukweli huu kuhusuhu Roho mtakatifu ndani ya Mwamini *,ukufungue ufahamu kwamba,Masaada Unaouhitaji kwaajili ya uponyaji , uzima au madaliko yeyote yakitabia na kimwenendo,Ujue hauko mbali na wwe upo ndani yako.*
-Hakikisha unamwamini nakumruhusu huyo Roho mtakatifu afanye kile unachotaka akifanye.Maranatha!

18/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Friday 18th of October 2019

*TUNAUHAKIKA WA USHINDI KATIKA MAJARIBU*

LUKA 4:1-13
1 *Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,*
2 *akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.*

Si kila tatizo au changamoto inayompata mtu ina sifa ya kuitwa JARIBU,ili shida au tatizo uiite jaribu,lazima hiyo shida ikufikishe njia panda(Mahala pakuchagua aitha uendelee kushik**ana na imani au uikane hiyo imani.)

Hiki ndicho tunachokiona katika tafakari yetu leo,Yesu ana wekewa mitego na shetani ili aikane imani na kupoteza na kuharibu kusudi la Mungu KUUKOMBOA ulimwengu

Katika habari hii Yesu alijaribiwa katika mambo yote na akaibuka na ushindi wakishindo na hii inatuhakikishia na ssi wa leo kushinda *k**a tujajua na kuzitii siri za mafanikio hayo* na siri hizo ni hizi :-

● *ALIKUWA MWOMBAJI* .
-Utaweza tu kuwa na7y nguvu kwa watu pamoja na kwenye majaribu *k**a utakuwa na mda wakutosha wakusemezana na Mungu.*
-Yale maombi yake ya siku 40 kabla,yalifanyika chachu ya ushindi wake.

● *ALIKUWA NA USHIRIKA NA ROHO MT.*
-Alijaa Roho mpaka ikawa rahisi kukubali kuongozwa naye nyikani.
*-Roho atakupa ujasiri,Nguvu na hekima katika mambo yote* ili uweze kujua na kupangua kila mtego na hila toka kwa mwovu.

*●ALILIJUA NENO LA MUNGU na ALIJIJUA YEYE NI NANI*
-Neno likae kwa wingi ndani yako tena kwa hekima yote *ili uweze kuyajua yapi na sio mapenzi ya Mungu Kwako*

● *ALIMTEGEMEA MUNGU SANA.*
-Kutoka kwake tupokee uweza nguvu na neema yakushinda majaribu.

Basi Mungu atusaidie hayo hapo juu kuwa sehemu yamaisha yetu ili tuwe na ushindi endelevu. *2Yoh.2:16-17* Maranatha!

MWANGAZA WA SIKUThursday 10th of October ,2019 *ITAMBUE NGUVU YA MAOMBI NA SIFA* Matendo 16:22-3425. _Lakini panapo usik...
10/10/2019

MWANGAZA WA SIKU
Thursday 10th of October ,2019

*ITAMBUE NGUVU YA MAOMBI NA SIFA*

Matendo 16:22-34
25. _Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za Kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza_
26. _Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi,hata misingi ya gereza ikatikisika,na mara hiyo milango ikafunguka,vifungo vya wote vikalegezwa._
_

Acts 16:25-26 _And at midnight Paul and Silas prayed, and sang praises unto God: and the prisoners heard them._
*_And suddenly there was a great earthquake, so that the foundations of the prison were shaken: and immediately all the doors were opened, and every one's bands were loosed._*
_

Tafakari yetu inatufundisha kwamba:-

●Kuishi maisha ya haki na uaminifu na utakatifu mbele za Mungu, *hakutatuepusha na majaribu au mateso* lakini Mungu ameahidi kutuponya na hayo yote.(Zabr.34:19)

●Kuna wakati Mungu hutuokoa toka katika mateso na hila za adui kwa silaha tusiyo ijua na tukajikuta tupo upande wa pili tukiwa salama,lkn katika kisa hiki cha Paul na Sila tunaona kwa Wazi ktk mstar.25-26 *kwamba MAOMBI NA SIFA kwa Mungu wetu ndizo zilizo sababisha Wokovu na Uhuru kwao na kwa familia ya Askari wa gereza.*

●Sasa Kwanini nisikuaminishe siri hii na Nguvu hii ya kusifu na kumtukuza Mungu dhidi ya vifungo vyako na mateso yako?
-Pata mda wakumsifu na kumtukuza Mungu(useme ukuu wake na uweza wake dhidi ya shida yako)naye kwa GHAFLA atatetemesha, atatikisa misingi yote iliyoshikilia shida yako na hatimaye kukufungua na kku weka HURU katika Jina la Yesu.Maranatha!

09/10/2019

Matukio kwenye sikukuu ya vijana

Address

Tabata Amani
Dar Es Salaam

Telephone

+255718820124

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tag Amani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Tag Amani:

Share